Live:Taifa stars vs DRC Taifa

Mashabiki leo hawajazomea. naona wamekosa la kushangilia hadi wanashangilia vituko vidogo vidogo.
 
Congo wanatushambulia sana na wachezaji wa Tanzania wanaonekana kuchoka.
 
deokanda katukosakosa tena baada ya mpira kudakwa na kipa. tanzania wamepata faulo. wamepiga mpira ukagonga rema mabidi ambaye hadi sasa anasikilizia maumivu ya tumbo.
 
waliofanyiwa mabadiliko hawaonekani kabisa na wao wameshachoka mpira wa kipindi cha kwanza ulikuwa mzuri kuliko cha pili. yaani wanacheza kama vile hawaendi kwenye mashindano. utafikili wapo mazoezi. hawajitumili wala hawana uchu na magoli.deokanda anawachosha kwa chenga za maudhi.
 
Asante kwa kutujuza mkuu tuitakie timu maandalizi ya nguvu wakijua watakutana na black mamba mwenye njaa
 
Huo mpira niliangalia dakika za mwisho mwisho, hiyo Taifa Stars ya Paulsen hamna lolote!!

Bora tungechukua under 17 na under 20 tuwaweke pamoja tunaongeza Nizzar na Samatta kwa maendeleo ya baadae.

Huyo Uhuru Selemani ameonesha uwezo mdogo saana kila mpira anapoteza au anapiga krosi fyongo!!! Hao mabeki sasa, yaani kuna beki wa kulia alipelekwa akarudishwa eti amekaa chini kama amesusa Mkongo akatia krosi! namkumbuka sana Maximo kipindi kile Stars ilikuwa inafungwa lakini inacheza pasi kama Arsenal!

Sisi kweli ni bichwa la mwendawazimu, wameshatunyoa sana sasa wataanza kututoa ngozi ya kipara!
 
Kocha hana jipya kwa kweli.
 
Back
Top Bottom