Live on Star TV: Tutanufaikaje na Uchimbaji wa Gesi, Urani na Mafuta?

Kama hatuna sera ambayo ndio mwongozo katika kuingia mkataba, hiyo mikataba iliyopo imeingiwa kwa kutumia sheria gani na ni nani aliyeamua hivyo na kwanini?

Je, atalipa fidia pale itakapoonekana ni alifanya makosa? Na asipofanya hivyo atachukuliwa hatua gani?

Huyu amehujumu uchumi, sheria ya uhujumu wa uchumi haipendekezi fidia, ni mvua za kutosha na kufilisiwa.
 
Yahya,

Swala gesi, urani na mafuta yalitakiwa yasitumike mpaka tutakapokuwa na uwezo wa kusimamia kutumia wataalam wetu. Teknolojia ya nje haiwezi kuendeleza nchi, huu ni uporaji wa kawaida.

Haya ni madini nguvukazi.

Tutakapofikia kuwa na teknolojia kutumia hizi rasilimali hizi tutaanza kuagiza nje?
 
Tatizo kubwa la nchi yetu kila Kitu kina mrengo wa kisiasa! Mikataba mibovu kunufaisha wananchi watawala wachache na nchi kuendelea Kuishi kwa umaskini mkubwa
 
Kitu ambacho kila siku najiuliza, kwa nini tunaridhika na kupata kodi tu kama ndiyo stahili yetu? Hivi, watu hawa wanapochukua raslimali zetu sisi tuna stahili kodi tu?

Hata hiyo royalty ni kodi tu nayo. Kwanini tusiwe na share ya 50:50 then, wote tulipe kodi? Hatuwezi kuendelea kuwa shamba la bibi.
 
Ni kampuni moja tu ndio imesaini mkataba.
Baada ya kujielekeza waziri aliwakabidhi wajumbe hao mkoba wenye mikataba 26 ya TPDC ili waipitie na kutoa mapendekezo yao ndani ya miezi mitatu.

Alisema Novemba 30 mwaka huu atakaa pamoja nao kujadili mkataba moja baada ya mwingine.

“Hapa tuna mikataba 26 baadhi yake ni mibovu, kazi yenu ni kuipitia upya ni lazima kila mkataba ufanyiwe auditing (ukaguzi). Mtanzania la September 27
Je kampuni moja Ritz ndio imesaini mikataba 26?
 
Kwa kweli watanzania hatujawa tayari kuvuna hata kuni kama taifa ni bora tuachane na rasilimali za taifa.

Tudili na mazao, samaki, ufundi ndo vitu tunaviweza yaani vitu ambavyo tutatumia nguvu yetu kuvizalisha lakini hivi ambavyo mungu katupa hatuna ubavu navyo na mifano ni mingi.

Madini=0
Utalii=0
Misitu=0
Umeme=0

Mimi nashauri tusubiri wazalendo wazaliwe.
 
Hivi kuna ubaya gani kujifunza mazuri kutoka kwa wenzetu,kwenye madini tumefeli wakati wenzetu wanachukua mrahaba wa hadi 37% katika madini sisi bado tupo 3%.

Kwenye gesi tumeanza kwa kushindwa mfano ni mabilioni yaliyowekwa na vigogo uswis.

Mafuta ndio kabisaa hatuwezi kwani hatuna sera wala viongozi wenye nia ya dhati ya kusimamia rasilimali za taifa, mfano ni viongozi waliopitishwa na CCM juzi, hakuna ubishi kuwa CCM bado ina nafasi ya kutawala na kama viongozi wenyewe ndo hawa tumeliwa.
Si wa CCM tu hata hawa wapinzani nao ni wezi tu! Kwanini wasiandamane kupinga mradi utakao ua uhai wa watanzania kama huu au wana maslai yao? Watu hata sheria ya gasi hakuna ya mafuta na madini hovyo kabisa ila wapinzani haiwagusi, haya ndiyo maandamano tunayotaka si maneno yao ya kisiasa ambayo hayana faida kwetu.

Hata wakishindwa tutumie nguvu kuzuia huu mradi mpaka kuwe na utaratibu
 
Mimi ninachojua nikikupa nyumba yangu tupu ukiweka duka unatakiwa kunilipa kodi lakini nikikupa duka langu likiwa na mali unatakiwa kuwasilisha mauzo ili mimi nikulipe mshahara.

Kwa hili la kulipwa kodi kwenye madini yetu akili yangu inakataa.
 
Mh. ZZK Amenithibitisha punde kuwa atakuwepo Studio zetu za DSM siku ya Jumanne wiki ijayo katika mjadala huu na Mada hii tutairepost kujibu changamoto zote hizi. Hivyo tunaweza kuendelea kuchangia ili kumpa nafasi zaidi kuendelea kupitia michango hii na kuijibu yote katika mjadala huo
 
Si wa CCM tu hata hawa wapinzani nao ni wezi tu! Kwanini wasiandamane kupinga mradi utakao ua uhai wa watanzania kama huu au wana maslai yao? Watu hata sheria ya gasi hakuna ya mafuta na madini hovyo kabisa ila wapinzani haiwagusi, haya ndiyo maandamano tunayotaka si maneno yao ya kisiasa ambayo hayana faida kwetu.

Hata wakishindwa tutumie nguvu kuzuia huu mradi mpaka kuwe na utaratibu
Mwizi hata kama hajakimbizwa bado atakuwa mwizi tu,na raia kama hawajamkimbiza hawezi kuhukumiwa kwa kutokumkimbiza mwizi.

Wenye mali ni sisi watanzania na tumeshagundua mwizi wetu ni ccm tuanzie hapo, wapinzani hawana serikali, hawana dola maandamano ni haki lakini unataka tuandamane mpaka wapi na kwa lipi kwani serikali ya ccm imeshindwa kila mahali.

Tukianza na maandamano ya maadili na mikataba hatutakaa tufanye kazi.
 
Madinikazi kama chuma, mafuta, gesi na urani haitakiwi kuchimbwa waache kama wanaona TZ haitanufaika. Wawekeze kwanza katika nguvukazi na sera ya teknolojia ya jinsi ya kutumia, ndipo tuingie huko. Huwezi kutegemea wazungu.

Waendelee kuchimba vito kama dhahabu na tanzanite. Ila kwa vile hatuna mpango wa kuendelea basi tuendelee na hii.
 
Kimsingi tumekurupuka hatuna sheria,kanuni,miongozo ya mafuta,gas na urani.Tuliowapa dhamana hawana uwezo, ni dhaifu! wachumia tumbo! waganga njaa!

My take: Tanzania itaendelea kuwa shamba la bibi a.k.a kichwa cha mwendawazimu.:frusty:
 
Hello Radio Free Africa na na Jopo la Wanajukwaa!!!..

Shukrani na heshima mbele kwa wachangiaji waliochangia kabla!.

Hawa wanasiasa wa Tanzania ni wa kuangalia kwa makini sana, wameanza na dhahabu sasa baadhi ya migodi inafungwa, dhababu kwisha, tumenufaika vipi kama taifa? watakimbilia kwenye gas na mafuta sasa kutumia mwanya wa udhaifu wa kutokuwepo sheria, sera wala kanuni za uendeshaji, endeleeni kucheka nao tu, hapa itakuwa Nigeria, Angola na sehemu nyingine zenye raana ya rasilimali asili katika Africa, hawa wanasiasa wengi watoto na familia zao ziko nje na majumba mmesia na akaunti zao uswisi, ni sisi masikini ndio tutakaoachwa kupambana na polisi wanaopewa kazi za kulinda mali zetu asili ambazo zinageuzwa haraka kuwa za wageni, na huku wanasiasa kadhaa wakiwa na share ndani either moja kwa moja au indirect ni jukumu letu wote kupambana na group hili dogo la makuwadi wa ubepari kwa manufaa yao na sio kwa manufaa ya Taifa, hali ikichafuka wao watakimbilia huko nje kwa mabwana zao na kutuacha sisi tukipambana na polisi wetu (ambao ni dada zetu na kaka zetu) wao haooo ng'ambo kula upepo na familia zao.

Ni jukumu letu wote kupambana kwa moyo mmoja, Radio Free Africa, Hongera Hebron Mwakagenda, Hongera wanaharati, ni Tanzania yetu, ni nchi yetu ni jukumu letu kuilinda, anayekuja kuwekeza iwe ni kwa faida yetu na yake pia, sio haya mambo tunayoyaona kwa sasa.

Inawezekana, timiza wajibu wako,

Mawio.
 
Yahaya, mimi ninaona ipo siku watanzania tutauana juu ya hizi raslimali za madini zilizopo hapa nchini kwetu.

Kwanini viongozi wetu wanajijari wao tu? Na si wananchi wanaowaongoza? Angalia tangu tuanze kuchimba madini yametusaidia nini?
 
Gentlemen,

Uchimbaji wa mafuta umeshaanza pale Mtwara, nilikuwa huko three days ago! The guys are shipping juu kwa juu.... Kuna meli kubwa zimepaki baharini huko, zinachukua mzigo moja kwa moja... Serikali inalijua hili... So sad.
 
Ndugu Yahaya,

Ili nchi inufaike na gesi na uranium,hatuna budi kutazama na kurekebisha mapungufu yote yaliyopo katika mikataba ya madini ambayo imesababisha hadi hivi sasa nchi kutonufaika na madini kama dhahabu na almasi!!Hatuwezi kukimbilia kuanza kuchimba gesi ili hali bado kuna mapungufu ktk mikataba na sheria za madini nchini!!!!
 
Kwenye miti hakuna wajenzi! Viongozi wetu wote isipokuwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, hawana uchungu na rasilimali tulizopewa na Mungu. Nenda Buhemba jirani kabisa na Mwitongo Butiama ukaone mashimo yaliyoachwa wazi baada ya wajanja kubeba mali. Mwalimu Nyerere hakujua kama Buhemba, Nyamongo na kwingineko kuna madini?

Nchi hii imebarikiwa sana lakini hatuna viongozi wazalendo wa kuweza kulinda baraka (rasilimali) ambazo wengine hawana (isipokuwa hewa,mwanga wa jua, mvua nk) na wanazitafuta kwa nguvu zote. Madini ya Tanzanite duniani kote yanachimbwa Tanzania tu! Manufaa yake kwa Taifa yako wapi? Mwenye madini ndiye wa mwisho katika soko duniani!

Rasilimali zetu zitumike kwa manufaa ya Taifa. Tukiangalia Libiya ya wakati wa Ghadafi si sawa na Libiya ya leo. Kanali Muamar Ghadafi aliipenda nchi yake na watu wake. Mabeberu na vibaraka wao wakamwita Dikteta! Hiyo ndiyo laana itokanayo na tamaa ya rasilimali hizi. Kuna faida gani waipatayo mabeberu (wawekezaji) katika rasilimali hizi ambayo si haki kwa Mwafrika?

Sasa hivi kumekuwepo na mijadala mingi kuhusu uwepo wa Gesi, Mafuta na Uraniamu hapa nchini. Lakini sera na mikataba iliyowekwa au inayokusudiwa kuwekwa imelenga kumnufaisha nani? Kwa nini mtu akamatwe na kisha baadaye kutoroka na madini katika mazingira yenye utata bila maamuzi magumu kuchukuliwa, huku viongozi wakitoa sababu zisizo na mashiko kabisa? Watanzania kuna nini hapa?

Tayari tumeishaona baadhi ya sera na mikataba mibovu iliyowekwa kuwa haina faida kwa Taifa. Sasa viongozi mliopewa dhamana ya kuliongoza Taifa hili maskini, kwa nini mnashindwa kusema neno moja tu na roho zetu zikapona? Gesi yenyewe inayozalishwa sasa hivi haina manufaa yoyote kwa Mtanzania hohehahe katika uhalisia wa matumizi yake, iwe mjini au kijijini!

Tumwombe Mungu akiepushe kikombe hiki cha laana zitokanazo na matumizi mabaya ya rasilimali adimu tulizopewa, kwa kuzielekeza laana hizo kwa viongozi wenye tamaa ya kujinufaisha wao binafsi na vizazi vyao na si kwa Taifa. Rasilimali hizi zilindwe na kutumika kwa manufaa ya nchi kama ilivyo nchini Venezuela, Botswana na kwingineko.
 
Ni kampuni moja tu ndio imesaini mkataba.

Hata kwenye madini ya dhahabu ilikuwa hivyo hivyo.
Ilianza kampuni moja tu (Geita Gold) kusaini mikataba, na nyingine zote zikafuata kisaini mikataba ile ile mibovu !!
Hapa tumeshaporwa, viongozi washachukua 10% zao, tayari ziko Uswisi kwenye akaunti zao.
 
tatizo ni kuwa na viongozi walafi,wezi na wasiowajibika.sera mbovu chini ya uongozi wa ccm ndo tatizo.uzalendo haupo kila mtu anaangalaia afanyeje ili afaidike yeye na familia yake!
 
Gentlemen,

Uchimbaji wa mafuta umeshaanza pale Mtwara, nilikuwa huko three days ago! The guys are shipping juu kwa juu.... Kuna meli kubwa zimepaki baharini huko, zinachukua mzigo moja kwa moja... Serikali inalijua hili... So sad.
mlowapa mamlaka ya kuunda selikali ndo walolipwa binafsi kwny a/c za uswisi
 
Back
Top Bottom