Lady Jay Dee ajibu hoja ya Wakurya!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Posted by Jide at 5:52 AM 0 comments

KUNA KITU KILINIKWAZA SANA JUMAMOSI

Nilikuwa nimejiendea kwenye starehe zangu, wakati nimekaa counter akaja sijui nimuite mvulala au mwanaume. Akaaniita we mapanga shaa, nikamuuliza hilo ndio jina langu??

Akasema si nyie watu wa musoma wakurya ni wauaji.

Kwanza nilitamani nisiendelee kuongea nae tena ila baadae nilikata shauri nikaamua nizungumze nae tu nijue mwisho wake.

Nikamwambia ina maana wauaji wote duniani ni wakurya? Mbona hata Mbeya hakuna hao wakurya na watu walikuwa wanachunwa ngozi?.

Au wanaouua albino duniani wote ni wakurya, basi kama ni hivyo kutakuwa na wazungu, wachina, waarabu na wahindi wakurya pia... Maana hata huko kuna wauaji.

Maana mwaka jana tu kuna kesi ya wahindi walimkata kata mwenzao wakamfunga kwenye box.

Ni sawa na imani ya kuwa wahaya wote wanapenda ngono, wakati tukiangalia picha halisi nani asieshiriki hilo tendo. Au kwakuwa hatuwaoni?

Tabia ya mtu na roho kama ni mbaya mbaya tu haijalishi kabila gani.

Niwafahamishe tu pia kuwa mimi sio mkurya, na sio kila mtu anaetoka mkoa wa mara basi ni mkurya......Na wapo wakurya wastaarabu tu na wenye roho nzuri, sio kama wengi wanavyodhani.

Kuwa mkurya sio sababu ya kuitwa muuaji, tuheshimu makabila ya watu.

Wahukumiwe wale tu wabaya tena kwa matendo yao.

Mimi kabila langu ni Msizaki halina uhusiano kabisa na Wakurya, natokea wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Wale mnaoniita mkurya nadhani mtakuwa mmepata jibu, na hata kama ningekuwa mkurya ningejivunia tu kwakuwa ndio lingekuwa kabila langu.

Na ndio maana huwa nakaa kimya hata nikiitwa mkurya, na watu wote wamekuwa wakifahamu hivyo kwa miaka nenda rudi, wala sioni kama ni tatizo...kwakuwa ndio kabila maarufu zaidi kwenye mkoa ninao toka.

Kwani kuwa mkurya ni dhambi jamani??

JayDee
source: ladyjaydee.blogspot.com
 
Ni sawa na imani ya kuwa wahaya wote wanapenda ngono, wakati tukiangalia picha halisi nani asieshiriki hilo tendo. Au kwakuwa hatuwaoni?

Tabia ya mtu na roho kama ni mbaya mbaya tu haijalishi kabila gani.

Niwafahamishe tu pia kuwa mimi sio mkurya, na sio kila mtu anaetoka mkoa wa mara basi ni mkurya......Na wapo wakurya wastaarabu tu na wenye roho nzuri, sio kama wengi wanavyodhani.

Kuwa mkurya sio sababu ya kuitwa muuaji, tuheshimu makabila ya watu.
Wahukumiwe wale tu wabaya tena kwa matendo yao.

Mimi kabila langu ni Msizaki halina uhusiano kabisa na Wakurya, natokea wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Wale mnaoniita mkurya nadhani mtakuwa mmepata jibu, na hata kama ningekuwa mkurya ningejivunia tu kwakuwa ndio lingekuwa kabila langu.

If 2+2 = 4 and 2X 2 = 4

then what is the logic in this statement ?.

same like saying:

2 x 0 =0 Or 0 x 2 = 0

Kulikua na haja gani ya yeye kuukana Ukurya, wakati huo huo anaonyesha kuutetea Ukurya?? kipi kinachofanya "Msizaki" kuwa bora zaidi kuliko Mkurya huko Musoma?..

Brain washed!
 
My point is people always want to id people based on their uniqueness! Think of this 'Kuna Msabato mmoja amekamatwa ugoni"

Lakini kama angekuwa M-catholic watu wasinge sema M-catholic amekamatwa ugoni its just "jamaa" Yawezekana wewe sio Mkurya lakini usishangae Wakurya kuitwa mapanga shaaa kwa sababu that is what come in the mind of people when they see a Mkurya Hiyo ndio Avatar yao! and in fact that is who they are!!

Nimesoma Tarime Sec Mambo niliyoyashuhudia hapo Tarime ni ya kuwaachia wao tu! Nimeona mke amekatwa panga kichwani alikuwa amebeba mtoto mgongoni na mtoto akapitiwa and its just a trivial domestic scuffle jamaa anabebea mke panga! What a stonyhearted people!!!!!!

Ishu ya juzi ndio imenimaliza kabisa Kichwa cha mtoto mdogo cut open, ng'ombe utumbo nje. Mpaka najiuliza kweli watu watu tuko diverse kiasi hiko, some cant even hurt a fly, some can do un-imaginable autrocity!!!
 
Lakini lipi ni jipya hapa?

Watu kuuana huko Musoma?

or Some Nyangema kuukana 'ukurya' wake?

Sidhani kaa kuna jipya
 
nadhani alijibu kwa hasira kutokana na huyo mtu alivyo mu-approach.kama angemwita kwa heshima basi yasingefikia hapo.

kwahio majibu ya jd kama yana mkera mtu yoyote mie naona ni vizuri kuyapuuzia na kuchukulia kwamba aliyaandika kwa hasira.
 
Jay Dee
Unachosema ni sahihi kabisa hasa kwa kuzingatia kuwa tabia ya mtu haitokani na kabila lake.
Kuwa mchaga haina maana ni mwizi kama ambavyo wengi wanavyodai, hii ni tabia tu ya mtu mmojammoja na si kabila in totality
Mbona tunawafahamu wakurya wengi sana na hawana hata chembe ya ukorofi huo, mbona Saddam Hussein aikuwa muuaji na si mkurya.....
 
Lakini kwa nini akubali kuitwa kabila lisilo lake kwa kuogopa virungu vya watu fulani wanaopendelea aitwe hivyo? Alikuwa anajibu kile anachoulizwa. Simple.
 
If 2+2 = 4 and 2X 2 = 4

then what is the logic in this statement ?.

same like saying:

2 x 0 =0 Or 0 x 2 = 0

Kulikua na haja gani ya yeye kuukana Ukurya, wakati huo huo anaonyesha kuutetea Ukurya?? kipi kinachofanya "Msizaki" kuwa bora zaidi kuliko Mkurya huko Musoma?..

Brain washed!
Mimi ndo ningekuwa Jide ningemfungulia huyo mtu mashtaka ya kuniita muuaji, halafu akifika huko athibitishe uuaji wangu. Hii ingekuwa ni fundisho kwa watu wote wanaopenda kulopoka, kwa maana huyo kijana au m-baba inaonyesha alilopoka. Sidhani kama Jide aliukana ukurya kiasi hicho yeye alichosema sio mkurya na hata angekuwa mkurya bado angejivunia kabila lake na ndo maana hata watu huwa wakimwita mkurya anakubali, hila inavyoonyesha huyo jamaa hakumtendea mwenzie haki. Halafu siku hizi naona jide amekuwa kweli, maana ingekuwa zamani sijui hapo pangechimbika.
 
My point is people always want to id people based on their uniqueness! Think of this 'Kuna Msabato mmoja amekamatwa ugoni"

Lakini kama angekuwa M-catholic watu wasinge sema M-catholic amekamatwa ugoni its just "jamaa" Yawezekana wewe sio Mkurya lakini usishangae Wakurya kuitwa mapanga shaaa kwa sababu that is what come in the mind of people when they see a Mkurya Hiyo ndio Avatar yao! and in fact that is who they are!!

Nimesoma Tarime Sec Mambo niliyoyashuhudia hapo Tarime ni ya kuwaachia wao tu! Nimeona mke amekatwa panga kichwani alikuwa amebeba mtoto mgongoni na mtoto akapitiwa and its just a trivial domestic scuffle jamaa anabebea mke panga! What a stonyhearted people!!!!!!

Ishu ya juzi ndio imenimaliza kabisa Kichwa cha mtoto mdogo cut open, ng'ombe utumbo nje. Mpaka najiuliza kweli watu watu tuko diverse kiasi hiko, some cant even hurt a fly, some can do un-imaginable autrocity!!!
I am proud to be a kurya, so what?
 
ha ha ha kazi kwelikweli!! kwani kosa kusema ukweli kua ye si mkurya?
 
mkoa wa Mara una makabila zaidi ya ishirini...ni mkoa unaoongoza kwa makabila mengi nchini
Mengi ya yanayojiita makabila kule Mara ni KOO tu. Makabila ya kweli yako matatu tu; Wakurya( humo utakuta Wasizaki ambao pia huitwa washashi wa JD, Wazanaki, Wangoreme, Waikoma, Wanata, Wakurya wenyewe, Waikizu, Waisenye, Wakabwa, Wasimbete, Wakiroba,... Kabila la pili ni Wajita( humo utawakuta Waruri, Wakwaya na Wajita wenyewe), kabila la tatu ni Wajaluo ambao nao wana viukoo vidogovidogo vya Wategi, Wasuba?, ...Makundi haya makubwa matatu ndio yanayounda mkoa ule wa watu jasiri sana, msimamo sana, na kuuana na kutwangana kwa sana!
 
asante wildcard kwa kunielewesha hilo maana mimi nilikuwa najua ni makabila....na je katika hilo kundi la wakurya kwa mfano, wanaongea lugha moja wote au kila mmoja ana lugha yake lets say waikoma na wangoreme wanasikilizana?
 
Back
Top Bottom