Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,309
- 19,179
Kuna wakati Tanzania ilijulikana kwa umahiri katika mapambano ya kivita, na jeshi letu JWTZ liliaminika sana katika uwanja wa mapambano. Hata waasi sehemu kama DRC walikuwa wakisema wazi, kwamba hawakuogopa kukabiliana na jeshi jingine lolote isipokuwa JWTZ ndio waliwaogopa sana. Tulijenga sifa pia upande wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kwamba tuna jeshi linalotumainika na kutegemeka.
Lakini baada ya hivi karibuni Msumbiji kupata matatizo na waasi, wamekimbilia Rwanda kuomba msaada, na sio Tanzania. Najiuliza sana, kulikoni tena Msumbiji wamegeukia Rwanda na sio Tanzania tena? Na habari kutoka Msumbiji zinasema jeshi la Rwanda limefanya maajabu Msumbiji na kukomboa sehemu iliyokuwa ikikaliwa na waasi.
Ukweli ni kwamba fursa za jeshi letu kutoa msaada wa kijeshi pale unapotakiwa ni fursa nzuri sana ya kulipa mazoezi halisi ya kivita. Wakati wa vita na Idd Amin, sababu moja iliyofanya tumpige kirahisi ilikuwa kwamba jeshi letu lilikuwa na uzoefu wa vita katika mapambano ya kupigania uhuru kusini mwa Afrika. Kwa hiyo Idd Amin alichokoza nchi ambayo wanajeshi wake walikuwa wamebobea vita, wakati wanajeshi wa Uganda walikuwa wameoteana vitambi na uzoefu wao ilikuwa kupiga raia wasio na silaha. Sasa nachelea sababu za Msumbiji kuamua kwenda Rwanda safari hii. Au wameona tuko busy na mabishano ya katiba mpya na kupambana na wapinzani wa siasa mitaani?
Reference: Rwandan, Mozambican troops capture rebel stronghold in Cabo Delgado