Kwenye hili,wazee walichemsha . . . . . . !!!!

Hivi Highlander hiyo capacity kubwa ambayo unadai Mungu ameweka ni ya nini?Umeipima na nini?

Ndugu Eiyer, the topic is too complicated ingawa unaweza kudhani rahisi--na pengine ndo maana tunabishana wawili tu tangu juzi. naomba tuachane nayo mkuu.
 
Highlander,kama umeamua tuache sawa,lakini kubishana wawili tu sio ishara ya kuwa complicate,wewe ndo unaifanya hivyo,pia tunaweza kubadilishana mawazo sisi wawili na tukapata faida kubwa pia sio lazima kuwe na lundo la watu na mizaha mingi isiyo na tija!
 
Last edited by a moderator:

Sawa ndugu yangu. Nimependa kuzungumza nawe katika uzi huu kutokana na kumbukumbu moja ya uzi wako mmoja mzuri sana miezi kadhaa ya nyuma ambao watu wengi walichangia tukajifunza mengi sana.

Hii subject ya leo ni complicated kwa sababu inaweza kuwa na mitizamo mingi sana, kama vile ya kidini, kiafrika, kizungu, kiume, kike, kikabila, n.k. Kama nilivyokudokeza awali, sijalifanyia research suala hili sana, lakini imani yangu imeegemea zaidi katika mila ya Kiafrika, hususan kabila langu ambako desturi ya kuoa wake wengi ipo hadi hii leo. Mimi binafsi SINA wake wengi, ambapo hata baba yangu mzazi hakuwa na wake wengi. Kwa hivyo mimi binafsi ni zao la ndoa ya mke mmoja. Lakini nimetafakari mara nyingi sana na kuona zinaweza kuwapo faida za mitala.

Unajua Eiyer, Mambo mengi sana yanayohusishwa na mila za kiafrika watu wanayadharau kwa sababu tu ni mila ya kiafrika. lakini ukichunguza kwa undani utakuta faida zinaweza kuwapo.
 
Highlander,inawezekana mambo mengi ya kiafrika yanapuuzwa,lakini faham kuwa sipuuzi na kupinga ndoa za wanawake wengi kwa sababu ni mila ya kiafrika bali ni kinyume cha ubinadamu na ni ulafi.Halafu pia sio waafrika peke yao wana utamaduni huu bali zipo jamii zingine pia.Utamaduni huu ulianzia kwenye umimi wa watawala na tamaa yao ya ngono,kila binti aliyeoneka mzuri eneo analoliongoza basi hakukua na mwanaume aliyekua na haki ya kuwa nae isipokuwa yeye.Ndipo utamaduni huo ukaenea,lakini hauna mahusiano yoyote na uhalisia!
 
Eiyer unatumia sana blanket statements. Sidhani kama ulafi pekee ndiyo chanzo cha mitala. Hebu jaribu kujiuliza kama ni wanaume tu ndo wanataka mitala, au panaweza kuwapo sababu mwanamke akawa ua uhitaji wa kushea mume na mke mwenzake. Mfano nzuri ukiwa mwanamke anapofiwa. Kwa nini hili lazima lihesabiwe kosa?

Mi naona kama kwamba Ulafi ni neno kali mno katika hili, hasa unapodai ndiyo sababu kubwa ya mitala miongoni mwa wanaume. Unanitamanisha kufanya utafitiki kwenye eneo hili kujua asili, malengo madhara na faida ya mitala. Mimi kwakweli kabla ya research hii naendelea kushikilia imani kuwa mitala inazo faida. Mungu katuumba na utofauti fulani katika mambo mengi. Wazungu wana nywele ndefu, sisi fupi. Wana pua ndefu, sisi fupi. Wana macho blu, sisi meusi. Wakati mwingine nimeshawishika kuamini pengine hata ukubwa wa ubongo wetu unazo tofauti. Maumbile ya Mwafrika ya via vya uzazi yana utofauti fulani na mzungu, kiasi kwamba hata capacity yake inasemekana ina utofauti fulani. Inasemekana wanawake wazungu ndio ambao wanatoa ushahidi huu.

Hivi kweli huoni uwezekano wa kuepusha zinaa katika mtu mwenye hamu kubwa ya ngono kwa kumruhusu kupata supply kubwa ya wanawake badala ya kumlazimisha kuwa na mke mmoja?
 
Ndugu yangu Highlander,usipende kuishi kwa assumption.Ni bora ukafanya utafiti.Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa utofauti wa ngozi upo mpaka kwenye viungo vya uzazi,huko unakotaka kwenda ni porini.Mwafrika na mzungu wakichunwa ngozi huwezi kuona tofauti yoyote.Nilisema mitala ni ulafi wa mwanaume kwa sababu hakuna mwanamke anaekubali kutoka moyoni kushare mume na mwanamke mwingine,wanaishi uke wenza kwa kulawishwa na dini au mila.Kwa taarifa yako hakuna mahali duniani mitala imeweza kuondoa uzinzi,Suleiman alikua na wake 700 na mahawara 300 lakini haikumzuia kuwa mzinzi,mwishowe akasema ni ubatili na kujilisha upepo!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom