List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

duh!!!
Hii mbona inanichanganya.

Mkono kajisafisha kisanii sana matokeo yake kajikuta anaface defamation worth Tshs 10 bn, Karamagi kajisafisha matokeo yake ananuka hata kumsogelea haifai, Chenge yeye kadai hawezi kujibu "utumbo", pia mkumbuke kuwa Karamagi alisema kuwa hawezi kujibu kwani hakuwa amepata taarifa rasmi za kutuhmiwa, I wonder kwa nini jana waandishi hawakumuuliza kama tayari kapata tuhuma rasmi, wengine bado wanapiga danadana tu, pia Kingunge si alisema kuwa wawapuuzie wapinzani na serikali /ccm hawawezi kudeal na "ujinga" wa wapinzani? Hii inaashiria nini ndugu zanguni wapendwa? Sijui che nkapa atasema nini.

The drama still unfolds na tutaona mengi na kusikia zaidi, bora Sokoine na Nyerere walijipumzikia zao mapema...
 
Nafikiri sababu wamesema washika makali "DONORS" hivyo lazima kila mtu atoke kivyake ingawa ni ki-usanii
 
Tuendelee kuwazomea kila waendako. Hakuna kwa kukimbilia mwaka huu.

Neno la Mafisadi linafaa kweli kweli.
 
Sijui huyu naye atasema lipi kwani kama ni suala la ufisadi wa BOT basi huyu ndio wa kukamatwa kwani ndio muidhinishaji mkuu wa fedha na malipo yote ya serikali.

Natamani naye aseme kuwa ataenda mahakamani ili kuweza kujipatia ukweli kwa ulaini zaidi kwani ataulizwa je? Ni kweli zimelipwa ama siyo.

Nasubiri kupata yaliyojiri huko.
 
nafikiri kwa speed hii, kitalelweka. Lets all continue to take interest in our country and rights. Tuhamasishane, kila mtu kwa nafasi yake ili hawa watu wasiendelee kusema au kuwaza kuwa '...watanzania kazi yao kupiga kelele kwa siku mbili halafu wanasahau..'! This time let it be the time for real change. ALUTA CONTINUA!!
 
Taratibu tunakaribia kufumbua kitendawili. Lakini tatizo hakuna hata gazeti moja lenye mlengo wa kushoto kuweza kutupatia habari mbadala.

God is with us
 
duh!!!
Hii mbona inanichanganya.Mkono kajisafisha kisanii sana matokeo yake kajikuta anaface defamation worth Tshs 10 bn, Karamagi kajisafisha matokeo yake ananuka hata kumsogelea haifai, Chenge yeye kadai hawezi kujibu "utumbo", pia mkumbuke kuwa Karamagi alisema kuwa hawezi kujibu kwani hakuwa amepata taarifa rasmi za kutuhmiwa, I wonder kwa nini jana waandishi hawakumuuliza kama tayari kapata tuhuma rasmi, wengine bado wanapiga danadana tu, pia kingunge si alisema kuwa wawapuuzie wapinzani na serikali /ccm hawawezi kudeal na "ujinga" wa wapinzani? Hii inaashiria nini ndugu zanguni wapendwa?Sijui che nkapa atasema nini.

The drama still unfolds na tutaona mengi na kusikia zaidi, bora Sokoine na Nyerere walijipumzikia zao mapema.

Na kweli hii drama ndio bado mbichi kabisa.

Sijui huyu naye atasema lipi kwani kama ni suala la ufisadi wa BOT basi huyu ndio wa kukamatwa kwani ndio muidhinishaji mkuu wa fedha na malipo yote ya serikali.

Natamani naye aseme kuwa ataenda mahakamani ili kuweza kujipatia ukweli kwa ulaini zaidi kwani ataulizwa je? Ni kweli zimelipwa ama siyo.

Nasubiri kupata yaliyojiri huko.

Sasa wezi wanafikiri wanaweza kuteteana. WTZ ni watu wenye huruma lakini hiyo huruma imekwisha kutokana na viongozi kutuona hamnazo. Dar hivi sasa hapakaliki.
 
Hivi huu si upuuzi kila mmoja atakanusha tu bila hoja. Hamna kipaya wanachoweza kutuambia. Bado hawajajibu hoja za msingi. Naamini nayeye atakimbilia mahakamani. Kusema kweli hii Migaidi ya Kiuchumi haina jipya. Comrade Mpayukaji!!!!!
 
Habari nilizozipata sekunde chache zilizopita ni kuwa Mgonja na yeye ameamua kwenda mahakamani na licha ya kumshtaki Dr. Slaa atalishtaki gazeti la Mwanahalisi Pia. Stay tuned
 
Naamini tutapata mengi wakienda mahakamani. Hivi hawa magaidi wana akili timamu? Gazeti limewanukuu akina Dr. Slaa sasa wanalishitaki kwa misingi gani? Kama si ulimbukeni? Jamani Nyerere si afufuke tu aone hii minyang'au inavyotafuna nchi kama mchwa!!!!! Naamini bado anaendelea kumuomba Mungu aendelee kuiadhibu mmoja baada ya mwingine.
 
Habari nilizozipata sekunde chache zilizopita ni kuwa Mgonja na yeye ameamua kwenda mahakamani na licha ya kumshtaki Dr. Slaa atalishtaki gazeti la Mwanahalisi Pia. Stay tuned

Hivi hakuna sheria inayo sema kesi ikiwa mahakamani swala hilo lisizungumzwe?

Nahisi wanatafuta jinsi ya kunyamazisha vyombo vya habari!
 
Hakuna aliyefungua kesi hadi hivi sasa kwa upande "wao" isipokuwa "wamewaagiza" mawakili wao kufuatilia...
 
Back
Top Bottom