Lissu kama una lengo la kweli la kushinda Urais 2025, basi njia hii hapa...

You don't know him at all. Lissu ndiye mpinzani wa kweli kwenye hii nchi. We will count a substantial number of decades before getting another Lissu. Trust me. Lissu anaweza kushinda urais 2025 landslidely. Watanzania niligundua wanampenda sana Lissu kuliko CHADEMA. I personally love him and not his party.
Mkuu unaposema kuwa Lisu ndio mpinzani wa kweli kwenye hii nchi unamaanisha nini? Ebu tuangalie kati ya maneno yako na ya kwake mwenyewe. I mean kabla na baada ya ujio wa Lowasa Chadema ili tujirizishe kama kweli Lisu ni mkweli au ndo wale wale wanaopambania matumbo yao.

images (7).jpeg


images (12).jpeg


images (11).jpeg
 
Jitu linawapanga wakurugenzi halafu linawapiga biti olewako umtangaze mpinzani kashinda uone utakavyonyolewa nywele za sehemu zote za mwili kwa msumeno halafu useme kuna uchaguzi hapo

Kuweni serious kidogo , upinzani tz ulipitia kipindi kigumu sn chini ya nduli
 
..Hapo nadhani umetuonea.

..Chadema wanapendekeza kipengele kinachowalinda viongozi wakuu wasishitakiwe kiondolewe.

..Msimamo huo unaonyesha kwamba Chadema wanaamini viongozi yeyote anaweza kufanya makosa, na wanataka akifanya makosa awajibishwe.

..Labda nikuulize mwana-CCM. Kwanini unaunga mkono kipengele cha katiba kinachozuia viongozi kushtakiwa ikiwa wamefanya makosa, madudu, au mauza-uza?
😂😂😂 Mm sio mwanaccm wala sina chama na sio watu wote wanaoipinga chadema au chama flan bc ni wanachama wa chama flani. Mm naona ni sawa viongozi wakifanya ujinga washitakiwe
 
Kwanza kabisa napenda kuwasalim wana jf wenzangu mliopo humu. Ama baada ya salam, niende sasa kwenye mada. Ndugu zang leo nimekuja na ushauri, au njia mbadala itakayomsaidia ndugu yetu Lisu na chama chake kuingia Ikulu kiulaini kabisa bila kutumia katiba mpya, tume huru, wala maandamano yoyote yasiokuwa na tija. Njia hizo ni...

(1) Kwanza arudi nchini kukijenga chama na kuendeleza mapambano ya hoja, na kusimamia sera za chama kikamilifu ili kutupa imani kuwa mpambanaji wetu kaamua kusimama na sisi katika nyakati zote za shida na raha kama vile kina mzee Nelson Mandela, Robert Mugabe, Hakainde Hichilema na wengine wa aina hiyo ambao waliweza kupata ushindi wa kuongoza nchi zao kupitia sera zao na mapambano yao ya ndani.

(2) Abadili aina ya siasa zake kutoka katika siasa za chuki, hasira na visasi, hadi katika siasa za upendo, umoja, mshikamano na uvumilivu. Haiwezekani ugomvi wake na hayati Magufuli, au ugomvi wa chama chake na CCM uufanye kuwa ugomvi wa taifa. Yan aufanye ni ugomvi wa watanzania wote dhidi yake au dhidi ya chama chake. Mpaka kufikia hatua ya kuwaomba wafadhili wetu watunyime kabisa misaada ya pesa ambazo huwa zinasaidia kuboresha elimu yetu kwa manufaa ya watoto wetu, au kusaidia kununua madawa kwa ajili ya afya zetu na za watoto wetu nk.. Kibaya zaidi alitaka tuwekewe na vikwazo, ili sisi wenzangu na mimi tusijaribu hata kupata fursa ya kufanya biashara zetu nje ya mipaka ya nchi yetu. Hii ilishangaza sana watanzania kuona mtu mwenye elimu kama Lisu anawezaje kufanya maamuzi ya kipuuzi, na kikatili kwa nchi yako na watanzania wenzako namna ile. Omba msamaha kwa hili, nina imani utasamehewa na kura utapewa.

(3) Ajaribu kuwa na misimamo thabiti isiyoyumbishwa na mtu yoyote, mwenye chochote. Sio leo atuambie hivi afu kesho abadilishe kauli yake atuambie vile, hiyo ni sawa na unafiki, uongo au uzushi. Lazima ajue kuwa siku zote ukweli hujenga, na uongo hubomoa.

(4) Awaombe msamaha wanachadema na watanzania waliomuamini, kwa kitendo chake cha kuwadanganya, na kuwachukulia kama wao ni maboya wasioweza kutumia hata kilo nzima ya akili zao kujua ukweli na uongo wa kauli zake, kama tunavyoona pichani.

(5) Mwisho namshauri ili aweze kujenga siasa zenye malengo, basi akamtafute ndugu Hakainde Hichilema amfunze siasa za kweli. Huu ndio ujumbe wangu kwake, najua hapa kuna wapambe wake watamfikishia. Unajua dunia ya sasa mtu anaweza asikupe chakula, lakini akakuonesha njia nzuri ya kukipata hicho chakula. Na kuna mtu anaweza akakupa chakula lakini akakataa kata kata kukuonesha njia ya kukipata hicho chakula.

Asanteni sana!
Hz zote propaganda za mtoa post point hapa kinachotakiwa ni tume huru ya uchaguzi pamoja na katiba mpya huo ndo mwisho wa ccm
 
Hz zote propaganda za mtoa post point hapa kinachotakiwa ni tume huru ya uchaguzi pamoja na katiba mpya huo ndo mwisho wa ccm
Mbowe, Zito, Lisu na wabunge wengine zaidi ya 100 wa upinzani washawahi kushinda ubunge kwa zaidi ya miaka 10 kupitia tume hiyo hiyo mnayojaribu kuikataa. Hii inashangaza sana aisee!
 
You don't know him at all. Lissu ndiye mpinzani wa kweli kwenye hii nchi. We will count a substantial number of decades before getting another Lissu. Trust me. Lissu anaweza kushinda urais 2025 landslidely. Watanzania niligundua wanampenda sana Lissu kuliko CHADEMA. I personally love him and not his party.

Watanzania gani mkuu
 
Mr Dudumizi ,

..kwenye suala la vikwazo umemtupia TL lawama asizostahili.

..kama nchi hii itawekewa vikwazo basi itakuwa ni kwasababu ya udhalimu na ukatili wa serikali ya CCM.

..nakumbuka 2016 tulifutiwa misaada ya mpango wa Millenium Challenge ya Marekani kwasababu serikali ya CCM iliharibu uchaguzi wa Znz.

..msaada huo ulifutwa bila kiongozi au mwanaharakati yeyote wa upinzani kuwaomba Wamarekani wachukue hatua hizo.

..Siyo kweli kwamba nchi wahisani zinasubiri wapinzani wakaishtakie CCM na serikali zake ili Tz iwekee vikwazo.

..Pia, ukali wa vikwazo na muda wake utategemea na mienendo ya serikali ya CCM na siyo mashinikizo ya wapinzani kwa wahisani.

..Zaidi, vipo vikwazo maalum / "TARGETED SANCTIONS" ambavyo huelekezwa kwa watu au taasisi maalum serikalini ili kupunguza uwezekano wa wananchi wa kawaida kuathirika na vikwazo.
 
Aaa wapi, yaani unadhani hatujui uhalisia? Au unataka mpaka yatokee machafuko ndio ujue watu wameichoka hiyo ccm? Hii kauli yako ni kama unataka kuhalalisha machafuko kuwa ndio dalili kuwa watu wamechoka. Ukishaona box la kura haliheshimiwi, hiyo ni dalili tosha kuwa chama kilichopo madarakani kimepoteza ushawishi.
tz hakuna chama Cha upinzani wa dhati. Ila Kuna vyama vya wasakatonge.
 
Chadema mlisema nchi inatakiwa impate dikteta ili isonge mbele, akaja Magufuli mkasema amezidi Bila shaka huyu mama ndio size yenu
Kwahiyo kuuwa, kupiga risasi watu,kuwapa watu kesi zisizozakweli ndio uongozi bora?

Kwani magufuli nchi ameifikisha waapi kimaendeleo?

Mlimpangia miaka mingi ya uongozi lakini Mungu akawapangulia na leo hii ameshaoza.
 
Ataomba ulinzi serikalini, na serikali itamlinda bila wasi wasi. Kuhusu ishu ya case hayo ni mambo ya mahakama, kama kesi inayomkabili haina ushahidi basi atashinda tu wala haina haja ya kuukwepa mkono wa sheria.
Ulinzi ameomba kabla ya shambulio lá kutakakumuua na baada na serikali hakuna walichpfanya kiifupi nikwamba ccm na serikali yake ndio waliotakakumuua ndio maaana hakuna chochote kilichofanya na serikali baada ya tukio hilo.
 
Dada dudumizi09 . Ushauri wako no. 4 haufai na hata zingine zina mushkel. TAL hakuwahi kuwa mtoro wa nchi hii mpaka mlipodhamiria kumuua. Na wenye dhamana na ulinzi & upelelezi wa kesi yake. Wanailemaza maksudically . Waliodhamiria kumuua wengine bado wanayo mamlaka na hawakuwajibishwa. Atarudi Je?!. Tofautisha wakati wa uchaguzi alikuwa akilindwa na Tiss. Leo hana ulinzi mdomoni mwa mamba wenye kiu na damu yake .

Ccm inaweza kushindwa hata na nld kama tu tume itakuwa huru.
CCM inaweza kushindwa hata na mgombea huru/binafsi kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki.
 
Back
Top Bottom