Lwiva
JF-Expert Member
- Apr 17, 2015
- 12,547
- 17,638
Wanawake wana uwezo mkubwa kwa kuwapima na wanaume wasio na akili tu maana kwa kifupi tu asilimia 99 ya wanawake awana akili yoyote ya maana kichwani ...hivyo hiyo asilimia 1% tu ndiyo inayo weza kushindanishwa na wanaume tena wanaume wasio na akiliWanabodi
Soma bandiko hili kwa utangulizi huu Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza? na Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ...
Leo tarehe 10 November, 2023 ni siku ya ukombozi fulani kwa taifa letu la Tanzania, Lile Fupa Lililowashinda Marais Wanaume kwa kipindi cha miaka 40!, Rais Samia, ambaye ni rais Mwanamke shujaa wa awamu ya sita, leo ameanza kuli gegeda fupa hili lililowashinda marais madume wanne!, tena mgegedo wenyewe wa fupa hili, Mwanamke shujaa huyu, ameanza kuligegeda akiwa ndani ya kipindi cha miaka miwili tuu na miezi kadhaa, kwa miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa Letu, inatua Bungeni Dodoma asubuhi hii kwa hati ya dharura!
Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kuondoa dhulma kubwa kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Japo bado sijafanikiwa kuona contents za miswada hiyo, lakini kitendo cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ambapo Rais Samia anastahili pongezi za dhati na kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye baadhi ya maeneo,
Kwa wenye access na TBC, macho na masikio yetu tuyaelekeze Bungeni Dodoma milango ya saa 4:30 asubuhi hii, hizi ngoma 3 zitashuka!.
NB: Pamoja na mabadiliko haya kutua Bungeni, ile hoja yangu Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa? is still valid!.
Karibuni
Paskali