Yahya Mohamed
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 270
- 317
Mjadala huu uliahirihwa hadi leo kusubiri uwepo wa Mh.ZZK, yupo studio na mjadala unaendelea kwa sasa hadi saa 3 kamili asubuhi karibuni kwa michango zaidi
Habari za Ijumaa GT's
Mjadala Mkuu Ijumaa ya leo utaangazia manufaa ya uchimbaji wa Gasi, Urani na Mafuta kwa Watanzania. Katika mataifa kadhaa pailipogunduliwa rasilimali hizi adimu zimeonekana kama laana na mkosi mkubwa kufuatia matokeo ya sintofahamu baada ya ugunduzi huu.
Watanzania tutanufaikaje? Mjadala huu unakuja huku kukiwa na malumbano mazito juu ya usimamizi madhubuti wa rasilimali hii kwa manufaa ya watanzania. Serikali ishatoa tamko kuelezea juu ya malumbano haya kuwa ni upotoshaji mkubwa ambao haukubaliki na kwamba mchakato wa kuandaa sera ya usimamizi wa rasimali hizi upo katika maandalizi na utakapokamilika umma utashirikishwa kutoa maoni.
Nini Mtazamo wako na maoni yako juu ya hili?
Karibuni kwa mjadala

- Unaweza pia kutoa maoni yako katika hatua moja hadi nyingine ya kipindi, kutoka habari, usomaji wa magazeti na makala kadhaa zitakazoonyeshwa katika mkusanyiko huu wa kipindi cha Tuongee asubuhi kuanzi saa 12 kamili asubuhi mpaka saa 3 kamili asubuhi
- Wageni Dar atakuwa Buberwa Kaiza - Publish what You pay (Mpango wa kuhamasisha makampuni ya madini kutangaza kila shughuli wanayoifanya Nchini) na Hebron Mwakagenda - Mwanaharakati (Tulihijata na kutoa mwaliko wa mapema kwa Viongozi wa CDM wametujulisha saa 5 usiku kupata udhuru ). Hakijaharibika kitu mawazo na michango yenu ni ya thamani kubwa. Juhudi za kumsaka ZZK kushiriki kwa njia ya simu kutoak Kigoma zinafanyika.
Karibuni kwa mjadala