Live:Taifa stars vs DRC Taifa

Jan 8, 2011
99
30
Mechi kati ya taifa stars na DRC inakaribia kuanza hapa uwanja wa Taifa. Nitakuleteeni live up date. Nyimbo za taifa ndo zinzpigwa na sasa wimbo wa tanzania unapigwa baada ya ule wa Congo
 
kama presha tumeshazoea....mkuu tunashukuru kwa updates., naomba uendelee kutuhabarisha
 
asante endelea kutuletea hata kama tutashindwa game la leo ndo halisi ya mpira wetu wa bongo
 
wachezaji wa tanzania wanaanguka hovyo hovyo. hawa congo wanaonekana wana afya kweli kweli yani ni mapande ya watu halafu wanachenga za maudhi. congo wana stamina kuliko tanzania. tanzania ni kama hawana mazoezi kwa jinsi wanavyo cheza.
 
javu mchezaji wa tz anajituma sana but anakosa wa kumsaidia.
 
mpira unachezwa bila ufundi wowote kwa timu zote. hii timu ya congo wachezaji 7 wanatoka tp mazembe akiwemo yule kipa anayechezesha makalio.
 
Back
Top Bottom