Swali la lazima kwa Wana-CCM: Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge si mafisadi (magamba)?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Walisemwa sana. Kwasasa wananchi wananong'ona chinichini kuwahusu. Urafiki na Serikali iliyopo madarakani unaimarika siku hadi siku. Kila mahala wanapokuwepo na kila maneno wanayoyasema, wanaisifu Serikali kadiri ya uwezo wao. Serikali hii ni ile ile iliyoingia ikijipambanua kuwa iko kwenye vita dhidi ya mafisadi. Rais huyu ni yule yule anayeuchukia ufisadi chamani na Serikalini.

Rostam, Lowassa na Chenge wako ndani ya CCM muda huu. Wako ndani ya chama 'kinachochukia' wizi na ufisadi. Wapo ndani ya chama kinachounda Serikali iliyo kwenye vita dhidi ya ufisadi na wizi chamani na Serikalini. Rostam, Lowassa na Chenge walipachikwa jina la 'Mapacha Watatu' chamani wakati ule wa Rafiki yangu Wilson Mukama.

Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi? Makada wa CCM tunapaswa kulijibu swali hili bila aibu wala woga. Nguvu waliyonayo chamani isifanye tumuache Rais na Mwenyekiti wetu ajongeane na 'mafisadi' hawa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
 
[QUOTE="...Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi?"

IJAPOKUWA MIMI SIYO KADA WA CCM (NA SINA MPANGO WA KUWA KADA WA CCM) NINASHAWISHIKA KUKUJIBU, NA JIBU LANGU NI HILI "ROSTAM, LOWASSA NA CHENGE SIO TUU MAFISADI, BALI NI MAFISADI PAPA"
 
Rais hana uwezo wa kumnawa au kumkarawia Mtemi Chenge.

Akimgusa Chenge tu ! Chenge anatoboa sefuria na haipikwi mboga wala ugali !

Chenge nyoka wa makengeza huwa hamwagi mboga wala ugali lenyewe lenyewe option yake ni kutoboa sefuria

Chenge ni zaidi tumjuavyo.

Poroduct ya Havard University.

Kuhusu Rostam na Lowasa sina maoni jiwe anajua,jiwe anajua,jiwe anajua,jiwe anajua
 
Walisemwa sana. Kwasasa wananchi wananong'ona chinichini kuwahusu. Urafiki na Serikali iliyopo madarakani unaimarika siku hadi siku. Kila mahala wanapokuwepo na kila maneno wanayoyasema, wanaisifu Serikali kadiri ya uwezo wao. Serikali hii ni ile ile iliyoingia ikijipambanua kuwa iko kwenye vita dhidi ya mafisadi. Rais huyu ni yule yule anayeuchukia ufisadi chamani na Serikalini.

Rostam, Lowassa na Chenge wako ndani ya CCM muda huu. Wako ndani ya chama 'kinachochukia' wizi na ufisadi. Wapo ndani ya chama kinachounda Serikali iliyo kwenye vita dhidi ya ufisadi na wizi chamani na Serikalini. Rostam, Lowassa na Chenge walipachikwa jina la 'Mapacha Watatu' chamani wakati ule wa Rafiki yangu Wilson Mukama.

Kutokana na mtiririko na historia yao chamani, Rostam, Lowassa na Chenge ni mafisadi au si mafisadi? Makada wa CCM tunapaswa kulijibu swali hili bila aibu wala woga. Nguvu waliyonayo chamani isifanye tumuache Rais na Mwenyekiti wetu ajongeane na 'mafisadi' hawa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Back
Top Bottom