Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,618
Wanabodi,
Leo ni kumbukumbu ya miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Katika Kipindi cha Kumepambuzuka ITV, mchambuzi wa mambo ya siasa, Fahami Matawili, anayazungumzia Mapinduzi hayo.
Fahami amesema utukufu wa Mapinduzi yale ni kuleta usawa kwa Wanzibari wote, kabla ya hapo, kulikuwa na matabaka, Wazungu, Waarabu, Wahindi, Washirazi na Wamatumbi, tabaka la Wamatumbi ambao ndio haswa na halisi wenye Zanzibar yao, ndio walikuwa dhalili, hawana Ardhi, hawana chochote, hawana lolote, wakati tabaka la Waarabu, ndio walikuwa na Ardhi yote, majumba, mashamba, na kila kitu. Kulikuwa na tabaka mbili kuu za mabwana na watwana. Mabwana walikuwa Waarabu, Wahindi, na Wazungu, watwana walikuwa Washirazi na tabaka la chini kabisa, la mwisho ni Wamatumbi. Hivyo utukufu wa Mapinduzi, yalileta usawa baina ya matabaka haya.
Fahami amezungumzia matunda ya Mapinduzi Matukufu ni muungano huu wetu adhimu, watwana wanamiliki Ardhi, watu wote wanapata huduma sawa za elimu, afya na fursa za maendeleo ni kwa wote, tukiwemo Watanzania bara kuwa huru kwenda Zanzibar na Wazanzibari na Wapemba wako huru kfanya shughuli zao popote ndani ya JMT.
NB. Fahami anaonekana ni Kijana mdogo, hivyo amekuja kuhadithia au kueleza kile alichoelezwa, kwa maoni yangu, media ya Tanzania, bado haijayatendea haki kabisa Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutotoa fursa popote ya kujua nini kilitokea hiyo January 12, mwaka 1964. Karibu wote wanaozungungumzia Mapinduzi haya kwenye media, ni watu wa kuhadithiwa tuu!, kwa nini media zetu siku zote zinakumbatia watu wa kuhadithiwa tuu, wakati baadhi ya waasisi wa Mapinduzi haya Matukufu, wangalipo wapo?.
Kipindi Kimemalizika.
My Take
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, bado yamezingirwa na baadhi ya mazonge mazonge fulani ambayo, its high time mapinduzi haya yawe defined crystal clear.
Nawatakia mapunziko mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali

- Ushauri kwa Uongozi wa ITV, kwenye baadhi ya mada muhimu kama hii ya Mapinduzi ya Zanzibar, wawe wanatafuta watu ambao wako deep kwenye hizi issues na sio kutuletea wauza sura. Kila alichokisema Mchambuzi huyu, mtu yoyote angekisema, hivyo there is nothing new alichotuongezea Mchambuzi huyu.
- It is high time media zetu, tuwatafute waasisi wa Mapinduzi, tuzungumze nao kuhusu nini haswa kilitokeo Zanzibar ile Januari 12, 1964, maana stories ni nyingi na ziko tofauti tofauti, wakati wengine wakiyasifu Mapinduzi hadi kuyaita Matukufu, kuna wengine wanayalaani na kuyaita mauaji ya halaiki!, ukweli ni upi?.
- Media ziende ndani Zanzibar zikazungumze na Wazanzibari na kuonyesha matunda ya Mapinduzi, watu waonyeshwe jinsi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yalivyoleta utukufu kwa visiwa hivyo.
- Pamoja na utukufu wote wa Mapinduzi haya, pia yameacha baadhi ya makovu, its high time Zanzibar takes time to heal the wounded kwa kuunda peace and reconciliation commission, watu waponyeshe vidonda vyao na kuyafuta makovu ya Mapinduzi hayo.
- Mwisho, essence ya kitu chochote, inatokana na wakati husika, kwa mwaka ule 1964 kulikuwa na haja ya kufanyika mapinduzi yale, lakini leo miaka 54 baadae, jee sababu za mapinduzi yale bado zingalipo?, bado kuna sababu za serikali ya Zanzibar kuendelea kuitwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, au baada ya mapinduzi yale, sasa serikali ya Zanzibar ni serikali ya kidemokrasia iliyochaguliwa na watu na sio mapinduzi Daima.