Kweli zoezi la sensa halijafanikiwa

HASSAN SHEN

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
428
69
Polisi wako mtaani kwangu muda huu maeneo ya magomeni wanawakamata wale wote waliokataa kuhesabiwa.
 
kamishna wa sensa kasema imefanikiwa kwa 90% nimemwona jana ITV habari.
 
mimi kwa upande wangu sioni sababu za kulazimisha watu kuhesabiwa, ata hvyo watu wengi sana wamekwepa hili zoezi
 
  • Thanks
Reactions: awp

wakati mwingine naona serikali yetu inapoteza muda na pesa nyingi kwenye mambo yasio na msingi na kuacha vitu muhimu. kama wangekua makini na kila kitu kama wanavyofanya kufuatilia sensa basi tanzania yetu ingepiga hatua sana
 
Kwani lengo la serikali ni kupata idadi kamili ya wananchi? au kupata MAKISIO na MAKADIRIO ya idadi ya watu Kwa mwaka 2012?
 
Polisi wako mtaani kwangu muda huu maeneo ya magomeni wanawakamata wale wote waliokataa kuhesabiwa.

Eneo nililopo mimi kuna waliokataa kuhesabiwa wakaitiwa police.....baada ya police kufika wamefanya kituko cha kufungia mwaka......wamekubali kuhesabiwa ila sasa kwenye lile swali la usiku wa kuamkia leo wamelala watu wangapi hapa utaipenda......kuna mmjoja amesema wamelala watu 20.....akaambiwa ataje tobaaaaa ameorodhesha nafikiri mpaka marehemu.....manake amewataja mfululizo bila kusita......alipoambiwa ataje umri wa hao watu akaanza kujichanganya.....mara anataja umri unaofanana kwa watu zaidi ya wa 3......karani wa sensa akamuuliza hao watu ni mapacha?.....akamjibu watakuwaje mapacha wakati nimewataja baba zao tofauti?......nyumba nyingine nako hivyo hivyo....nyumba ina baba , mama , na watoto wawili wanasema wamelala watu zaidi ya 10......kwa kifupi hili zoezi limeharibika serikali ikatae/ ikubali......na tena waache kutangaza kila siku tbc1 kuwa zoezi la sensa limeenda vizuri manake hakuna kitu kama hicho......labda waseme limeenda vizuri vile wao wamefanikiwa kujichotea mahela kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao!
 
Pole sana baba! Umehesabiwa lkn

Ahh! wapi!. Nakumbuka maneno Ya Bob Marley, katika wimbo wake STAND UP FOR YOUR RIGHT, "you can fool some people some times, but you can't fool all the people all the times. Now we see the light. Stand up for your right".
 
Kwani lengo la serikali ni kupata idadi kamili ya wananchi? au kupata MAKISIO na MAKADIRIO ya idadi ya watu Kwa mwaka 2012?

A Census measures absolutely everyone in the whole country. A representative Survey measures a small number of people who fit a particular category of people.
 
Eneo nililopo mimi kuna waliokataa kuhesabiwa wakaitiwa police.....baada ya police kufika wamefanya kituko cha kufungia mwaka......wamekubali kuhesabiwa ila sasa kwenye lile swali la usiku wa kuamkia leo wamelala watu wangapi hapa utaipenda......kuna mmjoja amesema wamelala watu 20.....akaambiwa ataje tobaaaaa ameorodhesha nafikiri mpaka marehemu.....manake amewataja mfululizo bila kusita......alipoambiwa ataje umri wa hao watu akaanza kujichanganya.....mara anataja umri unaofanana kwa watu zaidi ya wa 3......karani wa sensa akamuuliza hao watu ni mapacha?.....akamjibu watakuwaje mapacha wakati nimewataja baba zao tofauti?......nyumba nyingine nako hivyo hivyo....nyumba ina baba , mama , na watoto wawili wanasema wamelala watu zaidi ya 10......kwa kifupi hili zoezi limeharibika serikali ikatae/ ikubali......na tena waache kutangaza kila siku tbc1 kuwa zoezi la sensa limeenda vizuri manake hakuna kitu kama hicho......labda waseme limeenda vizuri vile wao wamefanikiwa kujichotea mahela kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao!

Nimeipenda hii movie, ila najua serikali dhaifu mwisho wa siku itatoa takwimu hata kama ni za kuchakachua, ingawa ukweli ni kwamba hili zoezi, limeonyesha kukabiliwa na changamoto ambazo zinaashiria dhahiri kabisa kwamba zoezi halijafanikiwa kama ilivyotarajiwa. Mbona kura zenyewe walichakachua, sembuse sensa??
 
Polisi wako mtaani kwangu muda huu maeneo ya magomeni wanawakamata wale wote waliokataa kuhesabiwa.

Magomeni ipi hiyo, na mimi naishi magomeni na sijahesabiwa mpaka sasa, wamewazaje kuwajua ambao hawati kuhesabiwa wakati wengine wengi tu hatujapata hiyo fursa?
 
Back
Top Bottom