KERO LATRA, wananchi tunaumizwa kulipia kuanzia Shilingi 1,000/= kwa tiketi kisa madalali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

ambagae

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
3,241
1,301
LATRA tunaomba mtuokoe na huu wizi wa mchana kweupe akitokea dalali akakuelekeza kwenye basi ujue utalipa nauli zaidi ya nauli halali. Hebu fichueni makucha yenu tuone faida ya uwepo wenu maana uwepo wenu ni kodi za wananchi
 
Ujinga mwingine ni pale kulipia online kwa mitandao ya Simu. Sioni mantiki ya kutuchaji kisa tunalipia kwa hizo njia.

Mfano hizi Pos za kulipia katika maduka na sehemu nyingine za mauzo mteja hachajiwi.

BOT pamoja na mamla zingine waangalie haya mambo ya kumchaji mteja kisa tu analipia kwa njia ya simu.

Hatushindwi kubeba fedha taslimu, ila hizo huduma kama ni lazima kuwe na gharama basi aibebe mlipwaji maana yeye anafaida nyingi zaidi kuliko wateja.
 
Sijui kwanini wameshindwa kuwaondoa madalali, few day ago tumepigwa Alisaidy tumeambiwa Iringa - Dar ni Sh 38000
 
Sijui kwanini wameshindwa kuwaondoa madalali, few day ago tumepigwa Alisaidy tumeambiwa Iringa - Dar ni Sh 38000
Sometimes issue ni mbili ,

#1. Uzembe wetu wa kujua bei halisi za safari zetu
#2. Uaminifu duni wa makampuni ya bus
 
Sometimes issue ni mbili ,

#1. Uzembe wetu wa kujua bei halisi za safari zetu
#2. Uaminifu duni wa makampuni ya bus
Ilitakiwa kila kampuni ilazimishwe kuprint na kubandika nauli zao kwenye mbao za matangazo na ofisini kwao
 
Ujinga mwingine ni pale kulipia online kwa mitandao ya Simu. Sioni mantiki ya kutuchaji kisa tunalipia kwa hizo njia.

Mfano hizi Pos za kulipia katika maduka na sehemu nyingine za mauzo mteja hachajiwi.

BOT pamoja na mamla zingine waangalie haya mambo ya kumchaji mteja kisa tu analipia kwa njia ya simu.

Hatushindwi kubeba fedha taslimu, ila hizo huduma kama ni lazima kuwe na gharama basi aibebe mlipwaji maana yeye anafaida nyingi zaidi kuliko wateja.
Sasa mkuu,kwa kawaida tu,linakuingia akilini? Mwenye basi,alipwe, kampuni ya mitandao ihusike kupokea hizo pesa,izitoe bure tu! Elewa kwamba,kupitisha pesa kwao,ni biashara kwanza. Kwa hiyo mlipwaji,nae anapozitoa,anakatwa.
Mfano unapolipia umeme, unapewa kiasi gani? Tozo ni za nani? Lipia wa elfu 50 ndo utajua unakatwaje! Mwanzo wa mwezi,ukinunua wa 1,500 si unapata unit 0!!! Hela yote inachukuliwa!
Na jiulize,wakilipia watu milioni 10, wao wenye mtandao wanapata Sh ngapi! Serikali inapata ngapi?! Nani aue biashara kisa mtu mmoja analalamika! Utalalamika lakini utalipia tuuu! Usiponunua tiketi,hata huduma nyingine utatumia. Wewe kikubwa kubaliana nalo.
Uliwahi angalia mchanganuo wa malipo ukiongeza salio?
 
Back
Top Bottom