Kwanini?

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,949
1,940
Katika kukaa kwangu hapa Dar kwa muda wa miaka 10 iliyopita kuna vitu vimekuwa vikiongezeka kila kukicha
1-makanisa yanaongeza sana
2-Bar na Grosery na Night Club
3-Sehemu za ukahaba zinaongezeka sana
4-Mahoteli na Nyumba za kulala wageni
 
Inawezekana makanisa yanaongezeka kweli, lakini umeshajiuliza kama waumini nao wanaongezeka kwa kasi hiyo hiyo?.,maana kama kasi ya kuongezeka kwa makanisa ingeendana na kuongezeka kwa waumini basi Bar, Grocery, Night Clubs na sehemu za ukahaba zingepungua sana kutokana na kukosa wateja.
 
Simple, Flow ya watu kuja Dar toka mikoani ni kubwa mno!..Kila basi linalowasili Dar toka mkoani at least linakuwa na immigrants wa kudumu 2!

Haya ni matokeo ya sera za Kiporipori za ku'centralize huduma zote za muhimu zikae Dar!
Tunajikaanga kwa mafuta yetu wenyewe!
 
Katika kukaa kwangu hapa Dar kwa muda wa miaka 10 iliyopita kuna vitu vimekuwa vikiongezeka kila kukicha
1-makanisa yanaongeza sana
2-Bar na Grosery na Night Club
3-Sehemu za ukahaba zinaongezeka sana
4-Mahoteli na Nyumba za kulala wageni

Wanywaji wanaongezeka ....wanaongezewa bar na vilabu.
Wakishalewa wanataka kupunguza stimu na kina dada wanataka pesa...sehemu za ukahaba nazo zinaongezeka.
Dada na mteja wake wanahitaji faragha....nyumba zinaongezeka.
Wakishavunja amri wanataka kutubu hivyo wanatinga kanisani.
 
ukiona hivyo ujue wajasiriamali ni wengi sana mujini.

watu wengi zaidi wamejiajiri
.....sasa wateja (wanywaji na wapenda chini) tusifungue bar? hoteli and Guest House?
.....sasa waumini (watu waliokata tamaa na maisha na wanaohitaji faraja) wapo, tusifungue makanisa?
 
Wanywaji wanaongezeka ....wanaongezewa bar na vilabu.
Wakishalewa wanataka kupunguza stimu na kina dada wanataka pesa...sehemu za ukahaba nazo zinaongezeka.
Dada na mteja wake wanahitaji faragha....nyumba zinaongezeka.
Wakishavunja amri wanataka kutubu hivyo wanatinga kanisani.

Wewe bana! majibu kama ya kupatia PhD!! kama mimi ndo supervisor wako ningekugongea 100% recommended to be honoured with a PhD immediately before next month.,

na hiyo avatar yako.....mhh!
 
Idadi ya watu nayo inaongezeka,hivyo huduma lazima iongezeke.
 
Kah ebwana ndio Lils nakukubali maana umetoa kitu kamili hapo hakuna uwongo mwana.Bigirita umeonaeee Lils alivyojibu mwake safi.
 
Ndio nchi inakuwa na kupanuka hayo mambo unavyoona DSM na kwingineko ni hivyo hivyo
 
Wewe bana! majibu kama ya kupatia PhD!! kama mimi ndo supervisor wako ningekugongea 100% recommended to be honoured with a PhD immediately before next month.,

na hiyo avatar yako.....mhh!

heheeheh asante kwakukubali jibu hilo mkuu....recommendation latter itapitia kwako kama hutojali.
 
Kuna vingine umevisahau.
Idadi ya watu nayo inaongezeka sana na hali ya umaskini nayo imeongezeka.
 
duh mkuu umetoa swali safi sana.Hata mie nilitegemea kuwa kuongeza kwa misikiti, makanisa,na masinagongi kungepunguza kasi ya maasi lakini wapi!!!.mambo ndo yamepamba moto!!!!.
 
Back
Top Bottom