palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,455
Lowassa amekana rasmi kuwa yeye hahusiki na mkataba wa Richmond!
Nanukuu:
Mwisho wa kunukuu
Hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo amedai kwamba siyo la kweli.
Chanzo: Mwananchi
Nanukuu:
"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa na kuitwa fisadi kwanini?".
"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,
"Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".
"Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"
Mwisho wa kunukuu
Hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo amedai kwamba siyo la kweli.
Chanzo: Mwananchi