Lissu atifulia vumbi Serikali kukiuka katiba wabunge walio RC/DC kuendelea na ubunge

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
images


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amesema kitendo cha wabunge wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuendelea kuruhusiwa kushiriki katika vikao vya Bunge ni kinyume cha Katiba.

Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi bungeni, alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akiulizwa maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma jana.

Alisema Katiba inakataza mtu ambaye ni afisa mwandamizi katika utumishi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuwa mbunge ama inamnyanga sifa yule ambaye ameteuliwa kuwa afisa mwandamizi kwenye utumishi wa serikali kuendelea kuwa mbunge.

Alisema kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao wamechaguliwa wakiwa wabunge na kwa hiyo wananyang’anywa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Alihoji kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu wakuu wa mikoa na wilaya hao kuendelea kuja bungeni wakati ni maofisa wa serikali.

Akijibu Pinda, alisema hana uhakika na linalosemwa kama ndio lilivyo. “Lakini kama ndivyo lilivyo bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo hapa analisikia atalifanyia kazi.”
 
Hilo liko wazi kwani katiba hii ya nchi nimbovu vitu viwili moja haifwatwi maana wanaojiita wakubwa wanaivunja na pili ni kwamba imepitwa na wakati kabisa.
 
Safi sana Lisu....

Nchi hii serikali yetu kana kwamba haina wataalamu wa sheria. Hoja ya Lisu imekamilika, lakini serikali itakubali kosa hilo au itatafuta hoja ya kuhalalisha kosa liendelee kuwa sheria?


[h=2]Lissu: Ma-RC, DC watimuliwe bungeni[/h]MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lisu (CHADEMA), ameibana serikali na kuitaka kuwatimua bungeni wabunge ambao ni wakuu wa wilaya na mikoa kwa kuwa wapo kinyume na Katiba.

Lisu alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kuongeza kuwa wakuu wa wilaya (DC) na wakuu wa mikoa (RC) ni maofisa waandamizi wa serikali, hivyo hawapaswi kuwapo bungeni.

Alisema Katiba ilivyo sasa inakataza ofisa mwandamizi wa serikali kuwa mbunge na kuhoji ni kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu watu wa aina hiyo kuwapo bungeni.
"Kuna wabunge wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na mikoa, hivyo wamenyang'anywa haki yao ya kuwa wabunge, kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu watu wa aina hii kuwapo bungeni wakati ni maofisa waandamizi wa srerikali?" alihoji.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, alisema kwa jinsi anavyofahamu utaratibu huo unamhusu mtumishi wa serikali (Public Servant) lakini DC na RC ni watendaji wa kisiasa, si moja kwa moja maofisa wa serikali, hivyo anaamini kuwa hawajakosea.
Katika swali la nyongeza, Lisu alisema katika Katiba ya mwaka 1965 ilieleza kuwa DC na RC si maofisa waandamizi wa serikali, hivyo waliruhusiwa kuingia bungeni, lakini baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1992 suala hilo liliondolewa, hivyo kuwaomba wataalamu wa sheria waliopo serikalini kulifanyia kazi suala hilo.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu alisema kuwa tafsiri inayotolewa na mbunge huyo si kama wao wanavyoitumia na kusisitiza kuwa suala hilo watalifanyia kazi, ili ukweli upatikane na baadaye serikali kulitoea kauli.
"Vingunge wenzio wanaojua madudu haya watalifanyia kazi na tutalitolea tamko, lakini bado naamini Waziri Mkuu hajakosea sana."

Wakati huohuo, serikali imesema inapitia upya mikataba ya wawekezaji mbalimbali na watakaobainika kushindwa kufuata mikataba wataivunja, ili wapewe watu wengine.

Pinda alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyehoji serikali inatoa tamko gani kwa wawekezaji wasiozingatia mikataba.
Alisema hakuna mwekezaji anayeruhusiwa kuingia moja kwa moja katika maeneo ya vijini kama hakuna ridhaa ngazi ya taifa.

"Utaona katika maeneo ya ardhi hilo halifanyiki, labda kama umepita katika mkondo tulioridhika ambao utawanufaisha wananchi, pengine kuna kupuuzwa kwa agizo hili. Tutafuatilia suala hili," alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, alisema kipengele cha dini kimeondolewa katika sensa kwa kuwa hakina tija kwa maendeleo ya nchi.

Alisema miaka ya nyuma kipengele hicho kilikuwapo, lakini kiliondolewa, ili kuondoa hofu ya kutokea mgogoro.

Pinda alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Susan Lyimo, aliyehoji kwa nini serikali imeondoa kipengele cha dini.


 
Bravo kamanda wangu mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni.

Tundu Lisu nakukubali sana mkuu nakuomba uendeleze mapigano kwa kwends mbele.
 
Daaah jamaa ni jembe hile mbaya
nilikuwa naangalia alivyo mbana lukuvi.
 
Subirini tu mtasikia suala hilo haliruhusiwi kujadiliwa maana liko mahakamani! Hii ndo TZ yetu bana, ni zaidi ya tunavyoifahamu!! Lol!!!
 
Serikali dhaifu haiwezi kuwa na uwezo wa kusimamia sheria. Vua gamba, vaa gwanda
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumjibu Lissu ndani ya serikali ya dhaifu!
Sio Pinda wala Werema.
 
images


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amesema kitendo cha wabunge wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuendelea kuruhusiwa kushiriki katika vikao vya Bunge ni kinyume cha Katiba.

Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi bungeni, alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akiulizwa maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma jana.

Alisema Katiba inakataza mtu ambaye ni afisa mwandamizi katika utumishi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuwa mbunge ama inamnyanga sifa yule ambaye ameteuliwa kuwa afisa mwandamizi kwenye utumishi wa serikali kuendelea kuwa mbunge.

Alisema kuna wakuu wa wilaya na mikoa ambao wamechaguliwa wakiwa wabunge na kwa hiyo wananyang’anywa sifa za kuendelea kuwa wabunge.

Alihoji kwa nini serikali inaendelea kuwaruhusu wakuu wa mikoa na wilaya hao kuendelea kuja bungeni wakati ni maofisa wa serikali.

Akijibu Pinda, alisema hana uhakika na linalosemwa kama ndio lilivyo. “Lakini kama ndivyo lilivyo bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo hapa analisikia atalifanyia kazi.”

Kamanda lissu unazidi kuwafumbua macho watanzania hili ulilizungumza wakati ukiwasilisha hotuba yako kama waziri kivuli wa sheria na katiba lakini wakalipotezea,leo tena umegonga Pm na ameonyesha kujichanganya lissu wewe wapakaze pili pili mikononi then wao wataizambaza machoni wenyewe.
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumjibu Lissu ndani ya serikali ya dhaifu!
Sio Pinda wala Werema.

Werema analo jibu rahisi kwa Lisu kwamba ana kichwa ambacho kazi yake ni kuotesha nywele zake lakini hakitumiki kwa kazi nyingine ya kufikiri.

Kuishiwa hoja nako mtu kama Werema anaishia kutapika nyongo kama hizi hadharani bila aibu.
 
Pinda kusema hana uhakika na alichokiongea mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani mbungeni Mh. Tundu Lusu ni kutudanganya sisi wananchi maana katika aliyoisoma lisu ndo hiyohiyo anayoitumia Pinda sasa iweje asifahamu kama mkuu wa wilaya/mkoa kuwa mbunge ni kosa kisheria
 
Pinda awamu hii kaogopa kujibu moja kwa moja kwani amechoka kuitwa muongo.
 
Wakuu
Swali langu hili limetokana na kile kilichojili bungen kwenye maswali ya papo kwa papo pale mhe Tundu lisu alipokuwa akihoji uharali wa wabunge ambao ni wakuu wa mikoa-RC na wakuu wa wilaya-DC kuendelea kuwepo bungeni hali ya kuwa ni maofisa wandamizi wa serikari,swali ambalo mhe waziri mkuu,mhe pinda alijibu kuwa wale si maofisa waandamizi bali ni viongozi kisiasa,Kipi ni sahihi ktk hili.Je mhe Lissu yupo sahihi au mhe pinda yupo sahihi
nawasilisha
 
Hili liko wazi. katika Katiba ijayo, hata Mawaziri hawatakuwa wabunge tena!!!

Zaidi ya hapo kwa nini wawe wao tu? Mbona nchi ina watu wengi kwa nini wasipeqe hiyo ajira wengine?
 
Hivi hapa lisiloeleweka ni nini ?
66. (3) Where a Regional Commissioner is elected a Member of Parliament representing a constituency or where a Member of Parliament representing a constituency is appointed a Regional Commissioner, the National Assembly shall be deemed to consist of the requisite number of members and its proceedings shall be valid notwithstanding that the ordinary total number of members in terms of this Article shall have been reduced by reason of such election of the Regional Commissioner or such appointment of a constituency member.
Tunaweza kujitungia sheria au kanuni halafu tushindwe kuzifuata, lakini sheria mama kama katiba! Inatisha!
 
Back
Top Bottom