Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi bungeni, alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akiulizwa maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma jana.
Alisema Katiba inakataza mtu ambaye ni afisa mwandamizi katika utumishi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuwa mbunge ama inamnyanga sifa yule ambaye ameteuliwa kuwa afisa mwandamizi kwenye utumishi wa serikali kuendelea kuwa mbunge.
Alisema kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao wamechaguliwa wakiwa wabunge na kwa hiyo wananyanganywa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Alihoji kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu wakuu wa mikoa na wilaya hao kuendelea kuja bungeni wakati ni maofisa wa serikali.
Akijibu Pinda, alisema hana uhakika na linalosemwa kama ndio lilivyo. Lakini kama ndivyo lilivyo bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo hapa analisikia atalifanyia kazi.