Takukuru isiishie ktk kuchunguza kufungiwa kwa Ahsante Tours tu ndani ya Tanapa. Iangalie ndani zaidi kuhusu namna wanavyotoa tenda ktk Shirika. Ni kweli wakuu wengi wa Idara hapo Tanapa makao makuu wana kampuni zao, na wanapotangaza tenda ni kama danganya toto tu. Kwani tayari wanakuwa wameshapanga ni nani atachukua tenda hiyo miongini mwao. Bahati mbaya huwa najizuia sana kutaja majina ya watu, lakini wababe hao wawili ndiyo wahusika wakuu wa mfumo huo na hata Mkurugenzi mkuu hana sauti kwao kwa sababu ya ukwasi walio nao. Kifupi ni kwamba si rahisi kupata tenda hapo Tanapa kama haumo ndani ya system.