PrN-kazi
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 2,900
- 444
Aiseee, hukupaswa kukaa kimya hivyo!! ilitakiwa walau utoe taarifa polisi ili huyo mu-asia na mwenye kutoa hiyo huduma ktk hiyo stationary wawekwe chini ya ulinzi, Huo ni ubadhilifu mkubwa: watanzania tunaibiwa sana. Daima tunatakiwa tuwe jasiri na tuthubutu kupambana na maovu kama hayo.Leo nilikwenda kutuma fax kwenye secretarial offices boot (mahali pa kununua huduma za fax nk) mara akaja M-tz mwenye asil ya Asia mzee mtu mzima. Alikuwa na zile karatasi za TRA za kulipia kodi mbali mbali benki. Ile karatasi ya kijani aliyokuwa nayo pale ndiyo iloyonishangaza. Penye sehemu ya mhuri wa benki palibandikwa kikaratasi cha mraba cha rangi nyeupe yenye kuonyesha Akiba Commercial; (nadhani), kilichoendelea ni yeye kuomba itolewe p/copy. P/copy ya kwanza ilipotoka ilionyesha mistari ya mraba (margins) ya ile karatasi nyeupe. Lakini nahisi ni wateja wa mahali pale, kilichofuata ni mtoa kopi kuingia chumba cha ndani, aliporudi kopi aliyokuja nayo haikuwa na zilemargins!! na ilionekana kuwa nakala halisi!!!! Yule Mwasaia lakini alikuwa mda wote akitetemeka. Bei ya payment voucher ile ilikua Tsh 36,000/= tu. Je, ni mangapi yanafanyika kama hayo? kwani niliwahi pia kukuta ikitolewa kopi ya cheti cha kuzaliwa na sehemu nyingine nilikuta cheti cha shule....