Hiki chama hakitakuja maliza migogoro hata siku moja, ni kuahirisha na kuanzisha mingine. Hapa JK anataka kufunika kombe kwa vile anajua sosi la tatizo linamzunguka mwenyewe hawezi kulikwepa. Tulizoea kusikia upande wa Nape tu aliyekuwa anawakilisha mawazo ya Kikwete sasa tutegemee Lowassa naye ataanza kuzunguka akieleza anayoyajua yeye. Kwa Lowassa kuamua kuanza kujibu mapigo badala ya kukaa kimya ni kuashiria kuwa moto mkubwa mbeleni unakuja.Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: "Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu".
Usichanganye Richmond na Dowans, haikutajwa Dowans kwenye hii habari. Tafadhali sana usipoteze mjadala.
........."kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo.
Ndio ilivyo sikio la kufa halisikii dawa, tena wamefikia hata kumwambia kaa anataka kuhama ahame wao hawatishiki. NI JK huyu huyu majuzi tu alikuwa akisema (kumuunga mkono Nape) ya kwamba wanaotakiwa kuvuliwa magamba wataondoka!.. maskini kabakia mtupu. Sasa mimi naomba sana nijue hiyo report ya kina Daud Mwakawago maadam Lowassa kaisema nadhani wananchi tuna kila haki ya kudai kujua report ile inasema nini...
Hili ndio tishio la Lowassa kwa JK kwa sababu wanajua swala hili ni wachache na Lowassa kasema kwa mafumbo ambayo JK pekee ndiye anajua kinachoendelea - Akiwa na maana mkuu wangu kumbuka tulikotoka! - Na ukiisoma vizuri hii hotuba ni kutaka muafaka baina yake yeye, Mkapa na Sumaye ili kurudisha Ufisadi wao wote kuwa chama kimoja. Lowassa amekuwa mpole kwa JK lakini mkali na mwenye matusi makubwa kwa Nape kiongozi wa chama ambaye anatimiza majukumu yake..
Wewe unafikiri Mkapa ndiyo angefanya nini...ni wale wale tu.....hebu soma kipande hiki..Hivi unafikiri ingekuwa ni Mkapa EL angethubutu kubwabwaja maneno kama hayo?
........."kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".
Hiki chama hakitakuja maliza migogoro hata siku moja, ni kuahirisha na kuanzisha mingine. Hapa JK anataka kufunika kombe kwa vile anajua sosi la tatizo linamzunguka mwenyewe hawezi kulikwepa. Tulizoea kusikia upande wa Nape tu aliyekuwa anawakilisha mawazo ya Kikwete sasa tutegemee Lowassa naye ataanza kuzunguka akieleza anayoyajua yeye. Kwa Lowassa kuamua kuanza kujibu mapigo badala ya kukaa kimya ni kuashiria kuwa moto mkubwa mbeleni unakuja.Kahangwa said:Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: "Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu".
Mkuu ni mawazo yako ukiwa mwanachama wa CCM sisi tunatazama tambala hili kutoka nje...Nape kafanya kazi alokabidhiwa na hakuwa mjinga kuinuka na kutaka Lowassa ajiuzulu pasipo kuwepo na maagizo ya kichama ama toka juu. Alipewa kazi hii makhsusi ili kumwangusha kisiasa kazi ambayo CCM ni wazuri sana kuwapa watu madaraka pale wanapojua watashindwa kutiiza..Kwanza vita kubwa ya ndani ni vijana ambao ni tishio kwa vizee vilivyokaa miaka nenda rudi nao walivyo mazuba wanakubali kuendeshwa kwa jina la bendera.Leo asubuhi katika moja ya thread inayomhusu Lowasa, niliandika kwamba Lowasa ni shujaa na mfano wa kuigwa kwa wenye upembuzi yakinifu. Amejitahidi kuvumilia hadi leo na katika uvumilivu kama binadamu kuna kikomo.
Masuala ya uongozi wa serikali si jambo la mtu moja, ila mmoja ndiye mwenye kubeba lawama. Tatizo la Umeme lilikuwa la nchi nzima na sote tulikuwa na matarajio ya kampuni iliyopata dhamani kufua umeme ingetupunguzia matatizo ya giza badala yake ndo mambo yakaharibika zaidi.
Kwa vyo vyote Mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kwa vile ndiye kichwa cha nchi na ndiye mwajibikaji number one. Kwa vile kinga ya urais kwa mfumo wa nchi yetu inavyohusudiwa kama ufalme, mwandamizi wake katika masuala ya serikali ambaye ndiye waziri mkuu alibeba lawama.
Lowasa alitumia busara na uamuzi mgumu kujiuzuru uwaziri mkuu kwa kulinda heshima yake, serikali yake na chama chake kama alivyosema, lakini uamuzi wake umetafsiriwa vibaya na wabaya wake wamepata hoja ya kusimamia. Mzee Ruksa kipindi cha Nyerere akiwa waziri wa mambo ya ndani alipata msukosuko kama huo hadi kujiuzuru na kwa heshima yake hiyo alifaulu kutetea heshima yake hadi baadaye kuwa Rais wa nchi, na kumbuka Nyerere ndiye aliyempendekeza awe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Tanzania wakati aliboronga katika moja ya wizara aliyomkabidhi. Kuna wengi walioborongo kipindi cha Nyerere lakini katu hawakuinuka tena, hii ilitokana na namna kosa lilivyofanyika na mhusika alivyopokea na kutambua kosa lake.
Makosa mengi mabaya kuliko aliyofanya Lowasa katika utumishi wake yametokea na hakuna hata mmoja aliyewajibika au kuwajibishwa, na jinsi anavyonyooshewa vidole na akina Nape si uungawana kabisa, wakati hao wanaomnyooshea vidole kichama ni wahaini kwa kuanzisha CCJ ndani ya CCM wakati hawajajivua UCCM.
Leo Lowasa ameanza kufunua baadhi tu ya yaliyofichika, na kama wasingetuliza vichwa mengi angeyatapika. Na hakuna uthibitisho wa ufisadi wa Lowasa, ila ni tuhuma ambazo hazina uthibitisha na hata kama alikosea basi si ufisadi ila uwajibikaji katika utendaji wake, na alitambua hilo na kwa hiari kutokana na msongo toka bungeni aliamua kuachia ngapi ili wengine wajipange upya.
Matokea mtoto wa Mkulima hana uwezo kabisa wa kuchukua uamuzi mzito. Kwa sasa imethibitika kwamba bora lawama kuliko fedheha. Mtoto wa mkulima ni fedheha tupu ndani ya serikali kuliko lawama za Lowasa.
Mkuu ni mawazo yako ukiwa mwanachama wa CCM sisi tunatazama tambala hili kutoka nje...Nape kafanya kazi alokabidhiwa na hakuwa mjinga kuinuka na kutaka Lowassa ajiuzulu pasipo kuwepo na maagizo ya kichama ama toka juu. Alipewa kazi hii makhsusi ili kumwangusha kisiasa kazi ambayo CCM ni wazuri sana kuwapa watu madaraka pale wanapojua watashindwa kutiiza..Kwanza vita kubwa ya ndani ni vijana ambao ni tishio kwa vizee vilivyokaa miaka nenda rudi nao walivyo mazuba wanakubali kuendeshwa kwa jina la bendera.
Halafu Lowassa kwa nini ayazungumze haya ya miaka 15 iliyopita katika mkutano wa CC hali angeweza kabisa kumkumbusha JK kwa barua ama wakiwa faragha. Kilitokea nini mwaka 1997 mbona hamsemi isipokuwa mnatuacha sisi tukisie tu kwamba JK alifanya jambo baya sana ambalo lingemwigiza matatizoni na yeye kama mshauri wa Mkapa aliweza kuyapoza.. Ati Leo asingekuwepo!...Wewe Mungu? na ndio majibu ya JK kulingana na imani yake Sii Mkapa wala Lowassa ambaye angeweza kuhukumu destiny yake..
Hii ni kashfa kubwa sana kwa rais wetu hayo makundi yenu nyuma ya Lowassa mtakuja jimaliza zaidi na beleive me JK haja solve kitu. Watanzania kwa ujumla wetu hatudanganyiki na watu wanaokitawala chama kuja vunjia heshima kiongozi wa Taifa ktk mkutano, maneno ambayo hakuna kiongozi yeyote mwenye uthubutu wa kuyasema kama sii kumtishia rais kitu gani...
Nape walitishia kuondoka na kuunda CCJ kwa sababu walipinga Ufisadi wa baadhi ya watu, leo nyie mnawakumbatia na kuwaita hawa waloona mabaya ni wasaliti.. Poleni sisi wengine tulishaondoka CCM zamani na wala hatuoni usaliti bali tunaitafuta haki na utawala unaojali maslahi ya Taifa.. Siasa za kubebana sii uzalendo wala utiifu bali ni ujinga, uroho na ulimbukeni..
Mwisho wa yote amefanikiwa kuyapata aloyataka na JK kavunja kikao cha Mafisadi na hivyo kumpa ruksa Lowassa kuanza kutimiza hasira yake maanake hamumjui huyu mtu alivyo na roho mbaya na visasi - Atawachafua kuliko kila kiti..Huyo Mtoto wa Mkulima unayemdharau ndiye kawashika wengi viongozi laa sivyo wengi wangekwisha malizwa na EL..Ni ushauri wangu tu mnaweza uchukua mama kuuacha lakini CCM haikuwa na matatizo haya kabla ya Lowassa kuwa na nguvu hii ndanio ya chama.
Mkuu mimi namlaumu JK kwa kuendelea kumpa free airtyme huyu jamaa, yaani alikuwa na nafasi mfano last year wangetoa jina lake kwenye ubunge, next kama walivyofanya kwenye kuwaondoa kwenye CC. Halafu wangemsongesha mahakamani awe bize huko. Sasa inavyoonyesha JK anaplay uungwana na huyu jambazi ambaye will stop at nothing kutimiza his personal dreams. JK amechelewa kiasi kwamba lolote litakalomtokea EL kwa sasa kuhusu tuhuma za ufisadi itaonekana JK anamwandama. Politics is so dirty!!!!!!!! Hivi unafikiri ingekuwa ni Mkapa EL angethubutu kubwabwaja maneno kama hayo?
Gamba limegoma...