Mwanagenzi
JF-Expert Member
- Sep 11, 2006
- 702
- 213
Kwa mujibu wa Uhuru habari hiyo hii hapa...
Asha-Rose Migiro bosi UN
Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu
Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro (50), kuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Maura Mwingira, uteuzi wa Dk. Asha-Rose ulifanywa na kutangazwa jana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani.
Dk. Asha-Rose anachukua nafasi ya Mark Malloch Brown wa Uingereza aliyekaa katika wadhifa huo tangu Aprili, mwaka jana. Kabla ya Brown, nafasi hiyo ilikuwa ikishikwa na mwana mama Louise Frechette wa Canada.
Kutokana na kuteuliwa huko, Rais Jakaya Kikwete, alisema hiyo ni heshima kwa Tanzania na Afrika kwa jumla kwa sababu ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo tangu kuanzishwa kwa umoja huo mwaka 1945.
Rais Kikwete alimsifu Dk. Asha-Rose kwa kusema anajua ameteuliwa kwa sababu ana uwezo wa kushika wadhifa huo na kutekeleza dhamana aliyopewa.
Kufuatia kuteuliwa katika wadhifa huo mpya, nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyokuwa akiishikilia, sasa inabaki wazi.
Uteuzi huo unaweka historia mpya kwa Tanzania na nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini katika Umoja wa Mataifa kwa kutoa mtu wa kushika wadhifa huo.
Kabla ya uteuzi huo, Dk Asha pia alikuwa ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje nchini tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961.
Dk. Asha-Rose Migoro alizaliwa mwaka 1956 na kupata elimu ya msingi Mnazi Mmoja, Dar es Salaam kuanzia mwaka 1963 hadi 1966 na baadaye kuendelea na elimu hiyo katika shule ya Korogwe kati ya mwaka 1967 hadi mwaka 1969.
Baada ya hapo aliendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Weruweru mkoani Kilimanjaro mwaka 1970 na kuhitimu mwaka 1973. mwaka uliofuata alijiunga na shule ya sekondari ya Korogwe kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita ambapo alihitimu mwaka 1975.
Mwaka 1977, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza ya sheria ambayo alitunukiwa miaka mitatu baadaye.
Alijiunga na chuo hicho hicho mwaka 1982 kwa shahada ya pili ya sheria na kuhitimu mwaka 1984. Mwaka 1988, alihitimu shahada ya uzamivu (Ph.D) katika sheria kwenye Chuo Kikuu cha Konstanz nchini Ujerumani.
Kwa upande wa ajira, aliajiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mkufunzi msaidizi mwaka 1981 na baadaye kupanda katika ngazi za mhadhiri msaidizi, mhadhiri hadi mhadhiri mwandamizi, cheo alichokuwa nacho mpaka mwaka 2000 alipoingia kwenye siasa.
Katika mwaka huo, aliamua kuingia kwenye siasa na kugombea ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa taasisi za elimu ya juu.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, aliteuliwa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, nafasi aliyoishika hadi mwaka 2005.
Januari, mwaka huu, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hadi kuteuliwa katika wadhifa wake mpya kwenye Umoja wa Mataifa.
Vile vile, Dk. Asha-Rose kisiasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Katibu wa Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa ya NEC. Kwa nafasi hiyo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.