Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?

Nilikuwa namaanisha Basutu ya Hanang,
Kwa upande wa mtama inabidi watu wawatembelee TBL. Hata kule Kilolo, Kaburu kapewa yale mashamba ya Tbl ya zamani, analima ngano.

Niwakumbushe, tusisahau apples za Njombe njia ya kuelekea kipengere, ni nzuri sana na zinazaa sana. Soko la ndani ni kubwa sana kabla hatujafikiria kupeleka Kenya.

Mkuu kule BASUTU kwa sasa ni historia na kwa ujumla mikoa ya Arusha wilaya zilizo kuwa zikilima ngano kama
1KARATU
2. MONDULI NA HANANGI SASA IKO MANYARA

Haya maeneo kwa sasa hawalimi tena ngano kwa wingi na hii ni kutokana na TBL kuagiza ngani karibia yote kutoka south Africa na wachache wanao lima hawalimi Bare tena bali wanalima ile ya kula ya kupikia mikate ambayo bado inasoko kwa viwanda vya mikate vya arusha, ila hii ya Bia hailimwi kwa wingi tena
 
Narubongo ekari moja ya ardhi Kongwa inakwendaje bei!?

hakuna bei maalumu ni wewe na mwenye shamba, mimi nilikodi hekari 15 kwa 125,000/=. Nguvu kazi ipo na bei ni ya chini sana kipindi ambacho kuna njaa lakini kama mwaka uliopita walivuna mazao mengi huwa wanaringa sana wale watu, ukimwonesha shamba la kupalilia anakwambia mbona majini marefu au udongo wenyewe mgumu hivyo halafu ananyanyua jembe lake anaondoka. Ukilima kongwa hautajuta
 
Msisahau kuna soko kubwa nje ya nchi la mboga zamaji zilizolimwa bila kemikali hasa ujerumani watu Tanzania Horticulture Association huwa wanaliongelea sana hili jambo tumewaacha Wakenya tu wanalifaidi hili soko,Maua ni ghali sana kulima na kutunza tuchangamkieni walau mboga za majani na mazao mengine ya kuexport kama vitunguu vyeupe ambavyo vinasoko kubwa nchi za scandnavia kufanya mmoja mmoja inaweza ikawa vigumu tunaweza kuunganisha nguvu tukiwa serious walau tukafaidi kuendelea kushuka kwa dhamani ya hela yetu ya madafu
 
Hivi Matikiti maji yanakubali Dodoma? mwenye data tafadhali

sijawahi kuona mtu ananunua tikiti dodoma, mimi nilikuwa nalishia nguruwe huko. yanakubali sana na tena unapanda kienyeji na wala hayapasuki kwakuwa mvua si nyingi dodoma ukizingatia matikiti huwa hayataki maji mengi. Yanapandwa kama mbegu za maboga kwenye shamba la mahindi, mtama
 
Msisahau kuna soko kubwa nje ya nchi la mboga zamaji zilizolimwa bila kemikali hasa ujerumani watu Tanzania Horticulture Association huwa wanaliongelea sana hili jambo tumewaacha Wakenya tu wanalifaidi hili soko,Maua ni ghali sana kulima na kutunza tuchangamkieni walau mboga za majani na mazao mengine ya kuexport kama vitunguu vyeupe ambavyo vinasoko kubwa nchi za scandnavia kufanya mmoja mmoja inaweza ikawa vigumu tunaweza kuunganisha nguvu tukiwa serious walau tukafaidi kuendelea kushuka kwa dhamani ya hela yetu ya madafu

Zao kama gilgirani ( spelling sijui) lina soko kubwa sana kwa Wahindi. Namini watu wakikomalia mboga mboga kwa viwango vya kimataifa tunaweza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi mkuu.
 
Pia kule Muheza, kuna potential kubwa sana ya kilimoi cha machungwa, eka 1 inaingia machungwa 82, na kila mti m1 baada ya miaka 3 unweza pata hata machungwa 1500, kam ukizingatia kanuni za kilimo bora. na ujue kuwa kila mwaka mazao yanongezeka kwa kuongezeka ukubwa wa mchungwa. machungwa ni matamu mno.

Ukishindwa kulima basi nunua ugrade ufanye packaging uexpot. wakenya wanajaa pale kuchukua mchungwa yetu na kwenda kuyaexpot kwao!!
 
Kila nikipita SUA kwa jamaa anayeuza miche ya miembe naona miche ya mizeituni ( Olive ), niliwahi kumuuliza huyu jamaa, miche ile hununuliwa na nani na anapeleka wapi. Jibu hakunipa, wala hajui hata shamba moja la mizeituni, lakini kila mwaka anauza mizeituni. Mizeituni inastawi Tanzania na inazaa, mafuta ya mizeituni ni adimu na bei mbaya sana. Soko ni world wide. Kazi kwetu.
 
thanx kwa taarifa ya mizaituni nitalifanyia kazi na utafiti zaidi. Na pia mbegu za ubuyu zinatoa mafuta ya vipodozi na bei yake kwa mtanzania wa kawaida hawezi kuimudu. soko lake zuri ni nje (UK) na hata hapa kuna jamaa alishawahi kuleta uzi yeye akiwa muuzaji lita 1 alisema ni 30,000/=
 
sijawahi kuona mtu ananunua tikiti dodoma, mimi nilikuwa nalishia nguruwe huko. yanakubali sana na tena unapanda kienyeji na wala hayapasuki kwakuwa mvua si nyingi dodoma ukizingatia matikiti huwa hayataki maji mengi. Yanapandwa kama mbegu za maboga kwenye shamba la mahindi, mtama

Eneo gani la dodoma............mmaana nimenunua tikiti hapa mjini kwa shs 6000!
 
thanx kwa taarifa ya mizaituni nitalifanyia kazi na utafiti zaidi. Na pia mbegu za ubuyu zinatoa mafuta ya vipodozi na bei yake kwa mtanzania wa kawaida hawezi kuimudu. soko lake zuri ni nje (UK) na hata hapa kuna jamaa alishawahi kuleta uzi yeye akiwa muuzaji lita 1 alisema ni 30,000/=

Unganisheni huo uzi hapa!
 
Unganisheni huo uzi hapa!

uzi wa jamaa wa ubuyu hapo chini. Nadhani jukwaa hili kwasasa limekuwa uwanja wa fujo maana post zote zinazohusu makampuni ya simu, siasa uchumi, govt construction plans na hata matajiri wa nje ya tz zote zinahamishiwa huku. Tuwe na jukwaa la ujasiliamali/wajasiliamali ndani ya business-and-economic-forum ili tusipoteze taarifa muhimu

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/203256-biashara-ya-mafuta-ya-ubuyu.html
 
Naunga mkono hoja hoja mheshimiwa
 
Kila nikipita SUA kwa jamaa anayeuza miche ya miembe naona miche ya mizeituni ( Olive ), niliwahi kumuuliza huyu jamaa, miche ile hununuliwa na nani na anapeleka wapi. Jibu hakunipa, wala hajui hata shamba moja la mizeituni, lakini kila mwaka anauza mizeituni. Mizeituni inastawi Tanzania na inazaa, mafuta ya mizeituni ni adimu na bei mbaya sana. Soko ni world wide. Kazi kwetu.

Mkuu Malila Mizeituni inakubali sehemu gani ya Tanzania? Una ABC zake like inachukua miaka mingapi kukua? Hii nchi bwana imebarikiwa sana
 
Mwenye data za Jatrofa tafadhali nilipita nane nane morogoro last year wakanipa sana moyo wa kuzipanda zinakubali sana Pwani,Morogoro na baadhi ya sehemu za Dodoma ila taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa hata wale wawekezaji wakubwa waliowarubuni wananchi wakishirikiana na serikali yetu tukufu kuwanyang'anya maelfu ya ekari wanavijiji maeneo ya kisarawe na Rufiji wametelekeza maelfu ya ekari za Jatrofa,ni nini kimetokea kwenye hili zao? limekufa soko ghafla?
 
nimeipenda hii kitu kuliko vyote jf. huko mbozi maparachichi yana stawi sana halafu hayali sana ardhi hekta moja au 2.5 acres unaweza panda miti zaidi ya miatano, ukizingatia kutakuwa na international airport business inaweza ikawa nzuri. kwa bei ya kibongo unaweza kupata zaidi ya laki kwa mti, chunya pia lake Rukwa valley linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji hasa mpunga and it is not well exploited, full ardhi!
.
 
Mkuu nilienda Chunya kwa mara ya kwanza about two weeks ago kwa shughuli nyingine tofauti na kilimo I was amazed with the agricultural opportunities available there nilifika hadi Mkwajuni karibu na ziwa Rukwa nilijaribu kuulizia wageni upatikani wa ardhi wanasema watu hawauzi ardhi kule ni ngumu kupata shamba ni kweli? Una taarifa zozote za upatikanaji wa mashamba? halafu wanasema unaweza ukapewa shamba ukajikuta limejaa maji wakati wa masika ile mito ina hama hama sana,kama wewe ni mwenyeji wa huko tupe taarifa tafadhali
 
Wakuu zabibu ni almasi na sasa hivi kuna benki zinafinance miradi ya zabibu mfano mzuri ni crdb wametufinance maeneo ya Ivumwe wao ndo wanauendesha mradi na collateral security ni shamba lako ntaenda field mwisho wa mwezi naweza kuja na data zaidi,wakuu hivi ngano Mbeya inakubali? ni aibu kwa nchi yenye ardhi kubwa na yenye rutuba kama hii kuagiza ngano toka nje ya nchi na sisi walevi ni soko kubwa sana la ngano (i.e TBL & Serengeti) nilisikia serengeti wanalima ngano dodoma sina uhakika wenye data wamwage ni maeneo gani ngano inakubali na upatikanaji wa ardhi

mbeya ngano inakubali sana na maeneo yote ya nyanda za juu hasa makete na ludewa japokuwa kuna milima sana, pale mbeya chuo cha uyole wana 1500 acres za ngano. rukwa nahisi kunaweza kupatikana ardhi rahisi. nasakitika wabongo tunakuwa wamachinga wa simu za kichina kariakoo wakati kuna mabilioni ya pesa udongoni just to pick up.
 
Back
Top Bottom