Lowassa ndiyo kimbilio letu Watanzania kuelekea kwenye mafanikio

Nakubaliana na wewe, mi nlkuwa najaribu kukuelewa kwenye ile post yako nyingine ambapo ulitumia wale wadau wetu wa kwenye "kahawa" ukasema (kwa nukuu isiyonyooka) "EL anakubalika na wabongo wengi nje ya hizi kelele za hapa JF"
Hyo ndio ilikuwa concern yangu.
Sawa mkuu. Ile ya kwenye tangawizi nilikuwa natoa ushuhuda tu wa niliyoyasikia na kisha ndio nikasema kuna watu wengi wanamuunga mkono. Sikuwa na maana ya ile idadi ya wanywa tangawizi wenzangu. Nilikuwa na maana ya watu wengine pia.Kusema kweli kwa sasa hivi baada ya ENL kuanza kuongea kumekuwa na changamoto kubwa kuliko wakati.alipokuwa kimya. Watu wanabishana mahala mahala juu ya yeye kuwa Rais ajaye.
 
Sikio la kufa halisikii dawa hata mumpake mafuta gani hasafishiki ati mbona vichwa vyenu vigumu?
 
Ni kweli hawa jamaa lazima wanavuata mshiko..tugawane basi mbona mnakula peke yenu?
Jamani ujasiriamali wowote ambao unaingiza pesa unakubalika, naomba mnPM na mimi ili nijiunge kwenye hilo kundi la kumsafisha Lowasa maana inaonekana limetengewa bajeti nzuri.
Msiwe na mashaka na mimi nitabadili ID na nitampigia kampeni kwa nguvu zangu zote maana hii njaa sasa imetamalaki.
 
Mwafirka ni ngumu sana kuja kuona kitu kinaitwa mafanikio kwene uso wa hii sayari ya Mwenyezi Mungu na kuwa na heshima kama wanadamu wengine. Mtu kama Lowasa watu wanampigia debe kuwa Rais? Eti vijana wanauliza kwa hii nchi nani si mwizi. Ina maana tunakubali wezi kama taifa? Mwalimu Nyerere hakuwa Mtanzania? Hatuwezi kuwa na watanzania bora kuliko Nyerere na kufanya makubwa kuliko Nyerere mpaka tujikombe kwa wezi kama kina Lowasa? Kwani wakati tunamchagua kilaza JK si kwamba tulimpa sifa kuliko Lowasa? Ila tunaoangalia mambo kwa umakini tulijua tumejiuza kwa kundi la wezi wa CCM. Je Edward Lowasa si kwamba atakuwa mdhaifu na rais mbaya kuliko yeyote aliyepata kuwako? hizo ndizo rekodi za kumchagua mtu kuwa rais? Eti kapeleka maji Shinyanga, eti alivunja mkataba wa city water. Kama kuna mtu kafaidika na pesa za city water ni Edward Lowasa na waziri mkuuwake wakati huo F. Sumaye. Kuna ndugu zangu walikuwa wizara ya maji na urafiki wao na Lowasa uliunganishwa na ulaji wa pesa za wizara kupitia city water. HANA USAFI WOWOTE MWIZI KAMA NYERERE ALIVOMVUA NGUO.
Maskini nchi yangu Tanzania.
 
Yeyote anayetekenywa na kiu ya kuliongoza taifa hili siku za usoni ni sharti awe ni mtu wa kuchukia rushwa; asiye na harufu ya visasi wale kuelekezewa kidole kwa namna yoyote akishutumiwa kutamani 'kutia kofuli' uhai wa wenzake kwa sababu za kisiasa.

Wana JF.
Historia inajibainisha yenyewe kwamba watu makini wa sampuli kama ya Lowassa hawachelei kurejea nafasi za hapo awali.

Na ujio wao huwa ni wa kishindo kikubwa na hicho kishindo ndicho haswa kinawatia viwewe wale mahasimu wake wa kisiasa kutokana na kuona wazi wazi kushindwa kuhimili historia ya utendaji kazi wa Lowassa unaotambulika na kukubalika ndani ya jamaii.

Sote tumeshudia utendaji wa Lowassa kwa nyakati zote tangu mwaka 1975, Mbunge wa Monduli kwa kipindi chote hicho kaweza kufanya mambo yanayoonekana kwa macho ambapo kwa namna mojo ama nyingine yataendelea kuwanafaisha waliopo na vizazi vijavyo.

Lowassa, alipigana vilivyo ongezeko la shule, hakuwapa nafasi ya kupumua wakuu wa mikoa wa wilaya katika ujenzi wa shule hizo.

Hali hiyo ilisababisha ongezeko kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 15,816 mwaka 2010 ambalo ni sawa na ongezeko la wastani wa shule 1559 hali iliyowezesha wanafunzi kuongezeka kutoka 7,541,208 hadi 8,419,305. Haya yote ni matunda ya kazi ya Edward Lowassa.

Tunakumbuka ya kwamba huyu huyu Lowassa aliweza kuvunja mkataba mbovu wa City Water kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Lowassa alipokuwa Waziri wa Ardhi alisimama kidete pale alipogundua Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wamempa mfanyabiashara eneo la Mnazi Mmoja.

Lowassa hakubaliana na uamuzi huo na kuamuru wananchi wauvunje uzio wake na mabati aliyoweka na hivyo eneo la uwanja kurudi kwa Serikali na Wananchi
 
Ndugu yangu hivi hunaweza kuyatolea ushahidi wa hayo maneno yako?

Tunapaswa kufahamu kuwa hakuna binadamu aliyemkamilifu kwa asilimia zote isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.

Hivyo kwa Lowassa kama binadamu, pamoja na wewe kila mmoja na ana mapungufu yake!


yES YOU ARE RIGHT. shida ni extent ya mapungufu yake.
 
Naona watu wamekosa mtu wa kuwaongoza vile baada ya viongozi kama Dr Slaa kutofanya yale waliyotarajia yafanyike 2011. Sasa kinachofanyika hapa saizi ni kujaribu kutafuta mtu anayeweza kuwafikisha wanapotaka, pamoja na hayo siasa za bongo zina safari ndefu sana. Watu watarudia rudia huu mchezo wa kumsifia Lowasa hadi atakuwa ndiyo kimbilio.

Tuna watu wengi zaidi ya EL jamani, sema watu wanaotajwa tajwa kwenye media ndiyo wanakuwa chaguo. Lakini ningependa tupate rais tusiyemfahamu hadi sasa, kama ilivyokuwa kwa Ben Mkapa. Tumfahamu wakati wa mchujo na kampeni harafu watanzania tuamue wenyewe.
 
Naona watu wamekosa mtu wa kuwaongoza vile baada ya viongozi kama Dr Slaa kutofanya yale waliyotarajia yafanyike 2011. Sasa kinachofanyika hapa saizi ni kujaribu kutafuta mtu anayeweza kuwafikisha wanapotaka, pamoja na hayo siahsa za bongo zina safari ndefu sana. Watu watarudia rudia huu mchezo wa kumsifia Lowasa hadi atakuwa ndiyo kimbilio.

Tuna watu wengi zaidi ya EL jamani, sema watu wanaotajwa tajwa kwenye media ndiyo wanakuwa chaguo. Lakini ningependa tupate rais tusiyemfahamu hadi sasa, kama ilivyokuwa kwa Ben Mkapa. Tumfahamu wakati wa mchujo na kampeni harafu watanzania tuamue wenyewe.
Mkuu mawazo yako mazuri lakini kwa siasa za Tanzania kwa sasa ni vigumu kumpata Mgombea ambaye hafahamiki hasa kutoka CCM. CCM kwa sasa inaongozwa na makundi hivyo mgombea wa CCM lazima atatoka kundi fulani ambalo lipo. CCM ingekuwa na mtu kama hayati JKN labda ingempata mgombea compromising asiye na makundi ndani ya Chama.
 
Lowasa namkubali kutokana na utendaji, jamaa ni kichwa pia ni mchapa kazi kutokana na kupiga kazi ndio maana akaingizwa kwenye mkenge wa Richmond ila ukweli ni kwamba Lowasa hausiki ktk richmon. mwacheni mbaba wa watu awasaidie watanzania maskini, wenye njaa , alafu mafisadi wapo mjini tunao wadogowadogo hao ndio wanakula uchumi wa nchi kama mchwa ni wengi sana .
 
Kama alifanya mazuri kwako na si nyumbani kwenu endeleeni kupanua midomo yenu kumsifia LAKINI mjue mnamtaka nyinyi NDG zenu wote nyumbani wakiwemo Wake/Waume zenu hawamtaki. Angalia msivunje mahusiano yaliypo msaada kwenu kwa ajili ya mtu ambaye wala hakujui anachowaza yeye ni biashara zake zikue ndani na nje ya TZ na huo Urais anaouota. Kibaya mmeanza mapema mno ni mwaka tu sasa na miezi 3 bado sana mnaop uhakika miaka miwili ijayo wewe na wengine na hata yeye mtakuwepo? Acheni kufanyakazi ya Mungu
 
Tupende tusipende, nchi yetu yapasa kuongozwa na mtu asiyeona haya, mithili ya kuvaa ngozi ya kondoo usoni. Nchi haiwezi kupiga hatua kwa kucheka, kutabasamu, kutotoa maamuzi, kutegemea misaada, kutokuwa na misingi ya kujitegemea kiuchumi. kutotolea ufafanuzi wa kina wa mambo mazito ya nchi hususan-UCHUMI.
Lowassa angeendelea kuwepo madarakani baa la njaa lingepungua kama si kuisha, alishaweka mikakati na premier wa Thailand juu ya kilimo cha mvua za kutengeneza...na alishazuru nchi hiyo kwa minajili ya kukuza kilimo na si KILIMO KWANZA.
Ukitazama kwa mapana:-
  • Alianza kwa suala la kujenga shule za chini na azma kuziboresha.
  • akaelekeza akisi kwenye kilimo na alishatembelea Thailand.
  • Ambacho angefatia nacho ilikuwa ni jinsi ya kutengeneza ajira mpya hususan kwa rika la vijana.
Japo anazo scandals pesa zikimkalia mbele...waila ni mtendaji zaidi na zaidi. Namwamini kiutendaji na ufuatiliaji wake.

Huoni hili hapa linatosha ku disqualify? HUKU Mnakotaka kumpeleka pesa zote si zitakuwa mbele yake?
 
Mfano mwingine unaoonyesha Lowassa anakubalika ni siku ile walipoenda na JK UDSM, JK alizomewa sana ila Lowassa alishangiliwa sana na wanafunzi na hata kufikia hatua ya kumwomba msaada awasaidie ktk kutatua matatizo ya wanafunzi pale UDSM. Jamaa ana nyota ya asili ya kupendwa na watu

Wako very strategic. Si hata wewe ulikuwa mwanafunzi one day? walikuwa wanataka kutumia pesa yao waliyokwapuliwa.
That is the only way you can use it.
 
Mwl Nyerere si alimkataaga huyu? watanzania wanataka mabadiliko.

Nyerere hakumkataa tu bali pia alindika kuwa (mfanyabiashara asiingie Ikulu) maana hapo Ikulu hakuna biashara. EL ni mfanyabiashara mkubwa na biashara zake ni kubwa za mabilion. Atafuata nini Ikulu!? Mkitaka aingie Ikulu hapo mnataka akafanye biashara ya viungo vya binadamu yeyote hata asiyekuwa albino. Angalieni kama si wewe viungo vya mwanao vitauzwa.
 
Nyerere hakumkataa tu bali pia alindika kuwa (mfanyabiashara asiingie Ikulu) maana hapo Ikulu hakuna biashara. EL ni mfanyabiashara mkubwa na biashara zake ni kubwa za mabilion. Atafuata nini Ikulu!? Mkitaka aingie Ikulu hapo mnataka akafanye biashara ya viungo vya binadamu yeyote hata asiyekuwa albino. Angalieni kama si wewe viungo vya mwanao vitauzwa.

Ila Mbowe anaruhusiwa kuingia ikulu kwa sababu biashara zake ni za lakilaki
 
Sawa kabisa mkuu. Hilo ndilo jina lao nilikuwa nashangaa kuwapa jina na gerezani united na Nungu FC!

Ha! Ha! Ha! Ha! Unanikumbusha mbali sana...Nungu FC juzi wamefiwa na mtu wao muhimu Mwenyekiti Babu Chela.
 
Back
Top Bottom