Kwanini wapenzi wa CCM wanaiona Richmond lakini hawaioni Escrow?

lengume

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
318
134
Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu washabiki wa Ccm kuizungumzia sana Richmond lkn hawaizungumzii Escro.

Ikumbukwe kuwa Escro iliisababishia hasara Serikali tshs 300 bilion. Lakini cha ajabu hawaizungumzii kabisa.

Sasa mimi najiuliza ni kwa nini Richmond na sio Escro?.
 
Ni swali linaloumiza akili sana ila jiulize pia kwa nn bwana nape na kina makonda wanamtukana el tangu enzi na kupongezwa vyeo,kwangu nashaka sana na aliyeingia na majina yake5 na ukizingatie ile clip ya el kua wananchi wanalalamika na viongoz wanalalamika je ni nani afanye maamuzi,na ukimalizia mzee alivyosema hajui kwa nn sisi maskini daaaaah!!lazma washikilie richmond japo sasa hata kuitaja tangu tarehe28 haitajiki kabisaaaa
 
Pia Jiulize kwa nini Chadema imempa Likizo ya Lazima Dr.Slaa? naskia Pendekezo la Lowassa ni Makongoro Mahanga kukaimu Ukatibu Mkuu!
 
Kina nape wanataka mabadiriko kuondoa kila aliyejihusisha na kashfa yoyote iwayo. Kashfa ni kadhfa, iwe Richmond au escrow na yeyote mwenye kashfa hastahili kuwa Rais wa Tanzania.

Hakuna hata mmoja aliyetajwa kwenye escrow amepitishwa na CCM kugombea urais.

Ni kukosa uzalendo kumsimamisha fisadi kugombea urais.

Hakuna zuri tunaloweza kumnasibihisha nalo Lowassa lakini Magufuli ana record katika usimamizi katika wizara alizosimamia
 
Lengo ni kuwaondoa mafisadi katika nafasi zote za uongozi nchini mwetu. Tuliwekeza kwenye CDM na huu ulikuwa ndio wakati lakini kumbe huko nako kuna mafisadi na wenye uchu wa madaraka kupindukia.

Wamemsimamisha fisadi kutuonyesha tu kuwa hawana nia ya mabadiriko bali kutunisha matumbo yao.
Watanzania tumtambue adui yetu kabadirisha rangi lakini fisadi ni yuleyule
 
msukule wa kikwete

Leo Yale Majina ya Rais wa Mioyo ya watanzania, Kamanda, Kiboko ya Mafisadi mmemvua Dr.Slaa mmemvalisha Lowassa!!!! Hahah bado Mbowe anabadilisha Gia angani dege likitulia anawashusha Bahari ya Hindi
 
Kina nape wanataka mabadiriko kuondoa kila aliyejihusisha na kashfa yoyote iwayo. Kashfa ni kadhfa, iwe Richmond au escrow na yeyote mwenye kashfa hastahili kuwa Rais wa Tanzania.

Hakuna hata mmoja aliyetajwa kwenye escrow amepitishwa na CCM kugombea urais.

Ni kukosa uzalendo kumsimamisha fisadi kugombea urais.

Hakuna zuri tunaloweza kumnasibihisha nalo Lowassa lakini Magufuli ana record katika usimamizi katika wizara alizosimamia

Mngewapeleka mahakamani sawa,kuna wengine kama jk ata kuwataja mnaogopa,mmeng'ang'ania zilizopita mkombozi bank,za stanbic mbona mpo kimya.Mnaitaabisha nchi na Mungu wa mbinguni amewaona,adhabu yenu inakuja tu,wakati huu ata malaika watakatifu watatumiwa kuzuia magoli ya mkono.
 
Eti bila aibu wanashangilia kusimama kwa Slaa ambaye ndie mwanamapinduzi wa kweli. Mbowe ni mfanya biashara ya siasa hawezi kupinga ufisadi.

Tuna elimu watanzania tusijitie ujuha na kufuata mkumbo. CDM ya Lowasa ni ufisadi kwenda mbele, hamna kitu hapo
 
Richmond hawakupata mgao ila escrow kila kada aliondoka na mfuko wa sandarusi umejaa mpunga
 
TunaongeleA Richmond kwasababu muhusika wake mkuu anautaka urais akatengeneze Richmond zingine. Muhusika wa escrow angekuwa anautaka urais pia pangechimbika
 
Ccm bna haiwezi kuwaondoa mafisadi bali inawakuza na kuwalea kama sivyo basi wangempitisha mzee wa maamuzi.
 
Natoa pole kwa CHADEMA iliyouzwa kwa Lowassa. Imejiweka kwenye hali mbaya unnecessary. Sasa CDM nayo inaanza kujihami kwa ufisadi kama CCM sababu ya Lowassa. Poor Mbowe na kamati yake.
 
Mngewapeleka mahakamani sawa,kuna wengine kama jk ata kuwataja mnaogopa,mmeng'ang'ania zilizopita mkombozi bank,za stanbic mbona mpo kimya.Mnaitaabisha nchi na Mungu wa mbinguni amewaona,adhabu yenu inakuja tu,wakati huu ata malaika watakatifu watatumiwa kuzuia magoli ya mkono.

Mimi na wewe ndio wa kuwashitaki na kwa sababu tuna nafasi katika box la kura ndio hapo tumshitaki Lowasa na mafisadi wenzake wote.

Si mmemuona mtu wa haki Dr. Slaa? Ameona hawezi kushiriki kuwadanganya Watanzania ameamua kukaa pembeni. Sasa huu ujinga tunaojivika wa kushabikia Fisadi tumelogwa?
 
Suala ni lowassa hawana hoja ya msingi ndio maana wanaacha kujadili mambo ya msingi wanamjadili MTU kama wangekuwa Na busara wangejadili ukiukwaji mkubwa uliofanywa dodoma kwa kuingia Na majina ya wawatakao mifukoni
 
Back
Top Bottom