List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

There is no way mtu akakaa sehemu sensitive kama ile for more that 10 years mtegemee awe mwadilifu.
Hayo ndo mazara yake amekaa mda mrefu sana pale na wanomuweka wana maana yao ambayo ipo siku iyo maana itawatokea puani
 
Hakuna aliyefungua kesi hadi hivi sasa kwa upande "wao" isipokuwa "wamewaagiza" mawakili wao kufuatilia...

Hiyo ni danganya toto basi, kwanini wanajiwahi kusema kabla ya kufungua kesi zenyewe? Na hisi wanatoa vitisho wasiandikwe!

Acha tusubilie tuone mwisho wake, Ila natamani wawahi kuzifungua hizo kesi ili kila kitu kiwe wazi na hiyo mikataba yao ya siri iwekwe wazi tuyaone madudu yote walio tufanyia!
 
Waache waede mahakamani tukawaone vizuri mafisadi hawa na kila kesi ikiwa mentioned tunaenda pale na kuwazomea wao na mawakili wao.
 
Vuguvugu hili limenikumbusha mapinduzi ya Rumania, maana yalitokea ni baada ya muda mfupi tu Mzee Shaushesho kushinda kwa speed tsunami na kila kona wakishangilia jina lake. Sasa kwa hali inavyokwenda Tanzania wakifanya makosa hasa JK na RO msistaajabu wananchi wakavamia nyumba za mafisadi hasa ya BWM. Kwa sasa RO anatakiwa kumpa ulinzi wa masaa 24 Dr. Slaa maana akidhurika na chochote hata kama ni bahati mbaya moto utakao ulipuka hautazimika. Jasusi upo?
 
nadhani kuna kitu prof.Chachage alitaka kutuambia kwenye kitabu chake cha makuwadi wa soko huria,binafsi nilisoma uchambuzi wake tu,lakini kitabu sijakisoma.leo nakitafuta nijue mle ndani alikua anasema nini hasa.
LAITI KAMA ANGEKUWEPO..................(Sijui ingekuwaje)
 
Mwache aende kwa pilato kama atatoka huu ni mtego wa panya ataingia aliyekuwemo na asiyekuwemo naona mpaka mzee kingunge naye atakuwemo katika hao mafisadi pengine slaa kamuonea huruma maana angemtaja basi ss hv tungelikuwapo makaburini kumzika.
 
Naamini tutapata mengi wakienda mahakamani. Hivi hawa magaidi wana akili timamu? Gazeti limewanukuu akina Dr. Slaa sasa wanalishitaki kwa misingi gani? Kama si ulimbukeni? Jamani Nyerere si afufuke tu aone hii minyang'au inavyotafuna nchi kama mchwa!!!!! Naamini bado anaendelea kumuomba Mungu aendelee kuiadhibu mmoja baada ya mwingine.

Hii hata mimi imeniacha hoi na kampuni iliprinti gazeti jamaa analishitaki.
Au ndio maana blogger wetu wa kitanzania hawaandiki chochote kuhusu BUZWAGI wanaogopa nao kushitakiwa.
 
....lakini uzuri wa haya mambo hakuna major figure inayoongoza hili sakata ni wananchi kwa ujumla na mbona hakuna gazeti ambalo liko mbele...waliingia kwa kishindo cha 80% lakini naona wakitoka kwa tsunami ya 90%
 
Mbona leo hata kwenye blog ya michuzi hakuna kitu, ama huyu jamaa kazungumzia kitu gani jamani ?

Niko na mcheche wa kumsema niliwahi kuandika siku moja juu ya uraia wa huyu jamaa, nasubiri alichosema.
 
Hii hata mimi imeniacha hoi na kampuni iliprinti gazeti jamaa analishitaki.
Au ndio maana blogger wetu wa kitanzania hawaandiki chochote kuhusu BUZWAGI wanaogopa nao kushitakiwa.


Kwa taarifa yako, gazeti ni shahidi no.1 wa mtuhumiwa, ndio maana mh. mmoja alisema asingejibu vitu vilivyoko hewani ambavyo hafahamu... mpaka waone kwa maandishi na ndivyo hivyo yametokea magazeti makini yaliepuka hilo yanajua joto ya jiwe yake!!!
 
Lakini bado hatujapata latest pls, jamani kama kuna mwenye details nini alichosema fisadi pls atujuze.

Na bado mwaka huu ni wa kwao na kama kuzaa watazaa tu
 
Naambiwa kuwa huyu naye ametishia kumfikisha Dr.Slaa mahakamani, je?hii ni mbinu ili kuwaonyesha wafadhili kuwa huu ni uongo na ndio maana wanasema kuwa wataenda mahakamani?

Nawawekea pepa ya DR. SLAA aliyowasilisha kwa wafadhili ili muweze kuuona na kuujadili ushahidi wake juu ya hizi tuhuma, sijui nianzishe thread mpya hii iwe ni kwa wale wenye uwezo wa kutuchambulia mambo ya ushahidi , natafakari.
 
weka humu humu ila kama itakuja na heading mpya na itahitajika uchambuzi wa kiujumla nakushauri anzisha thread
 
Naambiwa kuwa huyu naye ametishia kumfikisha Dr.Slaa mahakamani, je?hii ni mbinu ili kuwaonyesha wafadhili kuwa huu ni uongo na ndio maana wanasema kuwa wataenda mahakamani?
...anyway 'pride comes before a fall' - you will see
 
Waungwana,

Inaelekea ule msemo wa kifo cha nyani miti yote huteleza unajionyesha wazi hapa nyumbani. Yaani siwezi amini kuwa baada ya ile circus ya jana ya Karamagi na waandishi ambayo kwa taarifa ni kuwa alijipeleka kinyume na ushauri wa wengi bado Mzee makini kama Mgonja naye anaweza kuingia mkenge. Angalijua bomu lingene linalokuja ambalo kamwe hawezi kujinasua sidhani kama angefanya kosa hili la kujiweka katika spotlight.

Kuna taarifa kuwa nyang'au mkuu alitaka kuwasweka kina Zitto ndani akichukulia mwanya wa mwenyenchi akiwa nje lakini kabla ya kutekelezwa mwenye nchi akamshukia na mvua na kuwaarifu waliotwa manyang'au wote wajisafishe wao bnafsi bila ya kutumiwa mabavu ya dola. Na huu ndio ulikuwa msimamo wa Karamagi jana kuwa yeye alikuwa pale kama Karamagi binafsi na anajisafisha yeye binafsi ingawa katia statement yake amejitambulisha kama Waziri wa Nishati na Madini.

Inaelekea UTATU HARIBIFU unabomoka kwa mwendokasi wa mwanga....

Tusbiri kesho nini kitajiri....maana siku hizi ni uloda tu kwetu sisi wambeya wa kisiasa...

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom