Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Edward Lowassa ameibua mjadala muhimu sana kwa taifa letu, hasa ikizingatiwa kwamba taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa rasilimali kazi, hivyo ni muhimu tukafanya maamuzi juu ya wapi tuweke kipaumbele katika mipango ya kujenga na kuendeleza uchumi wetu.
Ni muhimu sana tukafanya hivi kwani miaka nenda miaka rudi tumeshuhudia jinsi gani serikali yetu imekuwa ikitumia matrilioni ya fedha za walipa kodi kuendeleza uchumi, huku matokeo ya matumizi hayo kwa watanzania walio wengi – in terms of ubora wa maisha, kuwa karibia na sifuri. Tatizo lipo wapi? Inawezekana tatizo ni ulege lege wa serikali juu ya nini viwe vipaumbele vya taifa, kwani bajeti za serikali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, vipaumbele vimekuwa vikibadilika kama kinyonga. Hatujawa taifa consistent in terms of prioritizing!!! Mwalimu Nyerere aliwahi tamka kwamba KUPANGA NI KUCHAGUA.
Je, tuweke kipaumbele wapi kama Taifa: Je iwe KILIMO au ELIMU? Ni bahati mbaya sana kwamba kama ilivyo ada, masuala mengi yaliyo muhimu kwa taifa letu huwa tunayajadili kisiasa zaidi, ambapo huwa tunatumia muda na juhudi nyingi sana kujadili WATU badala ya MASUALA (issues). Tabia hii inachangia sana kuzorotesha juhudi za ujenzi wa taifa letu.
Ingawa nia yangu sio kumjadili Lowassa na badala yake hoja iliyopo mbele yetu, ningependa kutumia muda mchache kumpongeza Lowassa kwa kuelezea msimamo wake juu ya vipaumbele vya taifa, hasa katika kipindi hiki ambapo tunaelekea kwenye mchakato kutafuta Rais wa Tano wa Tanzania. Ingawa Lowassa hajaelezea wazi iwapo atagombea, hatua yake ya kujitokeza mbele ya umma kuelezea misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa ni hatua inayostahili kupongezwa na kuigwa na wanasiasa wengine kwani ubora wa mgombea urais 2015 hautapimwa kwa hulka, haiba, mvuto au umashuhuri wa mgombea bali itikadi anayosimamia, hasa juu ya nini anachokiamini. Nina uhakika kwamba Watanzania wengi wangependa kusikia hawa watu wanaotajwa tajwa kwamba watagombea, wanasimamia wapi kuhusu masuala mbalimbali yanayowagusa wananchi. Kwa haraka haraka, mimi nadhani kero za wananchi wengi zipo katika maeneo yafuayato:
Je, wale wote wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM (na hata upinzani), wana simamia upande gani juu ya masuala haya nane? Nadhani wanasiasa wetu wakianza kujitokeza wazi, tutakuwa na nafasi nzuri ya kufahamu nani anaendana na matakwa ya walio wengi. Vinginevyo siasa za kujificha jificha, woga woga, na kutoa mipasho ya hapa na pale doesn't make one a better candidate. Watanzania wamechoka kuchagua viongozi kwa mazoea, haiba, hulka na umashuhuri wa wagombea. Tubadilike na kufanya uchaguzi mkuu wa 2015 uwe uchaguzi wa ‘ISSUES'; not ‘PERSONALITIES'.
Baada ya kusema hayo, sasa niingie moja kwa moja kwenye mada, hasa hili la Kilimo Kwanza, lakini Elimu Kabla.
ELIMU, KILIMO NA MAENDELEO
Kama tulivyokwisha ona, mjadala huu umegubikwa na utata mkubwa (controversies). Lakini hili sio tatizo iwapo wachambuzi, wataalam, watunga sera n.k, wanapambana kwa hoja. Kwa kawaida, mjadala juu ya umuhimu wa Elimu katika Maendeleo ya Uchumi huwa na makundi makubwa mawili ya hoja.
Kundi la Kwanza uamini kwamba Elimu itolewe ‘just for its own sake', lengo la kutoa Elimu likiwa tu njia ya kustawisha Ufahamu au Ujuzi miongoni mwa watu ili kuwapa uwezo wa kuendeleo zaidi towards their full personalities and potentials katika jamii husika. Dhana hii imekuwa ina influence sera nyingi za Elimu katika mataifa yaliyoendelea zaidi kiuchumi.
Kundi la Pili la pili uamini kwamba – nia ya elimu ni kumuandaa mtu aweze ku – perform functions ambazo ni muhimu katika kuleta mabadiliko (transformation) katika mazingira yake. Kwa mtazamo wangu, Lowassa anaegemea zaidi katika imani hii.
Ili kuelewa zaidi tofauti za kihoja zilizopo baina ya makundi haya mawili, ni vizuri kwanza tukakubaliana kwamba kwa kiasi kikubwa, Elimu imegeuzwa kuwa bidhaa (Education as a Good) katika mazingira ya soko huria ambalo linatawaliwa na Liberalization, Marketization na Privatization, huku serikali ikipunguziwa kazi ya uzalishaji wa huduma na bidhaa, na badala yake to play the role of a ‘facilitator'zaidi. Nchini Tanzania kwa mfano, hata pale serikali inapotoa huduma ya Elimu, haiwi bure mia kwa mia. Swali linalofuatia hapa ni, JE:
Elimu ni bidhaa ya namna gani, Bidhaa ya Ki-mjati (Capital Good) au ni bidhaa Ki-matumizi Consumer Good)?
Kwa jinsi navyomwelewa Lowassa, yeye ana amini kwamba Elimu ni bidhaa ya kimtaji zaidi (capital good) kuliko bidhaa ya kimatumizi (consumer good). Nitafafanua kwa kujadili kidogo dhana ya ‘MTAJI'.
Maana ya ‘Mtaji' inazidi kupanuka, na sio kama miaka ya zamani ambapo mtaji ulieleweka katika mazingira ya Fedha, Natural Resources, hasa Ardhi, na Physical Capital (kama majengo na viwanda); Hivi sasa, MTAJI WATU – Human Capital ni muhimu pengine kuliko mitaji mingine yote. Ilichukua muda mrefu sana kwa binadamu kuja kuelewa umuhimu wa mtaji huu, hasa mchango wake katika Maendeleo ya uchumi na kijamii. Mtaji Watu umekuwa ni input muhimu pengine kuliko inputs nyingine zote in the sphere of production, kwani Mtaji Watu sasa ni key determinant ya viwango vya ‘productivity' na ‘efficiency', na pia huwezesha mitaji mingine (kwa mfano Ardhi, Fedha, Viwanda, Migodi n.k) kwa na manufaa katika taifa. Mashuleni tunafundishwa kwamba kuna angalau four factors of production ambazo ni: Land, Labour, Capital and Entrepreneur. Ukitizama kwa makini, 50% ya mazingira haya ya uzalishaji yanategemea Mtaji Watu – yani Quality of Labour & Entrepreneurship. Lakini Mtaji Watu haushuki tokea mbinguni bali ni zao la mfumo wa Elimu katika taifa. Elimu plays the most important role in the creation and improvement of human capital na ina umuhimu mkubwa sana katika kukuza na kuendeleza uchumi, sekta ya kilimo ikiwa ni moja ya maeneo muhimu katika hilo.
Nadhani mpaka hapa tumepata mwanga japo kidogo juu ya umuhimu wa Elimu katika Maendeleo ya uchumi. Kinachofuatia ni kujaribu kubaini, Je, Katika Sera ya Kilimo kwanza, Elimu ina umuhimu katika hatua ipi, hatua ya awali? Hatua ya baadae? Au uwekezaji katika Elimu na Kilimo uende sambamba?
Ntachofanya ni kuchokoza tu mada, sina majibu ya moja kwa moja.
Iwapo Kilimo Kwanza kama sera, lengo lake kuu ni kuleta mapinduzi ya kilimo (Agricultural Transformation/Revolution), itakuwa ni vizuri tukatizama, Je, Kilimo Kwanza kinalenga kufanikisha nini hasa? Kwa mtazamo wangu, tutakuwa tumefanikiwa katika agricultural transformation iwapo na Sera ya Kilimo Kwanza itapalekea matokeo yafuatayo:
Kwanza – Pato la households vijijini likivuka viwango vya sasa vya umaskini – yani, income ya wakulima iongezeke na kuzidi poverty levels katika taifa.
Pili – uwepo wa specialization katika uzalishaji vijijini/mashambani – yani wakulima waweze kubobea katika shughuli yao – kwa maana nyingine, Kilimo kigeuke kuwa Taaluma.
Tatu – Wakulima wakifikia hatua ya kuendesha kilimo chao/mashamba kibiashara zaidi, huku wakiuza sehemu kubwa ya mazao yao katika soko na sio for private consumption (subsistence….
Nne – Wakulima wakifikia hatua ya kuwa na uwezo wa kuwekeza ‘heavily' kwenye mashamba yao, hasa kutokana na ongezeko la kipato katika shughuli yao ya kilimo.
Tano – Wakulima wakifikia uwezo wa kununua commercial inputs kwa wingi – , hasa uwezo wa kununua/kuajiri NGUVU KAZI (Labour) kwa wingi.
Mwisho – Wakulima wakifikia uwezo wa ku ‘adopt' into new technologies on a regular basis – yani, kila tekinolojia mpya inapopatikana sokoni, wakulima hawa wasiachwe nyuma, bali wawe: Kwanza, na ufahamu juu ya Maendeleo ya tekinolojia mbalimbali zinazohusu kilimo bora, Pili, wawe na uwezo (hasa skills) za kutumia tekinolojia husika, na muhimu pia – uwezo wa kununua tekinolojia hiyo/hizo.
Tukifanikisha haya, ina maana kwamba sekta yetu ya Kilimo itaweza:
Iwapo tunakubaliana na haya, sasa ili tufike huko, Je:
Tukishabaini hilo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujua ni wapi tuweke vipaumbele vyetu.
Tujadili hoja, Tusimjadili mtoa hoja.

- Muundo wa muungano.
- Utawala kwa mujibu wa sheria (Katiba).
- Ufisadi/uadilifu.
- Ajira.
- Afya.
- Maendeleo ya Kilimo.
- Elimu.
- Rasilimali za Taifa.

- To experience steady growth.
- Kilimo kitaboreshwa na kuwa cha kisasa zaidi.
- Ongezeko la pato la taifa kutokana na increase in productivity sekta ya kilimo hivyowa na fedha za kuendeleza sekta nyingine muhimu za uchumi, hasa sekta ya Viwanda.
- Kilimo kikigeuka kuwa cha kisasa, productivity ikiongezeka, na pato la wakulima likiongezeka, ina maana mishahara ya waajiriwa kwenye sekta ya kilimo pia itakuwa mizuri, ya kuvutia na ya uhakika, angalau kulingana na mishahara ya sekta nje ya kilimo, au pengine kupita mishahara inayolipwa kwenye sekta zilizo nje ya kilimo; hali hii italeta mwamko zaidi kwa watanzania wengi kuendelea kujenga taifa kupitia kilimo, huku pia wakifaidika na kipato kizuri.
- Ongezeko la pato la taifa kutokana na increase in productivity ya itasaidia Serikali kupata fedha zaidi za kuendeleza sekta nyingine za uchumi, hasa Viwanda, na taratibu, labour force (nguvu kazi) itakuwa released from sekta ya Kilimo na kuhamia kwenye sekta nyingine za uchumi (kwa mfano viwanda), hivyo kusaidia taifa kuondokana na tatizo la sasa ambapo Kilimo ndio main employer wa watanzania walio wengi, lakini sekta hiyo ina hali duni, isiyo na tija kubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.
Iwapo tunakubaliana na haya, sasa ili tufike huko, Je:
- ELIMU IWE KABLA YA KITU GANI?
- KILIMO KIWE KWANZA YA KITU GANI?