Lowassa na Tatizo la Uongozi CCM

Lakini Tatizo ni kwamba Viongozi wetu hawawekezi katika kuelimisha umma umuhimu wa sensa ili wananchi wajue faida zake kwa maisha yao, sana sana viongozi wetu ni kuwatisha na kuwachanganya tu wananchi juu ya zoezi hili kwa malengo ya kisiasa.
...Unapoona viongozi wanatumia vitisho, badala ya ushawishi katika mambo ya muhimu kwa taifa kama hili, kaa chonjo hali si nzuri.

Mapungufu ya Uongozi miongoni mwa wanasiasa wetu pia yanajitokeza katika suala la usimamizi wa sekta ya elimu. Kama tunavyozidi kushuhudia, sekta ya elimu ni janga kubwa, ila worse, it is a timing bomb. Baada ya ujio wa soko huria na ulegezaji wa uchumi, sekta ya elimu nayo ikageuka kuwa bidhaa inayoshindaniwa kwa nguvu za soko.
...Sijui Mhe. Sitta atakuwa na lipi la kusema katika topic kama hii, ukizingatia kwamba anatuhimiza kuzichangamkia fulsa zipatikanazo katika jumuiyah ya afrika mashariki.

...I hope, someday people will encourage colleagues to put their money where their mouth is at.

Lakini education administrators and policy makers hawajali kwani watoto wao hawasomi shule zinazokabiliwa na changamoto hizi.
...This will surely come to haunt us, big time, in the very near future.
 
DAR si LAMU...ahsante mkuu, nafikiri hatuna tofauti kubwa hapa ya kimsingi. Nimependa sana hii concept yako ya political and economic capital. Wapinzani wakiingia na political capital kubwa watajaribu nafikiri kujenga nchi na kufanya siasa kidogo kwa sababu watakua na safe mandate ambayo haiwezi kuexpire haraka baada ya miaka 5 tu. Hapa hata yale maamuzi magumu ya muda mrefu watayachukua. economic capital hamna labda tuseme yaani changamoto za kiuchumi ni kubwa na nyingi mno na hii itawafanya wapinzani wakiingia wasiwe na muda na long term planning kwa sababu matumaini ya watu ni makubwa na hapa wataziba ziba viraka tu hapa na pale huku wakipiga siasa wanasubiri uchaguzi ufike. hapa ni tatizo.
 
...My friend, let me take you head on. Nionyeshe nchi maskini yenye demokrasia ya kweli?....ipi, Zambia? Ingawa inafahamika kwamba nchi hiyo is as far as poor africa can get in democracy.

...Ukweli ulio wazi ni kuwa, hata "wapinzani" wakichukua nchi there is not much they can change. Kwa kuwa, nchi ishavurugika kabisa, and we are nearing the state of anarchy. Sasa, itabidi wafanye kazi kubwa kuweka mambo sawa, na hiyo itatokana na vitu vikuu viwili. First, their political capital [how they are being trusted by the people, especially on reforms]. Second, how much economic health we'll be left with, to carry those -at times- costly reforms. For sure, as things stands, the last one will be the most challenging.

...Wakati mwingine, hakuna formula ya kupata demokrasia, maendeleo, n.k. iliyo rasmi kwa jamii fulani fulani. Nakubaliana nawe kwamba strong and somewhat independent institutions ni muhimu kwa demokrasia kushamiri, hata hivyo kuwa na demokrasia katika jamii fulani ni mchakato. Infact, kuzaliwa kwa demokrasia ndio huleta hizo taasisi huru na zenye nguvu.

...Now, lets be real. Katika hali kama ya kwetu kwasasa, unategemea kwamba tusipokuwa na vyama vya siasa na uchaguzi tutapata hizo taasisi? Labda utufahamishe, zitazaliwa vipi?

...Je, unafahamu kwamba ni vyama hivi vya siasa na uchaguzi at least ulio huru, ndio uliopelekea kufahamika, kufichuliwa, na kuchukuliwa -angalau- hatua dhidi ya uozo mwingi, na kuwafanya watendaji kukaa chonjo?

...Tuko pamoja! Ila, unafahamu kazi ya kuelimisha jamii inavyozidi kufanywa siku hadi siku, na watu kama HakiElimu?

...Vuta subira ndugu, kazi kama hizo huchukua miaka kadhaa kuonyesha mafanikio yeyote.

...Swali la msingi kabisa. Hata hivyo haimaanishi kwamba hamna mtu kwasasa atakayeweza kuongeza mapato ya nchi. Ukiweka mazingira rafiki ya uwekezaji -hasa wa ndani- , ukapunguza rushwa -hasa katika utoaji huduma na haki- , Ukawekeza katika miundo mbinu [nadhani inafahamika], utakuwa umewatendea haki sana waTanzania katika kuwakwamua kwenye tope la umasikini. Hatimae, wakichangamkia fulsa hiyo, utaongeza kipato cha nchi.

...Tusipoweza kujiuliza maswali haya na mengine mengi kama wananchi, basi, hatuna chetu na hakuna wa kumlalamikia.

Hivi, just out of curiosity, nini unadhani zitakuwa ideal indicators za kupima performance ya serikali ya Chadema? Na zitakuwa under what time frame?
 
Jambo lingine ni kwamba hizo tofauti ulizozieleza, kwa wananchi wengi hawajui au hawawezi kuzipambanua na kuzielewa, wangezielewa wangeweza kuwa makini katika kuchagua viongozi sio wanasiasa, hivyo kutokana na ujinga wa kutokujua elimu ya uraia kama hii, matokeo yake wamekuwa wakichagua wanasiasa tena kwa ushabiki bila kujua kufanya hivyo inagharimu maisha yake na taifa kwa ujumla. Mimi nashauri kwakweli bila kuwapatia elimu wananchi wetu wakajua umuhimu wa kuchagua viongozi sio wanasiasa, nina hakika Tanzania inaangamia... kibaya zaidi hata haki za msingi wanachi hawazijui kwahiyo ni vigumu kuzidai na wachache wanaozijua wamekuwa waoga kwakuwa walio madarakani wanafahamu kuwa ujinga wa wananchi ndio mtaji wao kuendelea kutawala, na hao wachache kudhibitiwa kwa vitisho hata kugharimu maisha yao.

Hasa ujinga ni mtaji mkubwa sana kwa wanasiasia wa Tanzania. Ndiyo maana siasa za hapa kwetu ni za ushabiki tu na kupewa vitu vidogo vidogo kama t-shirts, khanga na leso za CCM tena nisisahau mlo wa siku moja vinatosha kununua kura ya mwananchi fukara wa kila kitu. Aibu sana
 
Hata usemeje, Lowassa ni mwanasiasa and a very ambitious one. He is just one and the same of his party comrades. Many if not all his decisions are self centred
 
Jambo lingine ni kwamba hizo tofauti ulizozieleza, kwa wananchi wengi hawajui au hawawezi kuzipambanua na kuzielewa, wangezielewa wangeweza kuwa makini katika kuchagua viongozi sio wanasiasa, hivyo kutokana na ujinga wa kutokujua elimu ya uraia kama hii, matokeo yake wamekuwa wakichagua wanasiasa tena kwa ushabiki bila kujua kufanya hivyo inagharimu maisha yake na taifa kwa ujumla. Mimi nashauri kwakweli bila kuwapatia elimu wananchi wetu wakajua umuhimu wa kuchagua viongozi sio wanasiasa, nina hakika Tanzania inaangamia... kibaya zaidi hata haki za msingi wanachi hawazijui kwahiyo ni vigumu kuzidai na wachache wanaozijua wamekuwa waoga kwakuwa walio madarakani wanafahamu kuwa ujinga wa wananchi ndio mtaji wao kuendelea kutawala, na hao wachache kudhibitiwa kwa vitisho hata kugharimu maisha yao.

Hasa ujinga ni mtaji mkubwa sana kwa wanasiasia wa Tanzania. Ndiyo maana siasa za hapa kwetu ni za ushabiki tu na kupewa vitu vidogo vidogo kama t-shirts, khanga na leso za CCM tena nisisahau mlo wa siku moja vinatosha kununua kura ya mwananchi fukara wa kila kitu. Aibu sana

Upo sahihi kabisa, na tatizo hili linachangiwa sana na kiwango cha juu sana cha illiteracy huko vijijini. Kwa mtazamo wako na katika mazingira haya, kazi hii ya kuwaelimisha ifanywe namna gani na kupitia vyombo gani? Kwa kweli hii ni shughuli nzito.
 
DAR si LAMU...ahsante mkuu, nafikiri hatuna tofauti kubwa hapa ya kimsingi. Nimependa sana hii concept yako ya political and economic capital. Wapinzani wakiingia na political capital kubwa watajaribu nafikiri kujenga nchi na kufanya siasa kidogo kwa sababu watakua na safe mandate ambayo haiwezi kuexpire haraka baada ya miaka 5 tu. Hapa hata yale maamuzi magumu ya muda mrefu watayachukua. economic capital hamna labda tuseme yaani changamoto za kiuchumi ni kubwa na nyingi mno na hii itawafanya wapinzani wakiingia wasiwe na muda na long term planning kwa sababu matumaini ya watu ni makubwa na hapa wataziba ziba viraka tu hapa na pale huku wakipiga siasa wanasubiri uchaguzi ufike. hapa ni tatizo.
...Hauko mbali na ukweli, na hiyo itakuwa katika miaka mitano ya kwanza -yatakayotokea baada ya hapo hatuyajui- na kama watakuwa na political capital ya kutosha kuweza kupata nafasi nyingine -ambapo dynamics za kisiasa zitakuwa zimebadilika- wanaweza kufanya kazi za maana zaidi.

...Nadhani tunaweza kuchukua mfano wa narc kenya -jinsi ambavyo hawakufanya mambo ya kuonekana wazi, kwa wingi- katika kipindi chao, lakini, pamoja na vurugu za uchaguzi baada ya dynamics za kisiasa, hivi sasa kinachofanyika kinaonekana.

...My point here is, we should not expect wonders. Mambo kugeuka itachukua muda, more than five years, give or take, ndio tunaweza ona dalili zake.
 
Hivi, just out of curiosity, nini unadhani zitakuwa ideal indicators za kupima performance ya serikali ya Chadema? Na zitakuwa under what time frame?
...Kwanza, sidhani kama hizi nitakazozisema naweza kuziita "ideal indicators". Nadhani itabidi tukubaliane vitu vipi tuviite ideal indicators. Pili, itakuwa vema kama tutawa-held accountable kwa ahadi zao, ambazo ni nyingi. Huwa napata shida na ahadi kuwa nyingi, bila time frame ya kueleweka.

...Tatu, nije kwenye indicators.

...Miaka mitano ya mwanzo, inabidi mfumuko wa bei ushuke -inaweza isiwe hivyo kutokana na external factors, au ukame, n.k.- ili tujue wanaweza kufanya kitu economy side. Hiyo mitano itakapokuwa inafikia ukingoni, tuweze ona matumizi ya serikali -wasteful/unnecessary spending- yamepungua. Hii isichanganywe na matumizi kuongezeka, development side. Kwa kuwa ahadi zao lazima wazitekeleze.

...Tusisahau, kupungua kwa ufisadi na rushwa. Baada ya miaka mitano itabidi tuone kitu cha maana kimefanyika.

...Elimu na Afya, lazima kuwe na some improvements, kama, kupanda kwa kiwango cha elimu, kukiendana sambamba na ubora wa mazingira ya kazi ya walimu. Likewise kwenye afya.

...Kama nilivyosema hii yote itatokana na waliyoahidi, lakini, muhimu pia hata vile ambavyo hawajaahidi na vinavyotusumbua kama jamii. I will not give anyone more than five years, to see if they are serious.
 
2. Kiongozi ni mtu ambae hufanya maamuzi yanayolenga maslahi ya taifa au jamii inayomzunguka; Mwanasiasa hufanya maamuzi yanayokilinda chama chake, lakini hasa kuwaimarisha wanasiasa au makundi yaliyomfadhili/yaliyompa nafasi yake ya uongozi.

Na hii purely ndiyo tabia aliyonayo rais wetu wa sasa. Rais wetu wa sasa ni MWANASIASA siyo KIONGOZI. Nimeipenda point kuhusu miradi kwamba mwanasiasa anawaza vimiradi vidogovidogo vya kipuuzi kwa maslahi ya muda mfupi ya kisiasa lakini kiongozi anawaza miradi mikubwa yenye impact kubwa kwa wananchi wake. Katika kutafakari hili, nimekumbuka MRADI WA BAJAJI ZA KUBEBA WAJAWAZITO.
 
...Kwanza, sidhani kama hizi nitakazozisema naweza kuziita "ideal indicators". Nadhani itabidi tukubaliane vitu vipi tuviite ideal indicators. Pili, itakuwa vema kama tutawa-held accountable kwa ahadi zao, ambazo ni nyingi. Huwa napata shida na ahadi kuwa nyingi, bila time frame ya kueleweka.

...Tatu, nije kwenye indicators.

...Miaka mitano ya mwanzo, inabidi mfumuko wa bei ushuke -inaweza isiwe hivyo kutokana na external factors, au ukame, n.k.- ili tujue wanaweza kufanya kitu economy side. Hiyo mitano itakapokuwa inafikia ukingoni, tuweze ona matumizi ya serikali -wasteful/unnecessary spending- yamepungua. Hii isichanganywe na matumizi kuongezeka, development side. Kwa kuwa ahadi zao lazima wazitekeleze.

...Tusisahau, kupungua kwa ufisadi na rushwa. Baada ya miaka mitano itabidi tuone kitu cha maana kimefanyika.

...Elimu na Afya, lazima kuwe na some improvements, kama, kupanda kwa kiwango cha elimu, kukiendana sambamba na ubora wa mazingira ya kazi ya walimu. Likewise kwenye afya.

...Kama nilivyosema hii yote itatokana na waliyoahidi, lakini, muhimu pia hata vile ambavyo hawajaahidi na vinavyotusumbua kama jamii. I will not give anyone more than five years, to see if they are serious.

Nakubaliana na wewe on most issues hapo juu; ila i find it very interesting kwa mfano Obama uchumi umemshinda kwa kiasi kikubwa kutokana na matatizo aliyoridhi toka kwa Bush na pia mwenendo wa global economy kwa ujumla lakini siasa za wenzetu wao hawatafuti visingizio kwamba bush this or bush that, na akifanya tu hivyo, he goes down the drain in november; inabidi na sisi tukomae na kufikia kiwango kama hiki - kwamba, fine, tumeiondoa CCM madarakani kwa mfano 2015, sasa 2020 mbona mambo yamekuwa ndivyo sivyo? Sasa hapo Chadema most likely itatumia vizuri sana utawala wa miaka 50 wa CCM au ujamaa au sijui kitu gani kama njia ya kukwepa lawama;
 
...My point here is, we should not expect wonders. Mambo kugeuka itachukua muda, more than five years, give or take, ndio tunaweza ona dalili zake.

Na this is what will land defeat kwa Chadema in 2020 kwani wamejisahau kabisa kuelezea umma kwamba kwa mfano tunaomba miaka mitano, kumi to reconstruct, then miaka so and so to develop, huku wakiaminisha umma kwamba watakaofaidika na changes za 2015 ni watoto na wajukuu, cha kufanya wao kwa sasa ni kuendelea kuvumilia kama walivyovumilia kwa miaka 50 but this time kwa faida ya watoto na wajukuu zao na indicators to measure performance and progress ziwe wazi; ni muhimu chadema kuambia umma kwamba faida watakayoipata immediately after 2015 ni immediate stoppage ya madudu haya na haya na kwamba things wont get worse; otherwise muda unazidi kuyoyoma na Chadema isnt working on sustainability, ndio maana nashawishika sana kwamba CCM itarudi madarakani in 2020 if not before;
 
Ukiondoa dhana ya ufisadi iliyopo kwa Edward Lowasa, ni yeye pekee ambaye ameweza kusimama kidete misimamo yake licha ya kupigwa vita kali ndani ya chama chake.

Lowasa amediriki kutamka waziwazi baadhi ya mapungufu ya sera za CCM jambo ambalo viongozi wengi wanafiki wameshindwa kuikosoa serikali yao. Ni majuzi tu Lowasa ametamka kuwa haungi mkono sera ya Kilimo kwanza kwani haina mwelekeo wa kumkomboa mkulima wa TZ.

Ndani ya Dhamira yangu ninaamini kuwa mtu hata awe mchafu kiasi gani akioga kwa sabuni ya CHADEMA lazima atakate, nadhani ni muda muafaka sasa kwa mtu kama Lowasa kujiunga na M4C japo mwenyewe kasema msemo wa waingereza "I will cross the bridge when i get there". Atavuka daraja akilifikia.
 
Hana mpinzani ndani ya ccm LOWASA , aende cdm akafanye nini? Wakina NAPE na SITTA washanyeng'enya.
 
Nakubaliana na wewe on most issues hapo juu; ila i find it very interesting kwa mfano Obama uchumi umemshinda kwa kiasi kikubwa kutokana na matatizo aliyoridhi toka kwa Bush na pia mwenendo wa global economy kwa ujumla lakini siasa za wenzetu wao hawatafuti visingizio kwamba bush this or bush that, na akifanya tu hivyo, he goes down the drain in november; inabidi na sisi tukomae na kufikia kiwango kama hiki - kwamba, fine, tumeiondoa CCM madarakani kwa mfano 2015, sasa 2020 mbona mambo yamekuwa ndivyo sivyo? Sasa hapo Chadema most likely itatumia vizuri sana utawala wa miaka 50 wa CCM au ujamaa au sijui kitu gani kama njia ya kukwepa lawama;
...Nadhani unafahamu by now kwamba uchumi haujamshinda Barry. Back then it seems like it. It was just a matter of time. Mambo yalikuwa hovyo.

...Sidhani kama CCM itaondoka madarakani mwaka 2015, but CDM will make history, and Tanganyika's politics will be transformed. Pengine itaondoka, but CDM will not win the election. Another, newer one will.
 
Na this is what will land defeat kwa Chadema in 2020 kwani wamejisahau kabisa kuelezea umma kwamba kwa mfano tunaomba miaka mitano, kumi to reconstruct, then miaka so and so to develop, huku wakiaminisha umma kwamba watakaofaidika na changes za 2015 ni watoto na wajukuu, cha kufanya wao kwa sasa ni kuendelea kuvumilia kama walivyovumilia kwa miaka 50 but this time kwa faida ya watoto na wajukuu zao na indicators to measure performance and progress ziwe wazi; ni muhimu chadema kuambia umma kwamba faida watakayoipata immediately after 2015 ni immediate stoppage ya madudu haya na haya na kwamba things wont get worse; otherwise muda unazidi kuyoyoma na Chadema isnt working on sustainability, ndio maana nashawishika sana kwamba CCM itarudi madarakani in 2020 if not before
...Watanganyika hawawezi kuelewa, i mean most of them. Ni ukweli unaouma, kwamba hatujui tunastaili nini

...Believe me on this one. Kama CCM watapoteza mwaka 2015, they will not come back. Watasambaratika. Infact, watasambaratika kabla ya kushindwa, kama itakuwa wanashindwa mwaka 2015. KANU style.
 
...Nadhani unafahamu by now kwamba uchumi haujamshinda Barry. Back then it seems like it. It was just a matter of time. Mambo yalikuwa hovyo.
Sijaelewa hoja hii, lakini kushindwa kwa Obama haina maana kwamba yeye ndiye wa kulaumiwa, bali he was and still is expected to make a difference, na kukaa mbali kabisa na hoja kwamba alipokea uchumi mbaya; ndio maana hata kwenye kampeni zake, ilikuwa nadra sana kwa timu yake kutumia hoja kwamba Bush ndiye wa kulaumiwa; Wenzetu wanaendesha siasa za kistaarabu na rational like - kama hauwezi, pisha wengine, tunajua nani aliharibu, lakini tunataka progress, sio excuses;

...Sidhani kama CCM itaondoka madarakani mwaka 2015, but CDM will make history, and Tanganyika's politics will be transformed.

Nakubaliana na wewe katika hili; Tatizo la CCM ni kwamba inataka sana kuendeleza siasa za mass - based political party whereby by, ushindi wa kishindo ndio kipimo cha kubalika; enzi za mass - based political parties zimeshapitwa na wakati, demokrasia ya uliberali hairuhusu mazingira hayo, ni muhimu CCM ikajiandaa kisaikolojia kuwa chama cha kushinda kwa asilimia moja, mbili, tatu, kama ilivyo katika demokrasia nyingine, na hata kama inavyotokea Zanzibar nyakati hizi; trend ndio ipo huko; Vinginevyo CCM kupata 50.01% 2015 ni kitu kidogo sana, unless kanuni za mshindi ni mshindi zibadilike kabla ya uchaguzi mkuu ujao;

Pengine itaondoka, but CDM will not win the election. Another, newer one will.
Sidhani kama itaondoka, hasa kwa kuzingatia hoja yangu hapo juu; Lakini nakubaliana na wewe kwamba hali ikiwa mbaya zaidi, CCM will have to go and pave way for another party, CDM will not win the election, this is almost a fact and we all know why, who, and how;
 
...Watanganyika hawawezi kuelewa, i mean most of them. Ni ukweli unaouma, kwamba hatujui tunastaili nini

Nakubaliana na wewe, na tumelijadili sana hili kwenye uzi mwingine;

...Believe me on this one. Kama CCM watapoteza mwaka 2015, they will not come back. Watasambaratika.

Nakubaliana na wewe only to an extent kwani kuna uwezekano pia wachumia tumbo wote wa CCM pamoja na mafisadi wakaondoka iwapo chama kitaanguka 2015, na kubakisha wachache ambao watakiendeleza chama; katika mazingira haya, CCM itakayobakia itakuwa na uwanja mpana zaidi wa ku scrutinize wanachama wasiofaa na kuwazuia mapema, lakini pia kurudia mazuri ya baba wa taifa, masuala ambayo kwa sasa ni vigumu kufayanya na sote tunaelewa ni kwa sababu gani;

Infact, watasambaratika kabla ya kushindwa, kama itakuwa wanashindwa mwaka 2015. KANU style.

Uwezekano wa kusambaratika pia upo lakini sioni possibilities kabla ya uchaguzi wa 2015, unless uzitaje na tuzijadili; Pia sioni suala hili kufuata mkondo wa KANU; Content and Context wise, KANU na CCM ni vitu viwili tofauti kabisa; ukitafiti kidogo juu ya forces zilizofanya TANU iporomoke, na pia juu ya coalition husika, utagundua kwa urahisi tu kwamba CCM lacks the necessary ingredients, which is a good thing in itself;
 
Mara nyingi siasa za Afrika hasa Tanzania ni ngumu kuzungumza bila kumtaja mtu, Hii inatokana na elimu zetu na uelewa wetu mdogo ktk mambo ya Siasa kwa ujumla.

Mada inaeleweka Ni big deal kujua ugonjwa unaokusumbua kwanza ndo utafute Tiba, kwani ni ujinga kutafuta Tiba bila kujua Ugonjwa Lowassa anajua Tatizo la CCM ni uongozi na kwakuwa CCM ndio uunda Serikali ndo Kauli ya Nyerere inapokuwa ya kweli Tusiwe yai tujivunje ili tuwe ktk ulimwengu Israel kila mara ufanya mabadiliko ya uongozi na utumia vyama v3 Labour, Likud na Kadima Labour ikiwa inaongoza serikali ikiyumba Israel inapoteza mwelekeo wananchi wanatoa maoni Wanataka uchaguzi then Likud inaingia hivyohivyo likud iliyumba Inaingia Kadima sasa ipo Likud,

El aliposema watu walipiga kelele hasa Waziri Mkuu Pinda, Mukama na Nape lkn mwisho Mkutano wa 8 CCM ikabadilika wakabadili sura wakaja kinana na Mangula

Tatizo letu hatuna uthubutu wa kuzungumza ukweli au uozo kwa kutojiamini au uwezo wetu wa kuona ni mdogo so Lowassa ameweza kusimama na kutoa mawazo yake yamefanyiwa kazi EL ni Kiongozi na Mwanasiasa kwa pamoja.

Mchambuzi wacha watu wajadili wanavyojisikia ila mwisho chambua yaliyo mazuri ndo uyachukue PUMBA HAZIKOSEKANI KTK NAFAKA
 
Sinshoo,

Umezungumza hoja za msingi sana bandiko namba 79; Mimi naona viongozi wote wa CCM ni wanafiki kwani suala la Lowassa kiini chake ni Azimio la Zanzibar (1992) ambalo liliua azimio la Arusha, jambo ambalo viongozi wote wa CCM ya sasa waliliafiki; Sasa iweje leo mwenzako kulitumia vyema ndio iwe tatizo? Kwa mwana ccm yoyote kuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi na maamuzi kuanzia 1992 hadi leo kumnyoshea kidole Lowassa ni unafiki, wivu na fitina; Haina maana kwamba Lowassa hana matatizo, hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba tatizo la Lowassa ni tatizo la viongozi wote wa CCM kwani wote in one way or another wametumia kikamilifu sera mpya ya Azimio La Zanzibar kufikia hapo walip - wana mishahara zaidi ya mmoja, wananyuma za kupanga, wana hisa katika publicly traded companies, the list goes on and so, wanachopishana ni magnitude and context, but not much on content;

Simtetei Lowassa bali nachojaribu kusema ni kwamba viongozi wa CCM ni wanafiki, wapo madarakani chini ya sera ya azimio la Zanzibar, lakini hapo hapo wanatumia azimio la Arusha kushambulia wengine; kwanini wasihame chama na kwenda Chadema na kwingineko ili wame na moral authority ya kuzungumzia Azimio la Arusha? Kwanini hakuna hata mmoja anayeliponda azimio la Zanzibar? Kwa kufanya hivyo, ndio wataweza kushughulikia suala la Lowassa; Lakini mpaka wakifikia hatua hiyo, ni lazima watakuwa wamevuka kikwazo kama kile cha jamii moja ambayo Yesu aliwakuta watu wakijiandaa kumpiga na kumuua mawe mtu mmoja, na alipouliza kulikoni, akaambiwa amezini; Alipowaambia wajitazame wenyewe kwanza na iwapo kuna msafi, basi arushe jiwe la kwanza, wote wakakimbia;

Suala la Lowassa ni wivu, fitina na unafiki wa Kisiasa na hakuna kiongozi hata mmoja katika CCM ya sasa mwenye moral authority ya kumwangamiza Lowassa; Such a moral authority ipo Chadema na kwingineko ambako hakuna strings attached juu ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ambalo ndio kiini cha wanasiasa kuwa na nafasi ya kujiendeleza kimaisha KIHALALI, Per azimio la Zanzibar;
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom