Lowassa amchangia Mufti Simba 13mil

kwa mujibu wa TBC ni shule ya kiislamu ipo kigamboni ila imepewa jina la kikristo yani EDWARD LOWASSA ISLAMIC SCHOOL kweli pesa si mchezo..

Hili la jina naona amekwenda mbali; waisilamu walivyo 'sensitive', Mufti asipoangalia hiyo shule anaweza akasusiwa na waumini wake.
 
Lowasa ni mjanja sana anawekeza kabisa kwa Mufti Simba, kesho na keshokutwa akijitokeza kugombea Urais Mufti Simba, hatakuwa upande wake!
 
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1

Jamaa jizi hili then linatia geresha ati limepewa na rafiki zake .... ... hata kodi halilipi damn! hata mkiliuliza linasema lenyewe halijui maana hizo fedha hazikutoka kwake ...... ... ameruka swala la kodi la hizo fedha khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeee lakini EL kumbuka mjanja hajinyoi.
 
Kweli pesa sio mchezo, fikiria unakutana na...Rostam Aziz Catholic High School au Bin Laden Anglican Teachers College

Nafikiri hii inawezekana kwa Tanzania tu

Wakatoliki si mchezo, shule hiyo itapewa jina la mtakatifu fulani toka kwemye mabuku yao ya kumbukumbu za wenye heri, St Mary's, St Antony, St Walburga, St Yafunani, St Nyerere nk.
 
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1
Mh! Ni akina nani hao marafiki?
 
Yote tisa, kumi ajivue gamba. Nchi hii iko hivi ilivyo kwa ajili yake. Umeme huoooooooooooooooooooooooooooo kwa ajili yake. Pokeeni lakini mjiulize fedha hizo alizipata wapi wakati alikuwa mwajiliwa wa serikali. Mufti usipokee hela za mashaka au (wizi) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hapo kwenye red ni 'kwa sababu yake' sio kwa ajili yake, vinginevyo inapoteza maana!

Otherwise, ni kweli kwamba EL ni fisadi wa kipekee huwezi mlinganisha na akina Chenge, Mramba nk. Ukiondoa tabia yake ya wizi sifa zote za uongozi anazo na pengine wizi wake kupitia Richmond ilikuwa maandalizi ya kampeni 2010 kupitia mkakati wa one-term presidency!

Anajitokeza sana in public, anajiandaa 2015. Let him come, Tz ni nchi huru! Ajitokeze tena na amwage mapesa siziiti pesa haramu kwa kuwa ni pesa za walipa kodi wa Tz mimi na wewe ila ziko kwenye mikono ya fisadi.

Nawasilisha!
 
Shule hiyo ilianza kujengwa mwaka 2006 na ilipewa jina hilo akiwa waziri mkuu. Tangu wakati huo wameshindwa kuimalizia na Mufti anasema walikuwa wanahijati sh 13mil tu kumalizia. Baada ya msaada huo, wataweza kuikamilisha na wanatarijia kuanza kazi mwakani!

Subiri mwaka 2015 kura za waislam kwa Lowasa. hapo ni mahesabu makali, anajua jinsi ya kuwapata ndugu zetu hawa ni pale unapowapa mshiko tu.
 
Allah! Mungu akuzidishie baba tatizo wakristo hawapendi waislam wasome ila wewe ni kiongozi usiye na ubaguzi wala unafiki kama Sitta mara anataka uraisi kwa CCM, mara CCJ mara CCM. Big up Lowassa
 
Wanajamvi kwa mtazamo wa kiislam(kuhusika BAKWATA) fedha hizo zina utata kutokana na mtoaji. Na uislam unakataza kujiingiza ktk jambo lenye utata, hivi Mufti wa Bakwata anakosa washauri wa kumuelekeza? Ama kweli kuna wanaouza dini yao kwa dunia. Haya ni maoni yangu ya haraka haraka.
 
Marafiki zake wakuu ni Rostam Aziz(KAGODA),Andrew Chenge(RADA) na JK(IPTL)

Mimi binafsi sina tatizo na msaada uliotolewa na Mhe. EL, hofu yangu ni jinsi fedha hizo zilivyopatikana. Tunahitaji maelezo ya kutosha marafiki zake wapi waliotoa hizo fedha vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa fedha hizo ni mazao ya fisadi mablimbali ambazo Mhe. EL anatuhumiwa nazo. Tukumbuke kuwa Tsh. 13m/- sio mchezo kuzipata hivi hivi tu, kuna watu huwa wanafanya harambee kisha wanaambulia milioni 1 taslimu na ahadi milioni 2!
 
Big up lowassa
Hivi kabla ya Richmond lowassa hakuwa na hela? Acheni kutupumbaza,eti hela mara fisadi hakuna issue hapo point ya msingi ni kuwa wanamuhofia kuwa anakubalika kutokana na kupiga kazi kwa hiyo mahasimu wake wanatafuta jinsi ya kumchafua,hata richmond ilikuwa ni hadithi ya kutunga,wale makanda walokataa mitambo isinunuliwe eti ni kukiuka sheria ya manunuzi ya umma,hivi leo symbon walivyonunua hiyo mitambo ni lini sheria ya manunuzi ya umma immerekebishwa kuruhusu kununua mitambo michakavu tena?
Kweli wa tz ni wepesi kuwadanganya
 
hiyo ni molam, ili baadaye atakapoleta greda barabara inakuwa safi kama ya lami. Bila kubaguliwa na dini.
 
Mh! Ni akina nani hao marafiki?

Mmh! Isije ikawa yule mwenzetu ameomba jina lake libaki kuwa "rafiki" ili asijekuhusishwa na udini? Hii ni very calculated move; kama kweli kuna shule inaitwa Rostam Catholic School na Lowassa Islamic School then strategy yakulainisha ajenda ya udini imetimia. Let's keep on watching.
 
Back
Top Bottom