Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?

wadau msisahau miwa pia viwanda vinne vya tanzania vinalima hekta 17000 za miwa sijajua outgrowers. kenya isiyokuwa na ardhi wala maji wana hekta zaidi ya 100,000 na viwanda zaidi ya saba acre moja unaweza limia kama 2m data za india lakini bongo sikupata data najua itakuwa cheap inaweza kuzalisha 40 tonnes za raw cane ambayo unaweza kupata zaidi ya 7m after processing japokuwa inahitaji kiwanda kama zabibu offcourse, kuna local means of processing na sio mpaka uprocess mpaka sugar also unaweza kufanya fermentation ukazalisha alcohol kwa ajili ya fuel kama brazil remember always there is a way round, kama gharama kubwa mnafanya joint venture ila nahisi kuzalisha alcohol sio gharama sana zaidizaidi ni moto wa distillation na macrusher moto unaweza kutumia mabaki ya miwa, maeneo kama ya bonde la rufiji, ruvuma na mito ya lindi kama matandu yanaweza kufaa.
 
Mkuu nilienda Chunya kwa mara ya kwanza about two weeks ago kwa shughuli nyingine tofauti na kilimo I was amazed with the agricultural opportunities available there nilifika hadi Mkwajuni karibu na ziwa Rukwa nilijaribu kuulizia wageni upatikani wa ardhi wanasema watu hawauzi ardhi kule ni ngumu kupata shamba ni kweli? Una taarifa zozote za upatikanaji wa mashamba? halafu wanasema unaweza ukapewa shamba ukajikuta limejaa maji wakati wa masika ile mito ina hama hama sana,kama wewe ni mwenyeji wa huko tupe taarifa tafadhali

nimekaa mkwajuni mwaka 2002 kwa miezi kama mitatu maeneo niliyoona yanajaa maji ni yale ya bonde la mto songwe ambao ndio mkubwa na hufurika, lakini ziwa lile ni kubwa kuna maeneo mengi japokuwa usafiri unaweza ukawa tatizo, lile ziwa liko kwenye bonde la ufa na water table yake iko juu kwa hiyo hata ukiwa mbali na ziwa irrigation will be possible and economical
 
uzi wa jamaa wa ubuyu hapo chini. Nadhani jukwaa hili kwasasa limekuwa uwanja wa fujo maana post zote zinazohusu makampuni ya simu, siasa uchumi, govt construction plans na hata matajiri wa nje ya tz zote zinahamishiwa huku. Tuwe na jukwaa la ujasiliamali/wajasiliamali ndani ya business-and-economic-forum ili tusipoteze taarifa muhimu

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/203256-biashara-ya-mafuta-ya-ubuyu.html

Naunga mkono hoja hoja mheshimiwa

MODS tunatoa mwito wa kuchuja...............tuondoleeni maada zisizohusu ujasiri amali wanaotangaza wapelekwe habari mcnahanjanyiko na tusaidie kuunganisha hii thredi iwe moja ikunganisaha zile zote kama hii na iwe sticky ...............pale juu...................Tutashukuru!
 
mbeya ngano inakubali sana na maeneo yote ya nyanda za juu hasa makete na ludewa japokuwa kuna milima sana, pale mbeya chuo cha uyole wana 1500 acres za ngano. rukwa nahisi kunaweza kupatikana ardhi rahisi. nasakitika wabongo tunakuwa wamachinga wa simu za kichina kariakoo wakati kuna mabilioni ya pesa udongoni just to pick up.

Umeongelea Makete na Ludewa vipi mtandao wake wa miundombinu ya barabara? sijakwenda huko nina miaka 20!
 
Mkuu Malila Mizeituni inakubali sehemu gani ya Tanzania? Una ABC zake like inachukua miaka mingapi kukua? Hii nchi bwana imebarikiwa sana

Sina kabisa,bali naendelea kumchokonoa huyu mkuu wa pale SUA anipe mawili matatu. Huku ukanda wa Pwani naona miti ya mizeituni inaota bila shida sana.
 
Umeongelea Makete na Ludewa vipi mtandao wake wa miundombinu ya barabara? sijakwenda huko nina miaka 20!

bararara mkuu sio nzuri hasa masika maana nimefika ludewa ila kwa miradi ya mchuchuma na liganga ilivyopamba moto mambo yataboreka soon, makete sijakaa ila kwa story za huko masika hali ni mbaya sana.
 
Kiasi Makete nakufahamu, hakuna ardhi kule, sehemu nzuri kwa kilimo cha ngano wanalima wenyewe Wakinga/Wamagoma/Wawanji. Vihamba vyenyewe ni vidogo kama taulo,vipande vingine wamepanda Miti ya mbao, eneo lingine ni milima mikali halilimiki. Sijawahi kuona shamba kubwa la eka 100 la mtu mmoja.

Makete ni potential kwa ng`ombe wa maziwa na matunda.
 
nimeipenda hii kitu kuliko vyote jf. huko mbozi maparachichi yana stawi sana halafu hayali sana ardhi hekta moja au 2.5 acres unaweza panda miti zaidi ya miatano, ukizingatia kutakuwa na international airport business inaweza ikawa nzuri. kwa bei ya kibongo unaweza kupata zaidi ya laki kwa mti, chunya pia lake Rukwa valley linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji hasa mpunga and it is not well exploited, full ardhi!
.

Ardhi ya mbozi ni ghari kidogo ukilinganisha na Chunya. Nashauri, kwa mwenye uwezo kupanda parachichi kwa bidii sana. Malamba Mby parachichi zinamea vizuri.
 
Sina kabisa,bali naendelea kumchokonoa huyu mkuu wa pale SUA anipe mawili matatu. Huku ukanda wa Pwani naona miti ya mizeituni inaota bila shida sana.

hii miti inaota popote maana nimeiona kwa wingi sana dodoma, mwanza Kwakifupi mizaituni inafanana sana na muoarobaini kuanzia majani, matunda etc na kama hauna uzoefu unaweza usione utofauti. mahali unapoota muarobaini na mzaituni pia utaota
 
Ngoja msimu huu nitapanda miwili ya majaribio, kama itamea basi nitaendelea kuiongeza kidogo kidogo.
 
Ngoja msimu huu nitapanda miwili ya majaribio, kama itamea basi nitaendelea kuiongeza kidogo kidogo.

itakuwa nzuri hiyo, uzuri wa hii miti ukishaipanda na kufikia kima fulani hapo ndio umeshamaliza kazi unasubiri mavuno. haina gharama kabisa na wala haihitaji umwagiliaji, kuna aina moja nilliiona dodoma uswahilini huwa inakuwa mikubwa sana na inatoa matunda mengi sana unaweza ukafikia urefu wa 20m na upana 10m, cha muhimu ni kuwa na ardhi kubwa.
tatizo mizaituni ni kwamba inanyonya maji vibaya sana na mizizi yake inakwenda chini sana (ndio maana kipindi chote cha mwaka huwa ni green hata kama kuna ukame) kwahiyo hilo eneo utakaloipanda usitegemee kupanda chochote kikakubali, haina tofauti sana na mikaratusi. Na pia hutakiwi kuipanda karibu karibu c'se mwisho wa siku miti yote itakufa kwa kukosa maji
 
Kuna vimaji fulani vinaleta shida shambani kwangu, ngoja nivipelekee mizeiutuni nione.
 
Mwenye data za Jatrofa tafadhali nilipita nane nane morogoro last year wakanipa sana moyo wa kuzipanda zinakubali sana Pwani,Morogoro na baadhi ya sehemu za Dodoma ila taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa hata wale wawekezaji wakubwa waliowarubuni wananchi wakishirikiana na serikali yetu tukufu kuwanyang'anya maelfu ya ekari wanavijiji maeneo ya kisarawe na Rufiji wametelekeza maelfu ya ekari za Jatrofa,ni nini kimetokea kwenye hili zao? limekufa soko ghafla?

JATROPH NI ZAO ZURI SANA NA KAMA MTAKUMBUKA LINA TOA VITU VIFUATAVYO
1. MAFUTA- YA KUENDESHEA MITAMBO KAMA MAGARI NA MAJIKO YUA KUPIKIA

2. MAFUTA YAKE YANATENGENEZA SABUNI NZURI SANA

3. MASHUDU YAKE YANATUMIKA KUPIKIA KAMA KUNI

Tatizo ni kwamba kwa sasa sijui wazungu wameshituka nini na kuna wazungu walikuwa wanafadhili mradi wa JATROPHA KWENYEMIKOA YA SINGIDA NA MANYARA KWA SASA WAMESHITISHA UFADHILI GHAFULA, so ni kweli kuna siri nyuma ya hii kitu
 
Naogopa sana kufanya kilimo kwa kutegemea soko la mtu mmoja au ufadhiri wa mtu, mwaka juzi mnunuzi wa paprica kule Kilolo aliingia mitini na kuwaacha Wakulima wa Kilolo ktk hasara kubwa, mnunuzi wa Pareto huko kusini aliingia mitini na kuwaacha hoi wakulima kwa miaka kadhaa. Hata lindi jamaa hawa wa jatropa wamekimbia shamba. Hapa ndipo suala la kulima na kusindika sisi wenyewe kama Taifa linapokuja.
 
kuna mtu ana data za kilimo cha ndizi kwa biashara, nilisoma za uganda ni average ya 15 tonnes/ ha japokuwa research institute wanafika mpaka 60. hivi mkungu by average una uzito gani?, sh ngapi? zaidi ya maeneo mengine zaidi ya kagera, mbeya na kilimanjaro ndizi zinaweza kustawi vizuri? mwenye data pls!
 
Kwa mtindo huo ntaendelea kulima Mahindi tu nikikosa mnunuzi nakula mwenyewe
 
Hatujazungumzia maharage wakuu huku Mbeya nimekuta kuna maharage fulani hivi ya njano wanaita maini nasikia ni mbegu toka Kigoma (I'm not sure) yanakubali sana huku mbeya na unaweza kulima marambili kwa misimu ya huku mwezi wa kumi na moja (Japokuwa utapata shida sana kuyakausha) na mwezi wa tatu ni kilimo kizuri pia kwa watu waliopo kanda ya huku ila nahisi Dodoma napo Maharage yanakubali
 
Kwa wale waliopo Kigoma na Tabora Mawese yana soko zuri na bei nzuri changamkieni hiyo fursa
 
kuna mtu ana data za kilimo cha ndizi kwa biashara, nilisoma za uganda ni average ya 15 tonnes/ ha japokuwa research institute wanafika mpaka 60. hivi mkungu by average una uzito gani?, sh ngapi? zaidi ya maeneo mengine zaidi ya kagera, mbeya na kilimanjaro ndizi zinaweza kustawi vizuri? mwenye data pls!

Nichangie kuhusu eneo, kule Mbingu Ifakara Mzuzu unamea vizuri sana, Kilosa morogoro ndizi zinakubali, mahenge Morogoro ndizi zinamea, tatizo la Mahenge ni kivuko. Kwa Dar pale Mabibo mkungu wa ndizi unafika 15,000/ kama bei ya juu kwa wastani. Hapa Lindi kuna maeneo japo si makubwa.
 
Back
Top Bottom