Lowassa, Membe and Sitta: Unfit to Lead, Unprepared to Command

Hawa wazee wameongoza miaka yote hii na wamejisahau wakafanya uongozi kama ni sehemu ya kufanya kitu chochote wanachojisikia kufanya bila kupata madhara yoyote yale. Unless tupate mtu atakayeweza kufanya tofauti, hawa watatoana macho kwenye hayo makundi yao.


Mwanakijiji leo kaja na nyingine kumuunga mkono Membe

sasa hata hatujui yupi ni yupi

mimi nasubiri Pasco atajibu vipi
 
You know what 2015 people will not choose CDM coz they have better solutions to their problems No way, It just becouse pple need Change!:poa
 
Watu kama AGUSTINE MREMA, DR SLAA, IBRAHIM LIPUMBA, ZITO KABWE, EDWARD LOWASA, FREDRICK SUMAYE, SAMWELI SITA.... wanapatamani saaaana.
 
Well said M.M. Its for us Tanzanians to make choose the right candidate to take us forward, but who is our messiah!?

Mkuu Limbani: Your comment leaves many questions unanswered. Kwa kifupi Tanzania tuko njia panda. Notice where I have written in red. You could have written the sentence like this: Its for us Tanzanians to choose the right candidate to .......... or Its foor us Tanzanians to make a choice for the right candidate to......................................................
 
I'll vote for Lowasa than Membe or Sita. Lowasa ni jasiri alikubali kubeba mzigo wa JK kuokoa jahazi. Sitta na Mwakyembe ni wasaliti, waoga na wapenda madaraka above all ni waoga. Membe hajulikani lakini nae pia ni muoga. Lowasa sio muoga, alimwambia ukweli JK ndani ya Halmashauri kuu ya CCM. Kama CCM 2015 chaguo ni hao, Lowasa is much better
 
Wenye uwezo wa kuongoza hawafiki juu katika uongozi wa CCM, kwa sababu kupanda ngazi kunahusisha kufanya mambo yanayowapotezea sifa za kuongoza. Leo hii, kwa mfano, si rahisi kuwa mbunge bila kuhonga na/au kudanganya wananchi.

Wanabaki na uadilifu wao kwenye uenyekiti wa vijiji huko. Hata hatuwajui katika kiwango cha siasa za kitaifa kwa sababu muundo wa siasa za kitaifa CCM una chujio maalum linalowaondoa waadilifu automatically.

Na tusipoangalia ugonjwa huu utahamia mpaka kwenye upinzani wetu.
 
Mchambuzi: Your article is simply wonderful!! Siku zote mawazo yangu yananipeleka kama ulivyoandika lakini uwezo wa kuyatoa kwa ufasaha na hekima uliyoonyesha sina. I am so happy the way you have analyzed the whole situation. Umenigusa kwa mengi lakini this section is just awesome!!!

Wana CCM wenzangu, tusiogope kushindwa hoja kuhusu CCM kufilisika kihoja mbele ya umma, kwani badala ya kutibu tatizo, tunaficha ugonjwa ambao utakuja kutuadhiri. Tukubali kwamba nchi yetu imeshakomaa kuruhusu demokrasia ya kupokezana vijiti. Wana CCM wenzangu, kushindwa 2015 (kama itatokea) sio mwisho wa dunia, and as a matter of fact, tutakuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kujipanga upya tukiwa nje kuliko tukiwa madarakani kwa sababu moja kubwa: Tukipoteza madaraka ya nchi, hapo ndio tutajua kina nani walikuwa wapo CCM kimaslahi na kina nani walikuwa wapo CCM kwa dhati kwani ni dhahiri kwamba wengi watakimbilia upinzani, na hii itawapatia nafasi wale wachache watakaobaki CCM kwani watakuwa na nia ya kweli ya kukirejesha Chama kwenye mstari.

Wana CCM wenzangu, CCM ni chama pekee katika dunia ya tatu kilichokaa madarakani kwa zaidi ya nusu karne, hasa katika mazingira ya liberal democracy. Sasa kama vipo vyama vinavyopoteza madaraka ya nchi kwa kutawala miaka mitano au kumi, sisi ni nani kuwa immune kiasi hicho? Unless madaraka kwetu ni kwa ajili ya kujipatia immunity na ufisadi ili tusifikishwe mbele ya sheria pale chama kingine kitakapochukua madaraka; au unless lengo letu ni kutumikia matumbo yetu na sio wananchi, vinginevyo watanzania wakiamua kututoa madarakani 2015, tukubali maamuzi ya wengi, lakini isiwe mwisho wa dunia kwetu kwani kwa mfano:



  • Ghana, kwa mfano Chama cha NDC kilipoteza madaraka mwaka 1992 kwa chama cha upinzani, lakini kikarudi madarakani mwaka 2008;
  • Uingereza, chama cha Labour kilikuwa cha upinzani kwa miaka 17 mpaka pale Tony Blair alipokirudisha madarakani;
  • Japan, chama Cha DP kilitawala kwa miaka 50, lakini kikashindwa miaka michache iliyopita, na hivi sasa kinajipanga na kina nafasi kubwa ya kurudi uchaguzi mkuu ujao;
  • Zambia, CCM ya Zambia (UNIP) ilitawala kwa miaka 27 na kuja kupoteza uchaguzi kwa Chadema ya Zambia (MMD), ambayo ilitawala kwa miaka 20 kabla ya kupoteza kwa chama kipya (DP) cha Satta ambacho tayari wananchi wengi wanaanza kufikiria tena kuwapa ridhaa yao MMD au UNIP. Hii ni ishara kwamba tatizo linalowakabili waafrika kwa ujumla ni umaskini lakini kuna uhaba wa vyama vyenye itikadi ya kutatua tatizo hili. Ndio maana huwa napingana na mawazo wa baadhi yetu humu kwamba hatuna haja ya vyama vingine vipya kwani CCM na Chadema wametosha.
Mimi binafsi viongozi wa CCM wamenimenikifu kwa jinsi wanavyofanya mzaha na mustakabli wa taifa.
Watanzania tuwe makini tuachane na siasa za ushabiki badala yake tujiangalie na tujitambue kuwa tunahitaji uongozi wa aina gani ili tusherikiane nao kujikwamua kwenye haya matatizo ambayo kabisa yanaweza kutatuliwa kama uongozi makini ukiwa madarakani
 
Mwanakijiji: Hoja inasisimua kweli kweli. Najiuliza wapiga kura wana "uwezo" wa kupambanua wamchague nani kutokana na mazoea, ushabiki na rushwa iliyokithiri? Rushwa katika taifa letu si siri. Viongozi wengi wanaoishupalia hawajatueleza wananchi ni jinsi gani wataishughulikia. Hatuoni mikakati dhahiri ya kuiondosha rushwa katika jamii yetu. Yu wapi mwana CCM kiongozi katika ngazi yoyote ambaye kwa hakika hajajihusisha na rushwa?

Wana CCM wakubali kuwa njia pekee ya kujisafisha ni kuachana na kutawala kwa muda wakajisafishe na kujipanga upya kama kweli wanajali mustakabali wa taifa. Wana CCM kutokana na uzoefu wa kutawala kwa zaidi ya nusu karne, wajitahidi kutoa mchango wao jinsi ya kurekebisha mapungufu ya mfumo wa utawala uliopo kwa kushirikiana na vyama vya siasa vyenye nia njema na taifa hili kama kweli wanalipenda. Katiba mpya izingatie kurekebisha mfumo wa sasa wa utawala na tume ya uchaguzi ujao iwe huru. Pengine hatua kama hizi zinaweza kutupatia viongozi bora kuliko ilivyo sasa.
 
Kaka,

Napata shida moja. Unasema hawa watatu hawafai. Ninavyofahamu mimi kwanza hawa watatu hawajasema watagombea, wanahisiwa tu. Aidha huendi mbele kutaja basi nani anafaa hata huko nje ya CCM. Mie kwa maoni yangu, suala zima la kugombea urais ni premature halafu tumejifunga sana kwenye majina machache ndani na nje ya ccm. Inawezekana baadhi ya majina ya ccm yasifae, lakini majina yanayotajwa chadema yaani mbowe na slaa pia hawafai. Kwa maneno mepesi, kwa kufuata hoja yako tunaweza kusema kuwa hatuna wagombea 2015. Naamini kusema huyu anafaa na huyu hafai ni kujipofusha. Tunaweza tu kusema huyu anafaana huyu hafai pale tutakapowapambanisha na wengine. Hadi sasa hatujampambanisha yoyote kuhusu urais tunachoongelea ni hisia tu na mapenzi yetu binafsi juu ya historia zao na nafasi zao walizonazo sasa. Tutamjua mgombea anayefaa atakapopambanishwa na wengine ndani ya chama chake kwenye primaries ambako wote wanaojihisi wanafaa watachukua fomu kuomba kuchaguliwa.

Kwa uelewa wangu mfupi, hadi sasa hakuna chama chochote ambacho kimeshafanya mkutano mkuu, CCM ni mwaka huu na CHADEMA nadhani ni mwaka huu au mwakani. Mikutano hiyo na safu mpya za uongozi zitakazotokana na mikutano hiyo ndio itatupa viashiria vya aina ya wagimbea watakaojitokeza na wenye uwezekano wa kupitishwa na vyama. Mathalan, baada ya mkutano mkuu, taswira ya NEC na CC ya CCM ikabadilika na kuingia watu wa mlengo wa Lowassa au Membe au Sitta tunaweza kubashiri ni aina gani ya mgombea atasimamishwa na CCM, maana mgombea hajisimamishi mwenyewe bali anasimamishwa na vikao vya chama. Vivyo hivyo, Baraza Kuu na Kamati Kuu ya CHADEMA nayo ikabadilika wakaingia watu wa maeneo mengine wenye kupinga ukristo na ukaskazini tunaweza kubashiri ni aina gani ya wagombea wenye uwezekano wa kupitishwa na kushinda.

Kwa kumalizia tu, tunapaswa kujiuliza, kwani watanzania ni raia wenye kufaa hadi wapate mgombea urais anayefaa? Kiongozi wa Tanzania atatokana na sampling frame iliyopo, kama Mbowe, Slaa, Lowassa, Membe na Sitta ndio waliopo kutokana na sampling frame yetu basi ndio wanaofaa ukilinganisha na makapi mengine ambayo tunayo. Wananchi irresponsible hawawezi kupata kiongozi responsible kupitia ballot box labda kupitia undemocratic means!

nakubaliana na yote uliyosema na zaidi yafaa tukumbuke manano ya mwanafalsafa aitwaye Joseph de Maistre, yasemayo “Every nation has the government it deserves.” (“Toute nation a le gouvernement qu’elle mérite.”)


 
Mkuu Limbani: Your comment leaves many questions unanswered. Kwa kifupi Tanzania tuko njia panda. Notice where I have written in red. You could have written the sentence like this: Its for us Tanzanians to choose the right candidate to .......... or Its foor us Tanzanians to make a choice for the right candidate to......................................................

Thanks for elaboration, I wanted to say " It is for us Tanzanians to make a choice for the right candidate to take us forward (lead us to the better Tanzania).. All in all, the message is clear I hope
 
Anne Makinda, membe, Lowassa, Sitta Dk.Salim, Mwandosya Dk.Slaa, Prof.Lipumba, Dk.Migiro, Sumaye, Zitto, Magufuli.

1.Je? Raisi atatoka katika kundi hili?
2.Kuna ambaye kati ya hawa unaona anasifa za kuwa raisi?
3.wewe ungepewa nafasi ya kupendekeza ungemchagua nani kati ya hawa?
 
Dr.slaa sidhani km kuna mtz hajui mchango wake, anafuatia kwa mbali sana mwandosya, lowasa najua kuwa walijianzishia kampuni feki yeye na kikwete na rostam km tuzo ya kazi nzuri ya kumuingiza kikwete madarakani
 
Back
Top Bottom