Lazaro Nyalandu vs Khamis Kagasheki vs Government Policy

Takukuru isiishie ktk kuchunguza kufungiwa kwa Ahsante Tours tu ndani ya Tanapa. Iangalie ndani zaidi kuhusu namna wanavyotoa tenda ktk Shirika. Ni kweli wakuu wengi wa Idara hapo Tanapa makao makuu wana kampuni zao, na wanapotangaza tenda ni kama danganya toto tu. Kwani tayari wanakuwa wameshapanga ni nani atachukua tenda hiyo miongini mwao. Bahati mbaya huwa najizuia sana kutaja majina ya watu, lakini wababe hao wawili ndiyo wahusika wakuu wa mfumo huo na hata Mkurugenzi mkuu hana sauti kwao kwa sababu ya ukwasi walio nao. Kifupi ni kwamba si rahisi kupata tenda hapo Tanapa kama haumo ndani ya system.
 
Maswali machache ya kujiuliza hapa ni haya:
-Asante Tours haidaiwi? Kwa nini idaiwe wakati watalii wanalipa?
-TANAPA ni taasisi ya UMMA kwa 100%, huyo mzalendo wa Asante Tours analijua hilo?
-Hivi mtu akishindwa kulipa anamkimbilia NW ili atoe AMRI?
-Nyalandu anafanyaje kazi na waziri wake Kaghasheki?
Tukumbuke pia kwamba walioziua taasisi za kifedha za UMMA kama NBC, NIC, THB, CRDB,..., ni WAZALENDO kama akina Mzee Mengi, waliokuwa wafanyakazi wa taasisi hizi, wanasiasa wetu,...

-
 
Kwa hakika style ya intervention ya Waziri Nyalandu katika swala hili inaamsha maswali mengi kuliko majibu; inatubidi tumuulize adeclare interest ndipo tunaweza kumuelewa japo kidogo!

Kabla ya kupiga yowe kuwaita TAKUKURU angejipa muda achunguze kwa kina swala zima; hawa kina Asante tours ni kina nani na ni kampuni ya aina gani kwa sababu sio kila king'aacho ni dhahabu, Tour operators in Tanzania come in all shades and colors; kuna wengine ni "Covert operators"!!

Kama anataka "kuwachonga" kina Asante tours na wengine wa aina hiyo kama Boss wake kule Bukoba alivyomchonga Meya akamrudi! yatamsibu pia kama yale yale pindi ukweli utakapodhihiri.

Waziri Marandu; No research no right to speak, Maliasili na Utalii itakuchezesha mdumange, mawaziri wenzio waliopita hapo wakaflop ilitokana na mbinu za "Covert operators" kama hao! watch out.
 
nyalandu ni fisadi kama mafisadi wengine,kuna taarifa sahihi kwamba mwezi julai mwaka huu akiwa bungeni mjini dodoma kwenye bunge la bajeti nyalandu aliagiza ndege ya swahiba wa mkurugenzi wa ahsante tours,cathibert swai aitwaye babu sambeke kupeleka wazungu wake wawili dodoma kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro( Kia),sasa anaposema hao wakurugenzi wa ahsante tours hawafahamu,na huyo sabeke alifahamiana naye lini hadi kupewa upendeleo wa wazungu wake kupelekwa bure dodoma kama si kupitia kwa cathibert swai wa ahsante tours?

kama hamna data za kutosha msichangie mada ambazo zitawaumbua baadaye,isitoshe nyalandu anapotosha umma wa watanzania,tanapa haikumkopesha ahsante tours,kilichofayika ni ahsante tours kupewa upendeleo wa kuingiza wageni kwenye hifadhi za taifa bila kulipa ada utaratibu ambao haupo kwa mujibu wa kanuni za tanapa,na kama nyalandu anabisha aonyeshe huo mkataba wa tanapa na ahsante tours waliowekeana saini ya kukopeshana hizo dola 70,000 kama anavyodai nyalandu.

tusiwapumbaze watanzania,sio wote ni hamnazo wapo wenye uelewa kumzidi mapa huyo nyalandu,ambaye anataka kuamsha hasira kwa mawakala wengine nao wahoji iweje wao hawapewi huo upendeleo?,kwa nini ahsante tours?,lazima nyalandu ana hisa hapo ahsante tours si bure wakubwa,

hivi huyo nyalandu anamfahamu vyema cathibert swai na mkewe?,cathibert swai ni mjanja wa mo-town,kule kenya wanaitwa wakora,hata alivyopata hizo mali kuna wingu zito nyalandu hawezi elewa chochote,awaulize wajanja wa mo-town watampa cv ya cathibert swai,hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza
 
Waziri Nyalandu amefanya la maana kumulika TANAPA.

Wazawa lazima wapewe kipaumbele maana wanatoa ajira kwa Vijana wa Kitanzania.

Kweli huu ni uzalendo Waziri Nyalanda Nakupongeza.

Pia Nafasi za Ajira TANAPA ziangaliwe, nafasi za Ajira ni kwa ufisadi na kujuana.

Ndo maana hata mambo mengine yanaenda Ovyo ovyo TANAPA.

Sasa naomba mawaziri wengine kama Mary Nagu na Anna Tibaijuka nao wafikiri na kuweke wazawa KWANZA.

Uwekezaji na Uwezeshaji ya MARY NAGU na Wizara Ya Ardhi Anna Tibajuka.

Nashangaa kwa nini wageni wanapata ardhi kwa urahisi wakati Mzawa hawezi kupata??

Kuna mwongozo gani katika hizi wizara ili mzawa aweze kupata ardhi na awekeze. Wasomi wetu wa Vyuo Vikuu watawezaji kujiajiri wenyewe bila kujua njia wazi zilizowekwa na hizi wizara????

Wake up you Ministers and follow path of Magufuli, Mwakyembe, Nyalandu etc. e.tc

Ole Medeye yeye hata wananchi wake Arumeru Mashariki ameshindwa kuwasaidia, sembuse Taifa....
Pole ndugu yangu! Usiamini hivyo manake swala la rushwa ni mtandao mpana mno! Hakuna kitakachopatikana manake hao takukuru wana link na Tanapa! Hivyo hwataplay part kuwalinda TANAPA!
Mimi nilichoka mno siku moja nilisimuliwa na dereva wa daladala kuwa kuna trafiki alikuwa kila siku anaomba rushwa! Yaani its like alikuwa Bosi mdogo so kila siku lazima naye akachukue makusanyo! Wakaenda takukuru siku moja! Wakachukua hela za takukuru tayari kwenda kuwapelekea trafiki wale! Wanachosadiki soon baada ya kuondoka takukuru wakawapigia simu wale trafik na kuwaeleza wametegwa manake walipofika pale wale trafiki siku hiyo wakagoma kabisa kukusanya zile hela kama ilivyokuwa kawaida yao kila siku
 
Hakuna MTALII anayekuja kutalii nchini kwa mkopo. Ahsante Tours wanaikopa TANAPA kwa nini? Tuziache taasisi za UMMA zijiendeshe zenyewe. TANAPA ina bodi yake ya wakurugenzi. Sheria iliyoianzisha TANAPA haimjui NAIBU WAZIRI. Mambo kama haya ndio yaliyoifikisha TANESCO hapo ilipo sasa.

Angalia sana mwenzetu. Mambo ya kuwaacha wenyewe ni ya hatari sana. Wanajichotea wanavyotaka huko TANAPA. Kumbuka wanakusanya pesa wao na kuzitumia watakavyo kama unavyopendekeza, Ndani ya TANAPA nani ataziacha?

Hiyo bodi ya Wakurugenzi unaifahamu ni akina nani? Unajua kwamba wabunge wamegoma kujiondoa ktk hizi bodi? Akina Jenesta Muhagama wamo ktk bodi za TANAPA! wana ufahamu wowote ktk uendeshaji wa mbuga/utalii? Kuna umoja kati ya TANAPA na hao watu wa Bodi. Wanachota watakavyo.

Mkurugenzi aliyeondoka, Bw. Bigulube, alichota mpaka akachoka na kuota kiburi. Alipoondoka ameajiliwa tena na hao hao waliochota naye. Huyu wa sasa naye, Kijazi, kisha anza. Ni mfululizo wa ulaji bila kikomo.

Makampuni mengi ya utalii yana miradi ya mawaziri na watumishi wa TANAPA. Kuna hao akina Zara ndo kabisa! pamoja na kujiita ni ya wazawa, imekuwa ni sehemu ya wanasiasa kununua au kuweka hisa zao. Vijana wanyonge unaodhani wanapewa ajira wanafaidi unyanyasaji wa makampuni. Kodi hukwepa kila siku kwa msaada wa wakuu wa TANAPA na wanasiasa. faida wanapeana pembeni.

Hii ni nchi iliyooza.
 
Takukuru isiishie ktk kuchunguza kufungiwa kwa Ahsante Tours tu ndani ya Tanapa. Iangalie ndani zaidi kuhusu namna wanavyotoa tenda ktk Shirika. Ni kweli wakuu wengi wa Idara hapo Tanapa makao makuu wana kampuni zao, na wanapotangaza tenda ni kama danganya toto tu. Kwani tayari wanakuwa wameshapanga ni nani atachukua tenda hiyo miongini mwao. Bahati mbaya huwa najizuia sana kutaja majina ya watu, lakini wababe hao wawili ndiyo wahusika wakuu wa mfumo huo na hata Mkurugenzi mkuu hana sauti kwao kwa sababu ya ukwasi walio nao. Kifupi ni kwamba si rahisi kupata tenda hapo Tanapa kama haumo ndani ya system.

Hebu ondoa tabia hiyo. Wataje ili tujadili kwa uwazi. Rais wetu alifika pale Bandari wakati anajidai kutembelea kila sekta ya serikali. Akasema wala rushwa wa bandari anawafahamu, eti naye (Rais) akashindwa kuwataja. Yako wapo?

Mika mingi imepita rushwa inashamili. Watajeni, tuwajadili. na hata mawaziri wa wizara yao ndo imekuwa kazi.
Mbona wabakaji vijijini wanatajwa???
 
Nyalandu ataumbuka muda si mrefu tusubiri tuone kwani nahisi moto aliouwasha hutazimika mpaka umuunguze na ndio itakuwa fundisho kwa aina ya mawaziri sampuli yake wanaokurupuka kwa faida za matumbo yao.
 
Unajua siku hizi kuna kampeni mpya ktk mitandao mingi: haya haya majizi, mafisadi yanatumia watu kuja ktk mitandao na kujipongeza, takia maisha marefu hata kama tayari tujividudu tunawatafuna, na then hawa kalumekenge wanakwenda kulipwa ujira mdogo wa kununulia chibuku..

Huyu hafai hata kuwa waziri, let alone sekretary lkn amewekwa pale kulinda maslahi flan flan ya wale wanaoanguka-anguka.
Tena kibaya, huyo maza zamani alikuwa mfanyakazi wa tanapa na fisadi mkubwa, na ameunganishwa na ntu flan flan ambaye ana dili chafu na huyu waziri na ndiyo maana akawapokea, wakapanga ***** wake na kuita press ! Angekuwa na uchungu mbona hashughulikii hao wanaoua faru, au ujangili, au hao wanaochimba madini ?? Mbona hafuatilii wanaokausha nyama na kuuza kila siku au wale wanaopakia wanyama kila siku ktk midege ya jeshi...!! Anapenda masifa tu huyu lkn hakuna kitu chochote.... siku za kujichubua karibu zitaisha... !!
Takururu wenyewe hao si ndiyo hao hao.... hoi bin vuuu..

unampongeza nyalandu kwa uzalendo gani anaouonyesha?,kulinda kampuni inayokwepa kulipa kodi au?,hiyo kampuni ya ahsante tours ni mabingwa wa kuiba njia na kupenyeza watalii kwa kutumia nia za panya na hata tanapa wanalifahamu hilo,sasa badala ya nyalandu kuagiza kampuni hiyo ichunguzwe kujua nani walishirikiana naye kuruhusu wageni kwenda mbuga za wanyama ama mlima kilimanjaro bila kulipa ada yeye anakurupuka na kuwaagiza takukuru wachunguze tanapa.

hapa kuna kitu kimejificha,hakuna utaratibu kwa mawakala wa utalii kupeleka wageni iwe kwenye mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro bila kulipa ada,huo utaratibu haupo na hata hao Ahsante Tours wanahafamu maana kuna kadi zinaitwa smart card zinazotumiwa na mawakala wote kulipa fedha benki ya crdb na kadi hiyo kuingizwa kwenye mfumo wa ki-electronic ambao husoma na kudhibitisha malipo kabla mgeni hajaanza safari ya kutembelea mbuga za wanyama au mlima kilimanjaro au mlima meru.

swali ni je hiyo kampuni ya Ahsante Tours ni katika mazingira gani ikaweza kupeleka wageni mara kwa mara bila kuwalipa tanapa hadi wakalimbikiza deni kubwa kiasi hicho? na ni kwa nini ni kampuni hiyo tu iliyopewa upendelea wakati yapo zaidi ya makampuni 200 ya wakala wa utalii wakiwamo wazalendo wenzetu kama huyo ahsante tours?

kwanza kampuni hiyo imemdanganya nyalandu kwamba ilipatwa na mtikisiko wa uchumi baada ya kutokea vurugu za kidini kule zanzibar miezi miwili iliyopita,kwa sababu wewe unayempongeza nyalandu pamoja na nyalandu mwenyewe hamna uelewa na masuala ya utalii pata somo kidogo hapa.

makampuni ya uwakala wa utalii hupokea booking mapema kutoka kwa wageni na malipo hufanyika kupitia booking hizo,hivyo basi mtalii anapofika nchini anakuwa tayari ameshalipia kila kitu na sehemu ya malipo hayo yanatumiwa na wakala kuilipa tanapa na kuonyesha idadi ya wageni na muda wa siku watakazotumia kama ni kwenye mbuga au mlimani.

swali ni kwa mazngira gani kampuni hiyo ikapokea mamilioni ya dola kutoka kwa wageni lakini yenyewe isilipe tanapa?,hapa nyalandu amekurupuka ama anatafuta sifa ambazo kwa wenye uelewa na masuala ya utalii wanamshangaa saana na asitumia neno uzalendo maana wazamendo ni wengi wapo pia wakwepa kodi kama kina ahsante tours nao ni wazalendo.
Kwa upande mwingine kuna harufu ya rushwa hata kwa hao ahsante tours na nyalandu mwenyewe,kwa nini wafunge safari kwenda kwa nyarandu,na akakutana nao bila kuhusisha maofisa wengine wa wizara yake?,alipewa nini na hao ahsante tours?.

Kwanza suala la kampuni hiyo kufungiwa kupeleka wageni halikufanywa na tanapa kama tanapa,ni maamuzi ya bodi ya tanapa,hivyo nyalandu anaingilia maamuzi halali ya bodi ya tanapa,je ana maslahi gani katika kampuni hiyo?,tunaomba takukuru wasiishie kwa tanapa wasonge mbele hadi kwa nyalandu maana ni nyalandu huyo huyo aliyekuwa na mgogoro na dk.chami kwa kutoa maamuzi kinzani na ya waziri wake ambaye ndiye sheria inamtambua na si naibu waziri

nampa ushauri wa bure nyalandu na wewe unayempongeza,fanyeni utafiti kwanza kabla ya kutoa maamuzi maana hata wewe umempongeza bila kufafanua unampongeza kwa lipi hasa la maana alilolifanya,ama kwa sabubu umesoma kwenye magazeti na kuingia kwenye jf kutoa pongezi zako bila kufafanua ili hali si wote wanaosoma magazeti.
 
Well said karagosi Mr ukwata kachemka aibu ataipa.
 
nyalandu ni fisadi kama mafisadi wengine,kuna taarifa sahihi kwamba mwezi julai mwaka huu akiwa bungeni mjini dodoma kwenye bunge la bajeti nyalandu aliagiza ndege ya swahiba wa mkurugenzi wa ahsante tours,cathibert swai aitwaye babu sambeke kupeleka wazungu wake wawili dodoma kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro( Kia),sasa anaposema hao wakurugenzi wa ahsante tours hawafahamu,na huyo sabeke alifahamiana naye lini hadi kupewa upendeleo wa wazungu wake kupelekwa bure dodoma kama si kupitia kwa cathibert swai wa ahsante tours?

kama hamna data za kutosha msichangie mada ambazo zitawaumbua baadaye,isitoshe nyalandu anapotosha umma wa watanzania,tanapa haikumkopesha ahsante tours,kilichofayika ni ahsante tours kupewa upendeleo wa kuingiza wageni kwenye hifadhi za taifa bila kulipa ada utaratibu ambao haupo kwa mujibu wa kanuni za tanapa,na kama nyalandu anabisha aonyeshe huo mkataba wa tanapa na ahsante tours waliowekeana saini ya kukopeshana hizo dola 70,000 kama anavyodai nyalandu.

tusiwapumbaze watanzania,sio wote ni hamnazo wapo wenye uelewa kumzidi mapa huyo nyalandu,ambaye anataka kuamsha hasira kwa mawakala wengine nao wahoji iweje wao hawapewi huo upendeleo?,kwa nini ahsante tours?,lazima nyalandu ana hisa hapo ahsante tours si bure wakubwa,

hivi huyo nyalandu anamfahamu vyema cathibert swai na mkewe?,cathibert swai ni mjanja wa mo-town,kule kenya wanaitwa wakora,hata alivyopata hizo mali kuna wingu zito nyalandu hawezi elewa chochote,awaulize wajanja wa mo-town watampa cv ya cathibert swai,hakika usilolijua ni sawa na usiku wa giza
Ok,kumbe ni ya Cathbert Swai?Na Nyalandu anadili na Babu Sambeke?

Anyways,mleta mada naona hakuiweka habari yote kwenye bandiko la kwanza,so ndiyo maana hata sielewi vyema,but thanks kwa maelezo hayo,ila kama kuna mwenye habari yote atubandikie hapa,maana mleta mada ametoa tu pongezi lakini habari iko nusu nusu.
 
Haya ndio matatizo ya kutumia wanasiasa ktk mambo ya msingi,nyalandu amesahau TANAPA inaendeshwa na body of trustees na sio wanasiasa.
 
Angalia sana mwenzetu. Mambo ya kuwaacha wenyewe ni ya hatari sana. Wanajichotea wanavyotaka huko TANAPA. Kumbuka wanakusanya pesa wao na kuzitumia watakavyo kama unavyopendekeza, Ndani ya TANAPA nani ataziacha?

Hiyo bodi ya Wakurugenzi unaifahamu ni akina nani? Unajua kwamba wabunge wamegoma kujiondoa ktk hizi bodi? Akina Jenesta Muhagama wamo ktk bodi za TANAPA! wana ufahamu wowote ktk uendeshaji wa mbuga/utalii? Kuna umoja kati ya TANAPA na hao watu wa Bodi. Wanachota watakavyo.

Mkurugenzi aliyeondoka, Bw. Bigulube, alichota mpaka akachoka na kuota kiburi. Alipoondoka ameajiliwa tena na hao hao waliochota naye. Huyu wa sasa naye, Kijazi, kisha anza. Ni mfululizo wa ulaji bila kikomo.

Makampuni mengi ya utalii yana miradi ya mawaziri na watumishi wa TANAPA. Kuna hao akina Zara ndo kabisa! pamoja na kujiita ni ya wazawa, imekuwa ni sehemu ya wanasiasa kununua au kuweka hisa zao. Vijana wanyonge unaodhani wanapewa ajira wanafaidi unyanyasaji wa makampuni. Kodi hukwepa kila siku kwa msaada wa wakuu wa TANAPA na wanasiasa. faida wanapeana pembeni.

Hii ni nchi iliyooza.
UMECHEMKA kaka, fanya utafiti kabla hujaandika kitu..
 
Majuzi tumeshuhudia tena kituko cha Lazaro Nyalandu [waziri mkuu mtarajiwa au foregn affairs minister wa Kambi ya Membe]...alipokuwa akizundua Caravan ya General George Marwa Waitara Independence Kilimanjaro Hiking Expedition.....akiwapiga mkwara kina Allain Kijazi kuwa atawaletea TAKUKURU kwa kuwapiga stop ASANTE TOURS ....HATUWEZI KULIONGELEA SANA HILI KWA UNDANI ...

Jana wakati wanawapokea wapanda mlima hao ....Mgeni wa heshima alikuwa waziri KHAMIS KAGASHEKI.....HOJA ya asante tours iliibuka tena ...safari hii ,MBUNGE LEMBELI akanena kuwa hao ASANTE TOURS ni wakwepaji wakubwa wa kodi za kuingia mbugani na wanadaiwa tozo nyingi tu...kila mtu anajuwa na kibaya wanapandisha watalii milima bila ya kulipa.....jamboo ambalo sio majungu bali linalalamikiwa kwenye vikao rasmi vya tour operators ndani na nje ya nchi.......WAZIRI AKAMUULIZA KIJAZI....JE NI KWELI HAYO...? KIJAZI AKASEMA .....NAAM!!!

WAZIRI AKAAGIZA KUWA ANAKUBALIANA NA UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUWASIMAMISHA ASANTE TOURS HADI WALIPE TOZO....WANAZODAIWA....

SASA TUNAJIULIZA ....HASIRA ZA NYALANDU KUWATISHIA BODI YA WAKURUGENZI KUWALETEA TAKUKURU ...ZINASUKUMWA NA NANI?? YEYE KAMA NAIBU WAZIRI KABLA YA KUTOA HILO TAMKO ZITO ...KWA NINI HAKUWASILIANA NA WAZIRI WAKE HATA KWA SMS .......ILI KUPATA BARAKA ZAKE ....KULIKO AIBU HII YA KUTOA UAMUZI UNAOTOFAUTIANA NA WAZIRI WAKE ...HASA WA KWAKE UKIONEKANA WAZI KUWA NA ARUFU YA UPENDELEO NA KUKOSA UCHUNGUZI....??

SIO MUDA MREFU UMEPITA HATUJASAHAU NAMNA NYALANDU ALIVYOKUWA AKITOFAUTIANA NA WAZIRI WAKE WA ZAMANI CHAMI KWA KUTOA MAAGIZO BILA BARAKA ZAKE ...MFANO KUWAFUKUZA WACHINA ...HALI ILIYOPELEKEA TAHARUKI YA KIDIPLOMASIA NA KULAZIMISHA SERIKALI KUOMBA RADHI......[HAKUWA NA BARAKA ZA WAZIRI AU BARAZA LA MAWAZIRI NA ISITOSHE HE IS TOO JUNIOUR]......

KUTOFAUTIANA NA WAZIRI WAKE KWENYE SUALA LA TBS....RIPOTI YA TBS IMETOKA NA KUMUONA IKEREGE HANA HATIA NA HADI SASA KUMEKUWA NA KIGUGUMIZI KIKUBWA CHA KUAMUA HATMA YAKE KAMA MTUMISHI WA UMMA....

KUKURUPUKA KWA NYALANDU KUNAFANANA NA KUKURUPUKA KWA MEMBE KUTANGAZA MAJESHI YETU KWENDA MALAWI AU KWENDA GOMA ....WAJIBU AMBAO NI WA AMIRI JESHI MKUUU.......NA IWAPO TEAM HII ITASHINDA URAIS MWAKA 2015 ...TUNAPATA PICHA YA AINA YA SERIKALI TUTAKAYOENDELEA KUWA NAYO..

HIVI MAWAZIRI WA KIKWETE HAWAPEWI MAFUNZO YA KUELEWA NAFASI NA WAJIBU WAO????
 
Hili la Nyalandu halina mshiko. Kwa nini asijadiliane na wahusika kwanza (TANAPA na Ahsante Tours)?
 
SAKATA la Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kudaiwa kuingilia utendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwa masilahi yake binafsi limezidi kuchukua sura mpya.

Safari hii, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ameilipua Kampuni ya Ahsante Tours ambayo Waziri Nyalandu anadaiwa kuikingia kifua.

Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama (CCM), aliilipua kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Utalii, Balozi, Khamisi Kagasheki na kudai kuwa kampuni hiyo imekubuhu kwa kupitisha wageni kinyemela.

"Hii kampuni ndio notorious(imekubuhu) kwa kuiba njia… wanaoingiza watu kinyemela huko ndani na Tour Operators (kampuni)zingine zinafahamu"alisema Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Bunge.

Lembeli alisema kampuni nyingine za utalii zinalalamika kuwa Ahsante Tours ambayo imekuwa ni utaratibu wake wa kuiba njia na kuikosesha mapato Serikali ndio wanapewa upendeleo.

"Wenzao wanaituhumu hii kampuni kuwa ni bingwa wa kuiba njia sasa wamebanwa ndiyo hayo yameanza kujitokeza" alisema Lembeli, kauli ambayo ilionekana kumshtua Waziri Kagasheki. Waziri Kagasheki alimgeukia Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi na kumuuliza kama shirika lina taarifa hizo na kukiri kuwa ni kweli tuhuma hizo zipo na zinatolewa na kampuni washindani.

"Kama ni kweli basi tuachane na kampuni hii" alisema Waziri Kagasheki na kusema suala la kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini ni kinyume cha sheria na kanuni zilizoanzisha Tanapa.

Kauli hizo za Waziri Kagasheki, Lembeli na Kijazi zilitokana na maswali ya waandishi wa habari waliohoji Kampuni ya Ahsante Tours iliwezaje kuikopa Tanapa wakati tayari walilipwa na wageni.

Utaratibu unataka kampuni ya utalii inayotaka kupandisha mgeni mlimani kulipia kwa kadi hiyo kupitia benki yoyote ya CRDB wakati kwa wanaotembelea mbuga za wanyama hulipia kupitia Exim.

Chini ya utaratibu huo, watalii binafsi ambao wana kadi za Visa au Master Card wanaweza kulipia ada zao moja kwa moja katika vituo vilivyopo kwenye malango ya kuingia katika hifadhi hizo.

Mgogoro huo umeibuka baada ya Tanapa kuifungia kampuni hiyo kwa udanganyifu, lakini Waziri Nyalandu akaingilia kati na kuiamuru Tanapa kukutana na Ahsante Tours na kumaliza mgogoro huo.

Kampuni hiyo ya mjini Moshi ilifungiwa baada ya kupitisha watalii katika hifadhi mbalimbali nchini bila kulipa ada na deni hilo kufikia Dola 80,000 za Marekani sawa na Sh155 milioni za Tanzania.

Lakini juzi Nyalandu aliitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akidai uamuzi wa Tanapa wa kuifungia Ahsante Tours ulikuwa ni wa dhuluma na kuituhumu Tanapa kwa rushwa.

Nyalandu alidai uamuzi huo wa Tanapa kuifungia kampuni hiyo ungeathiri mapato ya Tanapa kwa kuwa Ahsante Tours inatarajia kupata watalii 3,000 na pia imeajiri watanzania 600.

Lakini wakati Nyalandu akiituhumu Tanapa, taarifa mpya za namna anavyoingilia Tanapa zimeanza kuibuliwa ikiwamo ya kushinikiza Tanapa ikiuke maagizo yaliyopitishwa na Bunge.

Habari zinadai kuwa Bunge lilipitisha uamuzi kuwa kila mmiliki mwenye hoteli iliyopo ndani ya Hifadhi, ailipe Tanapa Dola 60 sawa na Sh99,000 za Tanzania kwa kila mgeni atakayelala hotelini.

Source: Mwananchi, 12/12/12
 
Huyu Naibu Waziri ana kiherehere sana angalia hata jimboni kwake tu, yaliyompata Chami na Kagasheki ajiandae!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom