Live on Star TV: Tutanufaikaje na Uchimbaji wa Gesi, Urani na Mafuta?

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Mjadala huu uliahirihwa hadi leo kusubiri uwepo wa Mh.ZZK, yupo studio na mjadala unaendelea kwa sasa hadi saa 3 kamili asubuhi karibuni kwa michango zaidi



Habari za Ijumaa GT's

Mjadala Mkuu Ijumaa ya leo utaangazia manufaa ya uchimbaji wa Gasi, Urani na Mafuta kwa Watanzania. Katika mataifa kadhaa pailipogunduliwa rasilimali hizi adimu zimeonekana kama laana na mkosi mkubwa kufuatia matokeo ya sintofahamu baada ya ugunduzi huu.

Watanzania tutanufaikaje? Mjadala huu unakuja huku kukiwa na malumbano mazito juu ya usimamizi madhubuti wa rasilimali hii kwa manufaa ya watanzania. Serikali ishatoa tamko kuelezea juu ya malumbano haya kuwa ni upotoshaji mkubwa ambao haukubaliki na kwamba mchakato wa kuandaa sera ya usimamizi wa rasimali hizi upo katika maandalizi na utakapokamilika umma utashirikishwa kutoa maoni.

Nini Mtazamo wako na maoni yako juu ya hili?

  • Unaweza pia kutoa maoni yako katika hatua moja hadi nyingine ya kipindi, kutoka habari, usomaji wa magazeti na makala kadhaa zitakazoonyeshwa katika mkusanyiko huu wa kipindi cha Tuongee asubuhi kuanzi saa 12 kamili asubuhi mpaka saa 3 kamili asubuhi
  • Wageni Dar atakuwa Buberwa Kaiza - Publish what You pay (Mpango wa kuhamasisha makampuni ya madini kutangaza kila shughuli wanayoifanya Nchini) na Hebron Mwakagenda - Mwanaharakati (Tulihijata na kutoa mwaliko wa mapema kwa Viongozi wa CDM wametujulisha saa 5 usiku kupata udhuru ). Hakijaharibika kitu mawazo na michango yenu ni ya thamani kubwa. Juhudi za kumsaka ZZK kushiriki kwa njia ya simu kutoak Kigoma zinafanyika.

Karibuni kwa mjadala
 
Swali langu mimi ni dogo sana:

Tayari gesi imeshapatikana, inachimbwa na inauzwa; mafuta tayari yameanza kutafutwa na zipo dalili za kutosha tu labda ndani ya miaka hii mitatu (kama siyo miezi michache ijayo) ikatangazwa kuwa kuna mafuta mengi yamegunduliwa ambayo yanatosha kuingia katika uzalishaji.

Sasa, iweje tayari tuna biashara ya gesi na utafutaji mafuta wakati hatuna sera ya kusimamia sekta hizo? Waliofikiria kuanzisha biashara hizi bila sera ambazo ndio msingi wa miundo mbinu, sheria na taasisi zakusimamia walikuwa wanafikiria nini kama siyo kutaka kutengeneza fedha za haraka haraka wakati ambapo hakuna mfumo mzuri wa kusimamia?
 
Swali langu ni moja;

Kwakuwa hatuna sera ya mafuta na gesi asili lakini tumeingia mikataba 26 na makampuni mbalimbali ya utafiti, uchimbaji(uzalishaji) na uuzaji; na kwakuwa tayari baadhi ya makampuni yanauza gesi.

Kutakuwa na hasara gani ama faida gani katika uchumi wa nchi kama serikali itasitisha ama itaendelea kuingia mikataba mipya (vitalu vipya) kwa makampuni mengine wakati huu ilipoiagiza TPDC kufanya mapitio ya mikataba hiyo 26 tuliyoingia na makampuni mbalimbali?
 
Yahya, nimesikia kwamba mikataba ya zamani ya utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi itapitiwa upya, si kwa nia ya kuiboresha au kuisitisha ile ambayo haina maslahi kwa taifa, lakini lengo ni kuangalia mapungufu na kuboresha mikataba ijayo.

Je, kuipitia bila kufanya maboresho si upotevu wa rasilimali muda na fedha? Hii mbona inatufanya wananchi tufikiri kwamba tuliowapa dhamana ya kusimamia rasilimali zetu hawana nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba rasilimali zetu zinatunufaisha wote? Na Je tukifikiri kwamba kuna 10% kwenye mikataba iliyopita tutakuwa tumewaonea.

Sera baada ya mikataba kusainiwa ni kichekesho. Tutaendelea kutokuwa serious kwenye issues serious.
 
Kama tumeshindwa kusimamia dhahabu na madini mengine tutawezaje kusimamia Gesi na Mafuta?

Tuwaachie wenye kuneemeka waendelee kuneemeka!

Ushauri wangu kwa watanzania ni kubadili system ili tuwape nafasi watanzania wazalendo waweze kufanya kazi ya kusimamia raslimali zetu.
 
Yahya Mohamed,

Kama kweli viongozi wetu wanadhamira ya dhati lazima wajipange, Tanzania inaweza kunufaika na sekta ya mafuta na gesi iwapo itajiingiza katika mikataba ya kimataifa baaada ya kutengenezwa kwa sera.

Wajifunze kutoka nchi zingine wanazochimba gesi kama Bolivia, Qatar, Peru, Oman, Venezuela, kuwa na sheria yenye uwazi zinazotekelezwa na taasisi za kitaifa zenye nguvu na wataalamu katika sekta hiyo.

Na lazima mapato yanayotokana na uchimbaji wa gesi na mafuta yatawaliwe na sheria kali, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, isije kuwa kama kwenye madini serikali iliyoingia mkenge.
 
Kama kweli viongozi wetu wanadhamira ya dhati lazima wajipange, Tanzania inaweza kunufaika na sekta ya mafuta na gesi iwapo itajiingi katika mikataba ya kimataifa baaada ya kutengenezwa sera.

Wajifunze kutoka nchi zingine wanazochimba gesi kama Bolivia, Qatar, Oman, Venezuela, kuwa na sheria yenye uwazi zinazotekelezwa na taasisi za kitaifa zenye nguvu na wataalamu katika sekta hiyo.

Na lazima mapato yanayotokana na uchimbaji wa gesi na mafuta yatawaliwe na sheria kali, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, isije kuwa kama kwenye madini serikali iliyoingia mkenge.
Tunafanya postmortem, mikataba ilishasainiwa Ritz
 
Yahya,

Kimsingi inadaiwa pesa mnazosikia zimefichwa ughaibuni zimetokana na ufisadi mkubwa uliofanyika kwenye sekta hii kati ya miaka ya 2004-2006.

Endapo Zitto 'atalipuka' bungeni mwezi ujao (Oktoba) ni wazi kuwa wengi watashangaa namna ufisadi katika sekta hii ulivyoanza mapema.

Kuna haja ya kujiangalia kama taifa; tukiruhusu walafi wachache wachezee keki ya taifa tutaangamia na tutaishia kuuana.
 
Kama hatuna sera ambayo ndio mwongozo katika kuingia mkataba, hiyo mikataba iliyopo imeingiwa kwa kutumia sheria gani na ni nani aliyeamua hivyo na kwanini?

Je, atalipa fidia pale itakapoonekana ni alifanya makosa? Na asipofanya hivyo atachukuliwa hatua gani?
 
Utashi na uzalendo wa viongozi wenye dhamana ya kusimamia sekata hii ni muhimu sana.

Viongozi hawa wa sasa hata sera ishushe na malaika hawawezi kusimamia vyema rasilimali zetu hususani gas na oil,viongozi hawa wa sasa wamejawa na tamaa ya utajiri wa haraka haraka. Wanaona kuuza rasilimali za nchi kwa maslahi ya familia zao ni sahihi na moja ya sera ya uongozi wao.
 
Hizi rasilimali zinatakiwa zimnufaishe mzawa ila mara nyingi utashang'aa kwamba ndo wananufaika wawekezaji zaidi.ukiangalia sehemu nyingi zenye rasilimali utagundua kwamba kuna matatizo mengi na hili ni kutokana na sera duni zinazotumika katika uchimbaji au uvunaji wa rasilimali husika.

Angalia kinachotokea Nigeria,South Africa na sehemu nyingine zenye rasilimali hizo Pamoja na hayo nimeona baadhi ya wawekezaji wameanza kuuza migodi yao na kuondoka hapa kuna nini na penyewe?
 
Mi sioni tatizo sana kama hiyo sera itakuwa nzuri, kuna sheria kama ile ya wakimbizi ya mwaka 1998 ilitungwa kabla ya kuwa na sera ya wakimbizi lakini baadaye mwaka 2003 ndo tukawa na hiyo sera.

Nina imani sana waziri, manaibu wake na katibu mkuu kuwa kazi itakuwa nzuri tu.
 
Yahya,

Kimsingi inadaiwa pesa mnazosikia zimefichwa ughaibuni zimetokana na ufisadi mkubwa uliofanyika kwenye sekta hii kati ya miaka ya 2004-2006.

Endapo Zitto 'atalipuka' bungeni mwezi ujao (Oktoba) ni wazi kuwa wengi watashangaa namna ufisadi katika sekta hii ulivyoanza mapema.

Kuna haja ya kujiangalia kama taifa; tukiruhusu walafi wachache wachezee keki ya taifa tutaangamia na tutaishia kuuana.

Waziri wa gesi wa Bolivia miaka ya 1980 alishawahi kusema gesi na mafuta ni kinyesi cha shetani.
 
Hakukuwa na haja yoyote ya kuchimba hayo madini kabla ya kujiandaa vya kutosha. Hiyo haraka ya kuchimba bila kujiandaa ni dhahri kuna jambo nyuma ya pazia ambalo viongozi wetu watakuwa wanalijua
 
Wataalamu wetu "Wizara ya Nishati na Madini" wanapokaa kimya bila kuisaidia Serikali kuweka Sera, Miongozo, Sheria, Kanuni na mifumo itakayotusaidia Watanzania kunufaika na rasilimali zetu; Ile dhana ya Baba wa Taifa kuwa tusichimbe madini kwa vizazi vijavyo, sasa imepitwa na wakati.
 
Tatizo nchi yetu imekuwa inakurupuka kuingia katika kutaka kuzalisha kila kinachogunduliwa nchini, mwalimu Nyerere alionya hizi mali asili si emergence kutufanya tukurupuke.

Tuna misitu, vivutio vya utalii na bandari vyote vinatushinda kuvitumia ipasavyo kupata kipato, ni bora tungejikita kwanza na vyanzo vilivyopo, hayo madini na urani tuviache kwanza mpaka tujenge uwezo siku zijazo vinginevyo tunanufaisha wageni na kubakiwa na athari za mazingira kuliko faida
 
Hivi kuna ubaya gani kujifunza mazuri kutoka kwa wenzetu,kwenye madini tumefeli wakati wenzetu wanachukua mrahaba wa hadi 37% katika madini sisi bado tupo 3%.

Kwenye gesi tumeanza kwa kushindwa mfano ni mabilioni yaliyowekwa na vigogo uswis.

Mafuta ndio kabisaa hatuwezi kwani hatuna sera wala viongozi wenye nia ya dhati ya kusimamia rasilimali za taifa, mfano ni viongozi waliopitishwa na CCM juzi, hakuna ubishi kuwa CCM bado ina nafasi ya kutawala na kama viongozi wenyewe ndo hawa tumeliwa.
 
Ukweli ni kwamba hii gesi watanufaika mabepari wa Tanzania na wale wa ughaibuni.

WITO WANGU KWA VIJANA:
TUAMKE TULINDE MALI ZETU,TUACHANE NA USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA AMBAVYO NI TAASISI NA MIRADI ZA WATU BINAFSI.

KAMA NI CHAMA KWA NINI? SISI VIJANA TUSIUNGANE NA KUSAJILI CHAMA CHETU AMBACHO KITAKUWA NA SURA YA KITAIFA NA MALENGO YA DHATI YA KUWALETEA WATANZANIA MASIKINI MAENDELEO,WATU WANAKUFA NA NJAA, MARADHI, NA UMASIKINI MKUBWA HUKU SISI TUNABAKI MASHABIKI WA VYAMA VYA MATAJIRI WANAOLENGA KULINDA MALI ZAO NA KUVUNA ZAIDI.

VIJANA Ni mwenyekiti gan wa vyama vya siasa ambaye ni masikini anayejua shida zetu au wanajua kwa kuambiwa na watu!

ATAKAYEKOMBOA TANZANIA NI MTU KUTOKA FAMILIA ZA KAWAIDA hakuna bepari aliyewahi kuleta mabadiliko kwa masikini. Tuachane na wezi hawa
 
Tatizo ni mikataba ambayo tunaingia kwani haiwezi kamwe kutunufaisha sisi watanzania bali wale wanaochimba hayo madini na uranium.
 
Back
Top Bottom