Lowassa avibana vyombo vya habari kiaina

MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
712
331
Napenda kumpongeza sana Mh. kwa namna alivyokua makini akiwa waziri na hatimaje waziri Mkuu. Kwa kweli nampongeza sana kwa namna alivyokua anafanya maamuzi hususani alipokua Waziri Mkuu. Ninaupongeza pia msimamo wake kwa kutoa hoja na kushawishi juu ya maamuzi magumu na mawazo mazuri ya kiuchumi hususani kwa vijana. Pia huwa naamini vyombo vingi vya habari hapa Nchini hujaribu kuandika mengi kuhusu watu maarufu Nchini, ila pia ukweli haipendezi pale wanapoandika mambo kuhusu fulni bila ya uchunguzi na vielelezo vya uhakika kwa habari husika. Ila pia kwa msimamo wake wa kusema sasa basi yeyote kuchafua jina lake kidogo ulinipa wasiwasi wakati akizungumza na wahandishi wa habari nyumbani kwake. Je angependa vyombo vya habari viandike mambo gani kuhusu yeye?.Kweli ninawasiwasi juu hili. Ningefurahi zaidi kama angesema wanahabari waandike makala kuhusu namna mipango yake ya kusaidia vijana kiuchumi, kijamii nk..Ninachoamini hata kama kuna wanaosema mabaya kuhusu yeye ila bado aviachie vyombo vya habari vifanye kazi zake kwani huwezi jua kama wanavielelezo au laa. Kwa mawazo yangu bado kuna kila sababu ya kuandika mambo yanayohusu viongozi wetu, alimradi tuu vina utafiti na data ambazo zitampa mhusika uhuru wakuziongelea na kujulisha wanaozihitaji.La muhimu pia waandishi wasiangalie kasoro tuu kwani hawa viongozi ni binadamu kama sisi. Mbali na maneno ya hapa na pale kuhusu baadhi ya viongozi kwa ufisadi bado wote wanahaki hadi itakapothibitika vinginevyo. Kimsingi kunaviongozi waliojiuzulu ila bado nawakubali kimaamuzi na kiutendaji na nadhani ni haki ya wanaowapenda kuendelea kupata bahari zao na mipango yao.
 
Back
Top Bottom