Leo ni Basi la HOOD (T 773 AVL )

marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,635
3,655
Wanajamvi leo nimefuata ushauri wenu,nikapanda Hood kutoka Morogoro kwenda Arusha!
Safari ilikuwa haina shida mpaka kufika kati ya Hedaru na Same!!Tukasikia mlio wa ajabu,hapa sidhani kama dereva alisikia maana aliendelea kuendesha gari mpaka abiria tulipoanza kulalamika!Harufu ya mpira unaoungua ilikuwa imetawala ndani ya gari!Dereva akasimama,tukashuka!Konda na Dereva wake wakagongagonga tairi baada ya muda tukaondoka!

Hatua chache mbele,harufu tena ya Moshi!!Ikabidi tushuke tena,mara moto ukawa unatoka kwenye tairi!!Dereva na konda wake wamefanikiwa kuuzima na safari yetu ndio imeishia hapa!

Dereva amepiga simu ofisini,msaada wa karibu ni kusubiri gari lililofika Moshi lirudi kuchukua abiria hapa tulipo!!

Sala zenu wanajamvi zinahitajika!!!
 
Poleni sana. Hebu angalia kama jirani kuna bar uanze kupunguza uchovu
 
Hakuna duka,bar,msikiti wala kanisa!!Mie niko chini ya mti penye kivuli!Nashukuru Mungu pana network napooza machungu kwenye JF

Asanteni sana!Kwa nguvu za Mola tutafika
 
tuwekee picha tafadhali kama great thinker najua fasta ushachukua picha ya tukio hilo hasa sehemu ya tairi iliyoungua. pole sana seems safari zako zote to and from moro this term zilitawaliwa na gundu balaaaa
 
Poleni sana wakuu ila mtafika salama

Hawa Hood kidogo wangeniulia wife mwaka jana maeneo ya Gairo ikitoka Mbeya............
 
poleni sana wote mliokuwa kwenye hicho chombo cha usafiri ambacho kina wataalam "waliobobea" kuangalia tairi kwa kuzigonga ngumi...teknolojia umekuwa sana wanaJF...elimu kwa wanaokabidhiwa hivi vyombo wabebe roho za watu inahitajika sana...iwe sawa sawia na vita juu ya mbu wamasababisha malaria....kauli mbiu iwe ajali hazikubaliki...
 
Hakuna duka,bar,msikiti wala kanisa!!Mie niko chini ya mti penye kivuli!Nashukuru Mungu pana network napooza machungu kwenye JF

Asanteni sana!Kwa nguvu za Mola tutafika

Dah! Mkuu kumbe tupo wote hapa! Mimi nipo huko kwenye kabonde hapa na hawa wazee! Ngoja nikucheck hapo!
 
nimepanda hood mara nyingi,sijapata matatizo nadhani ichukulie kama ajali.pole sana kwa misukosuko.
 
Dah! Mkuu kumbe tupo wote hapa! Mimi nipo huko kwenye kabonde hapa na hawa wazee! Ngoja nikucheck hapo!

Kwenye bonde?kuna vijana wamepita hapa wakatuambia hili eneo huwa lina simba,sasa wewe huogopi?
 
Poleni sana wakuu ila mtafika salama

Hawa Hood kidogo wangeniulia wife mwaka jana maeneo ya Gairo ikitoka Mbeya............


Kuna baadhi ya abiria nilisikia wakizungumzia ubovu wa haya magari!!wanasema yanaaribika mara kwa mara ina maana magari yameshachoka,yanalalamika yanataka kubadilishwa
 
Back
Top Bottom