Lionel Messi ni zaidi ya mchezaji japo naichukia Barcelona

Wale wabishi wabishi wa asili wenye kelele nyingi wakwapi? Wanaona aibu kujitokeza eti 🤣🤣😂😂😂Tena huko kwenu tunakuja kuwabomoa tena...hope next time Messi atawabamiza 3 or 4 goals.
 
Kwa kweli Messi ninamwona kama complete player katika kizazi hiki cha mpira wa miguu kwa sasa japo naichukia BARCELONA.

Jana aliweza kurudi uwanjani kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya taifa baada ya kubatilisha uamuzi wake na kutupia goli lililowapa ushindii pekeee.

Messi ni mtu wa kipaji cha pekee kwa kizazi hikii na sioni wa kumfananisha naye.

Nasema hivi maana naona kuna watu wenye performance ya juu kama Christiano Ronaldo, Bale lakini hawa naona wanatumia nguvu nyingi sana uwanjani kwa ubavu mwingi ila huyu bwana LIONEL Messi ni taratibu kama anaogelea kwenye dimbwi.

Pia katika mtazamo ninaona mpira wa leo na mpira wa miaka ya 1999 mpaka 2002 ni tofauti sana.

Nani anaikumbuka Manchester United hii ya
- Peter Schmeichel
- Jap Stam
- Phil Neville
- Gary Neville
- Nicky Butt
- Lionel Blank
- Roy Keane
- David Beckham
- Ryan Giggs
- Paul Scholes
- Ole Gunnar Solskjær
- Teddy Sheringham
- Dwight Yorke na
- Andy Cole

Bayern Munchen hii
- Oliver Khan
- Samuel Kuffor
- Bixsent Lizarazu
- Saint Cruz
- Oliver Beholf
- Steven Ephenberg
- Lothar Matthäus
- Jurgen Klinsman
- Elber na
- Sergio....

Alafu leo hii ufananishe Machester United iliyokuwa inacheza miaka ile na Buyern Munich fainali utagundua mpira wa sasa unanogeshwa na vyombo vya habari kwa sana ila si kama mpira ni mkali kama miaka ile.

Sitoisahau Manchester United inamuua Buyern katika dakika ya tisini, mchawi Tedy Shergam...ilikuwa nomaaaa

Je, unaikumbuka Real Madrid hii iliyopigwa na Buyern kwenye hatua ya makundi nje ndani ila nusu fainali Buyern Munich akapepetwa na Ronaldo de Lima miaka ya hio?

- Iker Casilas
- Ivan Campos
- Karanka
- Roberto Carlos
- Fernando Hiero
- Gutti
- Luis Figo
- Zinedine Zidane
- David Beckham
- Steve Mackmanaman
- Saviola
- Raul Gonzales
- Fernando Morientes na
- Ronaldo De Lima

Kwa kweli kwa miaka hii sioni timu yenye kikosi bora tena duniani labda Real Madrid kidogo inanipa raha hasa nikimuona Marcelo, shuka panda yake inakumbusha Roberto Carlos.

Arsenal hii unaikumbuka?
- David Seamen
- RayParlour
- Martin Keown
- Silvinho
- Patrick Vieira
- Emmanuel Petit
- Denis Bergkamp
- Marc Overmars
- Thiery Henry
- Sylvain Wiltord
- Fredrik Ljungberg na
- Nwanko Kanu

Arsenal hii haitokaa itokee kikosi kama hiki.

Ngoja wazee wenzangu waje waseme kuwa soka la leo lina vikosi vya aina gani ukilinganisha na enzi za 1999 to 2003.
ni bahati mbaya sana Arsenal uliyoitaja haikuchukua champions league, kilikuwa kizazi cha kipekee na ndio kilochonishawiahi nikawnza kuifuatilia ligi ya uingereza na kuwa shabiki wa arsenal!
 
ila mbona bado wazee wa miaka hiyo ya akina DELIMA hawaji na comments zao..ina naana wote humu ni kizazi cha messi na christiano...duh..kumbe wengi wachanga humu

Umejuwaje wote humu ni kizazi cha akina Messi? Mimi mmojawapo ni mtu mzima na nimewafuatilia LIVE wote hawa akina Zizu, Aimar, de lima, Batistuta, Gaucho, Requelme, Cambiasso, Damian Daf, Henry, JJ Okocha, Mustafa Hadji n.k...wote hawa na waliopita hakuna wa kumlinganisha na Messi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom