Lowassa au Mwandosya kuwa Rais wa Tanzania 2015?

Alichofanya mchambuzi siyo kibaya hata kidogo, tena ni jambo la kupongezwa! Sisi wabongo hatuna mazoea ya long time benefits, kwa kifupi wengi wetu (kubwa) tunaangalia leo, na kesho hatuangalii miaka 10-20 ijayo.

Mchambuzi hapo nakupa hongera, na itakuwa vizuri kabisa tukajua maovu ya hawa watu ambao ni potential presidential candidates mwaka 2015.

Hao watu wawili kwa mtazamano wangu hawafai kabisa, tena huyo LOWASSA ndio HAFAI, HAFAI, HAFAI, KABISA. Yaani nikisia tu LOWASSA basi kinachonijia akilini mwangu ni RUSHWA, MIGOGORO, VIRTISHO, UDIKTETA, KUJILIMBIKIZIA MALI, RICHMONDI, MAHOTELI YA KISASA, YAAAANI RUSHWA MTINDO MMOJA. Yaani huyu mtu nampinga kishenziiiii.
 
Hmmm! Is there a need to discuss 2015 race while we have political turmoil that we have never seen before in our beloved country!?
Kaka mimi nadhani ni muhimu kudiscuss 2015 race wakati huu. Maana kupata kiongozi bora wa kesho ni lazima tumsome alifanya nini jana,anafanya nini sasa na atatufaa vipi kesho.

This is very important ili kupata mtu sahihi wakututoa kwenye hii unayo iita political turmoil. Lakini mjadala huu ni muhimu pia kwa kuwa utatuwezesha kukemea njia zozote mbovu kama zipo za kumpata raisi wa nchi.

Tupo hapa kutafuta njia sahihi ya kuipatia tanzania nabii wa kuwaongoza kutoka kwenye umaskini. Zaidi mjadala wetu wa leo unalenga kutengeneza Tanzania bora ya leo na kesho kwa hiyo kujadili ya leo haitunyimi mwanya wa kujadili ya kesho.
 
sisi wabongo hatuna mazoea ya long time benefits, kwa kifupi wengi wetu ( % kubwa ) tunaangalia leo, na kesho hatuangalii miaka 10-20 ijayo.... na itakuwa vizuri kabisa tukajua maovu ya hawa watu ambao ni potential presidential candidates mwaka 2015...

Thats the problem with watanzania. wanasubiri waletewe walichochaguliwa then wanaanza kukiponda wakati walikuwa na nafasi ya ku influence the process. Any candidate wa 2015 akijua anakuwa monitored na JF ikafanywa kuwa source rasmi ya kipima joto cha watu waelewa, itasaidia sana kwa hawa candidates ku behave ili kujitengenezea chances for 2015.

Kuna mtu alijua mama clinton anagombea u-senate awe rais au running candidate wa democrats 8 years later?

We have exactly 8 years before JK ampishe mwingine na wakati wa kuanza kuwachambua likely candidates ni 2007-2010 period. After 2010 itakuwa too late.
 
Alichofanya mchambuzi siyo kibaya hata kidogo, tena ni jambo la kupongezwa! Sisi wabongo hatuna mazoea ya long time benefits, kwa kifupi wengi wetu (kubwa) tunaangalia leo, na kesho hatuangalii miaka 10-20 ijayo.

Mchambuzi hapo nakupa hongera, na itakuwa vizuri kabisa tukajua maovu ya hawa watu ambao ni potential presidential candidates mwaka 2015.

Hao watu wawili kwa mtazamano wangu hawafai kabisa, tena huyo LOWASSA ndio HAFAI, HAFAI, HAFAI, KABISA. Yaani nikisia tu LOWASSA basi kinachonijia akilini mwangu ni RUSHWA, MIGOGORO, VIRTISHO, UDIKTETA, KUJILIMBIKIZIA MALI, RICHMONDI, MAHOTELI YA KISASA, YAAAANI RUSHWA MTINDO MMOJA. Yaani huyu mtu nampinga kishenziiiii.

That made my evening.

Kusema kweli Lowassa sio presidential material na amri zake za siku saba, karibia kila wizara aliyokanyaga basi kuna ubadhirifu bado hajajibu watanzania mali kapata wapi kwa haraka namna ile.

Naona watu wamesham-rule out Membe
 
Ndugu mchambuzi umeleta mada nzuri sana,na inaonyesha ni jinsi gani unapenda kuangalia mambo ya mbeleni,maana wengi wetu tumetolea macho uchaguzi wa 2010,lakini wewe umeanza kufikiria 2015,hii ni hoja nzuri sana. Nakupongeza kwa kufanya hivyo.

Lakini uchambuzi wa hoja yako umeonyesha udhaifu mkubwa sana katika masuala ya kisiasa.Unamzungumzia Lowassa,wewe unaishi nchi gani,hadi usijue kuwa Lowassa ni dikteta?Je hili joto kali la siasa linaloendelea nchi,umeshindwa kusoma alama za nyakati,kuwa huenda ccm kuja kufika 2015 haitakua ccm tena uliokua unaifahamu.

Katika uchambuzi wako,umeonekana kutokua makini,pale unapozungumza masuala yaa Mwl Nyerere,je hivi kwa akili yako ya kuzaliwa achilia mbali hako ka elimu kako ka darasani,hivi kuna mtu katika Tanzania hadi sasa atatuletea sifa nzuri ndani na nje ya Afrika kama mwl Nyerere?Unaonekana kumponda mwl Nyerere,hii imedhihirisha ni jinsi gani hujui chochote katika historia ya nchi yako.Asingekua Nyerere,leo hii hoja yako ungekua umeiandika kwa kisukuma au kimakonde.Hebu tuambie Kikwete na ari yake mpya hadi sasa hivi kafanya mangapi,ambayo yanatanishawishi nimpigie kura 2010?

Umesema kuwa Salim hafai,kwa sababu angeleta siasa za mwalimu.Je hujui kati ya watu wachache clean tulionao nchini mmojawapo ni Salim?Katika hoja yako unaonekana si mtu makini,kwa kuonyesha udhaifu wa kuwachambua Mwandosya na Lowassa.Kwa taarifa yako kati ya hao wawili hamna anayefaaa,wote wamepitwa na wakati,umefika wakati sasa kila mtanzania amegundua tunapelekwa pelekwa tu kama nyani.

Tunaomba ukiwa unaleta hapa hoja,jiandae,usikurupuke tu,usije ukaibike.
 
Cant we get some new blood? i mean the youth?
Tunahitaji divai mpya iwekwe na tena ndani ya kiriba kipya for the sake of our country.
 
Asante sana kwa hoja zako nzuri. I can understand kabisa jinsi gani inawauma watu kama wewe kusikia mtu anasema mabaya kuhusu nyerere. Nina fahamu fika nyerere ni nani na amefanyia nini Tanzania. Ni kwamba tu nina mtazamo tofauti kama jinsi wewe ulivyokuwa na mtazamo tofauti juu ya kiongozi huyo. Narudia tena, i give Nyerere credit on 3 things tu:
-Amani na utulivu.
-Usawa wa hali na mali.
-Kutokuwepo ukabila.

Nje ya hapo, napinga kabisa mafanikio aliyoleta Tanzania kiuchumi. Nchi yetu haikuwa na ugumu sana wa ku transist from ukoloni kama iivyo kenya au zimbabwe. Haikuwa a settler economy na wakoloni waliacha mambo mazuri tu na watanzania wengi tulikuwa tunafanana kwa hali ya maisha. Tunge embrace what Kenya embraced instead of huo ujamaa tungekuwa mali tu. Inawezekana ndio isingeleta hivyo vitatu juu hapo - amani, usawa na ukabila but i can argue in 100 pages on the way tungeweza kuwa na alternatives on that.

Sifa za nyerere nje ya nchi nazitambua. Lakini sifa hizo zinaambatana na rekodi ya Tanzania kuwa nchi maskini sasa duniani. Napenda sana hoja yako na nadhani tunfungue mjadala wa nyerere na maendeleo ya Tanzania.

Salim A Salim unaongelea usafi gani ndugu yangu alionao huyu mtu. Naona hujafanya utafiti wako vizuri, unamchukulia tu ni mtu mzuri kutokana na ukaribu wake ne nyerere. Hajaiba na hajala rushwa ndio sababu ana ndugu zake waarabu wengi tu wenye hela ambao kpesa wanamtimizia kila kitu. Isitoshe, familia ya Salim Tanzania si zaidi ya watu kumi - au tuseme ukoo...
Sina haja ya kwenda mbali kuhusu Salim but huna ufahamu mzuri wa huyu mtu.

Mwandosya na Lowassa kutofaa for 2015, fine, kama unajengea hoja ni sawa tu kuwa na imani hiyo. Otherwise mimi bado naona mmoja ya hawa ndio anayefaa kwa sasa.
 
2015 ni mwaka wa opposition to lose. Kama sio wao, eti jeshi watashikilia nchi, ila siwezi fafanua.
 
Ninachokiona wewe unaenda nje ya point,wewe hoja yako ingekua nzuri endapo usingetuletea longolongo zako hapa.Umekiri kuwa Salim hajaiba wala hajala rushwa,je hiyo haitoshi tumuite msafi?Tena cha ajabu unaonekana mtu mbaguzi sana,Salim kuwa na ndugu zake uarabuni haituhusu hiyo,ukoo wake Tanzania kutofika watu 10 nchini,hilo si tatizo.Jinsi gani ndugu yetu umeishiwa hoja.Je wewe mwenyewe una uhakika gani ni mtanzania ,au kwa vile una rangi nyeusi?Kumbe unachompingia Salim ni kwa sababu ya rangi yake,tueleze ni wapi alipofanya makosa yaliyoliletea taifa hasara?

Huyo Lowassa una hoja zipi za kumjengea ili akubarike katika jamii,hujui Lowassa ni mmojawapo ya wala rushwa wa kubwa tokea awamu ya Mwinyi,unajua utajiri wa Lowassa unatoka wapi?Hivi unafikiri kuna tofauti kati ya Sumaye na Lowassa,ndo mle mle.
Ndio Salim anapewa hela na ndugu zake,je huyo Lowassa yeye anapata wapi hiyo hela?

Kuhusu Nyerere mambo aliyoyaleta Tanzania hayahesabiki,ni chungu nzima,wala hili halina mjadala hata kama utaandika page 1,000,000,000,kumpinga utakua unazunguka pale pale,na hakuna wa kukubaliana nawe.Kwa taarifa yako waliopo sasa ndo mbumbumbu,walioweka maslahi binafsi mbele kuliko uzalendo.Umesahau Richmond?Mbona tunakua wepesi kusahau,inabidi ifikie wakati watanzania tubadirishe vyakula ili memory zetu ziwe zinafanya kazi.

Umezungumza kuhusu rais wa 2015 kutokea bara,je hiyo umeipata wapi?Kwa mawazo haya potofu ya ubara,upwani,uzanzibar na uzanzibara,ni mawazo machafu sana,hatuchagui rais kwa kuangalia mtu anatoka wapi,ni sifa zake tu zitamfanya awe rais.Ukianza kuangalia mtu anatokea wapi,basi una matatizo makubwa ya kifikra,na hii Nyerere alituonya,dhambi ya ubaguzi.Mimi ni mbara,lakini rais wa 2015 na-suggest anaweza kutoka sehemu yoyote ile ya nchi,hata kama ni kisiwa cha Mafia,bomba tu,ili mradi awe mtu makini,mwenye kujali na kuipenda nchi yake.
 
Kila binadamu ana mapungufu yake na Nyerere(RIP) alikuwa na mapungufu yake lakini nadhani mema yake yalikuwa mengi, huyo Lowassa unayemtetea, mawaziri na wabunge wengi nadhani wamesoma bure wakati wa Nyerere(RIP), si ajabu wewe mwenyewe umesomeshwa bure vile vile. Fadhila zenu ndio hizo tunaziona sasa/
 
Ninachokiona wewe unaenda nje ya point,wewe hoja yako ingekua nzuri endapo usingetuletea longolongo zako hapa.Umekiri kuwa Salim hajaiba wala hajala rushwa,je hiyo haitoshi tumuite msafi?Tena cha ajabu unaonekana mtu mbaguzi sana,Salim kuwa na ndugu zake uarabuni haituhusu hiyo,ukoo wake Tanzania kutofika watu 10 nchini,hilo si tatizo.Jinsi gani ndugu yetu umeishiwa hoja.Je wewe mwenyewe una uhakika gani ni mtanzania ,au kwa vile una rangi nyeusi?Kumbe unachompingia Salim ni kwa sababu ya rangi yake,tueleze ni wapi alipofanya makosa yaliyoliletea taifa hasara?

Huyo Lowassa una hoja zipi za kumjengea ili akubarike katika jamii,hujui Lowassa ni mmojawapo ya wala rushwa wa kubwa tokea awamu ya Mwinyi,unajua utajiri wa Lowassa unatoka wapi?Hivi unafikiri kuna tofauti kati ya Sumaye na Lowassa,ndo mle mle.
Ndio Salim anapewa hela na ndugu zake,je huyo Lowassa yeye anapata wapi hiyo hela?

Kuhusu Nyerere mambo aliyoyaleta Tanzania hayahesabiki,ni chungu nzima,wala hili halina mjadala hata kama utaandika page 1,000,000,000,kumpinga utakua unazunguka pale pale,na hakuna wa kukubaliana nawe.Kwa taarifa yako waliopo sasa ndo mbumbumbu,walioweka maslahi binafsi mbele kuliko uzalendo.Umesahau Richmond?Mbona tunakua wepesi kusahau,inabidi ifikie wakati watanzania tubadirishe vyakula ili memory zetu ziwe zinafanya kazi.

Umezungumza kuhusu rais wa 2015 kutokea bara,je hiyo umeipata wapi?Kwa mawazo haya potofu ya ubara,upwani,uzanzibar na uzanzibara,ni mawazo machafu sana,hatuchagui rais kwa kuangalia mtu anatoka wapi,ni sifa zake tu zitamfanya awe rais.Ukianza kuangalia mtu anatokea wapi,basi una matatizo makubwa ya kifikra,na hii Nyerere alituonya,dhambi ya ubaguzi.Mimi ni mbara,lakini rais wa 2015 na-suggest anaweza kutoka sehemu yoyote ile ya nchi,hata kama ni kisiwa cha Mafia,bomba tu,ili mradi awe mtu makini,mwenye kujali na kuipenda nchi yake.

Nadhani tatizo letu sisi ngozi inferior ni kwamba background yetu ikitajwa vibaya basi inaonekana ni ubaguzi. Mimi kusema ana ndugu zake waarabu au ukoo wake Tanzania hauzidi watu kumi, ubaguzi upo wapi? Kwani ni uongo? Huo ni ukweli mtupu. Na Salim kwani sio mwarabu? Naomba unishauri ningetumia lugha gani kuelezea hizo facts and truth bila kuku offend.

Pia ni vizuri ukitambua kwamba ni background yake ya kiarabu na umemba wake wa chama cha hizbu...before hajaingia ccm ndiyo yamekuwa yanamnyima Salim nafasi ya uraisi since 1995. Sasa kama ni makosa kwangu kutumia neno mwarabu katika kuelezea kwanini ameshindwa wakati wote kuwa rais, which is a fact, sijui nieleze kwa lugha gani nyingine kuelezea the same fact.

Simpingi salim sababu ya ngozi yake. Si sahihi wewe kuja na hiyo conclusion on my behalf. Narudia tena, hana mkono mchafu in terms of rushwa. Lakini pia lazima ujue kwamba hes not as smart as people think in terms of elimu yake. Hes not competent neither. Mfano mzuri ni kwamba, angeweza kuibwa kirahisi sana na UN akiwa na umri wake mdogo hivyo wa early 60s after kutoka AU. Hana credentials zinazoendana na shule nzuri. Alichonacho ni experience na hiyo haitoshi. Huu ni ukweli na samahani sana maana utakuuma. But we can always talk about it.

Ila ujue pia kwamba - Further, just as JK alikuwa anapewa fedha na ndugu jamaa na marafiki for 2005, the same applied to Salim. Issue ikawa, je hizo fedha za Salim zitarudi vipi??? Maana hazitoki humu humu. Lakini for some strange reasons, mashabiki wa Nyerere do not dare to talk about that just because Salim alikuwa na support ya Nyerere, a leader that many anoint him as saint wa Taifa la Tanzania.

Pia inasitikisha sana pale ambapo ni maneno ya nyerere tu yanaendelea kuwa quoted hadi leo on such issues kama za Lowassa etc, as if he made a blue print for kila kitu cha Tanzania. Je asingesemwa na nyerere hali ingekuwaje leo hii?

Wewe unaweza andika page milioni on mafanikia ya nyerere, mimi page hizo hizo on his failures. No research is bad research as long as imefuata methodology and it is backed up with data. Both of us im sure will be capable to convince our readers in that regard.

Kuhusu uongozi wa Tanzania na udini, lazima utambue kwamba ipo kwenye unofficial constitution kwamba, rais akitokea bara, basi makamu visiwani and vice versa holds. Further, hakutatokea kwamba rais anayemaliza madaraka ni wa Bara then ajae awe wa bara. Provision on this is kama anayemaliza atakuwa mkristo then anaweza kuja mbara ambae ni muislamu. Nenda kaulize viongozi wa ccm on this na pia uwahoji ni kwanini wanafuata hii logic na haijaandikwa popote. Mimi nakuelezea tu how it works, i never created hiyo framework.

Lastly, kuhusu Lowassa, kwa wale ambao wanasema hawakusikia nyerere aliposema kwamba Lowassa ni kijana mzuri na ninamfahamu, ana nafasi bado, ajirekebshe... kama hakuna mtu humu ndani JF ambae anakumbuka maneno hayo wakati ule nyerere anasema EL pia ajielezee mali zake katoa wapi kwa muda mfupi, hii itakuwa ni evidence kwamba vichwa vyetu watanzania wengi vinaangalia mabaya tu, mema hayapewi nafasi.

Swali - hivi unajua kwanini EL alirudishwa kwenye cabinet baada ya kuachwa 1995? Mbona hamjibu hili?
Pia je, nini kiliwashinda kummalzia mbali lowassa after 1995 by hooks and crooks kama ilivyo jadi ya siasa za Tanzania, especially after nyerere ku endorse na hivyo ingekuwa rahisi kabisa kummaliza kisiasa, why didnt they do that wakati they had all the resources and instead wakamrudisha kuwa waziri na hatimaye 2005 akapita kwa over 90 pct endorsement ya wabunge as PM? Kwa wenye upeo finyu watasema bunge lipo corrupt etc. Kwa waelewa, wataelezea hadi hotuba za kambi ya upinzani kupongeza uteuzi wa EL kuwa PM.

Swali langu la kwanini endorsement ya nyerere on ubaya wa Lowassa haikufanyiwa kazi na kummaliza na badala yake akarudishwa na kuzidi kung'ara, naona majibu hapa hakuna. And this is the same reason why nazidi kumpa support lowassa kwa sababu lazima kuna jambo ambalo nyerere was not correct.
 
Nadhani tatizo letu sisi ngozi inferior ni kwamba background yetu ikitajwa vibaya basi inaonekana ni ubaguzi. ......

oh come on.... nani ana ngozi inferior....

Nilijua tu ni matter of time kabla hujatumia lugha ya bosi wako mwizi na mkoloni Rostam Aziz kutambulisha ngozi ya watu...

Hakuna mtu mwenye ngozi inferior hapa...

grrrrrrrrrr
 
Its all about perception. But napenda mwamko wako kwamba hakuna ngozi inferior. Ila more importantly, it shows kwamba message yangu imefika.

Inaonekana lakini huna hoja mwafrika wa kike. Ni yale yale ya watanzania wengi kurukia hoja na habari na kujifanya wajuaji bila kuwa na data au evidence. Mfano rahisi ni kwamba tayari rostam ameshakuwa bosi wangu. Ushahidi upo wapi? Ningekuwa na nafasi kama hiyo ningekuwa natafuta nini kwenye mtandao majira kama haya.

Mimi ni raia wa Tanzania mwenye uchungu na nchi yangu lakini i come from a different perspective. Please jaribuni to synthensize that.
 
Mchambuzi, Mwafrika wa kike;

Nadhani wote wawili mna nia nzuri ya Tanzania. Lakini mnagongana kutokana na preferance zenu za nani awe mkuu 2015. Kuongelea 2015 kwa maoni yangu sio jambo baya, kwa itakuwa vibaya mtu aibuke aseme i am insipring for a seat halafu hatumjui huyo mtu. Kwa hiyo kuongelea kwa sasa ni vizuri. Lakini nakubaliana na watao hoja nyingine kuhusu Lowassa, sio Kiongozi mzuri, ni dikteta, unintelligent, corrupt na mengine mengi mabaya.

Nadhani Mwafrika wa Kike angekuwa amefanya la maana sana kuhighlight why against prospective candidate A and B. Nadhani watu wengi wanao argue against EL kwa sababu ni obvious kuwa ni dikteta, ameonesha tabia za utoto, less intelligent na Corrupt(no need to prove the obvious). Sijui kuhusu Mwandosya, lakini sijasikia scandals zake.

Politics za udini ni upumbavu, lakini it is very right ndio zinazochezwa Tanzania kwenye urais whether you like it or not. Ni ujinga lakini ni ujinga unaendelea na utazidi kuendelezwa na wanasiasa. So mchambuzi na Mwafrika wa kike ni vizuri tukaanza wenyewe kujua ambitions za watu 2015.

Kusema JK atabwagwa 2010 ni ndoto ya alinacha otherwise utokee muujiza.
 
Its all about perception. But napenda mwamko wako kwamba hakuna ngozi inferior. Ila more importantly, it shows kwamba message yangu imefika.

Message iliyofika ni kuita watu kuwa wanangozi inferior au ni ipi?

Inaonekana lakini huna hoja mwafrika wa kike. Ni yale yale ya watanzania wengi kurukia hoja na habari na kujifanya wajuaji bila kuwa na data au evidence.

Ni okey ukisema kuwa mimi sina hoja... kwa sababu so far thats what you can do best...

Hili la kugeneralize kuwa watanzania wengi wanarukia hoja na kujifanya wajuaji unaliongea kwa authority gani... umefanya wapi scientific research kuthibitisha hili? au bosi wako mkoloni na mwizi Rostam Azizi ndio amekutuma kutukana watanzania wasomi na wenye uwelewo wa kutosha wa JF?

Mfano rahisi ni kwamba tayari rostam ameshakuwa bosi wangu. Ushahidi upo wapi? Ningekuwa na nafasi kama hiyo ningekuwa natafuta nini kwenye mtandao majira kama haya.

Moja ya email ulizotumiwa within the last 10 days imesajiliwa kwa jina la kampuni ya Rostam Aziz na huo ni uthibitisho wa kwanza kuwa yeye ni bosi wako.

Yeye ni bosi wako na kazi yako ni kuja kutukana wenzako humu kuwa wana ngozi inferior... matusi ambayo mkoloni na mwizi mkuu Rostam Azizi anayatumia sana
 
Mchambuzi,

Nyerere alikuwa na priorities zake. Hata kama angeanza kushughulikia uchumi baada ya uhuru kabla ya Mreno kutimuliwa Msumbiji au Kaburu kuondolewa Afrika Kusini Tanzania ingekuwa vile vile ilivyo hivi sasa. Hebu angalia Kenya. Nyerere alielewa fika kwamba bila kuondolewa Wareno Msumbiji, Ian Smith Zimbabwe na Kaburu Afrika kusini, Tanzania tungeyumbishwa tu kiuchumi. Angalia vile akina Mkapa walivyomshupalia Kaburu. Tofauti gani kati ya Mkapa na Banda?

Mwalimu alijihidi kujenga viwanda vya Watanzania--Mwatex kwa mfano, benki ya Watanzania kwa mfano, vitu ambavyo leo heroes wako wamevigawa kwa bei chee na kutuacha omba omba. Kwa hiyo kabla hujamkosoa Mwalimu angalia misingi aliyotuwekea. Haikuwa kazi ndogo hata kidogo.
 
Thats a good point. Essense ya mimi kuanzisha hii topic ni kwamba, are we aware kwamba hawa ndio watakuwa rais(mmoja wao)? au watanzania wasubiri tu kushtukizwa? Ni mbali sana 2015 but sio mbali. Kama hawa hawafai basi tuanze taratibu kuangalia nani atafaa na tujenge hoja all along kutokana na performance au events mbali mbali.

alichofanya mchambuzi siyo kibaya hata kidogo, tena ni jambo la kupongezwa ! sisi wabongo hatuna mazoea ya long time benefits, kwa kifupi wengi wetu ( % kubwa ) tunaangalia leo, na kesho hatuangalii miaka 10-20 ijayo.

Thats the problem with watanzania. wanasubiri waletewe walichochaguliwa then wanaanza kukiponda wakati walikuwa na nafasi ya ku influence the process. Any candidate wa 2015 akijua anakuwa monitored na JF ikafanywa kuwa source rasmi ya kipima joto cha watu waelewa, itasaidia sana kwa hawa candidates ku behave ili kujitengenezea chances for 2015.
We have exactly 8 years before JK ampishe mwingine na wakati wa kuanza kuwachambua likely candidates ni 2007-2010 period. After 2010 itakuwa too late.

I second that.

Haya ndio maneno. Ninashangazwa na watu wanaodai 2015 ni mbali, kwa hiyo tuyaache kwa sasa. Hili ni moja ya matatizo yetu si Waafrika, waTanzania to be exact, tunapenda 'quick fix'. Long term focus is a challenge to us, at least, mifano ya mapendekezo tunayaona humu humu ndani.

Kuna issues nzito dhidi ya viongozi tuliowakabidhi nchi (ubadhirifu na uhujumu uchumi zimechukua top spots), na hatuwezi kuwatoa kwenye hivyo viti kwa sasa. Least we can do, zaidi ya kuongea tu, is work on assessing someone before he is put in power. Tunaweza kufanya hivi kwa kueleza mass, nani ni nani, na amefanya nini kama ilivyosemwa na wajumbe wengine. Hii itasaidia hata wapiga kura na wachache waliokuwa na limited knowledge ya mgombea.

Kama Mchambuzi alivyo-suggest, tuanze kuwa-monitor, as JF members, let's do our part...
 
Mchambuzi,

Nyerere alikuwa na priorities zake. Hata kama angeanza kushughulikia uchumi baada ya uhuru kabla ya Mreno kutimuliwa Msumbiji au Kaburu kuondolewa Afrika Kusini Tanzania ingekuwa vile vile ilivyo hivi sasa. Hebu angalia Kenya. Nyerere alielewa fika kwamba bila kuondolewa Wareno Msumbiji, Ian Smith Zimbabwe na Kaburu Afrika kusini, Tanzania tungeyumbishwa tu kiuchumi. Angalia vile akina Mkapa walivyomshupalia Kaburu. Tofauti gani kati ya Mkapa na Banda?

Mwalimu alijihidi kujenga viwanda vya Watanzania--Mwatex kwa mfano, benki ya Watanzania kwa mfano, vitu ambavyo leo heroes wako wamevigawa kwa bei chee na kutuacha omba omba. Kwa hiyo kabla hujamkosoa Mwalimu angalia misingi aliyotuwekea. Haikuwa kazi ndogo hata kidogo.

You make very good points Jasusi.

Nyerere had his priorities kweli na aliangalia zaidi political independence kwa wanaomzunguka kwanza kabla ya kujenga nchi. From a pan african perspective, what he was attempting was just. But bahati mbaya i beg to differ from that approach. But you do have very good points.

Pia unasema alijitahidi kujenga viwanda kama mwatex etc. Rais yeyote angafanya hili lakini sio rais yeyote angepeleka effort to pan africanism zaidi na nationalism. Either way, the route inaweza kuwa sawa tu depending on how one argues.

Ninachosema nyerere did not do good ni development management. He wasted a lot of resources on vitu ambavyo havikutakiwa kuwa priority na vilikuwa vigumu.

*Sifa ya nyerere nje ni based on how he embraced socialism and deploy it in an african context. In the process, pia he gets good credit kwa effort zake za kujaribu kuwainua watanzania wote kwa pamoja bila tofauti za kidini, kikabila etc. Even further, hakujinufaisha with the process and instead he did stick with his beliefs na akakubali kushindwa na hatimaye ku quit bila kulazimishwa.

Hiyo ndio sifa ya Nyerere kimataifa. Ameweza kujenga Tanzania on social grounds - ukabila hakuna, udini haukuwa mkubwa na watu walilingana ki hali na ki mali. Ila hilo lilikuwa ni timing bomb for years to come ndio maana akaamua ku quit. Alikuwa very smart kufanya hivyo. Ila mashabiki wa kweli peke yake wa nyerere ndio wataliona hilo, wale wakina mwenzangu na mimi ambae tunamshabikia tu nyerere kwa kumpa credit regardless wont be able to see this.

Back to his economic policies - kama ali embrace vijiji vya ujamaa, making kilimo cha cash crops as a priority, kwanini asingeenda further na kuleta green revolution kama walivyofanya india kwa mfano? Ni kwa sababu India walikuwa wana practice ubepari in a way. If the revolution was very very much practised in china, angefanya the same bila kufikiria twice. Huu ulikuwa ubinafsi sababu hakusikiliza ushauri. Leo hii ndio tunazungumzia green revolution in Tanzania.

Instead aliweka kilimo chini ya usimamizi wa government machinery na kutumua fedha nyingi sana kuendesha makatibu tarafa kwenye ma land rover 109 wakizunguka vijijini na pia askari wakiangalia to make sure makazi ya makao mapya yanadumishwa. Huu ulikuwa ni udikteta wa ajabu sana.

Pia lots of funds was spent kuwapatia wananchi inputs bila kuwapa knowledge ya maana. CRDB/TRDB walikuwa wanapita nyumba hadi nyumba na kuwatupia tu wakulima mbolea etc milangoni mara kwa mara. Nyerere hakuwa na development planning ya maana in practice. In theory, oh yes, it was very elaborate, not in practice.

In the end kilimo kikawa kinakufa tu taratibu as yields from agriculture became poorer and poorer. hapa ndipo wakaibuka kina george kahama na kuanza kula from cooperatives, na walikula kweli kweli under the watch ya mwalimu. Why? most likely ni kwasababu waliona hakuna kinachoendelea so why not.

Nyerere hakuwa anafuata ushauri zaidi wa ndugu zake kina Butiku na watu kama hao. Wataalamu kama kina Edwin Mtei walipigwa sana vita mpaka kufikia hatua ya kuhamia IMF Washington.

Let me give you a little bit of data. Dola moja ya kimarekani ilikuwa sawa na 7 TZ shillings by the time of independence in 1961. South Korea, dola moja at that time ilikuwa ni 64 units za korea; India ilikuwa 4.8 rupees. We were not doing bad at all.

Kilimo kikawa kinawekewa mkazo, na hii ni sahihi ingawa sera zake hazikuwa sahii sababu zilikuwa zinaendeleza formula ile ile ya mkoloni ya kuzalisha mazao for exports than food crops or anything else for uchumi wa tz. Composition ya kilimo on total GDP ikawa inazidi kukuwa way more than sector nyingine za manufacturing, service etc. Wenzetu south korea, india, thailand walikuwa wanafanya opposite. Wanapunguza composition ya kilimo (as %ya total GDP) na kuongeza kwenye sekta nyingine. More importantly, contribution ya kilimo on GDP ilikuwa inapungua wakati real value yake inapanda. Nina mfano wa data:
1965 kilimo was 42% of GDP na kilikuwa kinazalisha dolla za kimarekani milioni 365. Korea, 1965, kilimo was 38% ya GDP na kilikuwa kinazalisha bilioni 1.

1967, % ya kilimo on GDP Tanzania was 41% na uzalishaji was 400 million dollars.

S. Korea, 1967 % ya kilimo on GDP was 31% (7 pct down from 1965) na uzalishaji kilimo wa dolla za kimarekani 1.4 billion.

The rest you can interpret yourself. Na korea was a very poor country in 1960s. What made a difference was sound economic policies. Look at them today.

For Tanzania, ni bahati tu terms of trade za mazao zilikuwa bado si mbaya but not for long. In the mid 70s likaja baa baya sana la njaa sababu we were not concentrating on food crops as much. Pia ukaja ugonjwa mbaya sana wa mazao na effect yake ikawa kubwa zaidi sababu technology yetu ya kilimo ilikuwa ya ovyo. Pia ni bahati tu kwamba world bank walikuwa bado wanatusaidia pamoja na sera za ujamaa sababu nyerere alikuwa anawazalishia rich countries more cash crops kama serikali ya kikoloni, so why care.

Mambo yakaanza kuharibika lakini pole pole na world bank wakaanza kumgeuka. Kina mtei etc wakampa ushauri mzuri sana wa jinsi gani to turn around - mtei akiwa gavana BOT. Akakataa ushauri na kujiona mjuaji. Shilingi ya Tanzania ikaporomoka very fast na huo ndio ukawa mwanzo wa currency yetu kuwa useless. Lakini he gave in by quiting in 1985. He wanted to quit in 1980 but he had hopes kidogo esp after kupewa ushauri na communists. But 1985 hali ikawa mbaya and he had to quit and pave way for reforms. We see them being implemented in 1986 onwards, reforms ambazo alizikataa miaka ya nyuma.

*pia hapa ntasema kwamba - kuna baadhi ya mashabiki wa nyerere wanasema ni yeye alileta vyama vingi i.e political reforms

:)

I could talk on a lot of things but in short and in my view, he had very poor economic policies and is why we are so poor today and we are having difficulties to bounce back coz hatuna strength na hatuna bargaining power. Hayo madini ambayo alisema yaachwe mpaka wapatikane watanzania wa kuweza kuyachimba, was a good vision but on whose terms? where in africa has that been achieved? angewaita hao hao wataalam wa nje na kuwaambia wafanye kazi na watanzania. Kwa miaka ile ambapo cold war ilikuwa bado ina power, investors wasingeweza kutuchezea, tungewa control tu. Badala yake ndio ikawa nationalization ya kila kitu 100%.

Then leo ndio watu wanahoji privitization na kulaumu awamu za baadae Tanzania kusahau makosa yalikuwa ni nyerere mwenywe. Na hao wataalamu ambao alikuwa anawa envision kuja kuwa geologists and mining engineers wazawa hakuwa anawatengeneza na alikuwa hawapi nafasi in terms of kupokea ushauri wao etc. Wengi either wakakimbia, au wakaishia kuwa lecturers, na wengine wengi wakapewa political positions. Hii culture ya kuwapa wataalamu wa mifupa, chemical engineers etc kazi za siasa alituletea nyerere lakini wapenzi wa nyerere hawaoni hayo.

Tatizo langu mimi on nyerere ni poor economic policies na pia udiketa. He was a dictator, i know itawauma watu humu but he was. many people walipata shida sana chini ya uongozi wake, wale ambao walikuwa hawakubaliani nae. We lost a lot of them to foreign countries na wengine wengi mpaka leo ni un accounted for.

CCM ilikuwa chini ya mtu mmoja - nyerere. Wengine wote walikuwa wamepandikizwa tu. Leo hii CCM ikiwa chini ya mtandao, si ni mazuri hayo jamani coz atleast kuna wengi ambao wana control, hata kama ni wa kambi fulani? Umoja wa ccm wa zamani ulikuwa wa kinafiki - ulikuwa wa chini ya mtu mmoja ambae alikuwa dikteta. ndio, pia aliweza kututengenezea maadili mazuri ya uongozi mfano kung'atuka, na pia kutokuwa mlimbikizaji wa mali. But kwa mtu smart, hivi unaweza kufanya kazi ya serikali na cheo cha uwaziri ukawa na mshahara wa shillingi elfu moja na ukaishi na familia yako? Ugumu wa kurekebisha mishahara leo upo wapi?? Hilo ndilo chimbuko la rushwa. By early 1990s, mshahara wa wazir ulikuwa haufiki laki nane. Hata ukichanganyana marupu rupu, alikuwa sana sana anapata milioni moja.

Umoja wa sasa wa kila kambi ya CCM 2005 - mfano wanamtandao etc ni umoja bora kuliko wa enzi ya nyerere in the sense that unaweza lead to kuvunjika kwa chama which is something good in itself. No wonder Nyerere said upinzani wa kweli utatokea chama cha mapinduzi.
 
Bwana mchambuzi una data nyingi sana,

Kwa mtu mwenye upeo mdogo wa fikra anaweza kukurupuka na kuona upo right kabisa,umeongea mengi sana ila inawezekana kati ya yote hayo ni o.0000001%; ambayo ni sawa na 0 tu, kuwa kwa mtazamo wako kuwa Nyerere angefanya hiki au kile Tanzania isingekua maskini. Ndio ni mtazamo wako tu,ila ukweli unabaki pale pale, kuwa Mwl Nyerere ndiye shujaa wetu aliyeipenda nchi yake, hadi leo hii kila mtanzania bado anamlilia.

Unakuja kutu-bore pale unapoleta hadithi za akina Lowassa madikteta na wezi wakubwa wanaouza nchi. Sioni ajabu kuona watu wanakuita mwajiriwa wa huyo ghabachori RA. Chonde chonde kama kweli na wewe unatumia na huyo gaidi, siku zenu zipo karibu tu. Watanzania wamewashtukia, mnanunulia kwa viji-cent mnauza nchi, moto umewaka sasa, subirini kitakochowatokea, ogopeni sauti ya umma. Wewe una ndoto za 2015 wakati Tanzania sasa tuna safari ya kuelekea Zimbabwe, hujui hili? Tafadhali bwana kasome alama za nyakati, watanzania wa leo si wa jana mzee, tafadhali.

Mbona nafsi yako inakusuta, achana na hii dhambi chafu ya kutetea haya manyang'au, acha kabisa, tena acha bwana, unajua unatutonyesha vidonda, wewe!

Unajua tumeshtukia kuna michezo michafu sanaaaaaaa katika nchi hii.
 
Mimi ni mtanzania mwenye uchungu na nchi yangu but i come from a different angle than most of you guys humu. Its that simple. Mimi sijawasema nyie mnaopinga uongozi wa sasa kwamba mmetumwa na walioshindwa kupata urais 2005. Na sitakuwa na hoja kusema hivyo. Na ndio hivyo mnapokosa hoja kwa kusema nawatetea waliopo sasa na nipo kwenye pay roll zao.

Naomba ujenge hoja za msingi kuliko kulalamika na kulia tu ovyo kuhusu nchi yako. Hiyo haitakupeleka popote. Isitoshe, na wewe inaonyesha umeingia kwenye hii discussion katikati, hujui natoka wapi na hoja zangu. Tafadhali take your time and go thread by thread then unirudie.

Asante.
 
Back
Top Bottom