Lowassa: Kuna dalili za 'udikteta' Serikalini Tanzania

_91193748_edwardlowassa.jpg

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa amemkosoa mpinzani wake rais John Magufuli kwa kile alichokitaja kuwa ''chembechembe za kidikteta'' nchini humo.

Akizungumza na mwandishi wa BBC John Nene nchini Kenya, amesema kuwa alitaraji kwamba rais Magufuli angeondoa urasimu serikalini lakini "kuna mambo mengine hayajakwenda sawa ", ijapokuwa alikataa kutoa mifano alipotakiwa kufanya hivyo.

Bwana Lowassa alikuwa katika chama tawala alipokuwa waziri mkuu, lakini mwaka uliopita alijiunga na upinzani wa CHADEMA ambapo alishindwa na Rais Magufuli wakati wa uchaguzi.

Magufuli aliyepewa jina Tinga (Bulldozer) anajulikana kufanya maamuzi yanayopendwa tangu achukue mamlaka mwaka uliopita, kama vile kufutilia mbali sherehe za uhuru wa taifa hilo ili kuhifadhi fedha.

Lakini wakosoaji wake wamemshtumu kwa kukabiliana vikali na wapinzani.

Gazeti moja linalodaiwa kuwa mkosoaji mkubwa wa uongozi wake hivi majuzi lilifungwa huku mtu mmoja akikamatwa kwa madai ya kumtusi katika mitandao ya kijamii.
_91195476_raismagufuli.jpg

Serikali yake pia imepiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja ile ya faraghani ya kisiasa.

Maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanywa dhidi ya serikali yaliahirishwa mwezi huu baada ya viongozi wa kidini kujitolea kuongoza mazungumzo na serikali.

Bwana Lowassa amesema kuwa maandamano yalilenga kupinga ''chembechembe za udikteta katika serikali'.

Aliambia wanahabari kwamba ana matumaini kuhusu mazungumzo hayo lakini hatosema kile upinzani utakachofanya iwapo yatafeli.

chanzo bbc
 
Tatizo lenu mmejaa unafiki. Alichokifanya Lowassa ni kuongea ukweli,ambao Magufuli asingeweza kuuongea
Kamwe Fisadi hawezi ongea ukweli, Ile mihela aliyo kua akigawa Makanisani na Misikitini alafu anasema alipewa na Marafiki zake, ivi ao rafiki zake wanafedha kiasi gani?
 
Chanzo: BBC Swahili

Fisadi lowasa anaijua system ya Tanzania klk mwana chadema yoyote yule, na anajua kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha Vita na Raisi wa JMTZ ndani ya ardhi ya JMTZ na akashinda, hilo haliwezekani kwa mujibu wa madaraka makubwa aliyokuwa na Raisi wa JMTZ na Raisi wa JMTZ ana uwezo kama akiamua wa kufanya maisha ya MTZ yoyote yule aishie ndani ya JMTZ kuwa magumu, lowasa analijua hilo na ndiyo maana amewaachia wajinga na wasiokuwa na akili kama Tundu Lisu kufanya uropokaji na kuishia kulala lupango bila kufanikisha chochote kile, wenzake huwa wanakubali kulala lupango kwa malengo lkn yeye (Tundu) hakuna alilotimiza!
 
Unamaanisha kwamba marafiki zake hawana uwezo huo au? Lakini pia kama huyu Mzee ni fisadi ni bora mumshitaki tu si kuna mahakama ya mafisadi imeanzishwa? sio kulalama tu kila siku
 
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa amemkosoa mpinzani wake rais John Magufuli kwa kile alichokitaja kuwa ''chembechembe za kidikteta'' nchini humo.

Akizungumza na mwandishi wa BBC John Nene nchini Kenya, amesema kuwa alitaraji kwamba rais Magufuli angeondoa urasimu serikalini lakini "kuna mambo mengine hayajakwenda sawa ", ijapokuwa alikataa kutoa mifano alipotakiwa kufanya hivyo.

Bwana Lowassa alikuwa katika chama tawala alipokuwa waziri mkuu, lakini mwaka uliopita alijiunga na upinzani wa CHADEMA ambapo alishindwa na Rais Magufuli wakati wa uchaguzi.

Magufuli aliyepewa jina Tinga (Bulldozer) anajulikana kufanya maamuzi yanayopendwa tangu achukue mamlaka mwaka uliopita, kama vile kufutilia mbali sherehe za uhuru wa taifa hilo ili kuhifadhi fedha.

Lakini wakosoaji wake wamemshtumu kwa kukabiliana vikali na wapinzani.

Gazeti moja linalodaiwa kuwa mkosoaji mkubwa wa uongozi wake hivi majuzi lilifungwa huku mtu mmoja akikamatwa kwa madai ya kumtusi katika mitandao ya kijamii.

Serikali yake pia imepiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja ile ya faraghani ya kisiasa.

Maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanywa dhidi ya serikali yaliahirishwa mwezi huu baada ya viongozi wa kidini kujitolea kuongoza mazungumzo na serikali.

Bwana Lowassa amesema kuwa maandamano yalilenga kupinga ''chembechembe za udikteta katika serikali'.

Aliambia wanahabari kwamba ana matumaini kuhusu mazungumzo hayo lakini hatosema kile upinzani utakachofanya iwapo yatafeli.

Chanzo: BBC Swahili
Akae pembeni Lowasa kwani uchaguzi uliisha Oct 2015,
 
LOWASSA SIKU ZAKO ZA UONGOZI ZIMEKWISHA KACHUNGE NG'OMBE. RAIS MAGUFULI SIO DIKITETA BALI MPENDA HAKI. HE IS OUR GOD SENT PRESIDENT. NI MUKOMBOZI WA MASIKINI TANZANIA. TUMUSHUKURU MUNGU KUWAGOMBANISHA WEWE NA RAFIKI YAKO JAKAYA MIPANGO YENU YA KUKABIDHIANA NCHI MUNGU AKAIVURUGA. ILIKUWA AKIMALIZA KIKWETE USHIKE USUKANI, KILA KITU KINGEUZWA TANZANIA. MASIKINI TUNGEISHIA KUSHIKANA UCHAWI KWA SHIDA. NDIYO RAIS ANA KAZI NGUMU KUSAFISHA UCHAFU ULIOACHWA HUKU AKIPIGANA NA WATU WENYE TAMAA YA MALI KAMA NYINYI LAKINI MUNGU HALALI HATARUHUSU MUTU KAMA WEWE KUSHIKA MADARAKA TENA. KATA TAMAA BABA NENDA KACHUNGE NG'OMBE. MUNGU HATARUHUSU WENGI WATESEKE NA WACHACHE WAFAIDIKE NDIYO MAANA AKATULETEA RAIS MAGUFULI.
Dalili zote zinaonyesha wengi wanafaidika wachache wanateseka. Kweli Magu kaletwa na Mungu. Ah....... nimekumbuka hata JK alikua chaguo la Mungu.

Askofu mkubwa alietamka hivyo akapata zawadi ya Escrow na benki yake 'kugawanyia' hiyo zawadi.
 
Fisadi lowasa anaijua system ya Tanzania klk mwana chadema yoyote yule, na anajua kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuanzisha Vita na Raisi wa JMTZ ndani ya ardhi ya JMTZ na akashinda, hilo haliwezekani kwa mujibu wa madaraka makubwa aliyokuwa na Raisi wa JMTZ na Raisi wa JMTZ ana uwezo kama akiamua wa kufanya maisha ya MTZ yoyote yule aishie ndani ya JMTZ kuwa magumu, lowasa analijua hilo na ndiyo maana amewaachia wajinga na wasiokuwa na akili kama Tundu Lisu kufanya uropokaji na kuishia kulala lupango bila kufanikisha chochote kile, wenzake huwa wanakubali kulala lupango kwa malengo lkn yeye (Tundu) hakuna alilotimiza!
Kwa hiyo unaiona sifa. Rais anayechaguliwa na watu aanze kazi ya kuyafanya maisha ya watu kuwa magumu. Kwani wewe kwa akili yako huyo Rais ni Mungu. Mwalimu aliwahi kusema kuwa ni kweli Katiba ya Tanzania inampa uwezo wa ki - Mungu kuweza kufanya lolote, lakini akaonya kuwa hawezi kufanya lolote alitakalo kwa sababu si utamaduni wa Mtanzaina. Sasa je, ni utamaduni wa Mtanzania mmoja kuyafanya maisha ya mwenzake yawe magumu kwa sababu mwenzake huyo kamkosoa na anacho cheo cha kufanya atakalo?
 
Elewa nilichokiandika nimesema ana uwezo wa kufanya, ila sijasema kwamba ameyafanya maisha ya yoyote yule yawe magumu!
 
Kosa lako mkuu katikati ya mistari yeyote asomaye ataona kuwa ulichoandika ni kama kitisho fulani hivi. Tunataka tuwe tunalala na kuamka tukiwa na imani kuwa kiongozi wetu ni mtu mwema na mweledi ambaye hata tukimkosoa hatatumia njia za ukandamizaji kutunyanyasa eti kwa sababu katiba inamruhusu
 
Kuna tofauti kati ya kumkosoa mtu na kutukana, kudhihaki na kumkebehi mtu, kinachotokea sasa kwa upande wa chadema siyo kukosoa bali ni dhihaka dhidi ya Raisi wa JMTZ, na hakuna Binadamu anayependa kudhihakiwa hata kama ungekuwa ni wewe kama una power halafu mtu wa chini yako anakufanyia character assassination hauwezi kumuacha, hiyo ni asili yetu Binadamu karibia wote!
 
Jimbo la kumpa nchi lowasa linaandaliwa
Ni kwaajili ya kampeni ya 2020
Mungu wangu magu atakuwa ajatekeleza mambo kede kede
Atakuwa amefeli sana
Hapo ndipo jimbo litapigwa na kila mtu atacheza kumpa lowasa nchi
Haha
Magu atafirisika tayar vikao vimeanza 2016hataree
 
Lowasa alikuwa waziri mkuu hakuna kitu alichofanya zaidi ya kupiga madili ya kifisadi

MUNGU YUPI WA MONDULI?

HUYU LAZIMA ALIKUWA MUNGU FAKE WA MONDULI. MUNGU HAPATANI NA WENYE MALI ZA WIZI, NA AMEONYA KWENYE BIBILIA TAJIRI ATAKUWA NA SHIDA YA KUINGIA MBINGUNI NI KAMA TEMBO KUPITA KWENYE SHIMO LA SINDANO. LABDA HUYO NI MUNGU WA MONDULI. MUNGU WA HAKI ANATAKA LISTI YA MALI ZOTE.
 
Back
Top Bottom