Lazaro Nyalandu vs Khamis Kagasheki vs Government Policy

Binafsi hanivutii katika utendaji wake. Namuona kama mtu anayejisikia. Nadhani anapaswa kutuonesha kuwa ni mchapakazi haswa
 
Wakuu naona mambo yanazidi kuchemka hapa, Huyu Naibu waziri mambo yanazidi kumkalia vibaya,

Mods mnaweza ku-update thread hii.

Tuendelee kujadili

SAKATA la Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kudaiwa kuingilia utendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa masilahi yake binafsi limezidi kuchukua sura mpya.
Safari hii, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ameilipua Kampuni ya Ahsante Tours ambayo Waziri Nyalandu anadaiwa kuikingia kifua.

Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama (CCM), aliilipua kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Utalii, Balozi, Khamisi Kagasheki na kudai kuwa kampuni hiyo imekubuhu kwa kupitisha wageni kinyemela.

"Hii kampuni ndio notorious(imekubuhu) kwa kuiba njia… wanaoingiza watu kinyemela huko ndani na Tour Operators (kampuni)zingine zinafahamu"alisema Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge.

Lembeli alisema kampuni nyingine za utalii zinalalamika kuwa Ahsante Tours ambayo imekuwa ni utaratibu wake wa kuiba njia na kuikosesha mapato Serikali ndio wanapewa upendeleo.

"Wenzao wanaituhumu hii kampuni kuwa ni bingwa wa kuiba njia sasa wamebanwa ndiyo hayo yameanza kujitokeza"alisema Lembeli, kauli ambayo ilionekana kumshtua Waziri Kagasheki. Waziri Kagasheki alimgeukia Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi na kumuuliza kama shirika lina taarifa hizo na kukiri kuwa ni kweli tuhuma hizo zipo na zinatolewa na kampuni washindani.

"Kama ni kweli basi tuachane na kampuni hii" alisema Waziri Kagasheki na kusema suala la kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini ni kinyume cha sheria na kanuni zilizoanzisha Tanapa.

Kauli hizo za Waziri Kagasheki, Lembeli na Kijazi zilitokana na maswali ya waandishi wa habari waliohoji Kampuni ya Ahsante Tours iliwezaje kuikopa Tanapa wakati tayari walilipwa na wageni.

Utaratibu unataka kampuni ya utalii inayotaka kupandisha mgeni mlimani kulipia kwa kadi hiyo kupitia benki yoyote ya CRDB wakati kwa wanaotembelea mbuga za wanyama hulipia kupitia Exim.

Chini ya utaratibu huo, watalii binafsi ambao wana kadi za Visa au Master Card wanaweza kulipia ada zao moja kwa moja katika vituo vilivyopo kwenye malango ya kuingia katika hifadhi hizo.

Mgogoro huo umeibuka baada ya Tanapa kuifungia kampuni hiyo kwa udanganyifu, lakini Waziri Nyalandu akaingilia kati na kuiamuru Tanapa kukutana na Ahsante Tours na kumaliza mgogoro huo.
Kampuni hiyo ya mjini Moshi ilifungiwa baada ya kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini bila kulipa ada na deni hilo kufikia Dola 80,000 za Marekani sawa na Sh155 milioni za Tanzania.
Lakini juzi Nyalandu aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akidai uamuzi wa Tanapa wa kuifungia Ahsante Tours ulikuwa ni wa dhuluma na kuituhumu Tanapa kwa rushwa.

Nyalandu alidai uamuzi huo wa Tanapa kuifungia kampuni hiyo ungeathiri mapato ya Tanapa kwa kuwa Ahsante Tours inatarajia kupata watalii 3,000 na pia imeajiri watanzania 600.
Lakini wakati Nyalandu akiituhumu Tanapa, taarifa mpya za namna anavyoingilia Tanapa zimeanza kuibuliwa ikiwamo ya kushinikiza Tanapa ikiuke maagizo yaliyopitishwa na Bunge.

Habari zinadai kuwa Bunge lilipitisha uamuzi kuwa kila mmiliki mwenye hoteli iliyopo ndani ya Hifadhi, ailipe Tanapa Dola 60 sawa na Sh99,000 za Tanzania kwa kila mgeni atakayelala hotelini.

Source hii hapa

Nyalandu ageuziwa kibao kuhusu rushwa Tanapa - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
ni pedesheee! we hujawahi kumuona leaders!akitunza wacheza shoo wa kike kwa kuweka pesa kwenye matiti?
 
Ni wakati sasa kila mmoja kuwajibika kwa "Udhaifu" wake. Kwa wenye kumbukumbu sahihi watakumbuka si miaka mingi Mhe. Nyalandu alikuwa mjumbe wa Bodi ya TANAPA. Siamini ubadhilifu katika shirika hili umeanza punde baaada ya sakata la Ahsante Tours, bali ubadhilifu ulikuwepo toka kipindi kile ndio maana amepata nguvu ya kusema Takukuru wakawachunguze wafanyakazi tena akaenda mbali kwa kusema pale Makao Makuu. Sina shaka hata kidogo Mhe. anaujua ubadhilifu unaoendelea TANAPA, ili kizazi chetu kisije kumhukumu baadae ni vyema akafichua ubadhilifu huo na si kusubiri Takukuru.

Ushauri:

1. Mhe. adhibitishe ubadhilifu wa TANAPA na wahusika kuchukuliwa hatua au yeye ajiuzulu kwa kulikebehi Taifa.
2. Ni vizuri utawala bora ukaheshimika.
 
Haya ndio matatizo ya kutumia wanasiasa ktk mambo ya msingi,nyalandu amesahau TANAPA inaendeshwa na body of trustees na sio wanasiasa.

Si dhani kama anaweza kusahau, maana hata yeye siku za karibuni alipata kuwa member wa Board hiyo; cha msingi ni kujua:

1. Hakuona ubadhilifu wa TANAPA wakati huo au ndio ule usemi wa "Rushwa hupofusha" unafanya kazi.
2. Amesema viongozi makao makuu TANAPA wamulikwe; yeye ni Naibu waziri, anafursa kubwa ya kusema na kushughulikia ubadhilifu unaofanywa na hao anaowajua.
 
Huyu naibu waziri hakuelewa alichokuwa anakisema, sidhani kama anaelewa wafanyakzi 600. Kama ukaguzi ukitokea hapo asante wanaweza wakaproduce list ya wafanyakazi 600 wanaolipa PAYE na Mafao ya uzeeni? Kwa nini porojo za majukwaani zinaendesha hili taifa letu. Wafanyakazi wengi sana wa Tanzania wanafanya kazi katika mazingira magumu sana huku wakikingiwa kifua na wakubwa.
 
Zitto,
Mashirika ya UMMA yahame kutoka kwenye usimamizi wa wizara mbalimbali. Vinginevyo kila waziri na naibu atakayeteuliwa au kuhamishiwa wizara flani breki na njaa yake ya kwanza atataka imalizwe na mashirika haya. Hatutafika.
 
Kama walitumia njia za panya kwa manufaa yao TANAPA wako sahihi kuwafungia Ahsante Tours kwani utaratibu unaeleweka kuwa lazima mgeni na Mtz walipie kabla ya kupanda mlima au kuingia ndani ya hifadhi. Lakini napata shida kidogo serikali imefahamu vipi kiasi tajwa kuwa ndicho walichopaswa kukilipia hao majaa? ina maana walikuwa wanawafanyia mahesabu ya kificho au walikula pamoja? Anyway Nyarandu pengine amepelekewa mezani hizo taarifa na hakuzifanyia kazi lkn kigezo cha kusema Ahsante Tours wanataraji kuleta wageni 3000 ndo kiwe kigezo cha kuachiliwa leseni yao mimi siafiki kama ni adhabu waitumikie wageni watabook na kampuni zingine ili mradi wako willing kuja.
PONGEZI KWA TANAPA ktk hili mmeonyesha njia.
 
Lakini wakati Nyalandu akiituhumu Tanapa, taarifa mpya za namna anavyoingilia Tanapa zimeanza kuibuliwa ikiwamo ya kushinikiza Tanapa ikiuke maagizo yaliyopitishwa na Bunge.

Habari zinadai kuwa Bunge lilipitisha uamuzi kuwa kila mmiliki mwenye hoteli iliyopo ndani ya Hifadhi, ailipe Tanapa Dola 60 sawa na Sh99,000 za Tanzania kwa kila mgeni atakayelala hotelini.

hii khabari haijakamilka...................yamaanisha Nyalandu hataki wazilipe hizo khela au imekaaje?
 
Majungu sio biashara useme uuze upate faida.

Sasa Majungu yako wapi hapo ....wakati Nyalandu kamuagiza HOSEA [takukuru] hadharani...na waziri wake kaja kufunga shughuli....Kampinga hadharani........bado utasema kuna majungu hapo????.....kama ni kiziwi ..hata picha huoni?
 
  • Thanks
Reactions: MKL

Nasikia Mike Tysoni kajibadili jinsia kawa demu, ushauri wangu kwa woote wawili ni kuwa wamconsult Tysoni nao wakapandikizwe jinsia nyingine kwani waliyonayo imewashinda.
 
nyalandu anakuwa sentimental na wazawa hajui kuwa wazwa nao mijizi,epa hawakuiba wageni!!ni hawahawa wakina lowassa na jk
 
Jamani Hii issue sio Kama mbavofikiri, Hapa ni watu wamerushana mombo ambae ndio muhifadhi na msimamizi wa kinapa alikuwa anapiga Dili na Asante tours kurushwa ndio akaamua kumwaga mboga bila yeye kuelewa Kuwa bado Ana ugly mkononi. Kupandisha mgeni mmoja kilimanjaro ni doll 633$ Ina maana ahsante tours wameingiza wagon 127 bila kuwalipia wakati kuna askari na bunduki na maredio call kila kona ata ukiingiza mgeni mmoja tuu hutoki salama. Swali Asante wamewezaje kuingiza wageni 127 bila wao kinapa au tanapa kujua? Nyalando yuko sawa kabisa sheria za park haziruhusu kukopesha sasa Asante walikopaje? Tanapa na kinapa ni wezi wamerushana Asante Ana wapagazi zaidi ya 600 ni kweli ila kazi ya upagazi hainaga nssf wala nini sababu unalipwa kila unapomaliza kazi na sio mwisho wa mwezi

SAKATA la Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kudaiwa kuingilia utendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa masilahi yake binafsi limezidi kuchukua sura mpya.

Safari hii, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ameilipua Kampuni ya Ahsante Tours ambayo Waziri Nyalandu anadaiwa kuikingia kifua.

Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama (CCM), aliilipua kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Utalii, Balozi, Khamisi Kagasheki na kudai kuwa kampuni hiyo imekubuhu kwa kupitisha wageni kinyemela.

"Hii kampuni ndio notorious(imekubuhu) kwa kuiba njia… wanaoingiza watu kinyemela huko ndani na Tour Operators (kampuni)zingine zinafahamu"alisema Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge.

Lembeli alisema kampuni nyingine za utalii zinalalamika kuwa Ahsante Tours ambayo imekuwa ni utaratibu wake wa kuiba njia na kuikosesha mapato Serikali ndio wanapewa upendeleo.

"Wenzao wanaituhumu hii kampuni kuwa ni bingwa wa kuiba njia sasa wamebanwa ndiyo hayo yameanza kujitokeza" alisema Lembeli, kauli ambayo ilionekana kumshtua Waziri Kagasheki. Waziri Kagasheki alimgeukia Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi na kumuuliza kama shirika lina taarifa hizo na kukiri kuwa ni kweli tuhuma hizo zipo na zinatolewa na kampuni washindani.

"Kama ni kweli basi tuachane na kampuni hii" alisema Waziri Kagasheki na kusema suala la kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini ni kinyume cha sheria na kanuni zilizoanzisha Tanapa.

Kauli hizo za Waziri Kagasheki, Lembeli na Kijazi zilitokana na maswali ya waandishi wa habari waliohoji Kampuni ya Ahsante Tours iliwezaje kuikopa Tanapa wakati tayari walilipwa na wageni.

Utaratibu unataka kampuni ya utalii inayotaka kupandisha mgeni mlimani kulipia kwa kadi hiyo kupitia benki yoyote ya CRDB wakati kwa wanaotembelea mbuga za wanyama hulipia kupitia Exim.

Chini ya utaratibu huo, watalii binafsi ambao wana kadi za Visa au Master Card wanaweza kulipia ada zao moja kwa moja katika vituo vilivyopo kwenye malango ya kuingia katika hifadhi hizo.

Mgogoro huo umeibuka baada ya Tanapa kuifungia kampuni hiyo kwa udanganyifu, lakini Waziri Nyalandu akaingilia kati na kuiamuru Tanapa kukutana na Ahsante Tours na kumaliza mgogoro huo.

Kampuni hiyo ya mjini Moshi ilifungiwa baada ya kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini bila kulipa ada na deni hilo kufikia Dola 80,000 za Marekani sawa na Sh155 milioni za Tanzania.

Lakini juzi Nyalandu aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akidai uamuzi wa Tanapa wa kuifungia Ahsante Tours ulikuwa ni wa dhuluma na kuituhumu Tanapa kwa rushwa.

Nyalandu alidai uamuzi huo wa Tanapa kuifungia kampuni hiyo ungeathiri mapato ya Tanapa kwa kuwa Ahsante Tours inatarajia kupata watalii 3,000 na pia imeajiri watanzania 600.

Lakini wakati Nyalandu akiituhumu Tanapa, taarifa mpya za namna anavyoingilia Tanapa zimeanza kuibuliwa ikiwamo ya kushinikiza Tanapa ikiuke maagizo yaliyopitishwa na Bunge.

Habari zinadai kuwa Bunge lilipitisha uamuzi kuwa kila mmiliki mwenye hoteli iliyopo ndani ya Hifadhi, ailipe Tanapa Dola 60 sawa na Sh99,000 za Tanzania kwa kila mgeni atakayelala hotelini.

Source: Mwananchi, 12/12/12
 
..Nadhani jana au juzi kuna mtu alikuja na hoja ya kumsifia huyu bwana mdogo ! Niliyoyaandika jana ndiyo haya yaliyotokea, kuwa huyu jamaa ni sifuri ila kawekwa pale kulipa fadhila nyingi ikiwemo mamaa, ambaye alikuwa mlimbwende, na amekuwa akisaidia kupiga krosi kama za Wilkot kwa fisadi mkuu, si unajua tena jamaa kwa kujiangusa-angusa majukwaani au hata akiwa ndani ya 18...lol

Anatetea majizi, na hata hao wa mahoteli pia wanamkatia na ni kafisadi kapya haka. Jumba lile wamemjengea pale arusha, lina maandaki, na madudu kibao so wakificha pembe mle huwezi kuziona kirahisi..
 
mtasikia mwingi mjue hapo maliasili mambo mengi yanafanyika kwa kujuana AMA kwa masilahi ya kundi au mtu Fulani kwa navyojua Mimi haikuwa vizuri kwa naibu waziri kuegamia upande wa kampuni bila kusikiliza maoni ya wataalam wake na Watu wa tanapa mawaziri Wengi hutafuta kuonekana wema mbele ya wananchi wanaofika ofisini kwao kulalamika wakisahau kuwa wao ni wasimamizi wa sheria.Kuna kampuni hazipendi kufuata kanuni na Taratibu za wizara husika ati kwa kuwa zikokaribu na wanasiasa na waziri husika.Anyway ni mtazamo binaries juu ya nyarandu ila Anajisikia Sana Huyu kaka,nakumbuka alikuwa Mlokole ameanza lini kuweka Pesa kwenye matiti? Mhhh
 
Naona hawa jamaa wamekuwa wakipigwa madongo bila sababu ya msingi Je ni sehemu gani Membe na Nyalandu wamekutwa na ufisadi? Mimi nona kwasababu hawa jamaa sio wana wa ushabiki watu wanawaogopa.
 
Back
Top Bottom