Lazima William Mhando,Ngereja wonq'oke

Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,768
3,232
Kutokana na tabia za uongo za viongozi hawa wawili huku wakipigiwa hapuo na Waziri Mkuu aliyekuwa mtoto wa Mkulima Pinda na Raisi wa nchi Mh. Dr.Jakaya Mrisho Kikwete anayejulikana kwa uzururaji dunia nzima huku akiacha nchi yake ikiwa gizani totoro, na wengine wakifa kwa kukosa chakula kutokana na ukame wengine wakiuuawa na mapolisi na uchumi ukiwa ukiporomoka kwa kasi huku wananchi wakizidi kupata msongo wa mawazo na kupoteza maisha natoa wito kwa wana Dar wote tukiacha itikadi nyuma jumatatu kuanzia saa kumi na mbili na nusu tukutane makao makuu ya tanesco huku kundi lingine wakikutana wizara ya nishati na madini kukaa hapo mpaka hawa viongozi wanq'oke madarakani kama njia ya kukomesha dharau ,unyanyasaji,uporaji wa haki za watnzania,ufujaji wa heshima ya nchi na udumishwaji wa ustawi wa uchumi na jamii kiujumla.
Wanaharakati nyie ambao ni wanafiki mumekaa kimya wakati nchi inateketea kutokana na uzembe wa hawa wazandiki muko wapi LHRC,TAMWA,TGNP, KIWOHEDE tunawasikia mnachonga sana tuu pale munapoona kuna maslahi kutoka kwa wafadhili wenu hebu tuwone sasa
Tume ya haki za binadamu pamoja na kuongozwa na Jaji aliyetukuka kwa kufuata misingi ya haki za binadamu mbona sasa muko kimya au haki za binadamu kwenu ni pale uchaguzi unapokwenda mrama
Chama cha wenye viwanda mumekaa kimya kwa sababu munapewa misamaha ya kodi bila kuzingatia sheria hamuoni uongo wa Ngereja na mhando kuhusu umeme ni janga la kitaifa
Na nyie vyama vya siasa wanafiki sana hali sasa ni mbaya kuliko mulivyokuwa munaandamana januari munangoja nini huku wananchi wakiteseka
nanyi wana habari kazi yenu vibahasha tuu embu oneni nchi inavyoteketea kwa uzembe wa watu hao wanne hapo juu
kila mwana dar usijiulize nyenyuka kama una sufuria,mwiko,karatasi bango tukutane hapo kila mtu aje mmoja mmoja na jiandae hatutaondoka tukifika hapo mpaka hao wang'oke uwizi mtupu
 
William Mhando anasema umeme utakuwa unakatika kati ya massa 5-12 ukweli ni muongo aliyepitiliza maeneo ya Mwenge,Mlalakuwa,Mbezi Beach ,Tegeta anakata masaa 16 na tunajua kwa nini adhabu yote hii tulimchagua Halima Mdee
 
Tuna zaidi ya nusu mwezi sasa hatuna umeme toka alfajiri hadi jioni!! Juzi ndiyo walitoa kali zaidi-walikata umeme saa 9 usiku!! Mgao wakuanzia saa 9 usiku!!!
Hali ni mbaya kwa kweli
 
Kwenye Majimbo Yote yanayoongozwa na Chadema hali ni mbaya. Ubungo, Kawe, Mwanza. Musoma , Mbeya, Moshi, Arusha...
Ngerejea aliwahi kunukuliwa kuwa Mgao wa umeme basi., this time yuko Busy na Posho bungeni. Wabunge wa Chadema nao kimyaa wanakimbizana nyama choma chako ni chako dodoma. Tusiandamane ila tujiandae kufanya mabadiriko makubwa 2015..
 
Wanatuona sisi mandust sana hawa watu,sasa tumechoka hatuwataki hakuna wanachofanya zaidi ya propaganda.
 
Kwenye Majimbo Yote yanayoongozwa na Chadema hali ni mbaya. Ubungo, Kawe, Mwanza. Musoma , Mbeya, Moshi, Arusha...
Ngerejea aliwahi kunukuliwa kuwa Mgao wa umeme basi., this time yuko Busy na Posho bungeni. Wabunge wa Chadema nao kimyaa wanakimbizana nyama choma chako ni chako dodoma. Tusiandamane ila tujiandae kufanya mabadiriko makubwa 2015..

Ninadhani tumesha lalamika vya kutosha na dunia imesha tuona hata sisi ni wajinga. Kwa nini tunakubali kuvumilia vitu vya namna hii. Tuingie barabarani tumshinikize huyu Ngelege aondoke. Ninadhani tungefanya live angalau kama mikoa mitano hivi tungewashikisha adabu na wizara nyingine zingejirekebisha, labda utendaji ungeweza kuchukua sura nyingine. Kama ni sababu tunayo na dunia inajua hawa wajamaa nchi imewashinda . Tujiulize ni asilimia ngapi inategemea umeme kwa ajili ya kuishi hasa watu wanao kaa mjini ni asilimia kubwa. Lakini serikali haijali inawakomoa wananchi na kutuletea wababaishaji wa mikataba feki tu. Mimi ninashangaa wabunge wanakubali wananchi wao wanaadhibiwa bila sababu wakati wao wakitoa ushauri wao wanabezwa. Hii wizara inatakiwa isafishwe kwel ikweli.
 
haina shaka mkuu heshima mbele tu hata misri walianza mbali we need change..
 
Hakika kulalamika bila kuchukua hatua tunajidharilisha wenyewe embu fikiri kiongozi hana woga wa kusema uongo kwa sababu anajua sisi watanzania ni madondocha wanaweza kusema chochote na tukasahau,maneno ya watanzania kuwa wasahaulifu yaliwahi kutamkwa pia na Luteni Makamba aka former Katibu mkuu wa chama cha Magamba alipohojiwa na BBC radio, inatia hasira wananchi fungeni vibwebwe jumatatu tukutane huko toa salamu kwa rafiki jirani yako kanisani popote pale
 
William Mhando anasema umeme utakuwa unakatika kati ya massa 5-12 ukweli ni muongo aliyepitiliza maeneo ya Mwenge,Mlalakuwa,Mbezi Beach ,Tegeta anakata masaa 16 na tunajua kwa nini adhabu yote hii tulimchagua Halima Mdee

Mkuu bora nyie masaa 16. Sisi tunakatiwa 12asbh, unarudishwa 12jion. Ikifika 5ucku wanauchukua tena mpaka kesho yake sa 4 au 5asubuh. Hayo ni jumla ya masaa mangap? Kazi tunayo!
 
kama mambo yenyewe yapo hivi, bac watz bado kushikwa mat.............. tu.
 
Hakika kulalamika bila kuchukua hatua tunajidharilisha wenyewe embu fikiri kiongozi hana woga wa kusema uongo kwa sababu anajua sisi watanzania ni madondocha wanaweza kusema chochote na tukasahau,maneno ya watanzania kuwa wasahaulifu yaliwahi kutamkwa pia na Luteni Makamba aka former Katibu mkuu wa chama cha Magamba alipohojiwa na BBC radio, inatia hasira wananchi fungeni vibwebwe jumatatu tukutane huko toa salamu kwa rafiki jirani yako kanisani popote pale

MIMI NINADHANI WATANZANIA WAPO TAYARI LAKINI LINALOKWAMISHA NI NANI AAZE, NA KAULI ITOKe WAPI. MFANO AJITOLEE MMOJA ASEME LIWALO NA LIWE WATU WANABANA KAMA NYUKI. HATA POLISI WATAUNGA MKONO KWA SABABU HATA WAO WANATAABIKA HUKO MITAANI. SASA INAMAANA WATANZANIA WOTE TUSHINDE KWENYE BLANKET NA MAGODORO NA WAO NDIO WAENDE KAZINI.
 
Nakubali. Combination hii haiwezi kuleta suluhu ya tatizo la umeme kamwe. Mhando yuko bize na rushwa na ukabila kazini na huyu boss wake ni rushwa na mademu. Huoni kama kuna dalili za ubunifu. Hakika nchi hii Rais wanamtesa sana watendaji hawa! Mungu ampe nguvu na hasira Rais ili awamwage fisi jawa.
 
Ndugu yangu sio huko tuuuu....sisi kinondon tangu juzi tunakatiwa umeme saa 12 jion na unarudi saa 2 au 4 asbuhiiii...kweupeeee.....mimi nipo KINONDON MOSKO HAPA.......NSHAPANDA KITANDANI
William Mhando anasema umeme utakuwa unakatika kati ya massa 5-12 ukweli ni muongo aliyepitiliza maeneo ya Mwenge,Mlalakuwa,Mbezi Beach ,Tegeta anakata masaa 16 na tunajua kwa nini adhabu yote hii tulimchagua Halima Mdee
 
Hiv mgao huu hauwaathiri wanachama wa ccm?????ambao hupenda kupongeza hotuba na bajeti za serikali yao????????
 
Naunga mkono j3 tukawang'oe!wanatudharau sana wananchi! narudia tena naunga mkono 100000000000000000..%hivi mtu na akili zake anazungumzia mtambo wa kuzalisha 60MW kwa kutumia dizeli mwanza wakati IPTL,na songea mafuta ya kuendesha mitambo tanesco inashindwa kupeleka mafuta.fxcx.WATANZANIA TUAMKE SASA!
 
Mimi kinachoniudhi ni kauli anazotoa Ngeleja,mara kibao amekuwa akiapa eti awamu hii Nitakomesha mgao itakuwa HISTORIA,hivi wewe unadhani unamdanganya nani??? Kwanini nyie viongozi mnakuwa WACHOKOZI? HIVI MNADHANI WATZ WATABAKIA Wavumilivu milele? you better be realistic kuliko kutudanganya.You are taking advantage ya uvumilivu wetu,but one day mtakuja kushangaa,mtasema hawa ni watz kweli?? Mtabaki kusingizia MUNGIKI.LOL!
 
Back
Top Bottom