Leteni changamoto zenu zote mapema, CCM iko imara

Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
783
525
Hapa najifanya msemaji wa Chama kwa kuwa nakipenda Chama changu, nakiamini na sina mpango wowote wa kukiacha, tunapoelekea miaka mingine mitano ya Samia, wapinzani wa ndani ya chama, mafisadi yaliyoko ndani ya chama, manyangau walioko ndani ya chama, leteni hoja zenu mapema, wanachama tutazijibu, na mtapata majibu ya kuwatosha.

Naonya machawa wote mnaopitapita kujipendekeza hata kwa yasiyofaa hamkijengi Chama mnakibomoa, Chama siyo cha DKT Samia ni cha waTanzania na tuko tayari kukilinda hatuko tayari kuruhusu kuona Nchi inamilikiwa na chama mamluki ambao fadhira zao ziko kwa mabeberu wa nje wanaoitamani Nchi hii ili waifyonze, tunayo mifano mingi katika Afrika na hatuko tayari kuiona amani yetu ikiparaganyika.
 
Gekul na chupa, Kuna Dogo keshaharibiwa uanaume wake? Nailaani sana CCM.
 
Gekul na chupa, Kuna Dogo keshaharibiwa uanaume wake? Nailaani sana CCM.
Gekulu ni CHADEMA aliyevaa kijani kwa tamaa ya mafanikio, mjasili haachi asili huko alikotoka ndo zao.
 
Kabla hatuja taja hizo changamoto,ili kupata suluhu kwanza tunapaswa kujiuliza,alise sababisha uwepo wa changamoto hizo ni nani ? Maana huyo ndo adui nambari moja,nae ni chama Cha mboga mboga,hivyo basi mwenye akili timamu hawezi peleka changamoto kwa aliye sababisha changamoto hizo ili kumpa sifa za kijinga za kisiasa.

Bali kuiondoa ccm kwenye utawala.
 
Back
Top Bottom