Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,627
- Wanabodi
Bandiko hili ni utangulizi wa mabandiko haya
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
- Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo
- Je Wajua kuna Fupa Fulani la Dhulma kwa Watanzania, Liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, Jee Mama Samia Ataliweza Fupa Hili?.
Miswada hiyo ni Mswada wa mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuunda Tume Huru ya Uchaguzi, Muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kuondoa dhulma kubwa kwenye sheria yetu ya uchaguzi na muswada wa kurekebisha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Japo bado sijafanikiwa kuona contents za miswada hiyo, lakini kitendo cha serikali ya awamu ya sita kuwasilisha tuu miswada hii ni uthibitisho wa nia njema na dhamira ya dhati ambapo Rais Samia anastahili pongezi za dhati na kuthibitisha Wanawake wana uwezo mkubwa kuliko wanaume kwenye baadhi ya maeneo,
The basis ya pongezi hizi kabla hata ya kujua contents za mabadiliko ya sheria hizo ni pongezi za just a Political Will to change something!. Nimepandisha mabandiko zaidi ya 10 kulalamikia sheria mbovu ya uchaguzi, toka enzi za Mkapa, JK na JPM, hakuna aliyechukua hatua, hivyo kitendo tuu cha serikali ya Samia kuwa sikivu na kuleta mabadiliko, kinastahili pongezi za dhati!.
Kwa wenye access na TBC, macho na masikio yetu tuyaelekeze Bungeni Dodoma milango ya saa 4:30 asubuhi hii, hizi ngoma 3 zitashuka!.
NB: Pamoja na mabadiliko haya kutua Bungeni, ile hoja yangu Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa? is still valid!.
Karibuni
Paskali