Lowassa na Tatizo la Uongozi CCM

Naomba mwongozo wako mkuu ili tujadili mada je tuombe admin abadilishe title ili tuwe katika nafasi nzuri zaidi ya kujadili mada husika badala ya mtoa mada? Ni dhahiri kwamba tukiweka uzito kwenye mtoa mada, hatutafikia muafaka wa maana zaidi ya he says she says pamoja na lawama na shutuma zisizo na kikomo. Naomba unisaidie ili tufanikishe lengo mkuu.
...Ndio.
 
Yeye ndiye pia behind your failures 2010 Je, unalijua hilo?
...Mkandara, can you defend this? Una maana huyu Mhe. ana akili kuliko wote huko? au ana nguvu kubwa ya ushawishi kiasi hicho?...Yeye anahusika vipi na watu kutotimiza ahadi zao kwa waTanzania? Its hard to believe!
 
Naomba mwongozo wako mkuu ili tujadili mada - je tuombe admin abadilishe title ili tuwe katika nafasi nzuri zaidi ya kujadili mada husika badala ya mtoa mada? Ni dhahiri kwamba tukiweka uzito kwenye mtoa mada, hatutafikia muafaka wa maana zaidi ya he says she says pamoja na lawama na shutuma zisizo na kikomo. Naomba unisaidie ili tufanikishe lengo mkuu.
Mchambuzi mkuu wangu usiandike kitu kwa woga wa mtu fulani ama kutaka sisi wote tufikirie kama unavyofikiri. Mimi nimekwambia ukweli ambao unaujua jinsi mtu huyu alivyokuwa nuksi na uchaguzi wa mwaka 2010 na wewe ulikuwa victim.. Unaujua vizuri japokuwa hatujuani. Hivyo ondoa sehemu zote zinazomhusu Lowassa weka mawazo na utafiti wako wewe, tumechoka kumsikia mtu huyu.

Lakini the fact remain, huyu ndiye shetani anayetaka kutupa Uzima wa milele, huyu ndiye shetani anayezungumzia kutupa maisha bora toka mwaka 2005. Again hata Hitler alikuwa akisema maneno mazito sana tena kumshinda El, lakini he ends up costing the world big time..Siye huyu alipigiwa simu na Mwakakijiji kuhusu wanafunzi Urusi akasema yuko lunch?..
Kuna wakati mwingine tupime maelezo ya watu hawa kwa kuwasoma wao halafu tunaunganisha. That's all Lowassa hafai hata kwa kulumangia na tunawajua wabunge wote waliopita kwa ticket yake ndio wanao liharibu hata bunge letu leo hii. Need to say more!
 
Tukirudi kwenye mada, je unakubaliana na mimi kwamba tatizo kubwa la CCM ni uongozi ambao umejaa aina tatu ya viongozi - Fake ideologues, political trouble makers and jesters (wapambe)? Je, Wapinzani wanaweza kujifunza nini katika hili, hasa ikizingatiwa kwamba hata vyama vyao haviongozwi kwa itikadi bali masuala mengine ambayo they dont guarantee consistency?
 
Hilo siyo tatizo la CCM tu, ni tatizo la nchi nzima. Watanzania hatujui mfumo gani wa kiuchumi tunaouhitaji au tunaoupendelea kwa sababu wengi wetu hatuna uelewa wa maisha kwa ujumla kuanzia sayansi, uchumi, siasa n.k
Watanzania wengi tumekubali mfumo wa rushwa kuwa kama ni halali. Polisi, madaktari, mahakama na kila sehemu yenye muhuri wa serikali ni deal kubwa, lazima utoe kidogo.

Matokeo yake, ni taifa lenye watu limbukeni and as a subset tunapata viongozi limbukeni, wanasiasa limbukeni, mapadre wetu na mashehe wetu wote ni limbukeni wa hali ya juu. Karibu kila mtanzania ni limbukeni anayefikiri kuwa anajua sana. Ukitaka kuhakikisha kuwa Watanzania wengi ni limbukeni, angalia msiba wa Kanumba, kuna watu wamezimia, viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi, bunge limesimama kwa dakika sijui ngapi ... wakati hawakumpa heshima hizo marehemu Kawawa.
Angalia uchafu wa miji au vyoo vya umma kujua jamii yetu ilipo kiustaarabu ndiyo utajua kuwa viongozi tulio nao ni reflection yetu sisi wananchi.
Na hivi vyama vya upinzani ndiyo hovyo kabisa!!, yaani they are a bunch of clowns whining about things that they don't even know, kwa mfano wabunge kususa vikao na kuondoka kisa kuna watu wanazama as if wataenda kuwaokoa. Wabunge wanawafokea regional commissioners, District commissioners na hata Mayors wa halmashauri zao. Hawajui kazi na mamlaka walizo nazo.
Kwa kifupi mkuu Mchambuzi, tatizo ni watu na naombea siku moja aibuke kiongozi atakayesema ukweli.
 
Kama alivyokujibu Kobello.. Hili ni tatizo la Kitaifa.. Watanzania wengi fake trouble makers na Jesters hata siku moja usikae ukamtazama rafiki au jirani yako bila kukumbuka haya mambo matatu..

Kuhusu vyama vya Upinzani elewa vinaongozwa na watu hawa hawa waliozaliwa na baba zetu wa CCM, ni Watanzania hakuna chama kinachoongozwa na watu kutoka nje. Ni sisi kwa sisi tusioaminiana na ni sisi kwa sisi tunaouzana na kudanganyana maana hakuna kiongozi Tanzania ambaye unaweza kunambia kabakia mtu yule yule aliyekuwa akiomba kura za wananchi sii CCM, Chadema wala CUF wote wamebadilika kuwa waoga zaidi ama wana kiburi zaidi. Kila mmoja wao amejijengea hekalu la Uheshimiwa, wananawiri sura zao japokuwa matatizo ya nchi ndio yanazidi. Hawa ndio viongozi wetu wengi ambao kuingia kwao siasa ni kutafuta umaarufu ama siasa zimemhakikishia maisha bora, usalama na mtaji tosha - Politics is just a way out of poverty!

Kwa hiyo vyama vya Upinzani vina tatizo kubwa zaidi ya CCM maana huko nafasi zimejaa, hivyo vijana wengi wanakimbilia huku kwenye Upinzani na hivyo kuwa kazi ngumu sana kwa viongozi waliopo kuwachuja. Je ni viongozi wazuri?.. sidhani wengi wetu ni wanasiasa na ndio watakuwa viongozi wa kesho.
 
Eti mchambuzi,Lowasa unaye mzungumzia wewe ni wepi,yule fisadi na mwizi ambaye nyerere alimuuluza kuwa wewe ni kijana mdogo sana huu utajiri umeupata wapi?Sipati picha kabisa na mambo uliyoyasema,tatizo la watu wengi humu jf wanakuja wakati wameshaongwa ili kuwasafisha watu.Lowasa hakuna mtanzania atakaye msikiliza wote wanajua kuwa ni mwizi,hilo kamweleze kabisa wewe kuwadi na mbwa wake na asijisumbue kwa lolote.Lowasa abebeki kama gunia la misumari.
 
Hilo siyo tatizo la CCM tu, ni tatizo la nchi nzima. Watanzania hatujui mfumo gani wa kiuchumi tunaouhitaji au tunaoupendelea kwa sababu wengi wetu hatuna uelewa wa maisha kwa ujumla kuanzia sayansi, uchumi, siasa n.k
Watanzania wengi tumekubali mfumo wa rushwa kuwa kama ni halali. Polisi, madaktari, mahakama na kila sehemu yenye muhuri wa serikali ni deal kubwa, lazima utoe kidogo.

Matokeo yake, ni taifa lenye watu limbukeni and as a subset tunapata viongozi limbukeni, wanasiasa limbukeni, mapadre wetu na mashehe wetu wote ni limbukeni wa hali ya juu. Karibu kila mtanzania ni limbukeni anayefikiri kuwa anajua sana. Ukitaka kuhakikisha kuwa Watanzania wengi ni limbukeni, angalia msiba wa Kanumba, kuna watu wamezimia, viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi, bunge limesimama kwa dakika sijui ngapi ... wakati hawakumpa heshima hizo marehemu Kawawa.
Angalia uchafu wa miji au vyoo vya umma kujua jamii yetu ilipo kiustaarabu ndiyo utajua kuwa viongozi tulio nao ni reflection yetu sisi wananchi.
Na hivi vyama vya upinzani ndiyo hovyo kabisa!!, yaani they are a bunch of clowns whining about things that they don't even know, kwa mfano wabunge kususa vikao na kuondoka kisa kuna watu wanazama as if wataenda kuwaokoa. Wabunge wanawafokea regional commissioners, District commissioners na hata Mayors wa halmashauri zao. Hawajui kazi na mamlaka walizo nazo.
Kwa kifupi mkuu Mchambuzi, tatizo ni watu na naombea siku moja aibuke kiongozi atakayesema ukweli.

Kimsingi nakubaliana na wewe;

Kiongozi anatakiwa wakati wote awe conscious with his/her political strategy or that of his party, a strategy that aims to deliver on the social and economic ends for the masses. Tatizo lililopo na viongozi wa CCM ni kwamba kwa wao, ilani ya uchaguzi CCM ndio msahafu, lakini mbaya zaidi ni kwamba ilani hiyo hata siku moja haishirikishi wananchi kubaini nini iwe kipaumbele, nini kifanyike sasa, na nini kifanyike muda wa kati na nini kifuate baadae. Viongozi wengi wa CCM wakishaingia kwenye madaraka husika, hujiona wao ndio wanaojua kila kitu, wanaojua mahitaji ya jamii, na wengine wanaweza kabisa kukupangia hata mahitaji ya wake zetu nyumbani.

When it comes to reconciling short term priorities with the long term objectives, viongozi wa CCM ndio wamefeli kabisa. Wameshindwa ku ‘manage' politics and the political institutions under them to meet the immediate requirements of the government as well as move the society towards progress.

Tatizo jingine ni kwamba serikali ya CCM ni serikali ya kikoloni kwa maana ya kwamba wakati wa ukoloni, the colonial government's loyalty was to the imperial power (mwingereza), not Africans, especially not the ones in the country side. Sana sana ilikuwa inajitahidi kuwaweka sawa waafrika in urban areas and the few educated/elite ili wasilete revolts. Nyerere alipotwaa madaraka, he became a contrast whereby as a nationalistic leader, he became an integral part of the African community as a whole, articulating and providing leadership for the hostility to foreign rule, dependence and dominance. Baada ya Mwalimu kung'atuka mwaka 1985 and eventually 1990, serikali ya CCM ikarudi kule kule kwa mkoloni – leo hii it exists to serve the interest of the external forces pamoja na vibaraka wao wachache wenye pesa nchi kwetu Tanzania. Mtanzania wa kijijini amesahaulika kabisa, mazingira anayoishi leo kwa kweli hayana tofauti kubwa na yale kabla ya uhuru.

Serikali ya CCM na viongozi wake have made very little effort to place their activities in the long run/perspective; they haven't articulated an integrated view of the longer term consequences of their present pursuits. Wanachofanya wao sasa is they seek to maintain order and to remain in power; pia wanawekeza zaidi katika maximizing their own advantage as well as the advantage of those in political alliance with them. Mbaya zaidi, wanatumia madaraka kwa faida zao na familia zao ili waiishi maisha yaliyojaa neema baada ya kustaafu.

Enzi za Nyerere, at least he attempted to initiate reforms that aimed to bring life in Tanzania nearer to its perception of how the society wished to develop. Nyerere had clear ideas on how the politics of the country could be managed during this transitional period (political independence to economic independence). In short, tofauti na CCM ya sasa, CCM ya Nyerere had a very clear political strategy in place that aimed to bring about a desired economic and social change kwa umma.

Leo hii, there is an absence of a political strategy. Watawala wa CCM are confident kwamba they know best what the country needs, and they pile this ‘gibberish', tena undemocratically, kwenye ilani ya uchaguzi. For them, that's the political strategy at its best. And they are confident kwamba the donor community ambao basically ndio wanao run our economy, will give them support hence help them further consolidate power.

Watawala hawa walitegemea kwamba they will continue to secure the cooperation and support of Tanzanians indefinitely and unconditionally, lakini sasa wanaona watanzania wamefunguka macho, na wapo tayari kufanya lolote lile kuwapofua.
 
Eti mchambuzi,Lowasa unaye mzungumzia wewe ni wepi,yule fisadi na mwizi ambaye nyerere alimuuluza kuwa wewe ni kijana mdogo sana huu utajiri umeupata wapi?Sipati picha kabisa na mambo uliyoyasema,tatizo la watu wengi humu jf wanakuja wakati wameshaongwa ili kuwasafisha watu.Lowasa hakuna mtanzania atakaye msikiliza wote wanajua kuwa ni mwizi,hilo kamweleze kabisa wewe kuwadi na mbwa wake na asijisumbue kwa lolote.Lowasa abebeki kama gunia la misumari.

Sina sababu yoyote ya kumbeba Lowassa. Nimbebe nimpeleke wapi na kwa malengo gani? Wanaombeba kama wapo basi they belong kwenye kundi la wapambe na wachochezi ambayo nimeyajadili. Hoja ya msingi hapa ni kwamba Lowassa ni kada mwenzangu ndani ya CCM na kasema jambo ambalo limenigusa, na kama unafuatilia, nimekuwa najikita zaidi kujadili hoja na sio mtoa hoja. Kama yeye hana sifa za kuwa kiongozi na badala yake ni mwanasiasa, hoja hiyo inajadilika na nadhani wengi wataifurahia hoja hiyo ingawa haitatupeleka popote kwani Lowassa sio msaafu wa CCM na muhimu zaidi, hatokuwa CCM milele. Kina Nyerere, Kawawa, Kolimba, Sokoine, na wazee wengine walikuwa CCM, maisha yao yakapita na wamepisha wengine. Lowassa hatokuwa tofauti na hawa. Ndio maana mimi simlengi Lowassa bali hoja yake.
 
Mchambuzi,
Maneno mazito sana uloyazungumza hapo juu kuhusu viongozi wetu na umenigusa haswaaa. Kumbuka hii ni hoja inayohusu watu zaidi ya msahafu wa chama chenyewe na ndio maana binafsi yangu huwataja WATU hawa ni kina nani maana kuzungumzia hoja ya mtu kulaumu viongozi wakati tunawajua kwa majina, hii ndio huitwa Nidhamu ya woga. Mkuu, Funguka - hatuna sababu ya kuogopa kusema ukweli maana events na idea huletwa na watu na hivyo tuwanukuu wao kwa hoja zao na pia maadam wao ndio wacheza tuna haki ya kuwapima na kujifunza vile vile kwani kauli ya mtu sii mtaji.

Nikirudi ktk Hoja yetu, Tatizo la CCM kama nilivyosema ni WATU sio chama kwa maana chama kimejieleza vizuri sana malengo na madhumuni yake na ni taifa gani chama kinataka kulijenga lakini on the ground tunaiona picha tofauti kabisa na sababu zipo mbele yetu. Kuna mada fulani inamzungumzia Mukama ajiuzuru na kwamba hafai kuiongoza CCM. Lakini wakati huo huo nikasoma bandiko la mtoa mada na kuchambua kama kweli Mukama hafai kuongoza CCM ya hii leo au vinginevyo.. Na nilichogundua ni kwamba CCM yenyewe kama chama haina mapungufu isipokuwa WATU waliojiunga na CCM hiki ndio wale wasiamini madhumuni na malengo ya chama hicho, hawa ndio hawatakiwi kujiunga na chama maana hawaamini yaliyomo hivyo kwa nini wamejiunga na CCM..

Kati ya madhumuni 18 karibu nusu yake hayakubaliwi na viongozi pamoja na wanachama wengi wa chama CCM leo hii, na niliyaorodhesha yote kuonyesha kwamba CCM ni chama cha kijamaa na kwa Wakulima na Wafanyakazi. Na ukitazama toka juu kwa mwenyekiti wao JK hadi wakuu wa wilaya na kata hakuna mtu anayeamini ktk madhumuni yale ya chama hivyo tuseme ukweli hatuna chama cha kijamaa leo hii, isipokuwa tuna vibaraka waliokivamia chama hicho. Sisi wengine tulishajitenga mapema sana baada ya kugundua mbwa kaingia msikitini na tukaijua haramu yake. Lakini pia wapo wale ambao hawaoni Uharamu wa mbwa kuingia msikitini kwa sababu ni kiumbe na mnyama anayestahili haki zake pasipo kubaguliwa. Hivyo tulichofanya ni kutafuta msikiti mwingine ibada ya sala mahala popote inakubalika..

Kwa hiyo mimi ningeomba tu Uongozi wa chama hiki, aidha warudi nyuma na kujitazama upya, wachukue madhumuni ya chama hiki kisha wajiulize viongozi wote juu ya imani yao na madhumuni hayo na jinsi gani wako tayari kuyatumikia. Itakuwa mtihani mkubwa sana na pengine tutaweza kupata majibu tofauti kabisa. Chama kimeingiliwa na wahuni ambao hawaamini ktk madhumuni ya chama na hivyo wamekiteka chama cha Wakulima na Wafanyakazi...Kwa kutambua hivyo sii makosa kabisa kuwataja watu hawa kwa majina yao maana ndio sababu kubwa ya madudu haya ya leo..
 
Mkandara nakubaliana na wewe kuhusu viongozi wa CCM kutofuata katiba ya CCM. Na ni lazima tuseme ukweli, kama mahakama zetu zitafuata sheria bila uwoga, basi uongozi wote wa CCM unatakiwa uwe umevuliwa madaraka kwa kukiuka katiba.
Hii inawezekana iwapo tu, wanachama watapeleka malalamiko mahakamani. Najua it sounds kinda funny but it is possible.Kuvunja katiba ni crime, hasa ukifanya on purpose. Nec ilivunja katiba ilipoazimia kule unguja na kuruhusu viongozi kumiliki hisa na nyumba za kupanga. From that, ndipo tulipoanza haya mambo ya ufisadi papa.
Tatizo ni watu.
 
Sina sababu yoyote ya kumbeba Lowassa. Nimbebe nimpeleke wapi na kwa malengo gani? Wanaombeba kama wapo basi they belong kwenye kundi la wapambe na wachochezi ambayo nimeyajadili. Hoja ya msingi hapa ni kwamba Lowassa ni kada mwenzangu ndani ya CCM na kasema jambo ambalo limenigusa, na kama unafuatilia, nimekuwa najikita zaidi kujadili hoja na sio mtoa hoja. Kama yeye hana sifa za kuwa kiongozi na badala yake ni mwanasiasa, hoja hiyo inajadilika na nadhani wengi wataifurahia hoja hiyo ingawa haitatupeleka popote kwani Lowassa sio msaafu wa CCM na muhimu zaidi, hatokuwa CCM milele. Kina Nyerere, Kawawa, Kolimba, Sokoine, na wazee wengine walikuwa CCM, maisha yao yakapita na wamepisha wengine. Lowassa hatokuwa tofauti na hawa. Ndio maana mimi simlengi Lowassa bali hoja yake.

Unafanya kosa la kujadili hoja bila kuangalia mtoa hoja katika hoja husika. Pwengine niende mbali kidogo na kukutaarifu kuwa, tatizo moja ambalo watanzania tumelipuuzia ni suala la maadili (Ethic and moral values) na hata reputations. Kwa bahati nzuri nchi zilizoendelea haya ni maeneo muhimu sana. Huwezi kuniambia kuwa mtumishi wa serikali mla rushwa akikemea rushwa, mimi niangalie tu maada ya kukemea rushwa bila kumuangalia yeye mwenyewe anavyotekeleza hoja hiyo. Hilo ni kosa kubwa.

Kwa maana hiyo binafsi siwezi kabisa kujadili hoja hiyo ya Lowasa bila kumuangalia Lowasa mwenyewe katika nyadhifa zake alivyokuwa anatekeleza hoja hiyo. Lowasa amekuwa na sura tofauti kila aliposhika nyadhifa tofauti.
  • Kwanza muangalie Lowasa kama Waziri wa ardhi
  • Akigombea kuteuliwa (mgombea ccm) urais wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi (wakati wa uhai wa Nyerere)
  • Waziri mkuu wakati wa Kikwete
  • Baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu.

Ukiangalia, hoja zake uzipendazo amezitoa sana katika kipindi hiki cha mwisho. Kabla ya kujadili hoja zake jiulize kwanza kwanini sasa hivi. Hata kama hoja zake ni za msingi, bahati mbaya amechelewa. Na ndio maana kimsingi watoa hoja wengi hawapendi kuhusisha hoja na mtoa hoja kama Lowasa. Kumbuka akina Lowasa wako wengi na hatutawaunga mkono kamwe hata kama hoja zao ni za msingi. Hawawezi kuwa ndume la kuwili na tukawakubali katika jamii. Lowasa habebeki hata kwa skania tani 24

Ushauri wa bure: Ili hoja hii ijadilike itoe wewe mwenyewe kama unavyoamini na ubadili kichwa cha habari. Kumbuka katika uandishi KICHWA CHA HABARI NI MUHIMU SANA.

L
 
...Ufumbuzi upo kwa wale wachache sana -ambao, at least wako sane na sober- waliobaki ku-take charge kusimamia na kupigia debe misingi bora ya utendaji kazi. Wakubali kuwa "wenye akili kwenye kundi la vichaa" bila kujali kama watapoteza favors au mapenzi ya wenzao, hatimae watafanikiwa kuwaonyesha waTanzania mwanga at the end of the tunnel.

Kama unaongelea viongozi, binafsi nadhani wapo kwa ajili ya kutafutia mwanga familia zao, sio kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania njia; sijui tatizo hili tutalitatua vipi hasa ikizingatia kwamba suala la uzalendo miongoni mwa viongozi limebakia kuwa voluntary;
 
kwa hyo mleta mada unachotka kusema ni kwamba lowasa ni kiongozi na si mwanasiasa sio??!!...naona umempalilia kweli

Ni swali zuri sana, nitajaribu kutoa maoni yangu then tutajaribu kutumia vigezo vyangu kumpima Lowassa na wengine.
Uongozi wa kisiasa ni mchakato ambao upo very complex; ni mchakato ambao mtu aliyepo in power (kwenye uongozi – madaraka) ana influence wananchi/anapata followers in the context of accomplishing societal goals. Viongozi wa kisiasa wanahitajika sana katika kuanzisha na kuchochea mchakato wa mabadiliko – kwa mfano mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kikatiba n.k. Katika michakato yote hii ya mabadiliko, uongozi wa kisiasa plays a prominent role.

Viongozi wa kisiasa hujikita katika mchakato wa mabadiliko kwa kutumia leadership attributes walizokuwa nazo – kwa mfano, their political beliefs ambazo ni relevant kwa mahitaji yaliyopo ndani ya jamii, their social values ambazo jamii pia inazihusudu; Ni lazima awe na characters ambazo sehemu kubwa ya jamii approves, na pia awe na wide knowledge na wisdom inayotokana na uzoefu wake katika uongozi na pia inayotokana na hulka yake ya kujifunza. Viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuelewa, Je, Jamii ina hopes na aspirations zipi? Viongozi wa kisiasa wanatakiwa kuwa na uwezo to identify malengo ya jamii, na wanategemewa sana in formulating Dira ya taifa lao na kuwashawishi wananchi wawe na imani na dira husika na wakubali kuifanyia kazi dira hiyo kwa matumaini kwamba, uongozi husika utawatengenezea mazingira yanayotoa opportunity for prosperity and success and an upward social mobility inayoendana na jasho la mtu.

Sifa nyingine za kiuongozi wa kisiasa ni hizi:

· Uwezo wa ku inspire wafuasi, hasa the common people;
· Uvumilivu na perseverance in pursuing malengo ya jamii;
· Maturity na wisdom ya kufanya maamuzi magumu na katika wakati muafaka;
· Strength of character ambayo ina set an example kwa jamii;
· Na mwisho – mental toughness ya kuweza ku face criticism when found wrong;
 
Mchambuzi,
Maneno mazito sana uloyazungumza hapo juu kuhusu viongozi wetu na umenigusa haswaaa. Kumbuka hii ni hoja inayohusu watu zaidi ya msahafu wa chama chenyewe na ndio maana binafsi yangu huwataja WATU hawa ni kina nani maana kuzungumzia hoja ya mtu kulaumu viongozi wakati tunawajua kwa majina, hii ndio huitwa Nidhamu ya woga. Mkuu, Funguka - hatuna sababu ya kuogopa kusema ukweli maana events na idea huletwa na watu na hivyo tuwanukuu wao kwa hoja zao na pia maadam wao ndio wacheza tuna haki ya kuwapima na kujifunza vile vile kwani kauli ya mtu sii mtaji.

Nikirudi ktk Hoja yetu, Tatizo la CCM kama nilivyosema ni WATU sio chama kwa maana chama kimejieleza vizuri sana malengo na madhumuni yake na ni taifa gani chama kinataka kulijenga lakini on the ground tunaiona picha tofauti kabisa na sababu zipo mbele yetu. Kuna mada fulani inamzungumzia Mukama ajiuzuru na kwamba hafai kuiongoza CCM. Lakini wakati huo huo nikasoma bandiko la mtoa mada na kuchambua kama kweli Mukama hafai kuongoza CCM ya hii leo au vinginevyo.. Na nilichogundua ni kwamba CCM yenyewe kama chama haina mapungufu isipokuwa WATU waliojiunga na CCM hiki ndio wale wasiamini madhumuni na malengo ya chama hicho, hawa ndio hawatakiwi kujiunga na chama maana hawaamini yaliyomo hivyo kwa nini wamejiunga na CCM..

Kati ya madhumuni 18 karibu nusu yake hayakubaliwi na viongozi pamoja na wanachama wengi wa chama CCM leo hii, na niliyaorodhesha yote kuonyesha kwamba CCM ni chama cha kijamaa na kwa Wakulima na Wafanyakazi. Na ukitazama toka juu kwa mwenyekiti wao JK hadi wakuu wa wilaya na kata hakuna mtu anayeamini ktk madhumuni yale ya chama hivyo tuseme ukweli hatuna chama cha kijamaa leo hii, isipokuwa tuna vibaraka waliokivamia chama hicho. Sisi wengine tulishajitenga mapema sana baada ya kugundua mbwa kaingia msikitini na tukaijua haramu yake. Lakini pia wapo wale ambao hawaoni Uharamu wa mbwa kuingia msikitini kwa sababu ni kiumbe na mnyama anayestahili haki zake pasipo kubaguliwa. Hivyo tulichofanya ni kutafuta msikiti mwingine ibada ya sala mahala popote inakubalika..

Kwa hiyo mimi ningeomba tu Uongozi wa chama hiki, aidha warudi nyuma na kujitazama upya, wachukue madhumuni ya chama hiki kisha wajiulize viongozi wote juu ya imani yao na madhumuni hayo na jinsi gani wako tayari kuyatumikia. Itakuwa mtihani mkubwa sana na pengine tutaweza kupata majibu tofauti kabisa. Chama kimeingiliwa na wahuni ambao hawaamini ktk madhumuni ya chama na hivyo wamekiteka chama cha Wakulima na Wafanyakazi...Kwa kutambua hivyo sii makosa kabisa kuwataja watu hawa kwa majina yao maana ndio sababu kubwa ya madudu haya ya leo..

Mkuu,

Umeongea maneno ya msingi sana ambayo hata vyama vya upinzani wanaweza kuwa victims wa masuala haya haya wasipokuwa makini. Ndio maana ni muhimu kwa upinzani hasa Chadema kutumia muda wao mwingi kujifunza kutoka kwenye mapungufu ya CCM kuliko kutumia muda wao mwingi kukibeza na kukicheka CCM. Ningependa kusikia mawazo juu ya masuala yafuatayo:

1. Je, unadhani ni CCM peke yake ambayo viongozi wake hawaamini au wanaenda kinyume na madhumuni ya chama?

2. Ni dhahiri kwamba unaposema chama kimetekwa na wahuni na kusahau walengwa wake ambao ni wakulima na wafanyakazi, unaongelea nguvu ya fedha waliyonayo baadhi ya viongozi; Je, kwa chama kama Chadema, suala la nguvu ya fedha lina play out vipi katika party politics? au lipo lakini halionekani sana kwa sasa kwa sababu chama bado kinakua lakini muhimu zaidi mambo haya yanakuwa overshadowed na the fact kwamba in the eyes of umma, Chadema ipo zaidi on offence while CCM ipo zaidi on defence?

3. Katika katiba yake, Chadema inajipambanua kama chama cha wakulima, wafanyakazi na wajasiriamali; suala la wajasiriamali halipo katika katiba ya CCM ingawa kivitendo ujasiriamali ndio lifeblood of the party, especially baada ya kuzaliwa kwa azimio la zanzibar mwaka 1992 ambalo lililizika rasmi azimio la arusha. Je, kuna ushahidi au vigezo gani kuonyesha kwamba tunapozungumza, Chadema hakichezi mbali na madhumuni yake ambayo yanalenga kuwatumikia wakulima, wafanyakazi na wajasiriamali wa nchi hii tofauti na CCM?
 
Nahisi mtoa mada unapoteza nguvu nyingi kumtetea mtu ambaye kashapoteza mvuto kwenye jamii. Kama unaweza andika yote haya; kwanini usimshauri EL maneno machache tu kuwa;-

1. Aombe radhi wa tanzania kwa kukiri alipokosea na kuahidi, kurudisha japo nusu ya alichowadhulumu.

2. Tunaelewa ushiriki wake katika Richmond/Downs a.k.a (kasungura kadogo). Atuambie watanzania wapi ameonewa katika hili? Atuweke wazi kwnini bado anadhani anaonewa na kulalamika kwa mafumbo kuwa hamna hatua aliyoifanya katika Richmond bila kumshirikisha JK.

3. Atuambie mikataba ya ujenzi wa jengo la umoja wa vijana, dawasa na maslahi yake katika haya. Vinginevyo watanzania tunazidi kujiaminisha Mwl Nyerere alikuwa sahihi kummulika, na kumwona hafai kuwa kiongozi zaidi ya mfanya biashara.

Vinginevyo mtoa mada, unapiga rangi upepo.

Kibanga Msese
 
Ingekuwa vyema zaidi kama unge nukuu sehemu ambazo una amini kwamba zinalenga kumpigia debe Lowassa halafu ndio ujenge hoja yako kuliko kuja na tabia ya ku-judge the book by its cover kwani kuna dalili kubwa kwamba haujaisoma hoja yote na badala yake umeishia kwenye kichwa cha habari cha uzi huu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom