Lowassa na Kilimo Kwanza: Wengi Hatujamwelewa

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Edward Lowassa ameibua mjadala muhimu sana kwa taifa letu, hasa ikizingatiwa kwamba taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa rasilimali kazi, hivyo ni muhimu tukafanya maamuzi juu ya wapi tuweke kipaumbele katika mipango ya kujenga na kuendeleza uchumi wetu.

Ni muhimu sana tukafanya hivi kwani miaka nenda miaka rudi tumeshuhudia jinsi gani serikali yetu imekuwa ikitumia matrilioni ya fedha za walipa kodi kuendeleza uchumi, huku matokeo ya matumizi hayo kwa watanzania walio wengi – in terms of ubora wa maisha, kuwa karibia na sifuri. Tatizo lipo wapi? Inawezekana tatizo ni ulege lege wa serikali juu ya nini viwe vipaumbele vya taifa, kwani bajeti za serikali katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, vipaumbele vimekuwa vikibadilika kama kinyonga. Hatujawa taifa consistent in terms of prioritizing!!! Mwalimu Nyerere aliwahi tamka kwamba KUPANGA NI KUCHAGUA.

Je, tuweke kipaumbele wapi kama Taifa: Je iwe KILIMO au ELIMU? Ni bahati mbaya sana kwamba kama ilivyo ada, masuala mengi yaliyo muhimu kwa taifa letu huwa tunayajadili kisiasa zaidi, ambapo huwa tunatumia muda na juhudi nyingi sana kujadili WATU badala ya MASUALA (issues). Tabia hii inachangia sana kuzorotesha juhudi za ujenzi wa taifa letu.

Ingawa nia yangu sio kumjadili Lowassa na badala yake hoja iliyopo mbele yetu, ningependa kutumia muda mchache kumpongeza Lowassa kwa kuelezea msimamo wake juu ya vipaumbele vya taifa, hasa katika kipindi hiki ambapo tunaelekea kwenye mchakato kutafuta Rais wa Tano wa Tanzania. Ingawa Lowassa hajaelezea wazi iwapo atagombea, hatua yake ya kujitokeza mbele ya umma kuelezea misimamo yake kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa ni hatua inayostahili kupongezwa na kuigwa na wanasiasa wengine kwani ubora wa mgombea urais 2015 hautapimwa kwa hulka, haiba, mvuto au umashuhuri wa mgombea bali itikadi anayosimamia, hasa juu ya nini anachokiamini. Nina uhakika kwamba Watanzania wengi wangependa kusikia hawa watu wanaotajwa tajwa kwamba watagombea, wanasimamia wapi kuhusu masuala mbalimbali yanayowagusa wananchi. Kwa haraka haraka, mimi nadhani kero za wananchi wengi zipo katika maeneo yafuayato:


  • Muundo wa muungano.
  • Utawala kwa mujibu wa sheria (Katiba).
  • Ufisadi/uadilifu.
  • Ajira.
  • Afya.
  • Maendeleo ya Kilimo.
  • Elimu.
  • Rasilimali za Taifa.

Je, wale wote wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM (na hata upinzani), wana simamia upande gani juu ya masuala haya nane? Nadhani wanasiasa wetu wakianza kujitokeza wazi, tutakuwa na nafasi nzuri ya kufahamu nani anaendana na matakwa ya walio wengi. Vinginevyo siasa za kujificha jificha, woga woga, na kutoa mipasho ya hapa na pale doesn't make one a better candidate. Watanzania wamechoka kuchagua viongozi kwa mazoea, haiba, hulka na umashuhuri wa wagombea. Tubadilike na kufanya uchaguzi mkuu wa 2015 uwe uchaguzi wa ‘ISSUES'; not ‘PERSONALITIES'.

Baada ya kusema hayo, sasa niingie moja kwa moja kwenye mada, hasa hili la Kilimo Kwanza, lakini Elimu Kabla.

ELIMU, KILIMO NA MAENDELEO

Kama tulivyokwisha ona, mjadala huu umegubikwa na utata mkubwa (controversies). Lakini hili sio tatizo iwapo wachambuzi, wataalam, watunga sera n.k, wanapambana kwa hoja. Kwa kawaida, mjadala juu ya umuhimu wa Elimu katika Maendeleo ya Uchumi huwa na makundi makubwa mawili ya hoja.

Kundi la Kwanza uamini kwamba Elimu itolewe ‘just for its own sake', lengo la kutoa Elimu likiwa tu njia ya kustawisha Ufahamu au Ujuzi miongoni mwa watu ili kuwapa uwezo wa kuendeleo zaidi towards their full personalities and potentials katika jamii husika. Dhana hii imekuwa ina influence sera nyingi za Elimu katika mataifa yaliyoendelea zaidi kiuchumi.

Kundi la Pili la pili uamini kwamba – nia ya elimu ni kumuandaa mtu aweze ku – perform functions ambazo ni muhimu katika kuleta mabadiliko (transformation) katika mazingira yake. Kwa mtazamo wangu, Lowassa anaegemea zaidi katika imani hii.

Ili kuelewa zaidi tofauti za kihoja zilizopo baina ya makundi haya mawili, ni vizuri kwanza tukakubaliana kwamba kwa kiasi kikubwa, Elimu imegeuzwa kuwa bidhaa (Education as a Good) katika mazingira ya soko huria ambalo linatawaliwa na Liberalization, Marketization na Privatization, huku serikali ikipunguziwa kazi ya uzalishaji wa huduma na bidhaa, na badala yake to play the role of a ‘facilitator'zaidi. Nchini Tanzania kwa mfano, hata pale serikali inapotoa huduma ya Elimu, haiwi bure mia kwa mia. Swali linalofuatia hapa ni, JE:

Elimu ni bidhaa ya namna gani, Bidhaa ya Ki-mjati (Capital Good) au ni bidhaa Ki-matumizi Consumer Good)?

Kwa jinsi navyomwelewa Lowassa, yeye ana amini kwamba Elimu ni bidhaa ya kimtaji zaidi (capital good) kuliko bidhaa ya kimatumizi (consumer good). Nitafafanua kwa kujadili kidogo dhana ya ‘MTAJI'.

Maana ya ‘Mtaji' inazidi kupanuka, na sio kama miaka ya zamani ambapo mtaji ulieleweka katika mazingira ya Fedha, Natural Resources, hasa Ardhi, na Physical Capital (kama majengo na viwanda); Hivi sasa, MTAJI WATU – Human Capital ni muhimu pengine kuliko mitaji mingine yote. Ilichukua muda mrefu sana kwa binadamu kuja kuelewa umuhimu wa mtaji huu, hasa mchango wake katika Maendeleo ya uchumi na kijamii. Mtaji Watu umekuwa ni input muhimu pengine kuliko inputs nyingine zote in the sphere of production, kwani Mtaji Watu sasa ni key determinant ya viwango vya ‘productivity' na ‘efficiency', na pia huwezesha mitaji mingine (kwa mfano Ardhi, Fedha, Viwanda, Migodi n.k) kwa na manufaa katika taifa. Mashuleni tunafundishwa kwamba kuna angalau four factors of production ambazo ni: Land, Labour, Capital and Entrepreneur. Ukitizama kwa makini, 50% ya mazingira haya ya uzalishaji yanategemea Mtaji Watu – yani Quality of Labour & Entrepreneurship. Lakini Mtaji Watu haushuki tokea mbinguni bali ni zao la mfumo wa Elimu katika taifa. Elimu plays the most important role in the creation and improvement of human capital na ina umuhimu mkubwa sana katika kukuza na kuendeleza uchumi, sekta ya kilimo ikiwa ni moja ya maeneo muhimu katika hilo.

Nadhani mpaka hapa tumepata mwanga japo kidogo juu ya umuhimu wa Elimu katika Maendeleo ya uchumi. Kinachofuatia ni kujaribu kubaini, Je, Katika Sera ya Kilimo kwanza, Elimu ina umuhimu katika hatua ipi, hatua ya awali? Hatua ya baadae? Au uwekezaji katika Elimu na Kilimo uende sambamba?

Ntachofanya ni kuchokoza tu mada, sina majibu ya moja kwa moja.

Iwapo Kilimo Kwanza kama sera, lengo lake kuu ni kuleta mapinduzi ya kilimo (Agricultural Transformation/Revolution), itakuwa ni vizuri tukatizama, Je, Kilimo Kwanza kinalenga kufanikisha nini hasa? Kwa mtazamo wangu, tutakuwa tumefanikiwa katika agricultural transformation iwapo na Sera ya Kilimo Kwanza itapalekea matokeo yafuatayo:

Kwanza – Pato la households vijijini likivuka viwango vya sasa vya umaskini – yani, income ya wakulima iongezeke na kuzidi poverty levels katika taifa.

Pili – uwepo wa specialization katika uzalishaji vijijini/mashambani – yani wakulima waweze kubobea katika shughuli yao – kwa maana nyingine, Kilimo kigeuke kuwa Taaluma.

Tatu – Wakulima wakifikia hatua ya kuendesha kilimo chao/mashamba kibiashara zaidi, huku wakiuza sehemu kubwa ya mazao yao katika soko na sio for private consumption (subsistence…).

Nne – Wakulima wakifikia hatua ya kuwa na uwezo wa kuwekeza ‘heavily' kwenye mashamba yao, hasa kutokana na ongezeko la kipato katika shughuli yao ya kilimo.

Tano – Wakulima wakifikia uwezo wa kununua commercial inputs kwa wingi – , hasa uwezo wa kununua/kuajiri NGUVU KAZI (Labour) kwa wingi.

Mwisho – Wakulima wakifikia uwezo wa ku ‘adopt' into new technologies on a regular basis – yani, kila tekinolojia mpya inapopatikana sokoni, wakulima hawa wasiachwe nyuma, bali wawe: Kwanza, na ufahamu juu ya Maendeleo ya tekinolojia mbalimbali zinazohusu kilimo bora, Pili, wawe na uwezo (hasa skills) za kutumia tekinolojia husika, na muhimu pia – uwezo wa kununua tekinolojia hiyo/hizo.

Tukifanikisha haya, ina maana kwamba sekta yetu ya Kilimo itaweza:

  • To experience steady growth.
  • Kilimo kitaboreshwa na kuwa cha kisasa zaidi.
  • Ongezeko la pato la taifa kutokana na increase in productivity sekta ya kilimo hivyowa na fedha za kuendeleza sekta nyingine muhimu za uchumi, hasa sekta ya Viwanda.
  • Kilimo kikigeuka kuwa cha kisasa, productivity ikiongezeka, na pato la wakulima likiongezeka, ina maana mishahara ya waajiriwa kwenye sekta ya kilimo pia itakuwa mizuri, ya kuvutia na ya uhakika, angalau kulingana na mishahara ya sekta nje ya kilimo, au pengine kupita mishahara inayolipwa kwenye sekta zilizo nje ya kilimo; hali hii italeta mwamko zaidi kwa watanzania wengi kuendelea kujenga taifa kupitia kilimo, huku pia wakifaidika na kipato kizuri.
  • Ongezeko la pato la taifa kutokana na increase in productivity ya itasaidia Serikali kupata fedha zaidi za kuendeleza sekta nyingine za uchumi, hasa Viwanda, na taratibu, labour force (nguvu kazi) itakuwa released from sekta ya Kilimo na kuhamia kwenye sekta nyingine za uchumi (kwa mfano viwanda), hivyo kusaidia taifa kuondokana na tatizo la sasa ambapo Kilimo ndio main employer wa watanzania walio wengi, lakini sekta hiyo ina hali duni, isiyo na tija kubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Iwapo tunakubaliana na haya, sasa ili tufike huko, Je:


  • ELIMU IWE KABLA YA KITU GANI?
  • KILIMO KIWE KWANZA YA KITU GANI?

Tukishabaini hilo, tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kujua ni wapi tuweke vipaumbele vyetu.

Tujadili hoja, Tusimjadili mtoa hoja.
 
Kimsingi Eddo kajaribu kuleta changamoto mpya ktk siasa ya bongo iliyojazwa na wanasiasa uchwara wasiojua wanasimamia nini, wengi wao ni vimbelembele na wasubiria fadhila toka kwa raisi wao dhaifu
Wengi hawana mapya zaidi wanasubiria jamaa wa kariakoo wawaandalie vya kusema
bravo eddo
 
Mchambuzi Ukijaribu kuangalia dhana ya kilimo kwanza haimnufaushi mkulima mdogo (nikiwa na maana ya mkulima aw jembe la mkono). Ni mpango uliondaliwa na watu wachache kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe (land grabbing).

Mkulima huyu hajaandaliwa vyema kwa maana ya elimu. Hajui kusoma majira ya mwaka (weather forecast) ajue ni wakati gani wa kutayarisha shamba na ni wakati gani wa kupanda. Elimu ipewe kipaumbele zaidi. Wakulima wafundishwe kuendana na mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa technologia katika kilimo. Hapo ndipo tutakapoweza kuleta mapinduzi katika kilimo.
 
Kimsingi Eddo kajaribu kuleta changamoto mpya ktk siasa ya bongo iliyojazwa na wanasiasa uchwara wasiojua wanasimamia nini, wengi wao ni vimbelembele na wasubiria fadhila toka kwa raisi wao dhaifu
Wengi hawana mapya zaidi wanasubiria jamaa wa kariakoo wawaandalie vya kusema
bravo eddo

Mkuu, haya sisi wananchi tuliochoka kudhulumiwa na hili li-serikali la kifisadi la ccm tunayajua, na ndio maana tunajipanga kuwaondoa hawa mafisadi/majambazi madarakani japo kabla ya 2015, ila tukichelewa sana basi hata hiyo 2015 sio mbaya. cha kujiuliza hapa, ni je huyu EL ndo anataka kutudanganya nini sasa hivi?? si ndo kikundi chake waliotuhujumu mpaka hapa tulipofika?? sasa yeye ana jipya gani na kalitoa wapi?? tusidanganyane bhana. huyu EL si ndio aliamua kukiuka kiapo alichoapa kuilinda katiba akaamua kutusaliti watanzania kwa kumlinda (RICHMOND) swahiba wake DHAIFU JAKAYA KIWETE?? this white headed man has nothing new, just a mere hippocrete.



Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, ili waelimike waling'oe madarakani hili li-serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
 
Binafsi naamini kilimo kwanza ni kauli mbiu ya kisiasa zaidi. Sio kweli kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu. Ukiangalia mchango wake kwa pato la taifa utakubaliana na mimi.

Mhe. Lowasa pia alikuwa juu juu kwa msimamo wake wa elimu kwanza, akitakiw kufafanua zaidi.....kwakuwa mpango wake wa shue za kata ulifeli....au angetuambia zaidi hio elimu itolewe vipi darasani kwa nadharia au shambani kwa vitendo....naamini pia naye ametumika kisiasa...
 
Namuunga mkono Lowassa mara mia.

Kilimo kwanza wakati elimu mbofumbofu kinasaidia nini? Ndo maana hata umuhimu wa kutumia mbolea na madawa hatuuoni matokeo yake tunavuna mavuno kidogo, kama hatujala au kuuza yote kabla hata hatujayavuna.....tunahitaji elimu itiliwe mkazo kwanza kabla ya haya matrekta ya pinda....akili ni kitu cha muhimu sana katika maendeleo.....

Kilimo kwanza cha kilimbukeni wakati hata mabwanashamba hatuna, wala mabwana mifugo? kazi trekta ni kuchimbua tu udogo halafu utunzaji wa mimea au mifugo unakuwa mbofu matokeo yake hata ile hela ya trekta unashindwa kurudisha kwasababu unavuna mabua.......

Lowassa anahitajika kuwa Rais wa nchi hii....
 
Mie mtazamo wangu upo zaidi katika utekelezaji wa hayo mambo ambayo huchukuliwa kuwa ni msingi... Naamini kuwa wote EL na MP wana Great ideas, ambazo once written on paper kwa mtindo wa nini kifanyike, nini kinatakiwa kufanikisha, nini kiwekwe kama tahadhari ili kuweza fanikisha bila kukwama na jinsi gani kuvuna matunda ya hiyo mipango na mikakati.

Kikianza Kilimo Kwanza kwa moyo safi na uzalendo kwa maana chini ya Kiongozi ambae anajua ni viongozi gani atumie (on the basis ya uwajibikaji na devotion katika kazi yao) ina maana hiyo mikakati itahusisha kutoa Elimu ya Ukulima bora kwa Wakulima, itahusisha kuweka wepesi katika shughuli nzima ya kilimo (kama kwa kuhakikisha vifaa kama tractors, mbolea, na yale yote yahusuyo) yanakuwa available bila vikwazo vovote vile; itahusisha pia kukuza technology kwa level ambayo tunaweza mudu na zaga zaga zote zihusuzo kuhakikisha Kilimo kinaendelea...

Vivo hivo ikianza Elimu. Likisimamiwa swala la Elimu inahitaji sio tu kutambua kuwa Elimu ni muhimu... Nadhani hio serkali tayari inatambua na ndio mana kuna shule nyingi za kata zimeanzishwa. However Kupata kiongozi ambaye ni devoted na mzalendo ambaye kweli inamuuma kuwa Elimu yetu ni mauza uza LAZIMA ataweka mikakati ya kuahakikisha elimu inakuwa na kuimarika. Akihakikisha kuwa elimu isilenge tu kwa mtu kuhitimu na kuota kuhusu kuajiriwa, bali pia kumjenga mtu katika kuweza kujisimamia whether kaajiliwa ama kajiajiri. Huyo kiongozi atahakikisha swala zima linalohusiana na kuboresha Elimu toka walimu, maabara, vitabu na accessibility ya elimu ya juu inakuzwa na kuboreshwa.

Mchambuzi nikirudi kwenye mada.. Samahani kama nakuwa kama natoka nje... Mie naona haijalishi nini hapo inaanza AMA nini hapo ni muhimu. Kinachojalisha sio tu viongozi kutambua na kuongea yalo ya msingi katika jamii, kinachojalisha ni wao jinsi ya kuwajibika na wanavotenda. NAAMINI kabisa kuwa kwa sasa tulipo Wantanzania hali ya Elimu na Kilimo pia, kama moja wapo ya hayo yangeshikiliwa na kufanyiwa kazi VILIVO na viongozi wetu kutakuwa na unafuu saana... In what way? Naamini watambua jinsi gani sector katika jamii zipo interrelated... Kufanikiwa kwa Elimu/Kilimo kwa asilimia tu zaidi ya 75 itakuwa moja ya achievement kubwa sana wka taifa kwa maeneo mengi sana.
 
Well Said Mr Mchambuzi. KURA yangu utaipata 2015.
Shout to them days when we used to kick it @ Safari Club on Bissonett near 59 HWY.
pamoja.
 
Obi

Kwahiyo Sera ya Elimu Kabla ni sahihi kuliko Kilimo Kwanza, right?
 
Last edited by a moderator:
Kitu ambacho nimependa ni Lowassa kuwa amekuwa muwazi, hajamumunya maneno anasema wazi wazi msimamo wake. Hakuna mwanasiasa ndani ya ccm anaweza kufanya haya, hata waliostaafu, wengi ni waoga na ndio maana wanashindwa kuisimamia serekali.

Tukirudi kwenye hali halisi, ukweli ni kuwa kilimo kwanza ni janga, hakukuwa na maandalizi ya kutosha, matokeo yake yameleta uporaji wa ardhi vijijini na kuongeza deni la taifa, kilimo kimeshawahi kupewa kipaumbele huko nyuma tukavurunda, kwa sababu hiyo hiyo ya kukurupuka, tunahitaji kuwaandaa watu wetu kimtanzamo kwanza, kwa utaalamu kabla ya kuwapa jembe.

Matokeo ya sera ya kilimo kwanza yatakuja kuwa haya.
1.Baada ya muda raslimali ya ardhi itakuwa mikonono mwa wachache wenye fedha.
2.Deni la taifa litaongezeka kwani wengi watashindwa kulipa zana walizokopa.
3.Njaa itarudi tena, kwani wenye ardhi wataamua walime nini na wauze kwa bei gani na kwa kuwa tutakuwa tumewaondoa wakulima wadogo.
4.Migogoro ya ardhi itaongezeka na kusababisha hata vita.
 
mambomengi

Ni kweli, mchango wa kilimo katika uchumi umepungua, kwahiyo dhana kwamba Kilimo ni uti wa mgongo imepungua uzito, lakini kusema hivyo ni tofauti na kusema kwamba umuhimu wa sekta ya kilimo umepungua, umuhimu upo pale pale kama sio kuongezeka.

Kilimo ni muhimu sana for food security, mapinduzi ya viwanda, lakini muhimu zaidi, bado ni mainstay when it comes to nguvu kazi, na ni muhimu kufanikisha mapinduzi ya kijani/kilimo ili tuweze ku - diversify uchumi wetu ili nguvu kazi katika sekta ya kilimo iwe more productive, lakini pia ianze kuhamia sekta nyingine.

Yote haya i.e. mapinduzi ya Kilimo yatafanikiwa iwapo tutafanya kilimo kuwa important sasahivi, sio baadae. Suala la elimu linaweza kuwa a complimentary good in the process...
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo Sera ya Elimu Kabla ni sahihi kuliko Kilimo Kwanza, right?

Kweli kabisa elimu kwanza, kungekuwa na elimu watu wasingekubali kurubuniwa vijijini kutoa ardhi yao kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo kwanza wa kitu wasichokijuwa.

Hata hao wanasiasa watetezi kilimo kwanza wangekuwa na uelewa sahihi wangeona athari ya hii sera, na wasinge kubali kuisimamia.

Lowassa kwa hili yuko sahihi, na ni vizuri kasiamama na kusema hadharani, nani anaweza kusema hili ndani ya ccm?,
 
Suala la elimu linaweza kuwa a complimentary good in the process...

Elimu sio complimentary ni necessity, ukiangalia kilimo kwanza ni extension ya ukulima mdogo wa kimazoea, hii sera itashindwa na ikifail mwisho watu watabaki na amashamba, embu tujiulize tukishalima tutauza wapi? Tutahifadhi wapi? Tuta-process wapi? Chain ya movement ya mazao ya kilimo ni kubwa kiasi gani kusoport uzalishaji mkubwa?

Haya yote yanahitaji maandalizi, sio kukurupuka, Kama kawaida Viongozi wetu wanaongoza nchi kwa matukio bila mipango, yaani njaa ikitokea wanaanza kilimo kwanza, zikitokea ajali ndio wanakuja na mikakati ya kupunguza ajali, watu wameongezeka ndio wanaongeza shule kila kata, kwanini hakuna mipango endelevu toka awalli, kukurupuka tu kwa kila kitu, hatuwezi kuendelea ka kukurupuka ni lazima tujipange.
 
AshaDii

Je una amini katika dhana ya kupanga ni kuchagua? Naelewa msingi wa hoja yako, na tumefkia hatua ambayo tunahitaji a 'balancing act' kwani pamoja na ukweli kwamba sekta ya kilimo bado ndio mwajiri mkubwa wa taifa letu, lakini ajira katika non-farming sector nayo inazidi kukua ingawa haya sio matokeo ya sera za makusudi za serikali kukuza ajira, bali ni ujanja ujanja tu wa wananchi kukabiliana na nguvu za Privatization, Liberalization na Marketization.

Mbaya zaidi ni kwamba, tofauti na how wenzetu experienced na maendeleo ya sekta ya kilimo (mapinduzi ya kijani), sisi hizi non-farming activities hazina linkage ya maana na sekta ya kilimo. Sasa implication yake kisera ni nini? Je, tuongeze uhudi kwenye Elimu kuongeza poductivity ya watanzania ili waweze kujiendeleza kwenye non - farming activities? Na je, tunapoongelea Elimu katika mazingira ya kilimo, tunaongelea elimu ya jumla ambayo inaweza tumika sekta yoyote au specifically for kilimo?

I remain convinced kwamba Tanzanai tuna utafiti wa kutosha wa kilimo, tena mwingi tu unaozalishwa na vyuo na taasisi zetu za kilimo zilizopo. Kwa mfano Koffi Annan na pia Rais wa EU walikuja mapema mwaka huu kutembelea research centre yetu ya Kilimo kule Mbeya n.k na kujionea mengi. So tatizo sio ukosefu wa utafiti kuhusu Kilimo bora, bali linkage baina ya utafiti uliopo na shughuli au hali halisi huko mashambani.
 
Last edited by a moderator:
babuwaloliondo

One could argue kwamba Elimu kwenye Kilimo ni complimentary input/ au tuseme ‘education is a necessary compliment' to agriculture. By complimentary good ni kama mfano Kiatu na Soksi au Chai na Sukari. Vyote hivi vinazaliwa katika mazingira tofauti lakini kwa nia ya kwenda ku – complement each other, na hiyo ndio ilikuwa maana yangu kwamba Elimu ni complimentary good, lakini sina maana kwamba Elimu sio necessity in this context. Katika amzingira ya kilimo, Complimentary inputs/goods/services kwa mtazamo wangu zipo angalau nne:

-Utafiti kuendeleza au boresha production possibilities;
-Extension – educational programs;
-Facilities za ku-supply inputs zitokanazo na tafiti mbalimbali, hasa mbegu na mbolea;
-Na taasisi to service agricultural production, hasa zile zinazo jihusisha na masuala ya credit, masoko, miundo mbinu n.k.

na kwa bahati mbaya, yote haya yapo nje ya sekta ya Kilimo, so ili individual farmers waweze kuwa more productive, serikali itahitajika kuingilia kati, SIO SOKO.
 
Last edited by a moderator:
Kitu ambacho nimependa ni Lowassa kuwa amekuwa muwazi, hajamumunya maneno anasema wazi wazi msimamo wake. Hakuna mwanasiasa ndani ya ccm anaweza kufanya haya, hata waliostaafu, wengi ni waoga na ndio maana wanashindwa kuisimamia serekali.
Tukirudi kwenye hali halisi, ukweli ni kuwa kilimo kwanza ni janga, hakukuwa na maandalizi ya kutosha, matokeo yake yameleta uporaji wa ardhi vijijini na kuongeza deni la taifa, kilimo kimeshawahi kupewa kipaumbele huko nyuma tukavurunda, kwa sababu hiyo hiyo ya kukurupuka, tunahitaji kuwaandaa watu wetu kimtanzamo kwanza, kwa utaalamu kabla ya kuwapa jembe.

Matokeo ya sera ya kilimo kwanza yatakuja kuwa haya.
1.Baada ya muda raslimali ya ardhi itakuwa mikonono mwa wachache wenye fedha.
2.Deni la taifa litaongezeka kwani wengi watashindwa kulipa zana walizokopa.
3.Njaa itarudi tena, kwani wenye ardhi wataamua walime nini na wauze kwa bei gani na kwa kuwa tutakuwa tumewaondoa wakulima wadogo.
4.Migogoro ya ardhi itaongezeka na kusababisha hata vita.

Nakubaliana na wewe katika mengi ya haya; Kwa mtazamo wangu, ili kilimo kwanza kifanikiwe, hatua ya kwanza na muhimu kuliko zote ni lazima iwe hatua ya maandalizi ambayo umeielezea; nadhani hatua hii tumeshaikosa. Ilitakiwa katika hatua ya maandalizi, serikali ije na sera zinazolenga development of agricultural pre-conditions i.e. kutayarisha mazingira yatakayopelekea sekta ya kilimo ‘to take off'. Katika hatua hii ya maandalizi, baadhi ya masuala muhimu ni pamoja na:

*Improvement of our land tenure system – tuna tatizo kubwa sana katika hili Tanzania. Uwepo wa unfavorable land tenure system kutakwamisha incentives for change miongoni mwa wakulima, hata kama asilimia kubwa ya wakulima watakuwa na elimu ya chuo kikuu.

*Ujenzi wa rural (positive) attitudes towards change – na hii ipo influenced na mambo mengi, kwa mfano awareness juu ya uwezekano wa technological improvements, uwepo wa masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo, miundo mbinu n.k. Mengi ya haya bado hatuna Tanzania na tutakuwa tunafanya makosa makubwa to assume kwamba all these pre conditions prevail, na matokeo yake ni kupoteza time and resources kwenye sekta ambayo haijafanyiwa maandalizi yaku ‘take off.'

Hali halisi iliyopo ni kinyume kabisa kwani:

Kwanza Land Tenure System yetu ni ya ovyo, licha ya tume ya ardhi ya Prof. Shivji kufanya kazi nzuri sana enzi za Mkapa na kutoa mapendekezo yake kwa serikali ambayo hayakufanyiwa kazi.

Pili, watanzania hawana mwamko tena na sekta ya kilimo in terms of kutafuta ajira; hili ni suala la attitudes nililojadili kidogo hapo juu; takwimu zinaonyesha kwamba majority of graduates wa darasa la saba na form four hawataki kuajiriwa kwenye kilimo bali non farming sectors; Sasa sijui hapa suala la Elimu Kabla litakuwa na mafanikio gani katika kuendeleza kilimo, hasa given udhaifu wetu katika masuala hayo hapo juu - yani poor land tenure system na negative attitude ya nguvu kazi (vijana) towards kilimo.
 
Mapungufu mengine ya kilimo kwanza ni kutokuwa na uhusiano na sekta ya mifugo, tunajuwa wafugaji wetu wanafuga kimazoea sana, wanaangalia idadi ya mifugo na kuhama hama, sasa ikiwa kilimo kwanza kinaenda katika kupora ardhi yote iliyowazi kwa ajili ya kilimo cha mazao, Je madhara ya migogoro ya wafugaji na wakulima si itaongezeka.

Kama kilimo kwanza kingeusisha na seka ya mifugo pia, kungeleta unafuu sana wa maisha kwa wafugaji! lakini kama kawaida ikishazuka migoro ndio watakuja na sera ya kilimo na mifugo.
 
Ndugu yangu Mchambuzi nashukuru kwa mada hii maridhawa.

Sikubaliani kimsingi na pendekezo la Lowassa ambalo ukiliangalia limekaa kwa maana ya "Elimu Kwanza, Kilimo Baadaye". Hivi ndivyo nilivyomwelewa hivi juzi na ndivyo nilivyomwelewa miezi kadhaa nyuma alipotoa hili pendekezo mara ya kwanza. Yeye anaamini - kwa kadiri alivyojenga hoja inaonekana- elimu imetangulia kilimo. Hivyo, wakati wenzie wanakuja na "kilimo kwanza" yeye anaona si sahihi bali ni bora kwanza iwe "kilimo kwanza". Hapa ndio mlio wa "kilimo baadaye" unapokuja. Naamini ni ulaghai wa hoja (fallacy).

Umegusia kidogo nadharia ile ya Mwalimu aliyoiandika kwa kirefu kuwa "Kupanga ni kuchagua". Ukiangalia Mwalimu alikuwa anaangalia hili kwa msingi wa kuelewa kuwa jamii(nchi) ina raslimali zinazokoma (limited resources). Hivyo, mahali popote penye limited resources mtu au jamii haiwezi kufanya kila kitu inachotaka. Hivyo, kwa Taifa letu tangu Uhuru kuna baadhi ya maamuzi ambayo yalifanyika at the expense of others. Kwa mfano watu wengi huwa wanapomlaumu Nyerere utawasikia wanasema "hatukuwa na TV, hatukuwa na magazeti huru" n.k Lakini wengi wasiojua historia hawajui kuwa wakati Nyerere anachukua nchi kazi kubwa ya kwanza ilikuwa ni kupanga matumizi ya raslimali. Je tusomeshe watoto wote shule za msingi wakati hakuna shule za kutosha za sekondari na vyuo ni vichache? Je tuanze kujenga mabwawa makubwa ya kufua umeme wakati wananchi wanakaa kwenye nyumba za tembe zilizotapakaa umbali mkubwa kutoka nyumba nyingine? Je tusomeshe walimu zaidi kuliko mainjinia, na polisi wengi kuliko madaktari? Kumbe uamuzi wa kupanga unaenda na kuchagua na kama wengine wanachosema na unapochagua inamaana unapangua!

Lakini dhana hii pia (ukimsoma vizuri Nyerere na ndugu yangu najua nawe ni Mwanafunzi mzuri wa Mwalimu) utaona kuwa siyo tu kupanga ni kuchagua kunahusisha suala la kupanga matumizi ya raslimali kidogo zilizopo lakini pia suala la maslahi yanayopingana (conflicting interests). Kwa mfano, kati ya barabara na maji tuweke mkazo wapi? Kati ya afya na elimu tuweke mkazo wapi? kati ya usalama wa taifa letu na uhuru wa demokrasia mkazo uwe wapi? Hapa ndio utaona kuwa kupanga ni kuchagua kunakuwa kwenye its optimal value. Wakati mwingine tunachagua kile ambacho tunajua kwa muda mrefu kilikuwa ni cha msingi zaidi. Tanzania ilichagua KILIMO.

Mambo mengine yote yalikuwa yanazunguka katika kuboresha kilimo ambacho kilikuwa (na bado) kimeajiri watu weng zaidi nchini kuliko sekta nyingine yoyote. Ndio sababu ya mara moja kuanza kujenga vyuo vya kilimo (vikubwa na vidogo) na kuingiza mitala ya kilimo kwenye shule za sekondari na kwa kiasi kikubwa kilimo kikawa sehemu ya sekta nyingine vile vile (magereza, JKT, n.k). Sasa kuchagua kilimo kwanza (original concept ya Nyerere siyo hii ya kuigiza ya stimulus package!) hatukumaanisha kuwa elimu inakuwa nyuma. Utakumbuka kuwa vyote vilienda sambamba na kweli elimu ilitumikia kilimo (education serviced agriculture). Tengeru, Lyamungu, Selian n.k vyote ni matokeo ya uelewa kuwa elimu inaenda sambamba kabisa na matakwa ya kilimo.

Lakini hoja ya Lowassa ina kosa kubwa zaidi la kimantiki. Unaweza vipi kuelimisha watu wenye njaa? Watu wasiokuwa na chakula bora na ambao usalama wao wa chakula haupo wataweza vipi kutulia darasani? Kumbe kimsngi kabisa na kimaisha (existential reality) ni lazima kutilia mkazo kilimo kwanza ili kuwezesha vitu vingine vyote viende sambamba. Hivyo, kilimo bado kina nafasi ya pekee kati ya sekta nyingine zote (ikiwemo ya elimu) na hivyo kinastahili kupewa kipaummbele zaidi. Hili ni kweli hasa baada ya habari za wiki hii kuwa bei ya chakula duni imepanda na kuwa maeneo ambayo yanaweza kusaidia kulisha dunia Afrika ni mojawapo. Wataalamu wametoa ONYO KALI juu ya hali ya usalama wa chakula wa dunia.

Hata hivyo, tukitambua ukweli kuwa KILIMO ndicho kinastahili kipaumbele cha pekee tunaelewa vile vile kuwa hatuwezi kuendelea kulima kwa namna za kijadi na kwa kutumia nyenzo na mbinu duni. Ili kilimo cha Mtanzania kiwe kweli chenye manufaa ni lazima kiwe kilimo cha kisasa ambacho kinaondokana kabisa na matumizi ya jembe la mkono na ambacho kimekuwa mechanized na ambacho kinabadilisha na kuwa ni cha kibiashara (iwe mazao ya chakula au vinginevyo). NI lazima kiwe kilimo ambacho kinachangia katika kipato cha mtu na pato la taifa. Ni wazi basi kilimo cha namna hiyo hakiwezekani isipokuwa mahali pale ambapo pana ujuzi na utaalamu wa kutosha na uelewa mzuri wa sayansi ya kilimo kuweza kubadilisha (kwenda juu) kiasi cha uzalishaji.

Hapa basi elimu ina nafas ya pekee. Lakini katika hili siyo "elimu" kama elimu tu bali elimu maalumu inayohusiana na kilimo. Suala la matumizi ya teknolojia, mbegu za kisasa, mfumo wa kufuatilai (tracking system ya mazao), n.k vyote vinaenda sambamba na uboreshaji wa elimu hii ya kilimo. Kumbe utaona ukichukulia elimu hii mahsusi bado hutumikii elimu kama elimu bado unatumikia kilimo! Kumbe elimu kwanza (ya kilimo) inatumikia kilimo kwanza na inathibitisha kuwa kilimo kina nafasi ya pekee.

Lakini kama nchi ina raslimali zinazokoma inawezekana vipi kugawa raslimali hizo kiasi cha kufanya elimu yote kuwa ichukue zaidi bila kujali matokeo yake kwenye kilimo? Kwa mfano, kina Lowassa wakaamua kujenga shule nyingi za kata, watoto wengi kwenda elimu ya juu na kuwa na taifa la wasomi wengi itakuwaje kama wasomi hao wengi hawajihusishi na kilimo? Ni kweli tunaweza kuwa na 'elimu kwanza' ambao wasomi wengi wa mambo ya biashara, madawa, wahandisi, maafisa uhusiano n.k wamejazana lakini hii itasaidia nini kama wote hawa hawajui mbinu za kilimo cha kisasa? Ni rahisi kuona matoke yake... tutakuwa ni taifa lenye wasomi "wengi" lakini linalokufa kwa njaa! Ukiangalia hiki ndicho kinachotokea sasa! Tanzania imehamisha raslimali nyingi kwenye vitu vingine vingi kweli isipokuwa kilimo na pale walipowekeza kwenye kilimo utaona ilikuwa kwenye stimulus package ya wazalishao pamba na mazao ya biashara!

Hata hivyo huku tunakoelekea uchaguzi hautakuwepo kama ni kati ya "kilimo kwanza" au "elimu kwanza" kama Lowassa anavyotaka tuamini. Uchaguzi naamini utakuwa kama tutachagua uongozi bora kwanza. Binafsi naamini hilo ndilo chaguo sahihi.. UONGOZI BORA KWANZA. Naamini huu unatangulia kilimo kwanza na elimu kwanza. Kwani uongoz bora kwanza utajifunza kuamua jinsi ya kugawa raslimali, kusimamia mapato na matumizi na kuhakikisha kuwa kidogo tunachopata kinatumika kuliinua taifa. Naamini changamoto kubwa zaidi siyo suala la hizi sekta ni suala la uongozi.

MIMI MSIMAMO WANGU NI UONGOZI BORA KWANZA. Kwani ni huu ndio unaweza kutuonesha unaelewa vizuri msingi wa matatizo yetu na uko tayari kufanya yote yanayowezekana. Mahali penye uongozi bora hakutakuwa na utata wa kugombea kama ni elimu kwanza au kilimo kwanza. Tunashuhudia hoja hii ya Lowassa kwa sababu chama chake kimetoa uongozi mbovu kwa taifa kwenye sekta hizo mbili na sasa wanataka kutuuzia garasa jingine. Kama kweli Lowassa angekuwa ni muumini wa "elimu kwanza" angekuwa wa kwanza kutaka bodi ya mikopo ivunjwe miaka zaidi ya mitano iliyopita ambapo wengine tulionesha kuwa serikali yake haithamini elimu! Angekuwa anaamini 'elimu kwanza" asingekaa pembeni na kuona wanafunzi wetu 31 wanarudishwa kutoka vyuo vikuu kule Ukraine ambako walikuwa wanasomea udaktari, uhandisi na biashara!

Sorry, I couldn't resist to take that shot!
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji

Unachokiongea ni sahihi kabisa ni lazima kutilia mkazo kilimo kwanza ili kuwezesha vitu vingine vyote viende sambamba. Tatizo tulilonalo ni utekelezwaji wa sera yenyewe, yanayosemwa mengine na yanayofanyika mengine.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom