Leo rasmi nimeanza kutumia dawa kwa ajili ya pressure. Naanza staili mpya kuishi

Ninashukuru Mungu nina 58 yrs sina Pressure ya aina yoyote ile na wala sina kilo nyingi mwilini mwangu. Pole sana bado kijana una Pressure? utatumia dawa za Hospoitali maishani mwako na pressure haito ondoka kamwe. Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia presha yako upate kuisikia katika Radio na TV upate kupona maradhi yako uguwa pole.
Kuna bandiko lako linaelezea kuhusu pressure nililisoma jana.
Nashukuru nitakutafuta.
 
Bibi yangu aliniambia kuna wakati inabidi upunguze kula baadhi ya vitu kabla daktari hajakukataza.

Over 40 ukianza kupunguza ulaji wa nyama na pombe na kuongeza ulaji wa mboga matunda na maji. Matokeo yake huwa ni 99% mazuri.

Kutembea kwa lisaa limoja kila siku ni tip nzuri pia.
Kifupi mimi sio mlevi. Naweza kupita hata wiki mbili sijanywa pombe. Sema life style lazima ibadilike. Sasa ni mwendo wa mbogamboga, nafaka na matunda.

Leo nilipima tena jioni hii saa 2. Imeshuka na kuwa 170/110.
Nimekunywa maji lita 5 leo hii.
 
Ukiweza punguza nafaka uongeze jamii ya maharage kwenye sahani mpaka utakapoweza kupunguza uzito.
 
Ninashukuru Mungu nina 58 yrs sina Pressure ya aina yoyote ile na wala sina kilo nyingi mwilini mwangu. Pole sana bado kijana una Pressure? utatumia dawa za Hospoitali maishani mwako na pressure haito ondoka kamwe. Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia presha yako upate kuisikia katika Radio na TV upate kupona maradhi yako uguwa pole.
Weka hapa hapa wengi wafaidike
 
Nimekuwa nasumbuliwa na pressure kwa muda sasa. Leo nimepima ilikuwa 187 juu na chini 115.
Baada ya mashauriano na dr nimeamua kuanza kutumia dawa.

Nimepewa dawa za kutumia wiki moja then nirudi kucheck tena.

Ndio kwanza nina 44 yrs. Nitazimiss sana lite, na lager.
Jaribu pua dawa za asili za miti. Achana na za kununua kuna za kuelekezwa ujatumia mwenyewe. Zinaweza kukusaidia sana
 
Pole ila ni changamoto ya kawaida. Kama una uwezo nunua mashine ya kujipima nyumbani.

Anza kufanya mazoezi mepesi hasa ya kutembea walau nusu saa kila siku. Kama una vinyongo au mawazo sana jitahidi kuepuka.

Kapime Chorestrol, malaria, na UTI kwa sababu hupandisha pressure. Usipunguze uzito kwa kukonda ila punguza uzito kupitia mazoezi.

Jitahidi mwili wako usiwe na shambulio la bacteria wenye madhara. Kama una bacteria, mfano wanaosababisha UTI kisha ukawa na shambulio la Virus kwa wakati mmoja, mfano Corona, mwili unaachana na virus kisha unapambana na bacteria. Wakati huo virus anakuumiza. Kumbuka virus wengi hawana dawa. Kwa hiyo unatakiwa kutibu bacteria ili mwili upate nafasi ya kushugulika na virus.

Punguza chumvi. Usitumie chumvi ya kuongeza mezani, ina madhara sana.

Kuhusu mazoezi ukiweza yagawanye mara tatu kwa siku: asubuhi 1/3, mchana 1/3, na jioni 1/3. Mfano kama unafanya mazoezi kwa dakika 60 kwa siku, asubuhi fanya dakika 20, mchana dakika 20, jioni dakika 20.

Sababu yake: unapofanya mazoezi mwili unazalisha kemikali inaitwa nitric oxidant ambayo huifanya mishipa kutanuka na pressure kushuka. Sasa ukifanya asubuhi tu basi hiyo oxidant inakuwepo kipindi cha asubuhi kisha baada ya hapo inaisha. Kwa hiyo jitahidi kuizalisha mara kwa mara.

Usipaniki kwa tatizo lililokukuta. Mpaka pressure inafika hapo jua kuwa tatizo lilianza siku nyingi hata miaka kadhaa nyuma. Kwa hiyo litapungua taratibu kadri muda unavyokwenda.

Kuhusu dawa, hilo daktari wako atakuwa amekushauri. Ila inapendekezwa kuanza na dozi ndogo kuufanya mwili kuanza kujitegemea kuliko kutegemea dawa. Pili, miili inachagua dawa. Itabidi ushauriane na daktari wako kuhusu ni dawa gani inaleta ufanisi kwako. Kama unaona dawa X ufanisi ni mdogo, unajaribu dawa Y.

Kama una uwezo kiuchumi tumia mafuta aina ya Olive kwenye chakula. Sifa yake ni kuwa hayagandi kwenye mishipa lakini pia ni dawa kwenye pressure. Ila bei yake kubwa 20,000/= kwa lita.

Ukipata nafasi kapime moyo na figo kama viko sawa. Kama vimeanza hitilafu usiogope. Jali kupunguza pressure baada ya muda viungo hivyo vitarudi hali yake.

Usijalumu kwa kupata pressure. Yawezekana ni biological factor uliyozaliwa nayo. Ndiyo maana kuna wazee wana 80 ila hawana pressure ila wenye 30 hawana pressure.

Jikague kama una Sleeping Apnea/Obstructive Sleeping Apnea, hu2a inapandisha pressure. Mojawapo ya dalili yake ni Kukoroma. Kama una mke/mme unayelala naye anaweza kukuambia kama upumuaji wako ni wa kawaida au sio wa kawaida. Kama sio wa kawaida akurekodi, ukiamka utasikiliza mwenyewe. Baada ya hapo unaweA mshirikisha daktari wako.

Mwisho uandishi wangu hauna mtiririko. Nakutakia Kupona Haraka. Mungu atakusaidia.
 
Nimekuwa nasumbuliwa na pressure kwa muda sasa. Leo nimepima ilikuwa 187 juu na chini 115.
Baada ya mashauriano na dr nimeamua kuanza kutumia dawa.

Nimepewa dawa za kutumia wiki moja then nirudi kucheck tena.

Ndio kwanza nina 44 yrs. Nitazimiss sana lite, na lager.
Mzee Wassira hii siyo ile pressure ya kukosa ubunge wa Bunda? We mze mbishi sana sijapata ona, unalilia machangu wako wa Dodoma wakati wenzako hawana mpango na wewe. Pumzika kwa amani, we ishi kwako ukijilia ugali wako na dagaa wa Ziwa Victoria, achana na machangu.
 
Nimekuwa nasumbuliwa na pressure kwa muda sasa. Leo nimepima ilikuwa 187 juu na chini 115.
Baada ya mashauriano na dr nimeamua kuanza kutumia dawa.

Nimepewa dawa za kutumia wiki moja then nirudi kucheck tena.

Ndio kwanza nina 44 yrs. Nitazimiss sana lite, na lager.

Habari yako ndugu, pole kwa ugonjwa na hongera kwa kugundua tatizo na kuanza matibabu. Ugonjwa wa shinikizo la damu ni ''silent killer'' na huweza kuchukua muda mrefu kabla ya kuanza kuonyesha dalili ila kipindi chote uharibu viungo vya mwili taratibu. Kitakwimu ni asilimia 40 ya wagonjwa wa shinikizo la damu wanajua kuwa wanaugua ugonjwa huu.​

Nakupa vidokezo vichache(tips) chache za kuweza kukusaidia :

  • Tumia dawa kama ulivyoelekezwa na daktari. Usiache wala kupunguza ama kubadili dawa bila maelekezo ya daktari hata kama unajisikia vizuri. Pia nunua mashine ya kupima presha ''digital BP machine'' ili uwe na uwezo wa kujipima maendeleo ya ugonjwa. Presha yako ilikuwa imezidi 180/110 mmHg ambacho ni kiwango cha dharura ''emergency/urgency'' kwa hiyo lengo la kwanza ni kutoka kwenye hiyo dharura yani isome chini ya 180/110mmHg na lengo la pili ni presha kusoma chini ya 140/90 mmHg na lengo la tatu ni kusoma chini ya 120/80mmHg.​

  • Chakula. Adui yako mkubwa kuanzia sasa ni chumvi, jitahidi kupunguza chumvi kwenye chakula na utumizi wa vyakula cha viwandani maana huwa na kiwango kikubwa cha sodium. Kiwango kikubwa cha chakula chako kiwe matunda na mbogamboga. Kama ni mtumizi wa pombe jitahidi kupunguza hadi chupa mbili kwa siku kama ni mwanaume au chupa moja na nusu kama ni mwanamke.​

  • Mazoezi. Jitahidi kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30 kwa siku, siku tatu kwa wiki. Hii itasaidia pia kupunguza uzito wa mwili na kupelekea kupungua kwa presha.​

  • Punguza msongo wa mawazo ''stress''. Jitahidi kupumzika vizuri maana msongo wa mawazo unachangia kwa kiasi kikubwa kupandisha presha.​
Nikutakie siku njema.
 
Ningekua wewe ningeanza na life style modifications approach kuimanage hiyo pressure.

Ningepunguza sana chumvi.
Ningeacha myama nyekundu
Ningeacha kahawa
Ningeacha pombe
Ningepunguza sana stress
Ningeanza mazoezi madogo madogo ya kutembea
Ningezingatia chakula chenye nutrients stahiki

Na kadhalika.

Zingatia: Miongoni mwa vyanzo vikubwa kabisa vya ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease (CKD)) ni pressure ya juu ya damu (Hypertension) . Hivyo, jitahidi sana pressure iwe controlled maana ukishaingia kwenye mambo ya figo, game over, your life will nevr be the same.
 
Dawa ya pressure ni kupunguza stress ndio dawa, kufanya mazoezi kwa sana
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Niwe mwazi kabisa. Dawa nilizoanza kutumia nimesitisha. Jana na leo sijatumia, na sababu za kusitisha ni kwamba baada ya kuanza tu kutumia, ahsubuhi yake nikaanza kusikia mwili hauna nguvu. Nikajua ni kwa kuwa nilikojoa sana usiku huo.
Ahsubuhi nikaanza kunywa maji. Nilikunywa maji lita 5. Nilikojoa sana. Jioni ile hali ya mwili kukosa nguvu niliendelea kuisikia mpaka jioni ya saa 2 usiku.
Nikanyanyua simu kuongea na dr m1 ambaye ni rafiki yangu. Akanishauri nikacheck tena, labda kipimo cha mwanzo hakikuwa sahihi. Nikaenda kupima, this ilikuwa sehemu nyingine. Kupima ikasoma 180/110 imepungua 7/5.

Nikarudi home, nikanywa dawa. Kukojoa kama kawa. Ahsubuhi ile hali ya kuishiwa nguvu nikaona kama imezidi. Nikaendele kunywa maji lita 5 nyingine. Mpaka jioni nikajiona sipo sawa tofauti na kabla ya kuanza kutumia dawa.
Kwa hiyo usiku huo sikutumia tena dawa. Nikaamka kidogo nipo poa. Jana tena sijatumia, leo nimeamka mzima kabisa.
Nimeamua kuacha dawa kwa muda na sasa nabadili staili ya vyakula.
Ni mwendo wa mbogamboga, matunda, kupunguza chumvi na mazoezi.
Leo jioni nitaenda kucheck. Nitaleta mrejesho hapa.
Ahsante.
 
Ningekua wewe ningeanza na life style modifications approach kuimanage hiyo pressure.

Ningepunguza sana chumvi.
Ningeacha myama nyekundu
Ningeacha kahawa
Ningeacha pombe
Ningepunguza sana stress
Ningeanza mazoezi madogo madogo ya kutembea
Ningezingatia chakula chenye nutrients stahiki

Na kadhalika.

Zingatia: Miongoni mwa vyanzo vikubwa kabisa vya ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease (CKD)) ni pressure ya juu ya damu (Hypertension) . Hivyo, jitahidi sana pressure iwe controlled maana ukishaingia kwenye mambo ya figo, game over, your life will nevr be the same.
Nashukuru kwa ushauri.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri. Niwe mwazi kabisa. Dawa nilizoanza kutumia nimesitisha. Jana na leo sijatumia, na sababu za kusitisha ni kwamba baada ya kuanza tu kutumia, ahsubuhi yake nikaanza kusikia mwili hauna nguvu. Nikajua ni kwa kuwa nilikojoa sana usiku huo.
Ahsubuhi nikaanza kunywa maji. Nilikunywa maji lita 5. Nilikojoa sana. Jioni ile hali ya mwili kukosa nguvu niliendelea kuisikia mpaka jioni ya saa 2 usiku.
Nikanyanyua simu kuongea na dr m1 ambaye ni rafiki yangu. Akanishauri nikacheck tena, labda kipimo cha mwanzo hakikuwa sahihi. Nikaenda kupima, this ilikuwa sehemu nyingine. Kupima ikasoma 180/110 imepungua 7/5.

Nikarudi home, nikanywa dawa. Kukojoa kama kawa. Ahsubuhi ile hali ya kuishiwa nguvu nikaona kama imezidi. Nikaendele kunywa maji lita 5 nyingine. Mpaka jioni nikajiona sipo sawa tofauti na kabla ya kuanza kutumia dawa.
Kwa hiyo usiku huo sikutumia tena dawa. Nikaamka kidogo nipo poa. Jana tena sijatumia, leo nimeamka mzima kabisa.
Nimeamua kuacha dawa kwa muda na sasa nabadili staili ya vyakula.
Ni mwendo wa mbogamboga, matunda, kupunguza chumvi na mazoezi.
Leo jioni nitaenda kucheck. Nitaleta mrejesho hapa.
Ahsante.
Bado inasoma juu sana. Hata kama unajisikia vizuri bado upo kwenye hatari. Naona tatizo hapo ni aina ya dawa. Rudi kwa daktari na kama unaweza muone daktari bingwa.
 
Back
Top Bottom