Lowassa anaona mbali

Mi nina hakika Lowasa akifunguka kwa kumshushia mtu mzima zigo lake siasa za Tanzania zitabadilika saana, na anajua anachokifanya Lowasa, wengine tunasema anasubiri kupewa penati 2 afunge gori
 
Nimecheka sana juzi nilivyosikia ishu ya JKT maana nikiwa napata picha sasa ndio wametoka JKT halafu wamejiunga na chuo halafu LOAN BOARD hawajawawekea mshiko wao, yaani watatemebezewa bakora kwa kwenda mbele na polisi nao wakija wakijipendekeza nao pia wanakula mbata....mmmh nendeni JKT mje tuwatie adabu hawa
 
Lowassa hajaona mbali. Ni opportunist. Ameanza kuimba ajira ya vijana baada ya kuona matokeo ya uchaguzi wa 2010 ambapo vijana wengi hawakuipigia kura CCM. Alikuwa wapi wakati wote kutambua kuwa tatizo la ajira ya vijana ni bomu linalosubiri kuripuka? Na ili kujiweka sawa kwa 2015 ndio akataja ajira ya vijana na kuanza kutoa michango makanisani. Hana lolote!
 

kwa viongozi wote wa ccm ni nani alishaliona hili raisi kila kukicha yuko angani hajuio
matatizo ya vijana na ndio waliomuweka madarakani ,naamini lowasa ana upeo mkubwa ndani ya ccm kuweza kuongoza nchi hii sababu lowasa hataendesha nchi kiswahili
 
Kwanza ndugu yangu Mungongo wewe una elimu gani? kwa maana ni vizuri kujuana viwango vya elimu ili tuongee kwa kiwango chako cha Elimu.
Hoja hapa si nani alifanya nini hapa ni tatizo la vijana kukosa Ajira ni ukweli ulio wazi ambao hata wewe juu ya kuandika pumba hizi huwezi kuukataa, sasa kama EL aifanya lolote ama hakufanya lolote lakini tatizo hilo lipo na anajaribu kuwakumbusha hata wale ambao wanajifanya hawalioni kama wewe na hata yeye EL.
Hoja ya msingi sana hiyo utaisaidia Tanzania zaidi kama utachangia kuwa tatizo hilo lipo na ni kubwa sasa tufanyeje kukabiliana nalo hata kama aliyelisema si NEPI ama MUkwama mbovu, ama yeyote. sasa kama unayo elimu ya kutosha nenda kwenye thread nyingine ili utoe maoni yako yatakayo somwa na watanzania yawasaidie, siyo kupinga kila kitu kwa vile aliyesema siyo Nape.
Lowassa naye anazungumza Pumba tupu... Rais ataweza vipi ku create ajira kwa vijana?. Ebu tuambieni hizo ajira kwa vijana unazianzisha vipi maanake muhimu ktk maendeleo ya nchi ni kuunda policies ambazo zinawawezesha wawekezaji kuwekeza zaidi ama kufungua miradi ya maendeleo nchini, nani anapata ajira hizo sii kazi ya rais. Sasa EL atueleze ni policies (sera) zipi zinazolenga kutoa ajira kwa vijana?..

Hizi habari za kusema wazee wamechoka vijana wachukue jukumu la kuiendeleza nchi ilihali uwezo wao hautofautiani na wazee wenyewe ni pumazo la watu kuamini kwamba vijana wa leo wana uwezo zaidi wa kuongoza na uzalishaji wakati shule zenyewe matokeo yanatisha. Binafsi yangu, Hili li nchi hili, limekosa Uongozi bora, limekosa kiongozi mwenye vision ya Tanzania ya kesho tunaishi siku kwa siku na kupangiwa mikakati ya bailout na IMF. Ni jukumu la vijana kuonyesha uwezo wa kuchapa kazi, na mabadiliko hutokea bila kulazimisha wazee wataondoka pale mnapokamata mpini nasii habari zakuweka madai ilihali uwezo hamna. Mbona wanawake wanajituma wenyewe wanaanzisha miradi mbali mbali nchini?.. Leo hii kati ya magari matano mjini yanayokupita, matatu wanasukuma wanawake..Vijana amkeni msimsubiri Lowassa na kumlalamikia Mungu.

Tuna kila uwezo wa kuwa na umeme, maji safi, shule bora na Hospital zakutosha hili pekee yake ni ajira millioni kwa vijana. Lowassa akiwa waziri mkuu hakufanya lolote zaidi ya kujijenga yeye na rahisi kwake kulaumu wakati anajaribu kujisafisha kama bata maana penye tope hapakosekani maji. Nirahisi sana kwa Bata kukoga tope akifikiri ni maji na ndio usafi wa bata hivyo inatakiwa umsome Lowassa anazungumzia nini (kukoga tope) ili ujue anazungumzia usafi upi..
 
Lowassa ni Mheshimiwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM.Kwa kuwa huwezi kusukuma gari ukiwa ndani ya gari kwa vile utasukuma uzito wako mwenyewe,utakuta kwamba nafasi pekee ya EL kurudi kileleni walau kwa maana ya kuaminiwa na umma ni kufanya mambo mawili matatu:
1.Aseme kweli yote kuhusu Dowans na Richmond hususan kumtaja mmiliki wa Dowans hadharani,
2.Aseme ukweli jinsi MTANDAO ulivyomtumia kuingia Ikulu na makubaliano maalumu ya kugawana madaraka na kama kuna namna yalivyokiukwa
3.Ataje mali anazomiliki na njia alizotumia kuchumia maana na wengine wangependa kumwiga ili wapate thawabu kwa kuchangia hafla kadha wa kadha

4.EL awe kama Zakayo wa kwenye Biblia yaani awe tayari kumrudishia yeyote aliyemdhulumu MARADUFU.Kwa kuwa atakuwa ameshataja mali zake zikahakikiwa,nusu awape maskini kwa njia yeyote.Kule Italia kwenye mji wa Torino miaka ya 1400 Baada ya Kristo,kuna tycoon alijenga Chuo Kikuu kwa ajili ya MASKINI!Leo Universita degli Torino ni Chuo Kikuu maarufu sana kule Turin,kijiji cha OLIMPIKI YA MAJIRA YA THELUJI .Kama kweli anaamini katika ELIMU KWANZA na si KILIMO KWANZA, pa kuanzia ni EDWARD LOWASSA MEMORIAL FREE UNIVERSITY,
5.Kwa kuwa EL ni Mlutheri mwenzangu,aamue kuongozwa sala ya kweli ya toba na MCHUNGAJI,siyo ASKOFU,wakati wa ibada au hata kwa style ya Nikodemo-anaijua sina haja ya kufafanua toba ya Nikodemo.
6.Akitembea hatua hizi TANO ATAKUWA AMEJIVUA GAMBA !Ataweza kuikemea CCM bila kujali hali, atakuwa ameijua kweli amewekwa huru,HALELUYA!
 
Wakati EL akiwa Pm alifanya nini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira, ili awe na nguvu ya kuwasema wenzie katika hilo?

Kibanga Msese

Hata kama hakufanya ila ukweli upo pale pale na tatizo la waTz ukiwaambia ukweli wanakuwa wakali sana mfano John Mnyika jana aliposema ukweli kuhusu jk wabunge wa ccm wamekuwa wakali sana angali wanalitambua hilo ila tu hawataki waambiwe ukweli wamezoea kudanganywa na kudanganya tu.
 
aisee wanaomzungumzia lowassa nadhani hawana cha kusema. ni bora wajinyamazie tu kuliko kujisumbua na huyu kaputi
 
Ajenda ya kuwa vijana wapewe ajira, hapo yeye hayupo sawa, ila ajenda ipo sawa. EL hayupo sawa kwakuwa alikuwa na fursa yakulitekeleza hili lakini hakulifanya akiwa PM, pili pamoja na mali zoote anazomiliki ametengeneza ajira ngapi kwa vijana (sio wanae na nduguze tu) bali kwa watanzania wote?

Kibanga Msese
 
Yan umemtaja lowasa,sasa utaona jinsi ccm walivyo dhaifu.
 
Wakati EL akiwa Pm alifanya nini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira, ili awe na nguvu ya kuwasema wenzie katika hilo?

Kibanga Msese


Sawa Kabisa Lowasa atujibu wakati alikua Prime Minister, alifanya nini kwa wavijana ?? Akiweza basi wavijana watamtetea lakini asitupe hewa tumechoka. Anasema kwa sababu anataka kwa Rais nae pia sio. ZERO GRAZING
 
sasa naona kwanini lowasa anapingwa na wanaccm mle ndani,lowasa hawezi kukubali mawazo ya mwanakwaya komba au mtu kama lusinde nape na wengine wa aina hiyo.sababu upeo wao wa kufikiri ni mdogo sana,lowasa aliposema ajira kwa vijana wapuuzi ndani ya ccm walimpinga sasa kwa mlango wa nyuma wanaanzisha jkt,wanapigania ajira kwa kutumia bodaboda hili si suluhisho kwani jkt ni kuwaweka pamoja bila future ili ccm iwatumie kuiba kura na kutumia bodaboda kutorosha masanduku ya kura.hivi ma dr wote na maprofesa ndani ya ccm hamuoni huruma kwa future ya vijana wetu kwa mpango huu iwapo ccm ya akina lusinde ikirudi madarakani tutegemee ya congo,mali,misri,algeria kwani hakutakuwa na mwelekeo:frusty:


Kwa taarifa yako hao wote uliowataja ni wapiganaji wakubwa wa jeshi la Lowassa. Hujui unachoongea!
 
Kiongozi mzuri atatoka ccm (Nyerere 1995). Hata mimi nakubaliana naye kwani ukitaka kuwa kiongozi mzuri ni lazima utoke kwanza ccm, kwani ukiwa huko bado utawaondea mafisadi aibu.
 
Kiongozi mzuri atatoka ccm (Nyerere 1995). Hata mimi nakubaliana naye kwani ukitaka kuwa kiongozi mzuri ni lazima utoke kwanza ccm, kwani ukiwa huko bado utawaondea mafisadi aibu.

umeona eeeh!
 
Kiongozi mzuri atatoka ccm (Nyerere 1995). Hata mimi nakubaliana naye kwani ukitaka kuwa kiongozi mzuri ni lazima utoke kwanza ccm, kwani ukiwa huko bado utawaondea mafisadi aibu.

Usichukue nusu tu ya quote ya Nyerere. Malizia na tahadharisho alilolitoa. Alisema: "kama CCM itashindwa kutoa uongozi bora Watanzania watautafuta kwingineko." Ndicho hicho kinachotokea sasa.
 
Back
Top Bottom