Lawama zetu ni kwa Idara ya Usalama wa Taifa kukosa uzalendo, weledi na kushindwa kumshauri Rais

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Jul 19, 2021
2,791
8,005
TISS ilitakiwa kuwa mbali zaidi kabla hata mkataba haujasainiwa. Idara ya usalama ilitakiwa iwe na wasomi wabobezi wa sheria, wenye roho za uzalendo na wenye uwezo wa kumwambia rais hapana, hili haliwezekani kwa maslahi ya taifa.

Leo ili mtu awe afisa, haàngaliwi uwezo wake wa kiakili, ni mwendo wa vimemo tu kutoka kwa wakubwa wa chama na Serikali.

Idara imejawa na watu wenye pua zisizonusa, macho yasiyo ona wala masikio yasio sikia hatari yoyote kabla haitokea.

Hili suala la DP WORLD ni matokeo ya uajili mbovu wa watu wasio na sifa za kiwemo kwenye taasisi nyeti kama Tiss.

Leo idara inatumika kulinda maslahi ya watawala na sio maslahi ya taifa. Hili ni janga kubwa, nchi iko uchi.

Tunaomba rais aivunje idara hii isukwe upya, na sheria ile iliyosainiwa na Bwana Ben Mkapa ifanyiwe marekebisho makubwa, ili idara kisiwe chombo cha chama chochote na kisiingiliwe na yeyote.

Watanzania tunataka idara yenye meno kwa wote, watawala wakubwa, wa kati, wachini na sisi tusio na mbele wala miguu tupate same treatment kwa maslahi mapana ya taifa letu.

Haya mambo ya DP WORLD yasiweze kujirudia tena. Hii ni kashfa kubwa kwa taasisi nyeti na nchi nzima kwa ujumla wake
 
Mwenyewe ndo unajiona mjuuuuuuzi wa mambo! Na vile jf imejaa wasomi jinga (mikubwa jinga) basi unatiririka tu na 'likes'
 
Hiyo IGA aina shida yoyote zaidi ya siasa na team mafisadi kujaribu kutengeneza confusion.

Ni mambo ya kuunga unga tu yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Uzao wa panya bado wamelala. Muda si mrefu watakuja hapa kutetea DPW
1690173234477.png
 
Back
Top Bottom