Lowassa amchangia Mufti Simba 13mil

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1
 
Huo ndio uungwana, ulichonacho unagawana na wengine.
Big up Ole Lowassa!
 
jamaa anamoyo wakutoa ila basi 2 hata mim ashawahi nitoa ofa ya gambe
 
Mmh Mmh ok, Fedha zote zimeandikwa '' Fedha halali kwa malipo ya shiling xx''.

Anazitakasa fedha za EPA.
 
kwa mujibu wa TBC ni shule ya kiislamu ipo kigamboni ila imepewa jina la kikristo yani EDWARD LOWASSA ISLAMIC SCHOOL kweli pesa si mchezo..
 
Mafisadi wananunua roho zetu kwa pipi ili tuwachie nchi waiuze kwa almasi wajaze mifuko yao!
 
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1

Yote tisa, kumi ajivue gamba. Nchi hii iko hivi ilivyo kwa ajili yake. Umeme huoooooooooooooooooooooooooooo kwa ajili yake. Pokeeni lakini mjiulize fedha hizo alizipata wapi wakati alikuwa mwajiliwa wa serikali. Mufti usipokee hela za mashaka au (wizi) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1
Hivi richmond walikuwa wanalipwa ngapi kwa siku (capacity charges)?
 
Big up Mzee Lowasa. Sio wengine kazi yao kuiba tu hata kututupia makombo hawatutupii!

Mkuu nimeipenda zaidi hiyo avator yako.

avatar46712_2.gif

"Welcome to Tanzania where you eat until you say I want to become a president"
 
Sioni tatizo kuitwa jina la mkristo Lowasa. Pengine ndiye ametoa msaada mkubwa kwa ujenzi wa shule hiyo. Tunajua wengine humu kila siku kulalamika,lakini ikifika hatua ya kuwasaidia ndugu zenu waislamu mnaingia mitini.
 
Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa amemchangia Mufti Mkuu wa Tanzania sh 13 mil kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo na shule ya watoto yatima kilichopo Kigamboni jijini DSM. Mbunge huyo amemkabidhi Mufti fedha hizo leo akisema amezipata kutoka kwenye michango mbalimbali ya marafiki zake ili kukamilisha ujenzi wa kituo na shule hiyo itakayojulikana kwa jina la Edward Lowasa.
Source ni TBC1

Mimi binafsi sina tatizo na msaada uliotolewa na Mhe. EL, hofu yangu ni jinsi fedha hizo zilivyopatikana. Tunahitaji maelezo ya kutosha marafiki zake wapi waliotoa hizo fedha vinginevyo tutaendelea kuamini kuwa fedha hizo ni mazao ya fisadi mablimbali ambazo Mhe. EL anatuhumiwa nazo. Tukumbuke kuwa Tsh. 13m/- sio mchezo kuzipata hivi hivi tu, kuna watu huwa wanafanya harambee kisha wanaambulia milioni 1 taslimu na ahadi milioni 2!
 
Back
Top Bottom