Lowassa, Membe and Sitta: Unfit to Lead, Unprepared to Command

Binafsi nimefurahishwa na makala ya mwanakijiji na sishangai anapopata mashambulizi kwani anakabiliana na system iliyotawala kwa miaka zaidi ya 50 mfululizo ambayo imezaa watu wanayoiunga mkono out of mazoea, wengine maslahi, wengine ushabiki na wengi zaidi ujinga (illiteracy/ignorance). Kuna utofauti wa kuunga chama na miiko/misingi yake vis a vis kuunga mkono chama na madudu yake. Hapa nalenga watu wanaokiunga chama na madudu yake. Mimi ni Mwana CCM lakini hiki sio chama ambacho kama ningekuwa nina ‘choice', ningependa kiwe katika hali ya leo. Lazima tukubali ukweli kwamba CCM imekosa mwelekeo. The only excuse we can have ni kwamba chama "hakijakosa mwelekeo" BUT "kinakoseshwa mwelekeo". Wana CCM, hivi ni mambo gani ambayo leo hii tunaweza kusimama majukwaani huko vijijini na kujenga hoja kwamba CCM ni chama chao? Zaidi ya kuja na ‘make up list' ya hapa na pale, kwa kweli hatuna hoja. Tusipoteze muda mwingi kwenda kwa wananchi kuwasemea upinzani, tutumie muda mwingi zaidi kwenda kwa wananchi kurekebisha mapungufu yetu kwa vitendo, hoja na kwa siasa safi.

Makala ya Mwanakijiji inapata upinzani mkubwa kutokana na mtatizo mawili makubwa: Kwanza, wengi tumekuwa wazito kuelewa dhana ya uhuru wa kutoa mawazo. Mimi sioni tatizo kama Mwanakijiji ni mfuasi wa Chadema. Na isitoshe, hata katika siasa za nchi za wenzetu waliokomaa kidemokrasia kwa mfano Marekani, kuna media organizations ambazo zipo aligned na vyama vya siasa na kwa uwazi kabisa. Kwa mfano, makampuni kama FOX, hawa ni republicans, na makampuni kama MSNBC, hawa ni democrats. Lakini pamoja na tofauti zao hizi ambazo hubebwa na utofauti katika ideological following or beliefs, vyama vyote vinasimamia maslahi ya taifa, wanachotofautiana au pishana ni njia ya kufuata towards a better America. Huwa namsoma sana Mwanakijiji hapa JF na kwenye magazeti, na mara nyingi hoja zake huwa ni za maslahi ya taifa kwa kweli kwani zina cut across mtu yoyote mwenye nia njema na nchi yetu. Inawezekana kuna nyakati anaonekana anaegemea upande fulani, lakini kama nilivyokwisha sema, hata kwenye nchi za wenzetu waliokomaa kidemokrasia, hili ni jambo la kawaida.

Pili, wengi wetu humu tupo busy kujaribu ‘to make sense of his (mwanakijiji) language' in the article instead of making sense of the issues that he is trying to address before us. Makala ya Mwanakijiji leaves us with an important question that is in dispute and must be settled. Binafsi ningependa kuiangalia makala ya Mwanakijiji kwa mapana zaidi, hasa kuhusu suala zima la jinsi ya kumpata rais wa Tanzania. Vigezo na utaratibu uliopo ni kama vile Rais wa Tanzania daima atatokea CCM, and to make matters worse, kuna dalili kubwa kwamba CCM na mashabiki wake wanajikita zaidi kuzalisha marais wengi (quantity) kuliko wingi unaoendana na ubora wa marais hao (quality).

Katiba ya sasa ya Tanzania (1977) ni Katiba ya CCM. Pamoja na kufanyiwa amendments za hapa na pale lakini bado ilitungwa ili kuhalalisha supremacy ya CCM. Ndio maana kwa miaka karibia kumi na tatu (1964 – 1977), tulikuwa tunaongozwa na katiba ya mpito na hatukujali hilo kwani Katiba ya TANU, hasa Azimio la Arusha, na uongozi makini wa Nyerere ulifanya wengi wetu tusijali sana hilo kwani Nyerere alikuwa ana deliver. Ilipofika mwaka 1977, Vyama vya TANU na ASP vikaungana na kulazimisha mabadiliko, na hapo ndipo katiba ya nchi ikazaliwa ili kuhalalisha utawala wa chama kimoja (TANU + ASP = CCM), na ndio maana sehemu kubwa ya mgogoro wa katiba yetu ni the "union question". Vinginevyo, baada ya 1977, Katiba ya CCM ikawa Superior kwa Katiba ya Nchi. Ipo mifano mingi juu ya hili lakini kwa haraka haraka niseme tu kwamba - viongozi wengi wa CCM na Serikali kwa ujumla walikuwa mara kwa mara wanakikiuka katiba ya nchi lakini hakuna aliyekuwa anawakemea, lakini ilipotokea kiongozi anakiuka Katiba ya Chama, huyo alionekana muasi, mhaini na kila lililo baya. Muundo huu ukatengeneza mfumo mbovu wa kutuzalishia viongozi, na ni hapa ndipo naungana na mwanakijiji kwamba mfumo wetu wa kutupatia viongozi (CCM) leo hii una matatizo.

Kwahiyo, tafsiri yangu ya hoja ya Mwanakijiji ndio hiyo i.e. ‘kimfumo zaidi' – hasa pale anaposema kwamba haoni jinsi gani CCM inaweza kupata Rais bora ajae ambae atatoka miongoni mwa wabunge (CCM) wa sasa. Tukituliza kidogo akili zetu na kutafakari hili, wengi tutakubaliana na mwanakijiji hata kama haitakuwa mia kwa mia. Nitajaribu kuichambua hoja ya mwanakijiji kwa kutumia Katiba ya sasa ya Tanzania kwani hiyo ndio inatoa vigezo vya mtu kuwa rais bila ya kujali rais anatoka chama gani. Lakini cha kushangaza kidogo ni kwamba katika mijadala kuhusu mapungufu ya katiba yetu, nje ya suala la umri na mgombea binafsi, hatuangalii sana suala hili la sifa ya mtu kuwa rais kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (1977).

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (1977), sifa za mtu kuwa Rais wa Tanzania, awe:

(a) Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia;
(b) Ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) Ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) Anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,
(e) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Nitajaribu kujadili vigezo hivi vitano kwa haraka haraka.
  • Kwanza ni suala la uraia – Siasa za sasa ni zamu ya upande huu au upande ule unatoa mwanya wa kutuletea Ma-rais wabovu ambao wanateuliwa ili kufanikisha zaidi malengo ya kisiasa. Kwa mfano, siasa ya zamu ya bara bila vigezo vingine vya msingi inaweza kutuletea rais wa ovyo lakini pia vile vile siasa ya zamu ya visiwani. Ni muhimu katika kumpata Rais, tukasukumwa zaidi na mahitaji ya watanzania in all spheres (kisiasa, kiuchumi na kijamii) badala ya kusukumbwa zaidi na siasa za muungano.

  • Pili ni suala la umri (miaka 40). Hili tumeshalijadili sana hivyo nitaliacha kwa sasa.

  • Tatu ni kuhusu mgombea lazima atokane na chama cha siasa – hili pia tumeshalijadili sana, huku wengi wetu tukihimiza umuhimu wa kuruhusu wagombea binafsi. Lakini ningependa kulisemea kidogo. Kwenye mdahalo baina ya Nape, Mnyika, Naibu Katibu Mkuu CUF (jina limenotoka), Nape alijaribu kujenga hoja kwamba hatuna haja ya mgombea binafsi kwani hata nchi kubwa kama Marekani wagombea binafsi hawana nguvu, hivyo kusisitiza msimamo wake kwamba Tanzania hatuna haja ya wagombea binafsi ndani ya katiba mpya. Hili ni suala ambalo hata Nyerere leo hii angepingana na Nape kwani hata yeye hakuona sababu za msingi za kuendelea kulikataa hilo kikatiba. Lakini nikirudi kwenye hoja ya Nape, anasahau kwamba Rais wa kwanza wa marekani ‘George Washington', hakutokana na chama chochote cha siasa, na ilichukua muda mrefu kwa marekani kujenga vyama vya maana. Pamoja na kuibuka kwa vyama viwili vya maana baadae, bado katiba ya marekani iliendelea kuwapa option wananchi kuchagua mgombea binafsi. Kinachofanya wananchi wengi waegemee wagombea wa vyama kuliko wagombea huru ni kwa sababu nchi imegawanyika karibia nusu kwa nusu kiitikadi. Hata hivyo, bado kuna majimbo ambayo wabuge wake wanapita kama wagombea huru. Lakini sisi CCM tunafanya maamuzi juu ya suala muhimu kama hili ina top-down fashion, na mbaya zaidi ni katika mazingira yanayotawaliwa na ombwe la kiitikadi (including CCM). Hivi sio kuwatendea haki watanzania.

  • Nne ni kuhusu sifa Rais lazima awe na sifa za kuwa mbunge: Je ni sifa zipi hizi? Kwa mfano katiba ya Tanzania inasema ili mtu kuwa mbunge ni lazima awe:
· ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
· na miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
· ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
· katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Tayari tumeshaona migongano mingi hapo, na kuna sifa nyingine ambayo sijaiweka hapo ambayo, wakati sifa kielimu (mbunge) ni angala darasa la saba, sifa kielimu (rais) ni angalau shahada ya kwanza.
Wengi wetu katika mjadala huu inaonekana hatupo tayari kumfikiria mtanzania ambae hayupo kwenye kundi la sasa la wabunge (CCM); tunaamini kwamba nje ya wabunge waliopo sasa, hakuna mtanzania mwingine mwenye uwezo wa kuwa Rais na Amiri Jeshi mkuu. Na wenye mtazamo huu hawajali kama ubunge wa mgombea ambaye ni chaguo lao, ubunge wa aliupata vipi - kama ulipatikana kihalali au kwa hila, vitisho, rushwa na ujanja ujanja wa kila aina. Kwa wenzetu hawa, hilo kwa sio muhimu!!


  • Na tano ni juu ya ‘kutiwa hatiani' kuhusu masuala ya kodi. Kwa kweli hapa tunachezeana tu akili kwani tumezidi kushuhudia jinsi gani wanasiasa wengi wanajificha nyuma ya pazia la ‘innocent until proven guilty', huku vyombo vyote vya kufanya kazi ya kutia watu hatiani vipo mifukoni mwao. Hivi kweli are we serious na kuachia maadili ya uongozi yapimwe na masuala ya kodi tu? Fine, tuseme suala la kodi ni muhimu, je nani asiyejua kwamba Azimio la Arusha lilivunjwa ili kuhalalisha wanasiasa kuwa na mshahara zaidi ya mmoja, nyumba za kupanga, na hisa katika publicly traded companies, na nyingi ya kampuni hizi zikiwa mstari wa mbele kuhujumu uchumi wetu?? Na je hivi kuna any transparency katika masuala ya ‘tax returns' miongoni mwa wanasiasa wetu wafanyabiashara? Lakini swali muhimu zaidi hapa ni je, hatia kwa kiongozi nje ya kodi hakuna kweli? What about kujihusisha rushwa na matumizi mabaya ya madaraka? What about kubaka au kutafuta hongo za ngono? What about kuwa raia wa nchi zaidi ya moja kinyume cha sheria? The list goes on and on…

Wana CCM wenzangu, tusiogope kushindwa hoja kuhusu CCM kufilisika kihoja mbele ya umma, kwani badala ya kutibu tatizo, tunaficha ugonjwa ambao utakuja kutuadhiri. Tukubali kwamba nchi yetu imeshakomaa kuruhusu demokrasia ya kupokezana vijiti. Wana CCM wenzangu, kushindwa 2015 (kama itatokea) sio mwisho wa dunia, and as a matter of fact, tutakuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kujipanga upya tukiwa nje kuliko tukiwa madarakani kwa sababu moja kubwa: Tukipoteza madaraka ya nchi, hapo ndio tutajua kina nani walikuwa wapo CCM kimaslahi na kina nani walikuwa wapo CCM kwa dhati kwani ni dhahiri kwamba wengi watakimbilia upinzani, na hii itawapatia nafasi wale wachache watakaobaki CCM kwani watakuwa na nia ya kweli ya kukirejesha Chama kwenye mstari.

Wana CCM wenzangu, CCM ni chama pekee katika dunia ya tatu kilichokaa madarakani kwa zaidi ya nusu karne, hasa katika mazingira ya liberal democracy. Sasa kama vipo vyama vinavyopoteza madaraka ya nchi kwa kutawala miaka mitano au kumi, sisi ni nani kuwa immune kiasi hicho? Unless madaraka kwetu ni kwa ajili ya kujipatia immunity na ufisadi ili tusifikishwe mbele ya sheria pale chama kingine kitakapochukua madaraka; au unless lengo letu ni kutumikia matumbo yetu na sio wananchi, vinginevyo watanzania wakiamua kututoa madarakani 2015, tukubali maamuzi ya wengi, lakini isiwe mwisho wa dunia kwetu kwani kwa mfano:


  • Ghana, kwa mfano Chama cha NDC kilipoteza madaraka mwaka 1992 kwa chama cha upinzani, lakini kikarudi madarakani mwaka 2008;
  • Uingereza, chama cha Labour kilikuwa cha upinzani kwa miaka 17 mpaka pale Tony Blair alipokirudisha madarakani;
  • Japan, chama Cha DP kilitawala kwa miaka 50, lakini kikashindwa miaka michache iliyopita, na hivi sasa kinajipanga na kina nafasi kubwa ya kurudi uchaguzi mkuu ujao;
  • Zambia, CCM ya Zambia (UNIP) ilitawala kwa miaka 27 na kuja kupoteza uchaguzi kwa Chadema ya Zambia (MMD), ambayo ilitawala kwa miaka 20 kabla ya kupoteza kwa chama kipya (DP) cha Satta ambacho tayari wananchi wengi wanaanza kufikiria tena kuwapa ridhaa yao MMD au UNIP. Hii ni ishara kwamba tatizo linalowakabili waafrika kwa ujumla ni umaskini lakini kuna uhaba wa vyama vyenye itikadi ya kutatua tatizo hili. Ndio maana huwa napingana na mawazo wa baadhi yetu humu kwamba hatuna haja ya vyama vingine vipya kwani CCM na Chadema wametosha.

Last but not least, niseme tu kwamba pamoja na haya yote, binafsi bado nina jina moja ambalo nina imani mtu huyo ana uwezo wa kulitumikia taifa hili vizuri (ngazi ya Urais) hata kama anatokana na wabunge wa sasa (CCM), kwa sababu amekuwa anapingana na the existing state of affairs (some of which nimezijadili) kwa muda mrefu. Lakini haina maana kwamba yeye ni bora kuliko wengine wa upinzani, na muda ukifika nitamtaja ili tumpime kwa hoja (sio kwa ushabiki, mazoea au maslahi).

Vinginevyo naunga mkono hoja ya Mwanakijiji kwa vigezo nilivyovijadili.
 
mkuu chama...CCM inaweza kua mbaya kwa watu fulani kwa sababu zao binafsi (wanaona watafaidi binafsi CDM ikiingia madarakani, wanatoka kaskazini, waliokata tamaa kabisa, au ni wale wasio na uwezo wa kuchambua mambo na upeo mdogo). Kwa mtu makini CDM siyo mbadala wa CCM angalau uchaguzi wa 2015 hata ule wa 2020. CCM inahitajika kuongoza kwa sababu sioni umakini wowote wa CDM na viongozi wake zaidi ya kua political opportunists.

Hatuwezi kulitupa taifa kwa mbwa kwa sababu Tanzania haiko katika life support ya utawala wala ya kiuchumi kiasi kwamba tumweke Dr Slaa au Mbowe kama Rais. Hawa siyo hao inspirational leaders MM anaowaongelea hata kidogo na kama hamna mbadala tufanye nini sasa?

Matatizo binafsi ya kiuongozi ya Jk na rafiki zake wachache yasifanywe kuihukumu CCM nzima, CCM bado kuna watu makini na wakipewa uongozi wa juu tutaona tamaduni mpya kabisa ya uongozi haswa katika mazingira haya ya siasa za ushindani.

mimi napenda mageuzi, lakini mageuzi makini siyo kukimbilia kuwapa wapinzani (ambao hawajiandaa) taifa lenye changamoto kubwa kama Tanzania yetu hii. Kila mtu anayetaka CDM ishinde sooner than later kama siyo hopeless youth, (who is filled with anarchy testosterone) basi ni msomi kama MM anayeangalia parochial interests tu.

CDM imejaa question mark nyingi sana kwa mtu makini kuwapa kura leo au kesho. wacha waevolve, wakue, wapate uzoefu kwani tanzania siyo nchi rahisi kuongoza kama wanavyofikiria.

Ningependa CDM waje na comprehensive policies zao kuhusu uchumi, siasa na za kijamii siyo hizi vague statements za M4C au opearation sangara zinazolenga ushabiki tu wa kisiasa kitu ambacho Tanzania haitaji tena kwa sasa.

Tena ukiwauliza ni ndani ndani ya Chadema anaweza kuwa entrusted na madaraka ya nchi huwezi kupata jibu. Hiki ni kikundi cha wana harakati ambao hawajaweka timu ya ambayo inatoa matumaini ya kuongoza nchi hii, na ndiyo maana huko nyuma wamekuwa wakilinganishwa na NGOs za wanaharakati au wale wanajeshi wa Mali ambao walipindua nchi halafu wasijue la kufanya au nai awe kiongozi wao. Ameuteurish leadership style waliyoionyesha so far casts a serious doubt with regard to their suitability to even lead their constituencies.
 
Nimekuwa nikisema kila mara na leo narudia tena kusema kwamba MM ni mtu ambaye humu JF anaonekana kama mfalme, kama siyo mungu mtu ambaye wale wanaoumuunga mkono wanafanya hivyo passionately kiasi cha kudhani kwamba kila neno analotamka basi ni gospel truth na hawaamini kwamba anaweza kukosea (na amekuwa akikosea na kupotosha mara nyingi sana). Wala hawajui kwamba ana phobia dhidi ya watu wengine na mania kwa wale aliowachagua in equal measure. Kwa msingi huo amekuwa na prejudices zake dhidi ya kile asichokiamini.

Kwa kukosa balancing na objectivity, ameshindwa kutuambia kwamba kwa vile hawa hawafai na hata chama chao hakifai, then ni nani anadhani anafaa na kwa sababu ipi. Huwezi kusema kwamba eti kwa vile kiongozi fulani hajawahi kukosoa, kujindoa au kutofautiana na chama chake basi huyo hafai au amefeli vigezi alivyoviweka Mfalme MM. Yeye mara zote amejidhihirisha kama mtu anayechukia CCM, tena bila hata sababu za maana. Ingeshangaza kama angewapenda viongozi wake. Ni hoja potofu kusema kwamba kama mfumo fulani au itikadi fulani imefeli, kwa maoni ya mtu mmoja basi hao walio kwenye mfumo huo wote hawafai. Kama ingelikuwa hivyo basi hawa akina Cameron, ambao chama chao kilishindwa au kudumuza uchumi wakati wa akina John Major wasingekuwepo. Na wala kujitoa hakumfanyi mtu kuwa shujaa au kiongozi bora (rejea kujitoa kwa Mrema).

MM ni kada maarufu wa Chadema na hilo siyo la siri na wala isingetarajiwa aipende CCM wala viongozi wake ambao ni mwiba kwa ndoto zake. MM ni aina ya wale watanzania walio nje ambao wamekimbia kulijenga taifa lao, wakiona fahari kuendesha maisha ya watu wengine na huku wakijifanya majasiri na wazalendo wa kukosoa tu serikali iliyoko madarakani bila kujua kwamba kuna mazuri vile vile ambayo yanapaswa kuangaziwa na kupongezwa.

On this MM has failed miserably and has demonstrated the highest degree of partisanship and stereotype that lingers in his otherwise sober mind. I take a serious exception to his line of thinking!


yours Mbopo is a classic ad hominem fallacy. Unafuata mkondo wa chama na mashabiki wengi wa CCM ambao hawawezi kujibu hoja bila kumshambulia mtoa hoja. Dalili ya watu wote kushindwa hoja ni pale wanapoanza kumuita mtoa hoja majina ya kejeli wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo hoja zao zinaonekana zina nguvu au kuvutia. Ni udhaifu mkubwa kwa mtu mwenye akili kumshambulia mtu mwingine. Ungetakiw kuja na kupangua hoja yangu kwa kusema ni kwanini Lowassa, Sitta na Membe wako fit to lead na prepared to command. Badala yake - kama chama alivyofanya - unanishambulia mimi kama mimi ili uonekane angalau umesema kitu.

Kwa miaka karibu kumi sasa nimeshazoea mashambulizi dhidi yangu na hata siku moja sitojitetea. Kwa wanaofahamu msingi wa mimi kutojitetea ni kuwa hoja zangu zinasimama wenyewe. Lakini mara zote watetezi wakubwa wa utawala huu mbovu ulioshindwa wenye sera zilizoshindwa wanashindwa kutetea chama chao na serikali yao na badala yake la kwanza wanachofikiria katika kujibu - nani kasema. "Anajifanya anajua sana", "kwanza ni kada wa CDM", "anatumiwa", "kanunuliwa".

Sasa majibu yenu yanawavutia watu wenye fikra kama za kwenu. Watu walio huru wanaweza kutenganisha jibu la hoja na kioja cha jibu!
 
Binafsi nimefurahishwa na makala ya mwanakijiji na sishangai anapopata mashambulizi kwani anakabiliana na system iliyotawala kwa miaka zaidi ya 50 mfululizo ambayo imezaa watu wanayoiunga mkono out of mazoea, wengine maslahi, wengine ushabiki na wengi zaidi ujinga (illiteracy/ignorance). ..
Vinginevyo naunga mkono hoja ya Mwanakijiji kwa vigezo nilivyovijadili.


NIsingeweza kuisema vizuri zaidi ya ulivyosema. Na mfumo huu ndio ambao tunagombana nao kwani hawaamini kabisa kuwa wanatakiw wabadilike au wabadilishwe. Wanaamini kuwa wao wanapaswa kutawala na mtu yeyote nje yao anastahili kupata kibali chao kwanza au baraka zao.
 
Kaka,

Napata shida moja. Unasema hawa watatu hawafai. Ninavyofahamu mimi kwanza hawa watatu hawajasema watagombea, wanahisiwa tu. Aidha huendi mbele kutaja basi nani anafaa hata huko nje ya CCM. Mie kwa maoni yangu, suala zima la kugombea urais ni premature halafu tumejifunga sana kwenye majina machache ndani na nje ya ccm. Inawezekana baadhi ya majina ya ccm yasifae, lakini majina yanayotajwa chadema yaani mbowe na slaa pia hawafai. Kwa maneno mepesi, kwa kufuata hoja yako tunaweza kusema kuwa hatuna wagombea 2015. Naamini kusema huyu anafaa na huyu hafai ni kujipofusha. Tunaweza tu kusema huyu anafaana huyu hafai pale tutakapowapambanisha na wengine. Hadi sasa hatujampambanisha yoyote kuhusu urais tunachoongelea ni hisia tu na mapenzi yetu binafsi juu ya historia zao na nafasi zao walizonazo sasa. Tutamjua mgombea anayefaa atakapopambanishwa na wengine ndani ya chama chake kwenye primaries ambako wote wanaojihisi wanafaa watachukua fomu kuomba kuchaguliwa.

Kwa uelewa wangu mfupi, hadi sasa hakuna chama chochote ambacho kimeshafanya mkutano mkuu, CCM ni mwaka huu na CHADEMA nadhani ni mwaka huu au mwakani. Mikutano hiyo na safu mpya za uongozi zitakazotokana na mikutano hiyo ndio itatupa viashiria vya aina ya wagimbea watakaojitokeza na wenye uwezekano wa kupitishwa na vyama. Mathalan, baada ya mkutano mkuu, taswira ya NEC na CC ya CCM ikabadilika na kuingia watu wa mlengo wa Lowassa au Membe au Sitta tunaweza kubashiri ni aina gani ya mgombea atasimamishwa na CCM, maana mgombea hajisimamishi mwenyewe bali anasimamishwa na vikao vya chama. Vivyo hivyo, Baraza Kuu na Kamati Kuu ya CHADEMA nayo ikabadilika wakaingia watu wa maeneo mengine wenye kupinga ukristo na ukaskazini tunaweza kubashiri ni aina gani ya wagombea wenye uwezekano wa kupitishwa na kushinda.

Kwa kumalizia tu, tunapaswa kujiuliza, kwani watanzania ni raia wenye kufaa hadi wapate mgombea urais anayefaa? Kiongozi wa Tanzania atatokana na sampling frame iliyopo, kama Mbowe, Slaa, Lowassa, Membe na Sitta ndio waliopo kutokana na sampling frame yetu basi ndio wanaofaa ukilinganisha na makapi mengine ambayo tunayo. Wananchi irresponsible hawawezi kupata kiongozi responsible kupitia ballot box labda kupitia undemocratic means!

Bwana wee hadithd ndeefu ya nini? Hivi kweli unaona kuna anayefaa kutoka chama cha magamba ilihali wote kuanzia wabunge an viongozi wa serikali wanatetea au kushiriki rushwa au kubariki ufisadi? Niambie mmoja wao na huyo nduye anayefaa to command
 
Tena ukiwauliza ni ndani ndani ya Chadema anaweza kuwa entrusted na madaraka ya nchi huwezi kupata jibu. Hiki ni kikundi cha wana harakati ambao hawajaweka timu ya ambayo inatoa matumaini ya kuongoza nchi hii, na ndiyo maana huko nyuma wamekuwa wakilinganishwa na NGOs za wanaharakati au wale wanajeshi wa Mali ambao walipindua nchi halafu wasijue la kufanya au nai awe kiongozi wao. Ameuteurish leadership style waliyoionyesha so far casts a serious doubt with regard to their suitability to even lead their constituencies.

Sasa tusiwe waoga comprehensive policies za CHADEMA ziko na zitahuishwa muda muafaka ukifika. Hizo za CCM zaidi ya miaka 50 zimetufikisha wapi? Let us bold to face changes although is scary.
 
kuna sentensi nyingine ukisoma hata unashindwa kuelewa mtu anamaanisha nini
Alichokosea ni kusema hakuna mtanzania mzalendo, muelewa, anayechukia maovu na anayependa nchi yetu anayeweza kumuamini mgombea kutoka ccm. Manake ni kuwa kama alivosema MMK kiongozi bora anayeweza kututoa hapo tulipo hawezi kutoka ccm. Vinginevo kama tutasema ndivo tulivo, wa hivi hivi, tusiokuwa na maana yoyote kwenye uso wa dunia hii hivo basi ngoja tu tuichague ccm.
 
Ulichokisema MMK ni ukweli unaouma. Unawauma sana, mashabiki, wapenda maslahi, wasio wazalendo, wala rushwa na wanazi wa ufalme wa rushwa wakiona huu ukweli kuwa ccm haiwezi tena kutoa uongozi unashika kasi. Japokuwa nina hakika kuna nguvu inayowadiscredit Lowasa, Membe na Sita ndani ya ccm ili kupalilia njia kwa wanamtandao hasa kutoka ukanda wa pwani kushika madaraka. Lengo ni kuwaweka pabaya kwenye public ili itakapofika wakati wa uteuzi ccm watu walioandaliwa kutoka ukanda wa pwani ndio waonekane wanafaa. Pamoja na haya yote ukweli kuwa hawafai wote. Awe Lowasa, awe Membe, Sita au hao wanaopaliliwa njia ambao ndio wabaya zaidi kuliko hawa watatu. Ukweli ni kuwa amini usiamini Lowasa anaweza kuwa nafuu kuliko hawa wote lakini ni KUWA wote hawafai. Tunapaswa kuangalia chama kingine ili kuanza enzi nyingine ya utawala na fikra katika nchi yetu. Najaribu kufikiria wakenya wangekuwa wapi kama bado wangekuwa na KANU. We must kick ccm out if we love this country.
 
NIsingeweza kuisema vizuri zaidi ya ulivyosema. Na mfumo huu ndio ambao tunagombana nao kwani hawaamini kabisa kuwa wanatakiw wabadilike au wabadilishwe. Wanaamini kuwa wao wanapaswa kutawala na mtu yeyote nje yao anastahili kupata kibali chao kwanza au baraka zao.

sasa Mzee mwanakijiji na mchambuzi kama mnakubaliana semeni nani wawekwe hapa tuwachambue wa cdm na ccm wote ili tuone nanii anatufaa 2015 na kuendelea. kusema tu huyu hafai na yule bila mdabala ni propaganda na ndiyo maana mnapingwa hapa.

Uongozi mara nyingi tunahisi ni wale wanaojua nini kinaendelea na wanataka kufanya kitu kurekebrisha hicho kinachoendelea sasa kama ndani ya CCM wote waoga na hawa ndiyo wanaojitokeza kwa nini tusiwajadili, kama ndani ya CDM hamna anayejitokeza au kusadikika kwamba anagombea au yupo lakini hapa JF haongelewi kwa sababu wanamageuzi wenye maslahi binafsi mmejaa wengi sisi wengine tungeomba awekwe tupime wote ndiyo tuseme huyu hafai na yule anafaa.

kuna watu wamechoshwa na uongozi mbovu wa sasa hivi wa CCM hata wana ccm wenyewe. lakini bado hawako tayari kuirusha nchi kwa mbwa kwa sababu ya mageuzi tu, watu wanauliza wagombea wote wanataka kufanya nini, itikadi na sera za ndani ni zipi za kichama na za mgombea? nyinyi akina MM na wenzako leteni taarifa \wasifu n.k ili sisi tuchague viongozi makini kwa 2015 bila ya kua na maslahi binafsi na chuki binafsi au kuchoka kwa fikra.

Tanzania kama taifa linahitaji kiongozi nafikiri mchambuzi unajua hili zaidi ya mwanasiasa atayeshabikia kua tumeshinda na sasa ni zamu yao kukaa upinzani, au ni zamu yao sasa kukaa benchi, au kua nje ya ulaji au sasa ni zamu ya kuweka watu wangu tu, tunahitaji a real stateman atayeijenga nchi bila kujali petty partisan politics kwani sisi watanzania tumepiga sana siasa na hakuna maendeleo hadi sasa.

sera za vyama hazina tofauti sana wote ni pro democracy na pro progress lakini je viongozi wapo wa kutekeleza? hapa hatuijtaji tu rhetoric ya kusema huyu hafai au yule anafaa tunahitaji uchambuzi yakinifu ili hata ikiwezekana tushawishi vyama vyetu viweke hawa watu makini zaidi ya kusema tu huyu hafai au yule hafai. tuweke list taifa linataka nini na nani anakidhi mahitaji hayo, fullstop na tuanze kulobby sisi sote kwenye vyama vyetu na magazeti, na mitaani kama kweli sisi ni wanamageuzi siyo vinginevyo.

tunahitaji zaidi ya majina tunahitaji kujua watafanya nini na kuhusu matatizo yetu ya kuiongozi kama ufisadi na uzembe watachukua hatua gani mahsusi..kuhusu mali zilizoibiwa na wahausika wakuu watafanyaje? kuhusu kupanua pato la taifa watafanya nini? kuhusu kilimo, kuhusu elimu, kuhusu gesi yetu, kuhusu mikataba iliyopo ya kinyonyaji ikiisha, kuhusu ushiriki wetu A.M, kuhusu muungano, kuhusu kupambana na ukuaji wa matabaka na tofauti za vipato, kuhusu ufisadi uliopita na uliopo, kuhusu ukuaji wa ongezeko la watu n.k

tunataka kusikia haya toka kwa hii sampling ya leaders ambao tunao kwa sababu wewe na mimi tuliogopa kua viongozi au hatukupewa fursa basi na kama jamii tunao hawa na wengine wachache walijojitokeza na wote tungependa waweke wazi misimamo yao kuhusu haya na mengineyo muhimu kitaifa..

tukishindwa kwa haya ni kuendeleza tu maslahi binafsi bila ya kujali uhalisi wa hali yetu na mazingira yetu ya sasa na baadae, kama hatuko makini sisi wenyewe, watafaidika wajanja wachache na sisi kuendelea kulalamika hadi siku utaifa utakapokua hauna maana na kuanza vita sasa. kwa hali yeyote ile CDM siyo mbadala wa CCM hadi tutakapotoa ile id ya kua wenyewe ni political opportunists ambao hawajaiva kiuongozi (wamepata umaarufu kwa sababu ya friction za ccm na retaliation votes basi na siyo sera zao nzuri)


Mharakati
 
sasa Mzee mwanakijiji na mchambuzi kama mnakubaliana semeni nani wawekwe hapa tuwachambue wa cdm na ccm wote ili tuone nanii anatufaa 2015 na kuendelea. kusema tu huyu hafai na yule bila mdabala ni propaganda na ndiyo maana mnapingwa hapa.

Kwanza ni kwamba naunga mkono hoja na ni kwa vigezo nilivyotoa, na sipo peke yangu kwani wapo wengi wanaounga mkono hoja hii hata kama wengine ni with some reservations. Kuhusu kupingwa - mimi sijaona hoja za kunipinga au kuni hoji, wa kwanza ni wewe, otherwise ningependa kujadiliana na watu wanao hoji msimamo wangu au mawazo yangu, lakini kwa hoja, kwani in essence ni kubadilishana mawazo yenye kujenga, sio kubomoa.

Uongozi mara nyingi tunahisi ni wale wanaojua nini kinaendelea na wanataka kufanya kitu kurekebrisha hicho kinachoendelea sasa kama ndani ya CCM wote waoga na hawa ndiyo wanaojitokeza kwa nini tusiwajadili, kama ndani ya CDM hamna anayejitokeza au kusadikika kwamba anagombea au yupo lakini hapa JF haongelewi kwa sababu wanamageuzi wenye maslahi binafsi mmejaa wengi sisi wengine tungeomba awekwe tupime wote ndiyo tuseme huyu hafai na yule anafaa.

Nani ni mwana mageuzi mwenye maslahi binafsi, una maana mimi na mwanakijiji? Na kuhusu suala la kutaja majina ya watu wapimwe, sidhani kama hilo lilikuwa ndio lengo kuu la mtoa mada, vinginevyo uwanja huo (wa kutaja majina tuyajadili) mimi nadhani upo wazi kwa kila mtu humu, hata wewe.

kuna watu wamechoshwa na uongozi mbovu wa sasa hivi wa CCM hata wana ccm wenyewe. lakini bado hawako tayari kuirusha nchi kwa mbwa kwa sababu ya mageuzi tu, watu wanauliza wagombea wote wanataka kufanya nini, itikadi na sera za ndani ni zipi za kichama na za mgombea? nyinyi akina MM na wenzako leteni taarifa wasifu n.k ili sisi tuchague viongozi makini kwa 2015 bila ya kua na maslahi binafsi na chuki binafsi au kuchoka kwa fikra.

Ni kweli, watu wengi wamechoshwa na utawala wa CCM, lakini muhimu zaidi, wengine wengi wana wasiwasi kama CCM inaweza kutupatia kiongozi mzuri 2015, na kwa kutumia dhana ya uhuru wa mawazo, ndio maana topic kama hizi za kuhoji utayari wa watu kama Membe, Sitta na Lowassa, zinajitokeza huku sote tukifunguliwa mlango kupingana au kukubaliana nae kwa hoja, na ikibidi kutaja majina ambayo tunadhani muundo uliopo CCM bado unaweza kuzaa rais bora kutoka CCM. Hawa watatu wanatajwa zaidi kwa sababu ni miongoni mwa wale walioonyesha dhamira ya kugombea 2015 in one way or another.

Tanzania kama taifa linahitaji kiongozi nafikiri mchambuzi unajua hili zaidi ya mwanasiasa atayeshabikia kua tumeshinda na sasa ni zamu yao kukaa upinzani, au ni zamu yao sasa kukaa benchi, au kua nje ya ulaji au sasa ni zamu ya kuweka watu wangu tu, tunahitaji a real stateman atayeijenga nchi bila kujali petty partisan politics kwani sisi watanzania tumepiga sana siasa na hakuna maendeleo hadi sasa.

Upo sahihi kabisa.


Tunahitaji kiongozi, sera za vyama hazina tofauti sana wote ni pro democracy na pro progress lakini je viongozi wapo wa kutekeleza?
Hapa umenigusa sana kwani angalau kuna watu kama mimi ambao nao wanaona kwamba sera za CCM na za Chadema ni zile zile. Lakini naomba niende mbali kidogo na kusema kwamba - Chadema akiingia Ikulu ataenda kutekeleza yale yale yanayotekelezwa na CCM, ndio maana donor community hawana tatizo na either of the two kuingia ikulu 2015. Wangekuwa na tatizo iwapo CCM ya before 1985 ndio ingeingia madarakani, otherwise CCM ya sasa ni ile ambayo ilikuja kukubaliana na mtazamo wa Mzee Edwin Mtei 1986, na ni CCM hiyo ambayo mpaka leo ipo madarakani, ndio maana sio World Bank, wala IMF (ambao walikuwa nyuma ya Edwin Mtei) wamewahi ku raise any issue since then.

The only way forward for this nation, hasa wanavijiji ambao ndio the majority wa watu nchini kwetu ni chama kuja na ideology yenye radical orientation, na haina maana kurudi kwenye ujamaa bali chama chenye itikadi na uthubutu wa kukemea maovu ya soko huria.

Hapa hatuijtaji tu rhetoric ya kusema huyu hafai au yule anafaa tunahitaji uchambuzi yakinifu ili hata ikiwezekana tushaweishi vyama vyetu viweke hawa watu makini zaidi ya kusema tu huyu hafai au yule hafai.
Nadhani mada ililenga zaidi kuelezea kwanini CCM haiwezi kutupatia rais bora 2015, au atleast hivyo ndivyo nilivyoelewa, na nimejaribu kufanya uchambuzi/kuijadii hoja ya mwanakijiji kwa kutumia vigezo vinavyotumika kumpata rais wa CCM and in the process kuelezea mapungufu yaliyopo.

tuweke list taifa linataka nini na nani anakidhi mahitaji hayo, fullstop na tuanze kulobby sisi sote kwenye vyama vyetu na magazeti, na mitaani kama kweli sisi ni wanamageuzi siyo vinginevyo.

Upo sahihi, na hili ni jukumu letu sote hapa;
 
Nadhani hata mwenendo wa lowasa, sita, na membe ni sehemu tosha kutathimini kuwa ni yupi chaguo la CCM, hata kama kamati kuu ndio muamuzi wa mwisho lakini tunaweza kuchanganua ni nani yuko sahihi. Swali langu ni kwamba iwapo mmoja wao akapita na kuwapiku wenzake je makundi yatavunjwa maana kila mtu ni kama paka na panya, hivyo naashiria kusema kuwa huu ndio mwisho wa CCM
 
Nadhani hata mwenendo wa lowasa, sita, na membe ni sehemu tosha kutathimini kuwa ni yupi chaguo la CCM, hata kama kamati kuu ndio muamuzi wa mwisho lakini tunaweza kuchanganua ni nani yuko sahihi.

Upo sahihi kuhusu mwenendo wa kisiasa....
Kamati kuu kazi yake ni kuchukua majina yote ya waliochukua fomu (hata yakiwa mia) na kuyachuja, sio kwa kuyapigia kura bali kuyajadili kwa vigezo mbalimbali. Vigezo hivi vilikuwa more strict wakati wa nyerere. Kamati kuu inatakiwa ije na majina yasiyozidi matano out of whatever number ya waliochukua fomu. Majina haya yatapelekwa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ambako kura zitapigwa na kubakisha tatu bora (kutokana na wingi wa kura); majina hayo yatapelekwa mkutano mkuu wa taifa yenye wajumbe kaam elfu mbili ambapo watajieleza na kisha kupigiwa kura ili lipatikane jina moja; huyo ndiye atakuwa mgombea wa CCM 2015; katika mchakato huu - tukianza na hoa yako juu kamati kuu ambayo tunajua haipo as strict baada ya nyerere kuondoka, unaposema hivi ( i quote) una maana gani? i.e.
hata kama kamati kuu ndio muamuzi wa mwisho lakini tunaweza kuchanganua ni nani yuko sahihi

Na tukirudi kwenye swali lako:
Swali langu ni kwamba iwapo mmoja wao akapita na kuwapiku wenzake je makundi yatavunjwa maana kila mtu ni kama paka na panya, hivyo naashiria kusema kuwa huu ndio mwisho wa CCM

Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, sioni dalili ya yeyote kati ya hawa watatu kupitishwa bila CCM kugawanyika/kuvunjika; kama nia itakuwa ni kukinusuru chama, atatafutwa mgombea ambae ataungwa mkono na makundi mengine yote. Nje ya hapo itakuwa kuweka mazingira ya CCM kuvunjika;

Bear in mind kwamba this is just my opinion; and I am entitled to my own opinion, but not my own facts; and so far, sina facts juu ya suala hili;
 
mchambuzi...labda naweza kua nimekosea kukuweka kwenye hoja ya MM, lakini kuna tatizo la kimsingi pale anaposema hawa wote hawafai huku akimaanisha ni kwa sababu wako ccm, hii ccm imekua a cult organization? mbona CDM inaashiria kua a cult zaidi ya hii CCM kama ukiangalia kwa umakini.

Tujue tunataka nini sisi kama taifa haswa na halafu tuweke sababu binafsi, tuweke sababu kichama, tuweke sababu kihistoria, tuweke sababu kimataifa, tuweke sababu kiutendaji uliopita n.k then tuseme sawa huyu hfai huyu anafaa....bila ya hivyo ccm bado ina dola na cdm inajitahidi kujihalalisha na kutushawishi kua wako makini kwa kufanya (kwenye majimbo yao) na kuelezea haya kwetu sisi ili tuwape kura.


Nway nashukuru kwa majibu na elimu mkuu...naona hatuna tofauti kuu za kimsingi.
 
Mharakati, nadhani wewe na Mwanakijiji kimsingi hampishani kwani mwaka jana nakumbuka uliwazungumzia Lowassa na Membe kwa mtazamo ambao haupo tofauti sana na wa Mwakakijiji katika uzi wake huu. Tukianza na Lowassa:
Ulimzungumizia ( I quote you) kama ifuatavyo chini ya heading…
"TANZANIA YA RAIS LOWASSA"

…kwa kiongozi aliyejiuzulu na skendo iliyomuhusu yeye mwenyewe ni vigumu baadae kuchukulia hatua au kuziba mianya ya wizi na ubadhirifu serikalini na ukichukulia yeye na watu wake wa karibu ni wafanya biashara kwenye nchi isiyo na uongozi madhubuti wa kisheria basi hatutakua na budi kuangalia maozo ya serikali zote zilizopita siyo tu yakiendelea bali yakiongozeka pia katika muda wake wa utawala.

Nyerere hakumtaka Lowassa na Malecela kwa sababu mbili tofauti, Lowassa kwa ugeni wake katika ngazi za juu za maamuzi ya nchi na chama na fedha zake za haraka haraka alizozipata kwa kipindi kifupi. Na kwa upande wa Malecela kwa sababu ya Kutaka kuhodhi madaraka yote ya Kichama na serikali. Network ya Malecela ilikua tishio kwenye CCM ambapo Nyerere hakutaka mtu mmoja kuwa na nguvu kuliko chama so akawaengua wote.Fast forward 2011 EL siyo tu kwamba ameongeza hela pia ana nguvu kwenye chama ambayo hakuwa nayo 1995 na hii ni shida kwa demokrasia yetu changa kichama na kitaifa.

Hii ina ubaya na uzuri wake. Ubaya ni kwamba hamna mtu atamkosoa kwenye chama, serikali, na atatumia nguvu hizi za umoja huu kudidimiza uhuru wa habari, upinzani na demokrasia nchini. uzuri unaweza kua ataweza kuharakisha mambo yafanyike haraka zaidi kwenye ngazi zote kichama na serikali, lakini je kama ataunda timu dhaifu haya mazuri hatutayaona kwa sababu serikali siyo mtu mmoja/rais serikali ni timu. Kama Nyerere's one man show ilishindwa EL hatoweza.

Tofauti na wenzake Rais EL atataka kiti cha urais kiwe karibu nae hata wakati akiwa amestaafu. Hapa tutaona atakavyojipa nguvu aogopewe kichama na kiserikali ili apate nafasi ya kumchagua mrithi wake 2025. Kama tulivyosema hapo juu atajipa nguvu kwa kuengua maadui, kujaza nafasi zote kwa watiifu wake, kubana vyombo vya habari au kutumia marafiki kuvinunua kama wanavyofanya sasa hivi, na kumaliza nguvu za wapinzani kwa kupachika watu wake ndani ya upinzani na kutumia nguvu za dola ambazo inaaminika ana uhusiano nao vizuri. siasa za urithishaji viti zitakua zimeanza rasmi Tanzania.

EL ana kiburi kisichofaa katika siasa za nyakati hizi za uwazi, ushirikiano na demokrasia zaidi. Kwani Katika skendo yake alijishirikisha mwenyewe sana bila kujali matatizo yanayoweza kumkuta na baada ya hapo hakupanga kuongelea hili kiundani na Rais, Spika wala kamati ya Bunge kumnusuru alikaa kimya kijeuri akiamini ataogopwa hatoguswa kinyume chake kamati ikafanya kazi ikabidi awajibike kwa shingo upande na kuanza kutafuta wachawi kila kona kusababisha nyufa wenye chama na serikali ambazo zimeathiri wananchi kwa kiasi kikubwa.

Je ujeuri huu, ubinafsi huu, umungu mtu huu unatusaidia vipi katika matatizo yetu Watanzania? Nafikiri haitusaidii kua na kiongozi wa aina hii haswa katika muda huu ambao tunataka uongozi unaoweka maslahi ya taifa kwanza.

Vile vile ulimzungumzia Membe kama mtu asiyetufaa kutuongoza chini ya heading ifuatayo (I quote you):
"MEMBE NI JK PART 2"

…kwa wale wanoandika andika hapa kuhusu mheshimiwa waziri wa mambo ya nje bernard membe kua anafaa kua urais nafikiri wanatoka familia ya Jk kwani membe hana tofauti na JK kiuongozi. hii ina maana mambo yatakua yale yale kwa watz wengine wasiotoka ukoo huo unaongoza kwa sasa..tafakari hatutaki tena episode za KiJK JK hizi zirudi

Mbali la kuwajadili viongozi hawa kwamba hawatakuwa chaguo bora, pia ulikuja na makala nyingine inayozungumzia umuhimu wa mageuzi ya kisiasa ingawa uliweka ulakini wa mageuzi hayo ya kisiasa kuleta mageuzi ya kiuchumi. Lakini the bottom line ni kwamba, given this article below, hata kama unampinga Mwanakijiji kuhusu CCM kufilisika kwa kila namna kuendelea kuongoza nchi yetu, ilitakiwa upingane nae with some reservations kwani hata wewe unakiri kwamba watanzania kwa miaka hamsini wamezidi kudidimia kuliko kusonga mbele kutokana na CCM. I quote you:

Watanzania baada ya miaka 50 wamechoka na kasi ndogo ya maendeleo ya taifa lao. Ukiachilia mbali matatizo sugu ya afya na elimu, miundo mbinu isiyokidhi haja, kuzidi kuongezeka kwa tofauti ya kipato, kukithiri kwa rushwa na ukosefu wa ajira, utendaji wa serikali na sarakasi za kisiasa zisizo na tija vimeongeza zaidi hamu ya mageuzi ya kisiasa nchini.

Tukiwa na msukumo mkubwa wa mageuzi ya kisiasa inabidi tujiulize na tufikiri kama haya mageuzi yatatatua matatizo yetu ya kimaendeleo na kiuchumi kwa ujumla. Kwani sisi kama binadamu na jamii tunahitaji kuishi kwa matarajio yaliyo na uhalisi vinginevyo tutapoteza hata nguvu ya kutumaini na kutarajia chochote.

Sasa mageuzi ya kisiasa hayakwepeki, lakini je ni mageuzi gani ya kiuchumi na kimaendeleo tutachuma/tutavuna kutokana na haya ya kisiasa?

Serikali ya kimageuzi ikiingia madarakani itarithi mikataba mibovu ya kinyonyaji inayolindwa na sheria za kimataifa ambayo tanzania ni mshiriki, kuna swala la madeni ya nje ya kitaifa, kuna suala la maamuzi ya taasisi za kimataifa za kifedha za nje.

Kupingana na yote haya ni sawa na kujipiga risasi kwenye mguu. ili kuongeza kipato serikali inahitaji ufanisi wa hali ya juu sekta ya kilimo, sekta ya madini, utalii, na viwanda na biashara (sekta ya mabenki na soko la fedha na bidhaa).

Kipato cha serikali ni kidogo kuweza kuwekeza kwenye sekta ya kilimo sawa sawa na hivyo kuinua sekta hii iliyo kubwa nchini, hapo hapo tunatakiwa kulipa madeni ili tupate misaada ya hapa na pale ambayo ni sehemu kubwa ya bajeti yetu, tukijinga na soko la dunia ili viwanda vyetu vikue ili tuweze kukusanya kodi na kuongeza kipato na ajira nchini tunapewa adhabu na hawa WB na IMF. Sekta ya biashara (mabenki na soko la bidhaa) haiwezi kukua bila kuongezeka kwa kipato cha taifa yaani cha serikali na wananchi kwa ujumla na kipato cha taifa kinaletwa na uzalishaji kwenye sekta nilizozitaja ambazo zinahitaji mkono mkubwa wa serikali (ambayo itakua imefungwa na mikataba, mahusiano ya kimataifa nk).

Serikali ya kimageuzi itapata shida hapa na pato la taifa halitaongezeka vile wengi tunavyotarajia. wanamageuzi wataongeza ufanisi wa serikali, watapunguza ufisadi kwa kiwango kikubwa, watapunguza ukubwa na hivyo gharama za serikali, lakini hayo yote yatakua na athari za kawaida sana kwenye ujumla wa pato la taifa na hivyo kero zetu za elimu duni, afya duni, ajira, nk hazitapungua kama tunavyotarajia wengi wetu.

Wanamageuzi angalau wataleta hari mpya, nguvu mpya na hamasa ya kujivunia tanzania yetu tena.

Mharakati, kwa mtazamo wangu wewe na mwanakijiji kimsingi mnakubaliana kwamba sio Lowassa wala Membe ambae ni chaguo bora kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Vile vile, kimsingi, unakubaliana na Mwanakijiji kwamba watanzania wanahitaji mageuzi ya haraka, huku ukionya kwamba Chama cha upinzani kitachoiondoa CCM madarakani kitapata wakati mgumu sana kuwaletea watanzania mageuzi ya kiuchumi kutokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na utawala wa CCM.

Muhimu zaidi unaweka bayana kabisa kwamba ari ya watanzania, hamasa ya watanzania na majivuno ya watanzania hayapo tena chini ya CCM bali upinzani. Tafadhali nisahihishe kama sipo sahihi.
 
Tuletee Shehe mwenye dhamira ya kweli na uwezi wa kutuongoza kwa haki, ujasiri, unyenyekevu, hekima na weredi uliotukuka uone kama hatutamuunga mkono.



Tumchukue Mufti SIMBA RAISI, KADINALI PENGO WAZIRI MKUU. KILAINI WAZIRI WA MAJI
 
Nadhani hata mwenendo wa lowasa, sita, na membe ni sehemu tosha kutathimini kuwa ni yupi chaguo la CCM, hata kama kamati kuu ndio muamuzi wa mwisho lakini tunaweza kuchanganua ni nani yuko sahihi. Swali langu ni kwamba iwapo mmoja wao akapita na kuwapiku wenzake je makundi yatavunjwa maana kila mtu ni kama paka na panya, hivyo naashiria kusema kuwa huu ndio mwisho wa CCM



Kama walivyoiogpa CUF wakasema Jakaya Kikwete chaguo la Mungu na wakampa Biblia awe anasom akiwa Magogoni. Safari tutaambiwa 2015 Kadinali Pengo aka Mutu ya kaota Membe Rais
 
Mharakati hapo juu, mimi nadhani una muunga mkono mwanakijiji unaposema weka majina ya wote. Ukweli ni kuwa hicho ndicho kitakachotokea. Lakini usisahau kuwa bado tuna miaka miwili, na siku moja kwa maisha ya siasa ni kubwa sana, kwahiyo vetting inatakiwa iwe taratibu. Wiki zilizokwisha umeona akina Zitto wakiwekwa sawa, haina maana safari imekwisha la hasha hii ni safari endelevu.

Nawe pia kama mwananchi unadhima ya kutoa maoni unafikiria nani anaweza kutukwamua bila kujali itikadi za kisiasa.
Usitupe mzigo huo kwa mtu mmoja, sisi ni nchi na kila mmoja wetu ana shea yake katika kujikwamua.

Nafurahi sana tunapowachambua viongozi wa chama, na hapa niseme kuwa CCM na kama wapo washabiki basi walipaswa kushukuru japo kuna mtu anaweza kuamsha fikra kwa upande wao. Sidhani kukaa kimya kunaisadia CCM na hakika kuogopa hoja ndiko kumeifikisha hapo.

Niseme tu hii ni safari na hakuna uwezekano wa kuweka majina yote kwasababu inawezekana 'The beautiful one is not yet born' kwahiyo tuwe na subira wakati tukivuta hatua.

Mchambuzi, kwa hakika umeeleza kwa ufasaha sana hapo juu. Kwa upande wangu nadhani Watanzania ni lazima tuangalie nyika kwa upana wake na si eneo lake tu. Tumefanya makosa na lazima tujisahihishe.

Tukumbuke kuwa sheria, taratibu na miongozo ni vitu vilivyoandikwa na kuna wakati haviwakilishi uhalisia wa hali yenyewe.

Hatupaswi kujikita katika katiba tu ni lazima twende extra miles katika vetting ya viongozi.

Kuna mambo ni constant kwa mfano umri na huo tunaweza kuujadili tu kihivyo pengine tusiwe na lolote lakufanya kwasababu kuna watu wameamua umri uwe kadha.

Lakini basi hatupaswi kuwaangalia wagombea kwa kigezo tu cha katiba au kanuni n.k.

Ni wakati sasa tuwaangalie wao kwa weledi wao wa nchi yetu, historia zao za utendaji, historia zao za uzalendo, historia zao za mambo kama maamuzi bungeni, ushiriki wao katika jamii na nje ya jamii, tabia zao kama viongozi n.k.

Tusipoangalia mbali zaidi tutarudi kule kule kwa huyu ana sura nzuri, huyu hana matatizo bungeni hata kama hajawahi kusema, huyu hatujui anasema ndiyo au hapana, huyu tunamjua kwasababu huwa tunasali naye kanisani au msikitini, huyu ni mwenzetu bwana! tumekuwa wote katika 'totoz' n.k.

Hayo ndiyo yametufikisha hapa na tujifunze. Tunachagua kiongozi na si mtawa, mlei,Alhabibi au Almaarufu, ngariba au bwana harusi.

Tunatakiwa tuwaangalie kwa undani sana busara zao, hekima, utashi na uthubutu.

Na kwa wanajamvi wengine hivi utamaduni wa kushambulia hoja umekwenda wapi? Kwanini unishambulie na usishambulie hoja? Siku zote huwa nasema matusi ni silaha nzuri na nyepesi kwa asiye na hoja.
 
Mchambuzi..ahsante sana kwa kumulika mawazo/michango yangu iliyopita ili kujaribu kuoanisha na mawazo ya MM katika hii topic tuliyonayo hapa. Niliongelea kutokufaa kwa waheshimiwa Membe na Lowassa kua maamiri jeshi wakuu wa taifa letu nikiwa nimetoa sababu (japo hata kama kidogo) na siyo kwa sababu wako tu CCM. hii kwanza, na;

pili niliongelea kuwa nchini kwa sasa kuna shauku ya mageuzi ya kisiasa ambayo yanakua siku hadi siku huku CCM ikiwa inaonekana kushindwa kuja na hoja mbadala na hivyo kuongeza dhana ya kwamba CCM inakufa au sasa inasubiri tu kifo na kila aliyemo ndani ana hii fatalistic view na kua hafai (kwa kua pessimist na unispirational achalia mbali kua na dira wala uzalendo kwa taifa hili). Hili ni kosa kusema kwamba ccm yote ni kitu kimoja hizi ni cheap propaganda na siyo objective reasoning. Kama CCM ni kitu kimoja kwa nini wapigana sasa wenyewe kwa wenyewe? kama siyo shauku ya mageuzi ya ndani ni nini sasa? Mageuzi ya nje yanaisukuma CCM kujaribu kuja na mageuzi ya ndani tatizo tu ni uongozi uliopo una deni kubwa sana la kulipa na hauko tayri kuyatekeleza haya mageuzi ya ndani. Nafikiri hiki ndiyo nilichokua nakimaanisha na ndiyo maana sikutaja chama chochote cha kisiasa. Mageuzi ni mageuzi tu yawe ndani ya chama au nje yake. huu ni ukomavu na dalili ya mabadiliko ndani ya CCM kuendana na taswira ya jamii na mazingira ya kisiasa ya sasa.
kumbuka mchambuzi hata kikwete alionekana kama vile ni mwanamageuzi kwa walie waliomuuza kwetu 2005 kama mtu atayeleta ari mpya,kasi mpya n.k tulisikia sana kuhusu kurudisha nyumba za serikali, tulisikia kuhusu mikataba ya madini n.k haya yalikua ni mageuzi tosha kwa wale waliochoshwa na mabaya ya Mkapa na serikali yake.

MM yake hajasema katika topic yake kama hawa wanamtandao (EL,Membe na Sitta) hawawezi kutuinspire tu kwa sababu wanahusika na serikali hii iliyopo na mchango wao ulikua upi haswa katika serikali hii kutufikisha hapa (mfano kuingia gizani na richmond, au sitta kuimaliza richmond bungeni bila mjadala kumalizika vizuri, au membe kua FA minister ambapo hakuna changamoto kubwa zozote za kitaifa zaidi ya ziara tu na kwa sabbau nafasi hiyo ilimtoa Jk hapo 2005 na sasa membe anaonekana/anafananishwa na Jk kiuonevu au la kwa sababu ya ugumu wa kujaji perfomance ya waziri wa wizara hii) MM ingebidi aseme kwa nini hawafit specifically na siyo kuonyesha vaguely kwamba wanatoka tu ccm.

naomba kukosolewa tena kwa haya niliyoandika hapa,

Mharakati,
 
Back
Top Bottom