Cristiano Ronaldo hatimaye ametupa taulo

NEGAN

JF-Expert Member
May 12, 2023
648
1,446
Ule mchuano mkali uliodumu kwa takribani miaka 18 wa wanasoka nguli kuwahi kutokea duniani wenye vipaji vya hali ya juu hatimaye unaelekea ukingoni.

Si mwingine bali ni mchuano kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Cristiano Ronaldo anasema umefika wakati sasa mashabiki kukubali ukweli kuwa wakati ni ukuta kwa kiingerea unaweza kusema"Magic era has come to an end"
IMG_20230907_124042.jpg


Wote hawa wanaheshimiana sana Ronaldo adai hajawahi kumchukia Messi. Vile vile Messi anamuheshimu sana Cristiano Ronaldo.
IMG_20230907_124527.jpg


Wote kwa pamoja wameshinda mataji mengi na kushinda tuzo nyingi zikiwemo tuzo 12 za ballon d'or kwa pamoja.

Messi ameshinda kombe la dunia na hivi karibuni ametajwa kuwania tuzo ya Ballon d'or kwa mwaka 2023 huku akipewa chapuo la kushinda tuzo yake ya 8 ya Ballon d'or mbele ya Erling Haaland wa Manchester City ambaye naye alikua na msimu bora sana.
IMG_20230907_124443.jpg


Era has come to an end.
 
Kwa kweli!
Ila Messi katisha zaidi.
Kutwaa "libalonindoo" mara 7 haikuwa kazi nyepesi kwake.
Baada ya kulitwaa "libalonindoo" mwaka huu kwa mara ya 8, nadhani utakuwa ndiyo mwisho wake ingawa huko Amerika nako ametisha mnooo
Libalonindoo😂😂🙌.
Watu wengine wanasema anachukua Haaland mwaka huu sababu ya rekodi ya EPL na treble aliyobeba
 
Hawa watu sijui kama kuna ambaye atafikia level zao.
We fikiria: Msimu huu ulipoanza CR7 alikuwa majeruhi na akakosa mechi mbili za ligi, na mchi zote hizo timu yake ilifungwa!! Alipopona na kurudi uwanjani, amecheza mechi 3 na kuongoza mkeka wa mfungaji bora wa ligi akiwa na magoli 6, akiwaacha nyuma waliocheza mechi 5!! Katika mchi hizo tatu timu yake ilishinda!! Kibabu CR7 lakini bado kinalkimbiza usipime!!
 
We fikiria: Msimu huu ulipoanza CR7 alikuwa majeruhi na akakosa mechi mbili za ligi, na mchi zote hizo timu yake ilifungwa!! Alipopona na kurudi uwanjani, amecheza mechi 3 na kuongoza mkeka wa mfungaji bora wa ligi akiwa na magoli 6, akiwaacha nyuma waliocheza mechi 5!! Katika mchi hizo tatu timu yake ilishinda!! Kibabu CR7 lakini bado kinalkimbiza usipime!!
Kwenye video moja ya LIE DETECTOR aliulizwa kama ataweza kuendelea kucheza mpira wa mashindano hata akiwa na miaka 40 akajibu ndiyo anajiona akicheza kwa kiwango cha juu mpira wa mashindano hata akiwa na miaka 40.

That is a monster mentality

View: https://youtube.com/watch?v=YpjwHazhknA&si=UWmRoODM5FO_Mk6k
 
Wote wawil nawapenda kwa Sifa tofaut walizonazo,
Ronaldo ni Hustler na Mwenye juhudi hasa za kuwa Bora zaidi ya jana.
Messi ni Mwaminifu na anamifumo ya Maisha ya Kipekee sanaaa nadhani ndiyo Siri ya Mafanikio yake.
Wote kwangu ni Mifano Pendwa napenda kuwareffer.
 
Mbona nimesoma ila sijaona Ronaldo alipotupa taulo? Au ngeli ndio imenipita kushoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom